البحث

عبارات مقترحة:

الإله

(الإله) اسمٌ من أسماء الله تعالى؛ يعني استحقاقَه جل وعلا...

الحق

كلمة (الحَقِّ) في اللغة تعني: الشيءَ الموجود حقيقةً.و(الحَقُّ)...

الشكور

كلمة (شكور) في اللغة صيغة مبالغة من الشُّكر، وهو الثناء، ويأتي...

Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?

السواحلية - Kiswahili

المؤلف Abulkariim bin Khalidi Al Harby
القسم كتب وأبحاث
النوع نصي
اللغة السواحلية - Kiswahili
المفردات تفسير طبقة الصحابة
Vipi tusome Tarekhe ya  Aal-Beit na Masahaba? UTANGULIZI Vipi tusome Tarekhe ya Masahaba? Mlango wa Mwanzo Sababu ya mwanzo SABABU YA PILI SABABU YA TATU : MLANGO WA TATU Jambo la Mosi : Jambo la Pili: Jambo la Tatu : Jambo la nne: Jambo la Tano: Jambo la Sita: Haya hujibiwa kwa njia mbili :  Wajhi wa mwanzo : Wajhi wa Pili MLANGO WA NNE  Miongoni Mwa Vitabu Muhimu vyenye Kutegemewa kwenye Historia Mlango Wa Tano  Vitabu vyenye matatizo na kuchafua historia ya kiislamu Hatima  Vipi tusome Tarekhe ya  Aal-Beit na Masahaba? UTANGULIZI Vipi tusome Tarekhe ya Masahaba?                                                                                                                                                                                                                Utangulizi wa mtunzi    Sifa zote njema zimemthibitikia Allah aliyejaalia historia ya waislamu waliotangulia kuwa yenye kung’ara na iliyo safi, na Sala na Salamu zimshukie yule aliyepelekwa na Allah kuwa Mtume na Nabii muongowaji pia sala ziwashukie jamaa na masahaba wake, na kila aliyekuwa mchaji.Ama baada ya hayo: Kwa hakika kuhifadhiwa kwa Historia yetu iliyosifika, na kuihifadhi kutokana na mikono ya wachafuaji, na uongo wa wenye chuki na ujinga wa wasioelewa, ni katika mambo ya wajibu juu ya wenye elimu na maarifa, hivyo isiachiwe kuwa kwenye mikono ya Mustashrikina wakaifanya kitambaa cha kufutia uchafu, wala kwenye mikono ya waliouacha mkono uislamu –kwa kusahau au kwa makusudi –ili iwaondoe toka kweye njia waliokuwa mababu na watukufu, wakachukuwa hili na kuwacha hili, kwa ajili ya haja zilizomo kwenye nafsi zao na Allah ni mwenye kufichuwa waliyokuwa wameyaficha.Na katika zama hizi tunaona mataifa na umma zinazojaribu kujifanyia historia yake, zinakusanya mawe na nyaraka, wanachimbuwa mabaki ya kale, wanavunja majumba na kuharibu misikiti, kwa madai kwamba humo imo historia na kumbukumbu, jambo lililowafanya watobowe, wachunguze na kuteketeza wakiwa na matarajio ya kupata historia inayodaiwa. Na hii siyo hali ya umma hizi tu ,bali ndiyo hali ya mataifa mengi katika zama hizi, bali katika kila zama.Jee ni ipi hali ya umma wetu; ulio na historia ing’arayo na iliyochapishwa wala hawaipi umuhimu wowote ?! Kwa kuanzia hapa ni lazima juu yetu kusoma Historia yetu kisomo cha utafiti na uhakiki, kuisafisha kutokana na taka zilizopakaziwa, kuitakasa kutokana na yaliyochanganyiwa, ili itoke ikiwa safi yenye kung’ara, watu wanufaike nayo, na iwe kama alivyosema Mola wetu (Subhanahu Wataalah) :{Ama povu basi hupotea, ama kile kinachowafaa watu basi hubakia kwenye ardhi, hivi hivi Allah hupigia mifano}[Ar Ra’d:17] Abdil Kariim bin Khaalid al ‘Harby. Mlango wa MwanzoSababu za kufanya mapungufu katika kusoma Historia inawezekana kuyarejesha mapungufu yaliyopo kwenye darasa nyingi za historia za zama za kisasa kwenye sababu tatu[1] : Sababu ya mwanzoHakika watoto wengi wa Kiislamu wameangukia kuwa mihanga kwa yale waliyoandika baadhi ya Mustashrikina, waathirika wao miongoni mwa kizazi chetu na waandishi wengineo wasioaminika, ambao hujikumbatizia uongo na uzushi uliozushwa kwenye Historia yetu ya kiislam kwa ujumla, na yale yanayoambatana na Aalil Beit Nabii (S.A.W) waliotoharika na Masahaba watukufu (ﷺ‬.a).Batili hizi huzifanya kuwa ni nguzo kwa wanayoyaandika, kama kwamba ni vyenye kusalimika, wakihamasisha usomaji wa maandishi hayo toka kwa wasomaji wasioona kitu ndani yake, wakitegemea sababu ya kuandikwa kwake kwenye vitabu vya kihistoria, kama kwamba kuwa kwake kwenye matumbo ya vitabu inatosheleza kupakia rangi sifa za ukweli na kuthibitishia upakaji matope kutokana na uongo na batili, wakijisahaulisha kufanyia kazi misingi ya utafiti wa kielimu na kupatikana kwa uhakika yale wanayoyakaribisha usiku na mchana. Pamoja na kwamba mengi ya wanayoyanukuu na kuyataja, ima yanakuwa ni yenye sanad dhaifu, uzushi, au yasiyokuwa na asili kabisa kabisa.Na wengi miongoni mwao wanauelewa uhakika huu isipokuwa wanajisahaulisha tu, kwa ajili ya kutia kasoro na kuiangusha historia yetu tukufu, wao huanza kuandika wakiwa na niya mbaya, malengo ya kiadui, yakilenga kwenye upakaji matope, kutia shaka kwenye nguzo za umma huu, kueneza fitina na kuanzisha uadui baina ya watoto wa umma huu, jee vipi itajuzu kwa muislamu awafanye hawa na wanayoyaandika kuwa ni viwakilishi baina yao na kumbu kumbu, dini na historia yake ?!Na hii haimaanishi kwamba mustashrikina wote wako sawa, wapo wa aina mbali mbali. Wapo miongoni mwao wanaokusudia kubadilisha, kutia kasoro na kutia watu kwenye shaka; kwa sababu ya chuki na husuda na malengo ni ustashriki wa kiadui wa kutawalia na kupora nchi kuuwa waja, na kudidimiza maendeleo ya kiislamu na utamaduni wake.  Na miongoni mwao –nao ni wachache- ni wale walioingilia kumbukumbu zetu kama kazi ya kielimu na utafiti, juu ya kudhihirisha mapungufu wanapokuwa kwenye mazingatio machache tu kutokana na ugeni wao kwenye dini hii, na ukosefu wa maarifa mazuri wa Lugha yake ambayo (ndio msingi wa mwanzo wa kumbu kumbu hizi na usukani wake), na katika haya ni uchapishaji wa kitabu (Al Waafii bil Wafayaati) cha Swalaa’hid Diini as Swafadiyyi, na utunzi wa (Muujamul Mufahras Lialfaadhil ‘Hadiithin Nabawiyyi Shariif ). SABABU YA PILIKuondoka kwa elimu ya kisheria, upungufu wa hima na maarifa, kujingikiwa na njia ya maulamaa wa historia na misingi yenye uhusiano na uandishi na kupanga riwaya ya kihistoria.Hivyo baadhi ya maulamaa mfano wa Maimamu wawili (At Tabary na Ibn Kathir) kamwe hawashurutishi kuleta riwaya sahihi kwenye vitabu vyao na kupuuza dhaifu kutoka na na riwaya za visa dhaifu vya matukio na mambo yaliyozuka, bali walifuata mpango maalum waliouashiria kwenye tangulizi za vitabu vyao; ili msomaji awe kwenye bayana ya jambo hili.Lakini wengi wa mufakirina, waandishi na walioendelea kwa ujumla walikuwa kwenye kifungo na bado wako kwenye misingi hiyo na vitangulizi, hivyo imekuwa kutoielewa na kuipuuza ni sababu ya kupotea tafiti zao na maandishi yao yenye kusadikisha –usahihi – na kufikia kwenye haki ..Hivyo ni katika mambo ya umuhimu kusoma utangulizi wa mtunzi wa kitabu chochote kile ili tupate uwazi wa sera ya kitabu chake. Na kwa kubainisha uhakika wa tuliyotanguliza; tunakuletea mfano wa umuhimu wa kuzingatia misingi na sera za wanahistoria, nayo ni sera ya Imam Ibn Jarir Tabary (ﷺ‬.a) kwenye kitabu chake cha Tarekhe.      Ubainishaji wa Sera ya Imam Tabary kwenye kitabu chake( Taarekhul Umam wal Muluuk) Huyu hapa Imam Ibn Jaririt Tabary[2] anafichua sera yake kwenye utangulizi wa kitabu chake anasema  "Zilizomo kwenye kitabu changu katika habari kutoka kwa baadhi ya waliotangulia, miongoni mwa yale yanayokataliwa na msomaji, au yanayochukiwa na msikilizaji wake, kwa kuwa hakuelewa njia katika usahihi wake, na wala haina maana kwa uhakika, hivyo ieleweke kwamba haikuja toka kwetu, ila imekuja toka kwa baadhi ya wanukuuji, na kwamba sisi hiyo tumeileta kwa namna tulivyofikishiwa.[3]mpaka hapa.Imam Tabary (ﷺ‬.a) anambainishia msomaji kwa uwazi kwamba kamwe hakushurutisha usahihi katika yale anayoyaleta kwenye kitabu chake hichi katika riwaya zake, na kwamba dhamana katika anayoyanukuu iko kwa wasimulizi walionukuu kabla yake, nae kwenye kitabu hichi alikuwa mnukuuji na muaminifu, na sio mhakiki mkosoaji. Hivyo baadhi ya aliyoyasimulia Tabary toka kwao walikusanya baina ya uongo na wingi wa riwaya, na miongoni mwao ni:1-Muhammad bin Hamiid Ar raazy sheikhe wa Tabary : Tabary amesimulia kwa wingi toka kwake kwenye kitabu chake (At Taariikh) na (At tafsir) pamoja na kwamba Muhammad huyu amerembewa kuwa ni muongo na mzushi wa hadithi, nae ni dhaifu mwenye hadithi zisizofaa toka kwa As Sawaadil A’adhwam toka kwa maulamaa wa Jerhe na Ta’adiil [4]2-Luut’ bin Ya’yaa Abuu Mikhnaf;Anazo riwaya nyingi kwenye (Taariikh Tabary ) zimefikilia riwaya (585), kwenye riwaya hizo ameingia kwenye matukio na mambo muhimu yaliyozuka kwenye historia ya kiislamu yakianzia kwenye kifo cha Nabii (S.A.W), mpaka kuanguka, kwa Dola ya Umawiyyah, na Lut huyu ni mwenye kutiwa ila mbele ya maulamaa wa Hadithi.Amesema Ibn MaiynAmesema ibn Ma’iin" ليس بشيء- -  sio chochote" -Na akasema Ibn ‘Hibbaan "anasimulia hadithi za uongo  toka kwa wenye kukubalika . يروي الوضوعات عن التقات":  : Nae Adh Dhahaby akasema:” mtowaji wa habari zilizofisidika”[5]”:"Kutokana na mfano huu umedhihiri umuhimu wa kuangalia sera na masharti ya maulamaa na kuyafahamu katika uandishi wa historia, na umuhimu wa kuzihudhurisha nyoyoni wakati wa kutalii kitabu cha Imam huyu au yule.Hali hii inahusika pia na vitabu vyengine vya habari na historia, bali pia kwenye vitabu vya kumbu kumbu na fani zake tofauti .Baadhi ya wanahistoria hawa sera yao ilikuwa ni kunukuu riwaya na habari hizi zikiwa na sanad zake bila ya kuzingatia hali za watu wala sanadi zake, kwa kwenda kwenye kauli iliyoenea :”Yeyote aliyeweka sanad basi huyo ameshategemeza kauli –hiyo-”, kwa kufuata hikaya za baadhi ya maulamaa wa hadithi katika uandishi wa hadithi, kwani wao huandika kila riwaya kwa sanad yake ikiwa kama hatua ya mwanzo; ama hatua inayofuatia – ni yenye kutofautisha baina ya wanahistoria na wanahadithi –ambapo hushughulika na kuzichuja na kuzitafiti, kuzihakiki na kuzitenganisha baina ya sahihi na dhaifu .Imam Ibn Hajar ameashiria hilo akibainisha njia na sera za wengi wa waliotangulia anasema "Wengi wa Muhadithina katika zama zilizopita toka kwenye mwaka wa mia mbili na kuendelea mbele walitaja hadithi kwa sanadi zake, wakiitakidi kwamba wamejiondolea dhamana yao.”  Kwa kawaida Al-haafidh anakusudia wasimulizi wanukuuji, sio maimamu wadadisi maulamaa wa Jerhe na Taadiil, walinzi wa dini kutokana na kuchafuliwa na kubadilishwa, wenye kutumia misingi na kanuni madhubuti za kukubalika na kukataliwa kwa msimulizi na chenye kusimuliwa, hiyo ni misingi isiyokuwa na shubuha wala mifano kwenye uzoefu wa kibinadamu na maendeleo yake .Ni wajibu wa msomaji-akiwa ni mwenye kufaa-ahakikishe simulizi za kitabu hichi au kile juu ya mwangaza wa misingi ya Muhaddithina wadadisi, nao ni ule unaoitwa "Elimu ya Mustalahi-alhadithi" uliojengeka juu ya kutafiti hali za masimulizi na habari na wanukuuji wake katika hali ya kukubalika na kukataliwa, kwa kukaa kati ya mambo mawili :Mosi :Utafiti na upekuzi kuhusiana na wasimulizi wanukuuji wa riwaya hizi wakitegemea kauli ya mabingwa wadadisi miongoni mwao, maimamu wa Jarhu na Taadili [6];hivyo anaefaa huwa ni thiqah; riwaya zake hukubalika, na asiefaa huwa dahifu riwaya zake hazikubaliki wala hazina hadhi yoyote ile.Pili :Kuangalia kwenye matini za riwaya hizi na kuzifanyia upekuzi kwa kuzilinganisha na kitabu cha Allah na Sunna iliyo sahihi iliyothibiti na misingi ya ujumla yenye kutegemewa kuhusiana na mambo mawili hayo, ili kuelewa zisizofaa toka zile zenye kufaa, zilizofuta –nasikh- toka kwenye zilizofutwa –mansukh- .Hivyo msomaji akiwa ni mwenye sifa ya kustahikiwa na kuendesha tafiti hizi na kuzifanyia uhakiki akiangalia wenye kushikamana na elimu hii tukufu na ya kina; na vyenginevyo itamlazimu kumuogopa Allah na jambo hili kulitegemeza kwa wanaofaa, watu maalum, watu wa utafiti na maarifa ya mathiqa waadilifu . SABABU YA TATU :Kile wanachofanyia danadana baadhi ya waandishi ya uwezekano wa kufanyiafanyia wepesi kwenye riwaya hasa zinazohusiana na zama za mwanzo katika Historia ya Kiislamu zikilinganishwa na ukali katika riwaya za Hadithi za Nabii (S.A.W) nalo wallahi likiwa ni katika makosa makubwa yanayotokea kwa watu wetu waliostaarabika, kwa vile ni aina katika aina za kuathirika na sera za kimagharibi ambazo hazitilii mkazo kwenye unukuuji wa sanadi, na mfano mkubwa wa hilo ni kwamba isnadi baina yao na (Injili) ni yenye kukatika kwa mamia ya miaka, nacho ndicho kitabu chao kitakatifu basi unaona vipi kwenye vitabu vyengine?! Hakika historia ya Ahlil Beit ya Nabii (s.a.w) na Masahaba (ﷺ‬.a) ni sehemu ya dini yetu na kamwe haisihi kuifanya sawa baina yake na ile historia nyengine, au kufanyia uzembe katika kuichukuwa na kuisimulia kwake, hivyo uzembe au kasoro yoyote katika haki ya Historia hii na kuithibitisha kwake basi athari yake kwa vyovyote vile itarejea kwenye dini, na juu ya kusihi kwa hadithi na usalama wake kutokana na ubadilishwaji na ugeuzwaji wake .Nasi tunao mfano wa wazi kwenye utiaji kasoro wa yule ambae ndani ya moyo wake muna chuki kwenye riwaya ya kusilimu kwa Abu Huraira Sahaba huyo mkubwa (ﷺ‬.a).  Hakika watafiti wanajitahidi kwa mapana katika kujadili baadhi ya matukio na mambo ya kihistoria yaliyozuka zamani na sasa, wapo wanaothibitisha na wapo wanaopinga, na kila upande unatanguliza dalili na hoja zake zilizowapelekea kuona hivyo, pamoja na kwamba baadhi ya matukio haya kamwe hayapelekei faida yoyote na amali kubwa, unadhania vipi kuhusiana na Historia ya Aalil Bait na Masahaba (ﷺ‬.a) wabebaji wa Sheria na ngome madhubuti ?!Hii haimanishi uwajibu wa kutendea habari zote za (zama za mwanzo) katika Historia yetu kama  zinavyotendewa Hadithi katika hali ya kukubalika na kukatalika, bali ni wajibu kutofautisha baina ya habari na riwaya.-Hivyo ikiwa habari na athari hizi ni kutoka kwa Aalil Bait na Masahaba (ﷺ‬.a) wanasimulia zuhudi, ushujaa, ukarimu, kujitowa kwao muhanga na wema wa tabia zao, mienendo yao bora na upole wa tabia zao na mambo hayo hayakutoka kwenye misingi mikuu ya kisheria, wala sio yanayokataliwa na maumbile yaliyo salama, hivyo hakuna pingamizi kutajwa, kusimuliwa na kuandikwa kwake, kwani mambo hayo hayagusi au kutikisa asili ya kisheria, na kamwe kwenye kusimulia kwake hakuna madhara au mguso kwa hadhi ya Aalil Bait na Masahaba (ﷺ‬.a) .-Ama iwapo habari hizo ndani yake zimo fitina, au baadhi ya misimamo ya kihamasa, au baadhi ya yanayochafua hadhi ya Aalil Bait na Masahaba (ﷺ‬.a), au ndani yake kimo kitu kinachokwenda kinyume na Misingi ya ujumla ya kisheria, au kumuingiza baadhi ya kasoro zenye kukatalika na maumbile yaliyo sawa.Hivyo aina hii ya habari ni lazima kuangaliwa kwenye sanad zake muangalio wa umakini na wa kina na kuhukumiwa kwa hukumu ya uadilifu .Mikakati hii mitatu ambayo ndani yake kumeingia mapungufu katika kusoma, kuonyesha na kunukuu historia ya kiislamu .            MLANGO WA TATUKanuni kuhusiana na kujibu shubuhati kuhusiana na Ahlil Bait:Inampasia muislamu awe na tahadhari juu ya mambo sita muhimu yanayoambatana na Aalil beit (ﷺ‬.a) Jambo la Mosi :Kwamba hadhi ya Ahlil Bait ni kubwa na imesaidia baadhi ya maadui wa uislam kujipenyeza baina ya waislam, nako ni kukuza kielelezo cha mapenzi ya Ahlil Bait na mawalii (wawachwa huru wao), kuzua hadithi kwenye ubora wao, kama ni matokeo ya watu kukubali fadhila za Ahlil Bait na mapenzi yao kwao kwa ujumla kwani wao walikubali hadithi hizo za uzushi bila ya kuzifanyia upekuzi na utafiti na hivyo tunaona Maimamu wa Aalil Bait ( ﷺ‬.a) wanalitaja jambo hili kwa kila uwazi, na kwamba ni uhakika uliotokea hivyo inawapasa vipenzi vya Aalil Bait ( ﷺ‬.a) kuchukuwa tahadhari miongoni mwa yaliyozuliwa juu ya Aalil Bait ( ﷺ‬.a) katika athari na habari zilizozushwa .Huyu hapa imamu miongoni mwa maimamu wa Aalil Bait tukufu (ﷺ‬.a) nae ni Jaafari Sadiq (ﷺ‬.a) anasema "Hakika watu wamependezeshewa uongo juu yetu "[7]   Naye (ﷺ‬.a) akiita kwa jina la Madwiyyatu akasema:"Hakika ni sisi Aalil Bait (a.s) ni wa kweli kamwe hatutovuka kutokana na muongo na anayotuzulia, basi ukweli wetu huporomoka kwa sababu ya uongo wake juu yetu"[8] Msikilize Shariih bin Abdil Lahil Qaadhy akiisifu kaumu iliyokaa pamoja na Jaafar, na kudai kusimulia toka kwao:"Amesema Abu Amril Kishy: Amesema Yahya bin Abdil Majid Al Hamany, kwenye kitabu chake Al Muallafu fii ithbaati Imaamati 'Ali bin Abi Talib ( ﷺ‬.a) "nilimwaambia Shariik Hakika watu wanadai kwamba Jaafar bin Muhammad ni mdhaifu wa hadithi, akasema "Ninakupa habari ya kisa, Jaafar bin Muhammad alikuwa mtu mwema, muislamu mchaji basi akakumbatiwa na watu wajinga wakawa wanaingia na kutoka kwake" na wanasema ametuhadithia Jafar bin Muhammad hadithi na zote ni Munkarat walizozizuwa toka kwa Jaafar, ili wawatake watu chakula kutokana na kufanya hivyo, na huchukuwa dirhamu toka kwao, waliokuwa wakileta kila hadithi munkar, hayo yakasikiwa na wasiokuwa na elimu, basi miongoni mwao wamo walioangalia, na wengine wapo waliozikataa .Vile vile akasema Imam Jafar Saadiq (ﷺ‬.a) :"Mughira bin Said alikuwa akitegemea kumzulia uongo baba yangu, huchukuwa vitabu vya wafuasi wake, na wafuasi wake walikuwa wamemficha ndani ya wafuasi wa baba yangu" huchukuwa vitabu vya wafuasi wa baba yangu na kuvipeleka kwa Mughira, akawa humo anaweka kufuru na uzandiki, na kuyategemezea kwa baba yangu, kisha anayapeleka kwa wafuasi wake na kuwaamrisha wayaeneze."[9] Jambo la Pili:Hakika hadithi za uongo zilizozushwa kwenye fadhila za Masahaba (ﷺ‬.a) hatua kwa hatua – zinazidi idadi ya Hadithi sahihi kwa makumi ya mara, hivyo sio wajibu kukubali hadithi za fadhila na kuzieneza na kuvukia kwazo mpaka wa sifa ila baada ya kuzitafiti sanadi zake na kuthibitisha usahihi wake. Jambo la Tatu :Hakika fadhila zilizothibiti kwenye haki za Aalil Bait (a.s) hazimaanishi kupwekeka kwao kwa fadhila hizo zilizokuja bila ya kuwashirikisha wengineo, na hivyo ni kwa kufata kanuni inayosema:( Kufanyiwa umakhsusi kwa makarama hakumaanishi kuondolewa kwa mwengine).Lau tutasema: Hakika Nabii (s.a.w) amesema kuhusiana na haki ya Ali ( ﷺ‬.a) – nae ni katika Aalil Bait ( ﷺ‬.a)-: "Bendera hii nitampa mtu ambae Allah atakomboa juu ya mikono yake anayempenda Allah na Mtume wake, naye anampenda Allah na Mtume wake"Jee kwenye hadithi hii ichukuliwe kwamba makarama haya yameondoshwa na hayawezekani juu ya Aalil Bait waliobakia (ﷺ‬.a), na kwamba Al Hassan na Al Hussein wao hawampendi Allah na Mtume wake (s.a.w)Kwa maumbile tu ni kwamba haiwezekani, bali wao ni mabwana wa vijana wa watu wa Peponi na hakuna shaka kwenye mapenzi ya Allah na Mtume wake (s.a.w) kwao, na kwamba lengo la habari ni kwamba Allah amempa hadhi na kumnyanyulia cheo chake kwa kufanyiwa umakhususi ya kutajwa, kwa mfano :Amesema Allah Taala kuhusiana na Aalil Bait (ﷺ‬.a) {Hakika Allah anataka kuwaondoshea takataka Aalil Bait na kuwasafisha msafisho ulio bora} [Al Ahzaab :33] Na akasema kuhusiana na Masahaba {Kamwe Allah hataki kukufanyieni uzito lakini anataka kukusafisheni na kukutimizieni neema zake kwenu }[Al Maaidah :6] Usafishaji ni wenye kuenea kwa waumini wote, lakini Allah amewafanyia umaalum Aalil Bait (ﷺ‬.a) kutokana na ubora wao, nawe pima juu ya hili, na hakuna shaka kwamba baadhi ya Aalil Bait ( ﷺ‬.a) wanayo mambo maalum na yanayowatofautisha na wengine ambayo kwayo hawashirikiani na yeyote yule, kama ambavyo baadhi ya Masahaba (ﷺ‬.a) wanayo mambo maalum na sifa za ziada wasizoshirikiana kwazo na mwengine yeyote yule hivyo ni wajibu kumpa kila mwenye haki; haki yake, na jambo lenyewe ni pamoja na Hadithi ya Kisaai mashuhuri ambayo ndani yake imo sifa kubwa kwa baadhi ya Aalil Bait ( ﷺ‬.a) na kuingiza baadhi ya watukufu wa Aalil Bait ( ﷺ‬.a) kama vile Hassan na Hussein, nao ni katika jamaa wa Mtume (s.a.w) ambao hawakuwa wakiishi kwenye nyumba ya Mtume (s.a.w) kwenye hukumu ya aya tukufu, hivyo haifahamiki sio katika wa karibu au wa mbali toka katika hadithi hii kubinya Ualil Bait ( ﷺ‬.a) kuwa wa Ali pekee, Fatma, Hassan na Hussein (ﷺ‬.a) na tukawakusanya pamoja nao, na pia katika hadithi hii haifahamiki kuingizwa na kutolewa kwa wengine, sio katika sharti la kuingizwa hawa ni kutolewa mama wa waislamu - Allah awaridhie wote- na rehema za Allah zimepanua kila kitu, hivyo kamwe hazimbinyi mmoja kwa ajili ya mwengine, lau mtu angesema nae anao ndugu kumi; Omar, Ali na Khalid ni ndugu zangu. Jee hii inamaanisha kwamba saba waliobakia sio ndugu zake? Haya huja kwenye maneno ya waarabu kwa wingi bali hata kwenye Quran Tukufu, mfano wa kauli yake Taala :{Hakika idadi ya miezi mbele ya Allah ni miezi kumi mbili kwenye Kitabu cha Allah siku Allah aliyoumba mbingu na ardhi miongoni mwao imo minne mitukufu (hurum), hiyo ndiyo dini iliyonyooka } [at Tawbah :26], yaani hiyo ndiyo dini iliyonyooka, na kwamba dini iliyonyooka imefupishwa kwenye idadi ya miezi na kuwa miongoni mwao imo miezi mitukufu, basi kadhalika kauli yake (s.a.w) kwenye hadithi ya Kisaa –nguo-"Hawa ni Ahlil Bait yangu " Anamaanisha watu wa nyumba yangu kama tulivyobainisha.Nasi tunaweza kusema kuwa iwapo Hadithi ya Kisaai inazuwia kuingia mmoja wa Ahlil Bait, basi vipi kaingia humo Ali bin Hassan bin Muhammad, Muhammadi al-baaqir, na Jaafar Sadiq na wengineo? miongoni mwa Itra watukufu waliobakia, na hawa bila shaka asilani hawakuwepo kwenye tukio la kutukuza kwa ajili ya Kisaa.[10]  Jambo la nne:Kwamba kutegemea nasabu pekee haitoshi; Kama ilivyo kuwa ni wajibu juu yetu mapenzi ya (Aalil Bait mmoja ), kwa sababu ya imani yake kwa Allah na nasabu yake na ujamaa wake kwa Nabii (s.a.w), basi ni wajibu pia kwetu kumchukia kwa kiwango cha maasi yake, hali yake ni hali ya mtu mmoja mmoja wa umma huu na "Na yeyote yule aliefanya upole wa amali yake basi kamwe nasabu yake haitomuharakisha."[11] Jambo la Tano:Ufanyaji wa Ualil Bait ( ﷺ‬.a) kuwa wa Ali, Fatma, Hassan na Hussein (ﷺ‬.a) na kwenye watoto tisa wa Hussein tu, kwa hali yoyote ile haisihi, ufanyaji wa Ualil Bait ( ﷺ‬.a) kuwa wao peke yao ni kinuyume na uhakika wa mambo . Na katika ufanyaji wa Ualil Bait ( ﷺ‬.a) kuwa wao peke yao wamefutwa wengi wa walio Aalil Baitin Nabawy iliyotukuka, na ndani yake umo unyimwaji wao wa nasabu hii iliyotoharika, na haki zinazotokana nazo kiibada, kimazingatio na kimali kwao na juu yao, Allah alizowateulia na kuwakadiridhia juu yao, hapa sipo pahala pa kuzielezea kwa urefu .Na katika yaliyokuwa hayana shaka ni kwamba ufupishaji wa ujamaa wa juu ya waliotajwa (ﷺ‬.a), kwa vyovyote vile kunapelekea upunguzaji wa kizazi cha Mtume (s.a.w) na haingii akilini mtu yeyote yule kuwa mtu anaweza kuleta jambo hili .Inatupasa kukuwauliza watu hawa :-Wako wapi maami wa Mtume (s.a.w) ?-Jee Hamza (ﷺ‬.a) sio katika watoto wa Abdil  Muttalib?Upo wapi utajo wake jee yeye siye simba wa Allah na Mtume wake, shahidi wa Uhud na shujaa wa Badri?  Na pale alipostashhadi Nabii (s.a.w) akahuzunika huzuni ambyo hajawahi kuhuzunika kabla yake ?-Jee Nabii (s.a.w) hakusema "Bwana wa mashahidi mbele ya Allah siku ya kiama ni Hamza"!?[12]Jee Abbas (ﷺ‬.a) sie katika watoto wa Abdul Muttalib na ameshuhudia ukombozi wa Makka, na mwenye kuthibiti siku ya Hunein pamoja na waliothibiti?Jee haikusimuliwa "Hakika Abbas (ﷺ‬.a) ni katika mimi na mimi ni katika yeye?"Jee vile vile Nabii (s.a.w) hakusema:" Enyi watu !Yeyote aliemuudhi ami yangu basi huyo ameniudhi mimi ; hakika ami wa mtu ni mfano wake" [13]Wako wapi watoto wa maami wa Mtume (s.a.w).?Jee Jaafar At Tayaaru – mwenye kuruka kwa mbawa – (ﷺ‬.a)   mtu mwenye mambo bora na yenye kushukuriwa?Jee yeye siye aliyesemewa na Nabii (s.a.w) (umeshabihi umbile na tabia zangu )? [14]Jee Yeye hakuwa mmoja wa watangulizi kwenye uislamu ?Jee hakuwa miongoni mwa waliohamia Uhabeshi, na kuendelea kuwa huko mpaka Mtume (s.a.w) alipohamia Madina, akaja siku ya ukombozi wa Khaibar, na Nabii (s.a.w) akafurahi furaha kubwa na kumkumbatia na kumbusu baina ya macho yake ?Imesimuliwa kwamba alimwambia :"Sielewi ni kwa jambo lipi mimi ni mwenye kulifurahia zaidi;ukombozi wa Khaibar au kuja kwa Jaafar?"[15]Pale Nabii (s.a.w) alipompeleka Muuta kuwa naibu wa Zaid bin Haaritha (ﷺ‬.a) alifanya kazi kubwa kwenye njia ya Allah, akapigana mpaka akakatwa mikono yake miwili na akastashhadi,  Allah akamlipa mbawa mbili kwa sababu ya mikono yake hiyo miwili Peponi, kama alivyotolea habari Assadiqul Masduq (s.a.w) basi tokea siku hiyo duniani akapewa jina "Attayaar" ?Nabii (s.a.w) zilipomfika habari za kustashhidi kwake alihuzunika huzuni kubwa na kusema "Usiku wa jana niliingia Peponi nikamuona Jaafar anaruka pamoja na Malaika. "[16]Na akasema (s.a.w) (Jaafar alinipita kwenye kundi tukufu la Malaika, huku mbawa zake mbili zikiwa zimepakwa damu zikiwa nyeupe).[17]Hivyo baadhi ya sifa zake zinazojulisha ukubwa wa hadhi yake na utukufu wa cheo chake duniani na akhera, Allah amridhie yeye na yeye amridhie. Jee Abdillah ibn Abbas wino wa umma –huu- na mfasiri wa Quran aliyeitwa wino kutokana na wingi wa elimu yake, fahamu zake na ukamilifu wa akili na wingi wa fadhila zake.  Kwanini isiwe hivyo, wakati Mtume (s.a.w) alimuombea dua ya kuwa na fiqhi ya dini na elimu ya utambuzi? [18] nae alikuwa katika walioshuhudia Jamal na Swifin pamoja na Ali (ﷺ‬.a), na Masahaba wakuu (ﷺ‬.a ) na Matabiina walikiri ubora huu kwake –Allah awaridhie kwa wema-.!  Kiko wapi kizazi cha Ali (ﷺ‬.a) nacho ni wengi ?Kiko wapi kizazi cha Hussein (ﷺ‬.a) kilichobakia na miongoni mwao ni wajukuu  wa Shahidil Kuufah, Zaidi bin Ali bin Hussein, na kizazi cha watoto wake waliobakia ?Zipo wapi haki zao hawa ?Jee wao ni katika Aalil Bait ( ﷺ‬.a) au sio ? Na iwapo wao hawamo basi ni nani huyo aliyewatowa?Na kwa dalili na hoja ipi inajusurishia tendo hili ?Jee ipo njama nyuma ya ovu hili ? [19]Mjadala wa maudhui hii na uwazi wake hapa sio pahala pake, ila tumetaja hayo kwa lengo la kumtanabahisha msomaji mpendwa kwamba Historia ya Aalil Bait ni pana, kubwa na tukufu kuliko wanavyoitaja baadhi.Aalil Bait ni wengi Allah awazidishe na kuwabariki, nao ni wale walioharamishiwa sadaka, ambao ni:  Bani Hashim, wake wa Mtume (s.a.w) nao ni katika ahli zake –jamaa wa kufuatia sio kwa uasili kama ambavyo makumi ya nasi zilizothibiti zilizowazi zilivyojulisha hivyo; hivyo ni kwamba kabla hawajaolewa na Mtume (s.a.w) hawakuwa kati aali wa nyumba yake na nasi mutawatiri ni nyingi kwenye vitabu na nasi ambazo zinabainisha tuliyoyataja ni kutowafunga Aalil Bait ( ﷺ‬.a) kwenye Ali, Fatmah na baadhi ya kizazi cha Hussein Allah wote awaridhie, amesimulia Muhammad bin Sulaiman al Kuufy :" Hussein bin ‘Uqbah alimuuliza Zaidil Aram :"Ni nani Aalil Bait yake ( ﷺ‬.a) jee wake zake sio Aalil Bait wake ( ﷺ‬.a) ? Akasema :"Hakika wake zake ni ahli zake, lakini Ahli beit yake ni wale walioharamishiwa sadaka juu yao baada ya yeye akamwambia Hussuein "Ni nani hao ewe Zaid?" akasema ni jamaa wa Jaa'far, jamaa wa Aqiil na jamaa wa Abbas "[20]Khuily nae ameeleza hivyo, na akasema kwenye Kauli yake Taala:{Na wenye ujamaa} [Al Hashr:7] "Yaani jamaa wa Nabii (s.a.w) nao ni aal -jamaa wa - Ali , aal-jamaa wa -  "Abbas, aal-jamaa wa Jaafar na aal-jamaa wa- 'Aqiil (ﷺ‬.a), na kamwe hakushirikiana na yeyote mwengineo, na wajhu huu ni sahihi kwani unawafikiana na madhehebu ya Muhammad (s.a.w)  "unajulisha wale waliotajwa kwao wao"[21]Amesimulia Assidiq kwamba Ali (ﷺ‬ a) amesema "Ewe Mtume wa Allah hakika wewe unampenda Aqiil: Akasema "Naam Wallahi, hakika mimi ninampenda mapenzi mawili: mapenzi kwa ajili yake na mapenzi kwa ajili ya Abi Twalib kwake, na kwamba mwanawe atauliwa kwa sababu ya kumpenda mwanao.. mpake pale aliposema: "Nashitakia kwa Allah kwa yatakayowakuta jamaa zangu baada yangu"[22]  Hivyo akamuingiza Uqail na wanawe wawili kwenye wanaoitwa -jamaa waliotoharika (al ataratit taahirah)-. Jambo la Sita:Nyingi ni kauli baina ya kurasa za vitabu vyenye shubuha ambavyo vinadai kwamba Aalil Bait ( ﷺ‬.a) wamedhulumiwa na kukandamizwa miaka kadha tokea kifo cha Nabii (s.a.w) na kupitia kwenye zama Makhalifa waongofu mpaka kwenye Dola ya Umawiyyah na Abbaasiyyah na hakuna yeyote yule miongoni mwa Aalil Bait ( ﷺ‬.a) ila ameteseka kwa kufungwa, kuuawa, kuhamishwa, kutiliwa sumu au madai zaidi ya hayo . Haya hujibiwa kwa njia mbili :  Wajhi wa mwanzo :Kwamba msingi wa ahli Sunna wal Jamaa na jambo ambalo halina khitilafu katika hilo na kuwa makubaliano baina yao ni kuwaheshimu Aalil Bait ( ﷺ‬.a) kujuwa fadhila na ujamaa wao kwa Nabii (s.a.w) na wasia wake kwao amesema: Nabii (s.a.w) ''Na watu wa nyumba yangu nakukumbusheni Allah kwenye watu wa nyumba" "nakukumbusheni Allah kwenye watu wa nyumba yangu","nakukumbusheni Allah kwenye watu wa nyumba yangu  "[23] Hivyo Aqida ya Ahli Sunnah wal Jamaa imo kwenye vitabu vyao; vitabu vya Hadithi vitabu Aqidah, vitabu vya Fiqhi, vitabu vya Tarajum na Sirah ambamo kila mwenye kitabu hutaja kwenye sehemu iliyo na mnasaba na habari hiyo. Hivyo kwenye vitabu vya Hadithi utaona milango kuhusiana fadhila zao,, kwenye vitabu vya Aqida utaona ubainishaji wa itikadi kuhusiana na wao, kwenye vitabu vya Fiqhi utaona milango kuhusiana na yanayohusina nao katika ahkami, kama vile kuharamishwa sadaka juu yao, na vitabu vya Tarajum na Sirah vinataja utajo wao, maelezo kuhusiana na wao na taarifa zao.Huu ndio msingi kwa Ahli Sunnah, msingi huu kamwe hauwezi kuporomoka ila kwa dalili iliyo ya wazi, na tunaposoma Historia na tutaona kwamba hayo yanayodaiwa na baadhi yao kuhusiana na ukandamizaji wa Ahli Sunnah na viongozi wao kwa aal beit ni batili yasiyosihi wala kuthibiti ila pale panapokuwa na kinyang'nganyiro juu ya uongozi na madaraka kama ilivyotokea kwenye mapinduzi ya Imam Zaid, Allah amrehemu yeye na wengine.Amesema Sheikhul Islaam Ibni Taymiyah (رحمه الله) "Ama yule aliyemuuwa Hussein, au kusaidia basi huyo amethibitikiwa na laana  " ya Allah. Malaika na watu wote"[24]  Hivyo haisihi kabisa muislamu kupaka matope historia ya Aalil Bait (ﷺ‬.a) iliyosafi na mapenzi ya waislamu kwao kwa kisa cha batili au riwaya ya uongo kama vile anavyofanya Al Asfahaany kwenye kitabu chake (Muqaatilut Twalibiin), kitabu cha Al Asfahaany kilichopewa anwani ya (Muqaatilut Twalibiin) ni kitabu kilichojaa batili na uongo wa kihistoria ambao mwandishi yeyote anashindwa kuyathibitisha kabla hajawarembea ahli Sunna wal Jamaa uongo huu ulio mkubwa .Vitabu vya kihistoria vimesheheni habari za kuheshimiwa kwa Aalil Bait (ﷺ‬.a) na Makhalifa, kuwapenda na kuwapa kwao hadhi :Amesema Abu Bakri (ﷺ‬.a) "Mchungieni Muhammad watu wa nyumba yake"[25] Na akasema (ﷺ‬.a) "Naapa na yule ambaye nafsi yangu iko kwenye mikono yake hakika ujamaa wa Mtume wa Allah (s.a.w) kwangu mimi ni bora zaidi kuliko asili ya jamaa wangu "[26] Nae (ﷺ‬.a) akasema vile vile akiwa anazungumza na Fatma na Ali "Wallahi kamwe sikuwacha nyumba wala mali, na jamaa na watu wa nyumbani, ila kwa kutafuta ridhaa ya Allah, ridhaa ya Mtume wake na ridhaa ya jamaa zake"[27]Abu Bakri (ﷺ‬.a) alipeleka mmoja wa wake zake nae ni Asmaa bint Umeish kwenye nyumba ya Ali kwa lengo la kumuhudumia kwa tiba Fatma (ﷺ‬.a) wakati wa ugonjwa wake bali pia akashiriki kwenye kumkosha Fatma Az Zahraa na kumvisha sanda (ﷺ‬.a)[28]   Amesema Umar Ibn Al khatab (ﷺ‬.a) kumwambia Fatma (ﷺ‬.a) "Ewe binti wa Mtume wa Allah hakuna yeyote kipenzi zaidi kwetu katika viumbe kuliko baba yako na hakuna yeyote kipenzi zaidi kwetu katika viumbe baada ya baba yako kwetu kuliko wewe.[29] Inatosheleza kwamba Omar alimteua Ali (ﷺ‬.a) kuwa katika jumla ya kundi ambalo ndani yake muwe na khalifa wa waislamu baada yake" Na Omar Alimuoa binti ya Ali -Ummu Kulthuum- (ﷺ‬.a)Hivyo hivyo hali pamoja na Khalifatir Rashid Othman bin Affaan, historia yake ni yenye kumeremeta kwa wingi kutokana na misimamo ya kushirikiana baina yake na baina ya Aalil Bait ( ﷺ‬.a) na namna alivyokuwa akishauriana na Ali kwenye kadhia kadha, bali uhakika wa uhusiano huu wa kidugu unatudhihirikia namna Ali alipowasimamia wanawe kwenye kumlinda Othman bin Affaan siku alipostashhadi kwenye nyumba yake (ﷺ‬.a) na hivyo ni kwa ajili ya mapenzi kwake na mapenzi ya Othman bin Affaan kwake kwani msimamo wao ni kujizuwia na vita.[30] Imeelezewa kwamba Harun Rashid alikwenda kwenye kaburi la Nabii (s.a.w) akijifakharisha kwa watu, akasema Assalamu Alaikum Ewe Mtoto wa ami-yangu – kwani yeye ni katika kizazi cha Al Abbas bin Abdil Muttalib, akaja Musa bin Jaafar kamwambia; Assalamu 'alaika ewe baba yangu, Harun Rashid anaangalia, akasema Wallahi huku ni kujifaharisha.   Harun Rashid akasema "Nimepata habari kwamba wengi wananidhania mimi namchukia Ali bin Abi Talib, na Wallahi mimi kamwe simpendi yeyote kama ninavyompemnda yeye."[31]Khalifa Muadilifu Umar bin Abdilaziz alimwabia Fatmah bint Ali bin Abi Talib (ﷺ‬.a) "Ewe bint Ali Wallahi kwenye uso wa ardhi hii hakuna Aalil Bait ( ﷺ‬.a) vipenzi kwangu kuliko nyie na nyie ni vipenzi zaidi kwangu kuliko jamaa zangu"[32]Watu walijikumbusha Zuhudi na Mazuhadi basi kundi moja likasema fulani na jengine likasema fulani Umar bin Abdilaziz akasema: zahid kuliko yeyote yule ni Ali bin Abi Talib (ﷺ‬.a)"[33] Wajhi wa Pili Hakika jambo kubwa na lenye hadhi kubwa toka kwa watu na hasa hasa akiwa ni katika wema wa umma na maulamaa wake Allah (S .W) analomfanyia mtihani ili amnyanyulie hadhi na daraja yake kwenye Pepo zenye neema, hivyo mwenye kupata mtihani mkubwa au kuuawa miongoni mwa ahlil Bait kama ilivyotokea kwa Hussein (ﷺ‬.a) -Shahidi mwenye kufanikiwa, basi huwa ni namna ile (Allah anapompenda mja humfanyia mthani), na jambo hili sio maalum wala kukusudiwa ahlil Beit (ﷺ‬.a) tu bali dhuluma imetokea juu ya maulamaa wengi wa Sunna na wakuu wao kama vile Said bin Jubeir, Imam Abu Hanifa, Imam Malik na, Imam Ahmad na wengi wengineo miongoni mwa wema wa umma wa Muhammad (s.a.w).Dhuluma, ukandamizaji na mabalaa yamewatokea Manabii wa Allah (a.s) na wema waliokuja baada yao, huyu Daniel (a.s) aliekutana na mabalaa ya aina ya mwisho ya ukandamizaji aliyofanyiwa na mfalme mwenye kiburi "Bakhtanasir" kwa kumfunga na akamuingizia simba wawili lakini Allah akamuhifadhi na kumlinda dhidi yao.[34] Hivyo hivyo kisa cha Nabii wa Allah Yaqoub (a.s) kwa kupotelewa na mwanawe, Nabii wa Allah Zakariyyah, Nabii wa Allah Mussa (a.s) mbele ya mwenye kiburi Firaun, Nabii wa Allah Issa (a.s) pamoja na mayahudi, Nabii wa Allah Muhammad (s.a.w) akiwa na Makureshi na makafiri wa Makka, na visa vyao ni mashuhuri vyenye kujulikana.Na baada yao ni Masahaba wa Nabii (s.a.w) waliohama toka kwenye nchi zao, mali na jamaa zao, waliadhibiwa kwa aina za adhabu na kuendelea mpaka baada kufariki kwake Nabii (s.a.w) yalitokea yaliyotokea kwa waliokuwa kabla yao miongoni mwa watukufu, Omar al Faruq (ﷺ‬,a) aliuawa kwa khanjari ya khiyana na chuki, akiwa anasalisha kwenye mihirabu, hivyo hivyo Shahidudaar Othman bin Affaan (ﷺ‬.a) aliyeuawa kwenye nyumba yake akiwa anasoma Quran, hivyo hivyo ndivyo alivyouawa amiiril Muuminiin Ali (ﷺ‬.a) akiwa anatangaza :"Enyi watu sala! Sala!, na wengineo katika Masahaba wema, na kadhalika balaa na ukandamizwaji yamewapitia maulamaa wengi na wakuu.Huyu hapa Imamu Al Awaza'iy –Allah amrehemu –alifikwa na balaa kubwa mbele ya mmoja wa wenye jeuri na kukaribia kumuawa, Habari za Imam wa Ahli Sunna Imam Ahmad–Allah amrehemu – pamoja na Khalifa Muutaswim ni mashuhuri na zenye kujulikana, hakika alimuadhibu na kumpiga viboko mpaka mgongo wake ukachanika na kuchunika ngozi, akamfunga gerezani na kumbana [35] Pale Fatimiyina walipotawala Misri waliwakandamiza maulamaa na miongoni mwao alikuwa Imam Abi Bakri An Naablisy, wakaamrisha kupigwa kwenye siku ya mwanzo kisha siku ya pili kutundikwa mbele ya watu, kisha siku ya tatu yake kuchunwa na kutolewa ngozi toka kwenye nyama yake, kwa kisu cha kiyahudi .[36] Imam Nuaim bin Hamad aliekufa akiwa amefungwa kwa minyororo gerezani na kumuondowa akiwa maiti wakamrembea shimoni bila ya kuoshwa .[37]Imam al Harawyil Answaary anasema:"Nilionyeshwa upanga mara tano, siambiwi rudi kwenye madhehebu yako, ila naambiwa nyamazia waliokutangulia, huku nasema sinyamazi ."[38]  Mifano ni mingi mno, na lengo ni ukandamizaji na dhuluma juu ya Ahli Sunna na maulamaa wake, kama ilivyotokea kwa wenginewe, na mtukufu hufanyiwa mitihani, na kamwe hawatowachwa kufanyiwa mitihani.   . MLANGO WA NNE  Miongoni Mwa Vitabu Muhimu vyenye Kutegemewa kwenye HistoriaMwenye lengo la kujuwa vianzio vya Tarekhe vyenye kukubalika, anaweza kupata kwenye vitabu vya tarekhe na Hadithi zenye kuwekewa sanad maalum kwa maelezo ya historia za watu na watu maalum na historia zao, ni sawa iwe watunzi wake wamejiwekea sharti atika maulamaa wenye kukubalika usahihi kwenye kuzitaja kwao, au kwa kutolea maelezo juu ya riwaya kuhusiana na usahihi na udhaifu wake, hivyo vitabu vimemtoshelezea msomaji wake tabu za kutafiti na uhakiki, ama vile vitabu ambavyo wasimulizi wake wanasimulia kwa sanadi bila ya kubainisha hali zake basi ni wajibu juu ya msomaji wake kuhakikisha usahihi wake. Na hivi hapa ni baadhi ya vianzio vya Kihistoria ambavyo inawezekana kutegemewa katika usomaji na kuandika Historia ya kiislamu ,tunavitaja minogoni mwao:     1.       Kitabu" Tabaqatil Kubraa"  cha Ibni Saad aliyefariki mwaka 230 H:Nacho ni kitabu muhimu katika mlango huu ; kwani yeye –Allah amrehemu –anataja riwaya kwa sanadi zake, hivyo msomaji hana kazi yoyote ile isipokuwa kufanyia utafiti sanadi hizo ikiwa ni mwenye uwezo wakufanya hivyo, na katika sifa zenye kutofautisha kitabu hichi na chengine ni kwamba ni katika vitabu vilivyotangulia na vianzio vya Sira ya Nabii (s.a.w), Tarajumi na habari, mtunzi wake aliwahi karne ya pili hijriyya pamoja na kuchukulia tahadhari riwaya za Waaqidiy, na madhaifu na matrukina (wenye kuwachwa riwaya zao) na wenginewe, au kama haelewi basi aulize wanaolewa kama alivyoamrisha Allah Azza wa Jalla kwenye Kitabu chake kitukufu. 2.       Taariikh Khaliifati bin Khayyaat ":Nacho hata kikiwa ni kidogo zaidi kuliko  kitabu 'Tabaqatil kubra" ila ni kwamba kinayo sifa ya ziada ya usalama wa matini zake katika udhihirishaji wa fitina ,na mara nyingi yaliyotokea kwenye zama za Masahaba (ﷺ‬.a).3-(Tarekheil Umam wal Muluuk) maarufu (kwa Tarekhet Twabary) Nayo ni Tarekhe iliyojaza habari, athari na riwaya, lakini imechanganya yaliyokonda na yaliyonona, na hakuna lawama kwa Twabariy, kwani yeye ameweka sanadi kwenye riwaya hizi, na mwenye kuwekea sanad basi huyo ameshajiondoshea dhima na lawama, na tumeshabainisha kwa uwazi kwenye utangulizi wa kitabu .4-Al Bidaaya Wan Nihaaya Cha Imam Ibni Kathiir:Mtunzi wa kitabu cha “Tafsiiril Quran al Karim “,kitabu hichi hata pamoja na kwamba ananukuu riwaya zake toka kwenye baadhi na vianzio vilivyotangulia ila tu ni kwamba kinayo maelezo juu ya riwaya nyingi za kihistoria kuhusiana na usahihi na udhaifu, kutokana na kuwa kwake Imamu kwenye hadithi na elimu zake, na chapa bora zaidi ni chapa ya Daaril Hijra chini ya usimamizi wa ‘Abdillahi Turky. 5-“Taariikh Dimashq “ cha Ibn ‘Asaakir:Nayo ni historia iliyojaza ni makhsusi kwa walioingia Damascus miongoni mwa maulamaa katika masahaba na wengineo mpaka kwenye kipindi cha mtunzi, nacho kinatofautiana na vyengine kwa kuwa na sanadi kwa kila tukio’6-“Tarekheul Islaam” cha Shamsid Diin Adhdhahaby Nacho ni kitabu kikubwa chenye manufaa makubwa, husimulia kisa kamili cha historia ya kiislamu, na vielelezo vyake na matukio yake muhimu, kina sifa ya ziada inayotokana na maelezo ya imam juu ya taarifa za matukio ya kihistoria, matukio na athari. Nae imam Dhahaby ni bahari kwenye elimu ya Jarhu na Taadiil  ni katika maimamu wakubwa katika fani hii, na Daktari Bishar Awaadh Maaruuf amefanya kazi kubwa ya kufanyia uhakiki, kitabu hichi kinahesabiwa kuwa ni katika chapa bora zaidi.7-“Siyaru ’Alaam Nubalaa” cha Hafidh Adhdhahaby (رحمه الله) Nacho ni kitabu chenye manufaa vilevile, kinatowa sira na habari za nyota na muhimu katika maulamaa zilizojulikana katika historia ya kiislamu tokea mwanzo wa kipindi cha Masahaba (ﷺ‬.a) mpaka karibu ya kifo cha mwandishi (رحمه الله), nae ameambatanisha na kitengo maalum kwa Sira ya Nabii (s.a.w) na historia za Makhalifa wanne waongofu na chapa bora zaidi ni ile chapa ya Muasasat Risaalah.8.”Taariikhul Madiinah cha Ibn Abii Shaibah Ni kitabu kilichojaa faida, Ibn Abi Shaibah ametilia umhimu mkubwa utajaji sanadi kwenye hadithi na habari zilizo nyingi, na ndani yake zimo riwaya muhimu kuhusiana na fitina na mauaji ya Shahidi Othman bin Affaan (ﷺ‬.a), na kitabu kina kosoro ya baadhi ya maudhui zake kutokana na kupotea kwa baadhi ya miswada, kwa mfano ukhalifa wa Abi Bakr haumo kwenye kitabu.[39].9- “Tarekhe Ibn Khulduun”10-“Al Muntadham fiy Att arikh “ cha Ibnil Jawzy .11-“Awaaswim minal Qawaasim” cha Abi Bakr bin Al ‘ArabyKimehakikiwa na kutolewa maelezo na sheikh Muhibbudini al Khatib (ﷺ‬.a), na kitabu hichi kimechapishwa mara nyingi, na kukubalika kwa wasomi wakuu na wengineo kutokana na nafasi na hadhi ya mtunzi wake ambaye ni katika maimamu. wa Kiislamu Abi Bakr bin Al ‘Araby na kutokana na hoja zilizowazi na majibu yanayotosheleza kwa masuala mengi muhimu, hivyo kitabu ni cha aina yake kwenye uwanja wake, anakuja na (Qasima) shubuha, anaifuatanisha na uchambuzi na kuweka wazi shubuha (‘Aswima ), na kuijibu  kwa hoja, dalili sahihi.Hivi ndivyo vitabu muhimu vilivyotolea umuhimu uelezaji wa tarekhe  na matukio ya kiislamu , na vyenginevyo vipo vingi katika uwanja huu ,ni sawa viwe vya zamani au vya kisasa .Kamwe haituondekei kwenye kiini chake kuashiria kwamba vipo vitabu sio makhsusi kwa Tarekhe, na humo mumewekwa matukio muhimu, na habari za kimsingi kwenye Tarekhe ya kiislamu, na hasa kwenye zama za mwanzoni, mfano kama vile vitabu vya hadithi, Masanidi Maajim, na muhimu vyao :1-“Asahihi “ ya Imam Bukhariy .2-“Asahihi “ ya Imam Muslim .3-“Sunanul Arb’a” ya Abi Daud, Annasai, At Tirmidhy, na Ibn Maajah .4- “Al Musnad “ cha Imam Ahmad bin ‘Hanbal.5- Al Muswannaf cha Ibni Abi Shaibah .6-“ Mustadrak “ ya Haakim Nisapury. ·                  Ama vitabu vya tarajumi za Masahaba –wakiwemo Aalil Beit- (ﷺ‬.a) vya kimsingi n amuhimu ni kama :- ·                   1-Al Istii’aab fiil Ashaab cha Ibni ‘Abdil Barr .2-“Usudul Ghaabah fii tamyiiz Sahaabah “ cha Ibni;l Athiir .3- Al iswabah fi Tamyiiz Sahabah cha Ibn ‘Hajaril ‘Asqalany .Vitabu hivi ni vyenye habari na athari, na tunakumbusha kwamba habari na athari hizi vinalazimikiwa na mizani ya uhakiki na utafiti hasa katika kufahamu sanadi na kuhusiana na Jarh na Taadiil; ili kujuwa sahihi kutokana na dhaifu .·                  Ama vitabu vy kisasa :Wapo watafiti waliosafisha na kudadisi riwaya, wakabainisha sahihi toka kwenye dhaifu zake, hapa tunaashiria baadhi ya vitabu muhimu katika vitabu hivi, mfano,  Mtungo wa vitabu vya Daktari Ali bin Muhammad As Swallaaby  Allah amuhifadhi na ambariki katika kuwepo kwake :·                   I -Al Inshiraah fii raf -i dhiiq siirati Abii Bakr.2-Faswlil Khitaabi fii siirati Amiiril Mu-u- miniin Omar ibn Khatab shakhsiyyatuhu wa Asruhu .”3- Taysiiril Kariim fii sirati ‘Uthman bin ‘Affaan ‘’ 4- Asmal Matwaalib fii siiratilAmiiril Muuniin Alibin Abi Talib “5- Amiiril Muuniinal ‘Hussein bin Ali–Shakhsiyyatuhu wa ‘asrih I”6-“Muawiya bin Abi Sufyaan “7-“Omarbin ‘Abdil ‘Aziiz “8-“Ad Dawalatul Umawiyyahtu ‘Awaamilil Idizdihaar wa Tadaa’iyaatil anhiyaar”Kadhalika vipo baadhi ya vitabu muhimu, mfano :1- “Mausuatu Taariikhil Islaamy “ cha Muhammad Shaakir2-Silsilatu KutubulMahmuud  Muhammad Shaakir kuhusiana na shakhsiyati[40] za kiislamu .3-Siiratiu ‘Aaisha bint Ummul Mu-u –miniin “ cha Annadawy .“Ahdathi wa ahadithi fitina".cha Daktari Abdil ‘Aziiz ad Dakhkhaan :Nacho ni kitabu chenye umuhimu wa kiwango cha juu katika kufanyia uhakiki msimamo wa Masahaba kuhusiana na fitina zilizotokea, na utafiti wa udadisi kwa wingi wa riwaya zilizokuja kuhusiana na jambo hili, pamoja na maana ya fitina, msimamo wa Masahaba kuhusiana na fitina hiyo, kubainisha sababu na athari zake, msimamo wa muislamu kuhusiana na fitina hiyo na kitabu ni kutokana na risala ya udaktariri na kimechapishwa na Maktabati Swahaabah Sharjah chapa ya Mwanzo.5- ‘Hiqbatun minat Tarekhe  “ cha Sheikh ‘Uthayman Khamis :Kitabu hichi kinahesabiwa kuwa ni vitabu muhimu vya wakati huu mtunzi ametolea umuhimu kutaja miongoni mwa habari zilizosihi katika habari na athari zilizokuja baada ya kifo cha Nabii (s.a.w), mpaka kipindi cha kuuawa kwa Al Hussein (ﷺ‬.a) pamoja na kuweka rai wa usahihishaji baina ya rai hizoViwanda vingi vya kupiga chapa vimekipiga chapa, na chapa yake bora ni ile chapa ya Maktabatil Imamil Bukhaary -Ismailiya Misri-.6-“Tahqiiq Mawqifis Swahaabati minal Fitan" cha Daktari Muhammad Amhazuun.:Nayo ni kazi ya risala udaktari, mtafiti ameshughulikia ndani ya kitabu hicho riwaya na athari muhimu zilizokuja kwenye Ukhalifa wa Makhalifa wane kisiasa (ﷺ‬.a).Kimepigwa chapa na Dar twayyibah, na Maktabatil Kawthar Riyadh chapa ya tatu .7-‘Asrul Khilaafaashidah” cha Daktari Akrau Dhiyaail ‘Umary Nacho ni kitabu  chenye kudadisi riwaya za kihistoria kilicho mbali na kushadidia au kufanyia wepesi .Kimepigwa chapa na Maktabatil ‘Abiikaan chapa ya nne. : 8- Akhtwaa Yajibu an tusahhah Minat Tariikh “:Cha Daktari Jamaal ‘Abdil Haady na Duktuurah Wafaau Juma . Nacho ni kitabu chenye mtungo wa vitabu vyenye kushughulikia makosa na ufahamu uliokosewa ni mashuhuri kwa baadhi ya waandishi na wasomaji, humo mumetokea upakaji matope wa kukusudiwa kwenye Tarekhe yetu kuu ya kiislamu.9- Tarekheul Islaamiy  Mawaaqifu wal ‘Ibar  cha Daktari ‘Abdil ‘Aziiz ‘Humaidiy .10- ‘Abullahi bin Saba-i wa Atharuhu fii ahdaathil Fitinah fii Swadril Islaam .Cha Sheikh Sulaimanil ‘Audah.11 “Li adhaa Yuziifuuna At Tariikh wa Ya’abathuuna bil ‘Haqaaiq” cha Isma’ill Kaylaaniy .12-atharul ‘HYadiith fii Nash-tit Taariikh ‘inda l muslimiin “  cha Daktari Bashshaar ‘Awwaad Ma’ruuf .13- “ Manhaju Kitaabatit Taariikhl Ialaamiy “ cha Muhammad Swaamilil Islaamiy .14- “Abu Mi’hnaf wa Dawruh ufii Nash-ti kitaabati Tarekheiyyah “  cha ‘Al y Kaamilil Qar’aaniy .15- Al Mu-a-rrikhunal ‘Arab wal Fitinati lKubraa” cha Daktari .’Adnaan Mal’ham 16- “  Marwiyyaat Abi Mi’hnaf fii Tarekheit ‘Twabariy” cha Daktari Ibraahiim Al Ya’hya.17- Iilaamul aanaam bima Yajibu Na’hwal A’alaam” utunzi wa ‘Abdil ‘Hamiidil ‘Hasuunaah. Mlango Wa Tano  Vitabu vyenye matatizo na kuchafua historia ya kiislamu Isije ikatuondokea kumbukumbu kwamba, baadhi ya vitabu ni wajibu kwetu kuvichukulia tahadhari wakati wa kuvisoma na kunukuu toka kwenye vitabu hivyo, kwani kuvisoma bila ya kujuwa kanuni zilizopita au kuwa na tetesi juu ya sera za watunzi wake au kuvifanya kuwa ndio vianzio vya msingi katika utafiti, kumewaingiza watafiti wengi kwenye makosa mabaya na ya hatari, yenye kupelekea kufanya vipenzi (Walaa) na kujitenga (Baraa) na uchoraji wa picha za kiza kwa baadhi ya vielelezo vya umma wa kiislamu. MasahabaKwa hakika hivi ni vitabu vya kisanii sawa na asali iliyochanganywa na sumu, watunzi wake ni wakeshaji kwenye mizaha na upuuzi, hivyo wanapopata nukta yoyote ile huitowa bila ya kujali ni ya kweli au uongo .Tumetangulia kuashiria uwajibu wa kuangalia kwenye habari na riwaya, habari na athari hizi zikiwa ni kuhusiana na Ahil Beit na Masahaba zinasimulia zuhudi na ushujaa, ukarimu, kujitowa kwao muhanga, tabia zao njema, uzuri wa mienendo yao na upole wa desturi zao, na hazikuwa ziko nje ya misingi ya ujumla ya kiislamu wala kuwa ni yenye kukaliwa na maumbile yaliyo salama, basi hakuna pingamizi kutajwa, kusimuliwa na kuandikwa kwake, kwani hazigusi wala kutia dosari msingi wowote ule wa kisheria, wala kusimuliwa kwake hakuleti madhara au kasoro kwenye hadhi ya Ahil Beit na Masahaba (ﷺ‬.a)Ama habari hizo zikiwa ni zenye fitina, au baadhi ya misimamo ya kihamasa, au baadhi ya mambo yanayotia dosari cheo cha Ahil Beit na Masahaba (ﷺ‬.a) au ndani yake kimo kitu kinachokwenda kinyume na misingi ya kiujumla ya sheria au ndani yake mumeingia baadhi ya kasumba zinazopingana na maumbile sahihi; basi aina hii ya habari lazima sanadi zake zifanyiwe utafiti, na kuhukumiwa kwake kwa hukumu ya uadifu; kwani kuwatia dosari Ahil Beit na Masahaba ni kuitia dosari sheria na walioibeba., na hasa kwamba vitabu hivi sio asili ya tarikh ya Ahil Beit na Masahaba (ﷺ‬.a).na kwenye vitabu vyenye kutegemewa yamo yanayotosheleza kwa uchoreaji wa sura yenye kung’ara ya historia ya wema hao watukufu, kizazi bora kilichowahi kujulikana na jamii ya mwanadamu na bado hali inaendelea kuwa hivyo.Miongoni mwa vitabu hivyo vimo ambavyo ni wajibu kuvichukulia tahadhari wakati wa kusomwa kwao : 1-“Al –aghaaniy “cha Abil Faraj Al Asfahaaniy:Hichi ni kitabu cha kukeshea –kwenye kumbi za starehe-mashairi na taarabu, kamwe hakina uhusiano wowote ule na Tarekhe kwa hali yoyote ile.Al Asfahani amekiingizia uongo na ukosefu wa haya, ubaguzi wa kiuadui na pia utiaji dosari juu ya Makhalifa wa umma huu, na kwenye baadhi ya watu muhimu katika Ahil Beit (ﷺ‬.a) kama vile Sakinata bintil Hussein (ﷺ‬.a) na wengineo, kwenye majaribio wenyekutiwa shubuha ili kutoboa ukuta madhubuti wenye kutilia nguvu jamii za kiislamu kwenye kumbu kumbu zake za kiroho na mirathi yao ya kiungu, ili kujiwepesishia kuutenganisha toka kwenye ngome mshikamano wa uliojikita na zama zake tukufu zilizopita baada ya hapo, ili uwe wenye kuandaliwa kwa hujuma na mashambulizi, mara baada ya kupoteza kwake kujipa nguvu kwake kwa misingi ya asili zake iliyopita –kwenye sura anayoitaka Aswfahaaniy na wenginewe – pahala pa kutilia shaka, baada ya kupata simanzi kutokana na marashi ya kitakatifu waliyokuwa wakiyapata kutokana na kusoma historia ya Ahil Beit na Masahaba (ﷺ‬.a) .Hivyo kuvunja mipaka ya kiislamu kadha iliyowazi kwa Asfahany katika kutaja riwaya na habari kwenye kitabu chake cha -“Al –Aghaaniy" Kwa mwenye kuzingatia kitabu hichi na kama tulivyosema kwamba yeye hakika amevunja mipaka ya heshima hadi akafikilia kuvunja heshima za nyumba ya Nabii (S.A.W) iliyotawalia nafasi ya mapenzi, heshima, utakatifu na fadhila katika nyoyo za waislamu, hakika Asfahani ametowa taswira kwa Sukaina bint Al Imam Hussein na mjukuu wa Az Zahraa Fatma bint Mustafa (s.a.w) amemuweka kwenye sura anayoikataa na kuichukia kila muislam, basi iweje kwa binti Al -Hussein bwana wa vijana wa watu wa Peponi ?!Miongoni mwa sura hizi ni ile aliyoitaja kwenye kitabu chake -“Al –Aghaaniy“ (42/17) kwamba Sakina bint Al Imam Hussein (ﷺ‬.a) alikuwa akimpenda muimbaji aliyetubu kwa Allah kutokana na kosa la kuimba, hivyo yeye kama alivyofanyiwa taswira na Al –Aghaaniy ni mwenye kuumizwa na kughumishwa na toba ya muimbaji huyu, nae anachokitaka toka kwake arejee kuimba, nae anafanya jitihada zake katika kumpoteza –Tunajikinga kwa Allah kutokana na hayo -!!Visa na uongo zaidi ya huo, Al Asfahaaniy, amesahau au kujisahauliza kilichomfika Sakina bint Al Imam Hussein baada kustashhadi kwa baba yake Al Imam Hussein na mateso ya familia yake kule Karbalaa, kwenye mitikisiko yote haya yamo mambo yanayotikisa akili na kutiribua nyoyo, basi uko katika hali gani moyo wa Sakina bint Hussein ?![41] Kadhalika .Al Asfahani ameleta tendo baya sana nako ni kule kupinga kwake kuwa ni kasida ya Firdaws ambayo kwenye kibwagizo chake inasema “Huyu ndiye anayejulikana na Buta’haa ” iliyosemwa kuhusiana na Zainil ‘Aabidina’Ali binil ‘Hussein (a.s) nae Daktari Waliidul ‘Adhwamy –Allah amlipe kheri –amekishughulikia vilivyo kwenye chake  cha aina yake “As Seful Yamaany” fii Na’hril .Al Asfahaniy Swa’hibul al Aghaaniy ” [42]Hivyo tunatahadharisha umma kutegemea kitabu cha “Al –Aghaaniy" kusoma historia ya Ahil Beit na Masahaba (ﷺ‬.a) na kipindi cha mwanzo miongoni mwa watu muhimu wa umma na tunatahadharisha juu ya yale yaliyotajwa ndani yake miongoni mwa fedheha na misiba aliyoiashiria Al Aadhamy kwenye “As Seful Yamaany”, ama yasiyokuwa hayo miongoni ya yale yaliyo na Fasihi, ya Mashairi yanayolingania watu kwenye tabia njema kujitenga na maovu na kuchunga heshima, na yale yasiyokuwa na madhara kutajwa kwake, hayo hakuna ubaya kufaidika nayo, kwani kitabu kinayo mashairi, na habari za kifasihi zilizo nyingi na kinachotoshelezeka kwa chenginecho.“Al ‘Aqdil Fariid cha Ibni ‘Abdi Rabbihi”: Hichi ni kitabu cha fasihi na hikaya za visa vigeni hakuna zaidi ya hayo, basi inakuwaje kwa mwenye akili mwenye kuzingatia kufanya mfano wa kitabu hichi kuwa ni kianzio cha msingi cha utafiti kwenye zama miongoni mwa zama muhimu za kihistoria ?!Muhakiki wa kitabu hichi anasema, "Kitabu ni chenye kuchanganywa usahihi wake na habari zisizokuwa na msingi, ni chenye kuondolewa isnadi na wasimulizi, na ametegemea vianzio ambavyo haijuzu kunukuu toka humo .”[43]  3-“Al Imaamah was Siyaasah" kilicho nasibishwa Na Ibni Qutaiba ( رحمه الله ):Nacho ni kitabu alichonasibishiwa kwa uongo hii imetokana na sababu kadha muhimu zao ni wale waliotowa historia ya Ibni Qutaiba kamwe hawakutaja au kumnasibishia kitabu chochote kile kwa jina la “Al Imaamah was Siyaasah” .Mtunzi anasimulia toka kwa Ibni Abi Laila kwa hali inayoonesha kukutana toka kwake, na Ibni Abi Laila huyu ni Muhammad bin Abdir Rahman bin Abi Laila Al Faqiih Qadhi wa Al-Kufah, aliyefariki mwaka (148H), Anaelewa kwamba Ibni Qutaiba hakuzaliwa isipokuwa mwaka (219H), yaani baada ya kifo cha Ibni Abi Laila kwa miaka sitini na tano !!.Anaeangalia kitabu ataona tokea mwanzo kwamba mtunzi wake alikuwa ameishi Damacus na Moroco (au nchi za Magharibi ya arabuni), wakati kinachojulikana ni kwamba Ibni Qutaiba kamwe hakutoka nje ya Baghdad ila kuelekea Daynuur.Na zaidi ya mmoja katika waandishi na watafiti wamefanya kazi ya kubainisha kwamba kitabu hichi amezuliwa nacho Ibni Qutaiba ; miongoni mwao :1-Daktari Thawrat Ukasha kwenye uhakiki wake wa kitabu “Al Maarif ” cha Ibn Qutayba na Daktari aliongoza “Wizara ya Elimu “ Misri katika miaka ya sitini .2-Muhammad al Iskandaary kwenye utangulizi wa kitabu “’Uyuunil Akhbaar” cha Ibn Qutayba.3-Mu’hibbud Diinul Khatiib kwenye utangulizi wa kitabu “Almaisaratu Qidaa’h “ cha Ibn Qutaiba.4- Daktari Muhammad Najm kwenye “Al Imaamah was Siyaasah,Al Mansuubtu Li Ibn Qutaiba Man huwa Mu-a-llifuhu ” Majallatul Ab’haath na vyenginevyo katika tafiti .5-Muruujudh Dhahab” cha Al Mas’uudy :Nacho ni kitabu kisichokuwa na Isnad kilichojaa khurafati, hikaya za kiajabu ajabu, amesema Sheikhul Islaam Ibni Taymiyyah –Allah amrehemu- "Na katika Taariikhul Mas’uudy umo uongo asioweza kuujuwa Ila Allah Taala, basi vipi atakuwa na imani na hikaya iliyo katika isnadi yake, kwenye kitabu kilicho mashuhuri kwa uzushi wake.Akasema Ibni Khulduun, "Katika vitabu Masuudy na Al-waaqidy ni katika vitiaji kasoro na kejeli ulio mashuhuri baina ya mahafidhi na wanaokubalika “[44]6-Sherhe Nahjul Balagha Abduhamiid bin Abil Hadiidil Muutazily:Nae ni dhaifu kwenye vipimo vya maulamaa wa Jerhe na Taadiil, bali mwenye kuzingatia sababu ya kutunga kwa Ibn Alhahihid kitabu chake hichi ataiona nafsi yake ni yenye kulazimika kwa kutilia shaka kitabu na mtunzi wake, kwani alikiandika kwa ajili ya Waziri Ibnil  ‘Al-aqam ambaye alikuwa ni sababu ya katika kuuawa kwa waislamu milioni moja katika Baghdaad kwenye mikono ya TataarAmesema Al Khansaary kuhusiana na kitabu hichi cha Ibn Alhahihid: “ Alikitunga kwa ajili ya hazina ya vitabu vya Alwazir Mu-ayyidudin Muhammad bin ‘Al-qamy “[45]Mpaka imefikilia kwamba watu wengi wamemponda mtunzi wa kitabu hichi na kitabu chake; amesema Al Mirza Habiibul Llahi Al khaiyyu akimuelezea Ibn Alhahihid “ Yeye sio mwenye kujuwa na athari na kwamba rai yake ni mbovu na nadhari yake ni yenye kuporomoka na kwamba yeye ni mwingi kuliko kiza na kwamba yeye amepoteza wengi na amepotea toka kwenye njia iliyo sawa”. Ama kuhusiana na kitabu chake; basi Mirza amekielezea kwa sifa kadha miongoni mwao :Ni kiwiliwili bila ya roho anazunguka kwenye ganda bila ya nyama, hakina faida nyingi ndani yake zimo taawili na tafsiri ngeni zenye kutetemesha maumbile, na kukimbiza masikio.[46]6-Kitabu “As Saqiifah” cha Salim bin Qais:Ni shakhsiyyah isiyoeleweka, na njia ya kufikilia kitabu chake ni dhaifu kwa wote, ndani ya kitabu chake muna upakaji matope kwa Aalil Beit mkubwa sana, ametaja baadhi ya riwaya za uzushi na za batili zenye kuporomosha hadhi Amiril Mu-u-minin Ali bin Abi Talib shujaa. -Kwamba yeye ni mwoga –Allah atulinde- wa kunyang’anywa haki yake. .-Kwamba yeye alimpandisha punda Fatma Zahraa (ﷺ‬.a ) ili avute huruma za Muhajiirina na Answar na wasimame pamoja nae kuvua Ukhalifa wa  Abi Bakr (ﷺ‬.a) . - Kwamba yeye aliificha Quran iliyo sahihi, na kuwaacha watu wategemee Quran iliyopungufu .- Kwamba yeye aliwaachia Masahaba wakimpiga mkewe bibi wa watu wa Peponi Fatamtiz Zahraa (ﷺ‬.a ) mbele ya macho yake bila ya kutaharaki akiwa ametulizana, na habari nyengine ambazo akili iliyo sahihi haizikubali wala kuziridhiwai, kama alivyobainisha hivyo zaidi ya mmoja kama mfano wa Aayatullah Muhammad Fadhlullahi aliyekana riwaya zinazosambazwa na wanaotaka kuhemua ghadhabu za watu, kuwafarikisha na kuwaweka mbali na ukweli wa mambo yenye kuwatenganisha, kama anavyofanya mwenye kunukuu toka kwenye kitabu cha Salim bin Qais na wenginewe, hivyo Aayatullahi Muhammad Fadhlullahi amechukizwa na kuenezwa mfano wa riwaya hizi batili ambazo zinataja kwamba Omar (ﷺ‬.a ) alivamia nyumba ya Ali (ﷺ‬.a) na kuvunja au kuunguza mlango wake, na kwamba alivunja ubavu wa Fatma Zahraa (ﷺ‬.a ) na kuidondosha mimba yake, na Fadhlullahi akabainisha kwamba jambo hili haliwezekani wala hakuna akili inayolikubali akibainisha kwamba mapenzi ya waislamu kwa Fatma Zahraa (ﷺ‬.a) ni makubwa yenye kuzuia watu kufanya mfano wa tendo baya kama hili.[47] Wengi wa wenye akili wametilia nguvu rai ya Fadhlullahi mfano Ustadh Ahmad al Khatib[48] Lakini harakati hizi za usahihishaji na zenye kutolea maelezo zimekabiliana na hujuma kali toka kwa baadhi ya wakereketwa mpaka kufikilia watu hawa kumkufurisha Fadhlullahi, na kutilia shaka kwenye imani, itikadi ikhlasi yake, yote haya ni kwa ajili ya kukana hadithi batili isiyosihi, na kwa anayetaka kuangalia fikira za Fadhlullahi na kutiwa kwake dosari kwa sababu ya kukana kwakwe jambo hili arejee kwenye kitabu “Fitinatu Fadhlillahi”cha Muhammad baaqir As Swaafy. Na kitabu Maasaatuz Zahraa” cha Ja’afar Al ‘Aalamiy, na kitabu “awzatul ‘Ilmiyyatu Tadiinul In’hiraaf” cha Muhammad Ali Haashimiy Al Mash-hadiy .Ama kitabu cha “As Saqiifah” ambacho kinataja mfano wa hikaya hizi batili ni chenye kutiliwa shaka mwanzo mpaka mwisho.Amesema Sheikh wa A’Twaaifatil Mufiid:” Hakika kitabu hichi hakikubaliki, wala haijuzu kufanyia kazi nyingi ya taarifa zake kwani, ndani yake mumepatikana uchanganyikaji uongo na hadaa-.” [49]Amesema Al Ghadhaairy:” kwenye tarajama ya Abaan bin Ayaassh" Ni dhaifu hazingatiwi na maulama wetu wanamnasibisha na kuzua kwake kitabu cha Salim bin Qais"”[50]Pia amesema Haashim  bin Ma’aruuf al ‘Husseiniy "Salim bin Qais ni mmoja wa wenye kutiliwa shaka na kutuhumiwa kusema uongo, na pamekuja kwenye kitabu kilichonasibishwa nae kwamba Muhammad bin Abi Bakr alimpa mawaidha baba yake wakati wa mauti yake pamoja na kwamba alikuwa mwenye umri miaka sitini “.[51]7- Kitabu “As Saqiifah” cha ‘Abdil ‘Azizil Jawhariy ;Ni kitabu kisicho na uzito wala kima kwa vigezo kadhaa:Kigezo cha Mwanzo :Kwamba mtunzi wake ni hajulikani wala uadilifu wake haijulikani kwenye vitabu vya jarhi wa Taadiil na Rijaal, wala hamna utakaso au ukubalikaji wowote ule isipokuwa vile alivyotaja Ibni Abi Al-hadiid kwenye sherhe yake juu ya Nahjul Balaagha kuhusiana na kumtakasa kwake, na tumetangulia kubainisha hali ya Ibni Abi Dunya mwenyewe, na kwamba yeye sio katika watu wa kujuwa na athari . Na kamwe utakaso wake hauhesabiwi kabisa!,amesema Al Khaw-iy, nae akiwa anapinga utakaso wa Ibni Abil Hadiid kwa Al Jawhariy” Mtu huyu utakaso wake haukuthibiti –akimaanisha al Jawhariy kwani utakaso wa Ibni Abil Hadiid hauzingatiwi [52]Na katika sababu zinatuzidishia uyakini kwamba Al Jawhariy hali yake haijulikani amefanya hivyo At Tuusiy kwenye “ Al Fihrasa ” pale alipomtaja Al Jawhariy, na kubainisha kwamba anacho kitabu cha  As Saqiifah. Na kwa kurejea kwenye utangulizi wa At Tuusisy wa kitabu chake “ Al Fihrasa ” tunamuona anasema :” Hivyo ninapomtaja kila mmoja wa watunzi na wenye vitabu asili basi lazima niashirie kwenye kilichosemwa kuhusiana nae yanayohusiana na Jerhe wa Taadiil, na jee anakubalika kwenye riwaya zake au laa?!”[53] Na At Tuusisy wakati wa kumtaja kwake Al Jawhariy hakutaja Jerhe wala Taadiil na hili ni miongoni mwa yanayojulisha kutokubalika kwake” [54]Kigezo cha Pili: Wakati wa kufungua kurasa za kitabu cha As Saqiifah tutaona kuwa muandishi analeta Munkaraat, katika riwaya na maneno ambayo hakuna aliyeyasimulia na kamwe hazikunukuliwa na yeyote yule asiyekuwa yeye, jambo lililotufanya tutilie shaka kuhusu kitabu na hasa mtunzi wake, na kwamba anazungumzia kuhusiana na awamu ya hatari na muhimu, haikubaliki kauli yoyote ile isipokuwa kwa hoja na dalili madhubuti za wazi na sanadi sahihi.Kigezo cha Tatu :Nyingi za isnadi a wasimulizi wa kitabu cha As Saqiifah ni dhaifu, na ndani yake wamo wasiojulikana na madhaifu anaowajuwa Allah -pekee- kwa mfano, Jawhary anasema "Ametuzungumzia Ahmad bin Ishaq bin Saleh toka kwa A’hmad bin Yasaar toka kwa Said al Answaary toka kwa wasimulizi wake”.Hivyo Ahmad bin Is’haaq ni yupi na sisi hatumuelewi!!, na ni nani hao wasimulizi wa Said, Allah ni Mjuzi zaidi ![55] 8-“ Taariikhul Ya’quuby:Huchukuwa vianzio vya riwaya kama ndio vianzio vikuu toka kwa Al Waaqidy na Abi Mi’naf Luutw bin Yahya, kitabu kinaelezea historia ya Ahalil Beit na Masahaba (ﷺ‬.a) kwa namna ya Mursal hamuna isnad, nae amezidisha kutaja ibara za udhaifu na unyonge, mfano imesemekana, imesimuliwa, na wamesimulia baadhi yao, na wamesema baadhi yao …”[56]Ya’quuby huyu anafanya kiburi na kuchupa mpaka na kuwa na kedi kuhusiana na kuwaita Abu Bakri na Omar na’Uthman kwa jina la Khalifah , wakati anamuelezea Ali kuwa ni wasii wa Muhammad (s.a.w), na huku ni ukandamizaji, na kedi kusikokubalika toka kwa alieshika kazi ya uandishi wa historia ya Ahil Beit na Masahaba (ﷺ‬.a).Mtu huyu anao msimamo wa kiadui dhidi ya Masahaba watukufu (ﷺ‬.a) maamuzi ya dhana iliyotangulia kabla ya kuandika kwake historia , sifa ambazo ni katika mambo yanayokosesha kuaminika .Kitabu cha Al Ya’quuby kimegawika kwenye sehemu mbili::Sehemu ya mwanzo :Ndani yake amekusanya maneno yasiyokuwa na kichwa wala miguu na khurafaat toka kwa umma zilizotangulia na mara nyingi hutolea dalili Injili na Tawrati juu ya habari za Manabii na kuwacha Quran isiyokuwa na shaka wala kutilika  wasiwasi , basi hili lizingatie.Ama sehemu ya Pili :  Humo anazungumzia kuhusu Sira ya Nabii (s.a.w) :na Makhalifa baada ya yeye kwa muhtasari wenye mapungufu na yenye kujaa riwaya zilizokatika na zisizokuwa na sanadi na za uongo.Kima cha kielimu cha kitabu hichi ni kidogo sana ;amesema Daktari Muhammad Swaamil As Sulamiy –akiwa anzungumzia “Taariikhul Ya’quuby" Hichi ni kitabu kinachowakilisha upotevu, na upakaji matope uliopatikana kwenye uandishi wa historia, nayo ni marejeo ya wengi wa mustashrikina na walioathirika na umagharibi baina ya wale waliotukana kwenye historia ya kiislamu na Sira za watu wake .[57] 9-“Faraaidus Samtwiin “  Kitabu cha al Hamwaity .Amesema Al ‘Hafidhul Adh Dhahaby kuhusiana na yeye :na kuhusiana nae na kitabu chake "Alikuwa muokota kuni usiku, amekusanya hadithi sisizo na mashiko bali ni za batili.”[58]10- “Al Mukhtswar fii Akhbaar Seyyidil Bashar “ Cha Abil Fadaa  Hichi ni kitabu kama kile kilichokitangulia, ndani yake muna hadithi zabatili na habari za kuzuwa kwa wingi . Hatima1-Umuhimu wa kutangulizwa wa mpango Quran na Sunna wakati wa kuzungumzia kuhusiana na Ahil Beit na Masahaba (ﷺ‬.a) na kipindi cha mwanzo cha kiislamu (ﷺ‬.a).2-Kutilia umuhimu wa kusihi kwa unukuuji na masimulizi kama ni msingi wa kisheria, haisihi kufanyia wepesi –uzembe – kwa hali yoyote ile. 3- Kubainisha vitabu muhimu ambavyo vinapasa kutegemewa wakati wa kupanga, kuandika na kusoma Historia ya kiislamu.4- Kutahadhari kutokana na hatari za kutegemea marejeo yasiyokuwa ya asili na yasiokubalika, jambo ambalo hupelekea kupata maalumati yasiyokuwa sahihi au yenye kupaka matope, ni sawa iwe ni kwa lengo la nia mbaya, au kutojuwa na kutochukua tahadhari .5- Mwisho :Inapasa juu ya muandishi na msomaji wa Tarekhe ya kiislamu kutojiachilia, akaandika hadithi au kutowa hukumu bila ya mpango, au kujitegemeza kwenye upande, msingi au kadhia, katika mambo ambayo huenda yakampelekea kuangukia kwenye kosa kubwa, na huenda utajaji wa hadithi ukawa mpungufu au wa upakaji matope, au hukumu huenda zikaja za kudhulumu, au zisizozakukiinaisha, au zisizokuwa na misingi na asili thabiti na sahihi, kitu ambacho kinapelekea kupoteza haki na kuzifuta.Na shukurani zote zimemthibitikia Allah, na sala na salamu zimshukie Nabii wetu Al amini na jamaa na Masahaba zake Al Ghurrul Mayaamiin..KIMEKAMILIKA KITABU KWA IDHINI YA ALLAH[1] Sababu hizi zimetajwa na Daktariri ‘Abdil ‘Aziz Khan Allah ampe salama kwenye kitabu chake المانع النافع –Matukio na Matukio ya Fitna zenye kuenea –uk. (73-74) na tumezidisha juu yake kutolea baadhi ya dalili muhimu na maalumati ya lazima.a[2] Tabary:ni Imam :Muhammadbin Jariir bin Yaziid Abu Jaa’far Tabary.Mfasiri ,Muha’haddith ,mwanahistoria ,na mwanazuoni wa Usuli Fiqhi na mwanafiqhi ,Imam mujtahid .Alizaliwa Aamaal ‘Tabaristaan mwaka (224) na kufariki (310H).Miongoni mwa tunzi zake ni (Tarekhe l Umam wal Muluuk)na Jaami’iBayaan fii Ta-awiilQur-aan).        [3] Tarekhe l Umam wal Muluuk.(52/1)        [4] Angalia Miizaan wal I’itidaal)(530/3-531).[5] Angalia kitabu :Marwiyyaat Abii Ma’hnif (Luutw’ bi nYa’yaa Abuu MakhnafAl Azdy ) Kwenye Tarekhe at Tw’wabary :zama za khilafti Raashidiah) (uk. ) cha Daktari Ya’hya bin Ibrahim Al Yahya (Chapa .1.Daarul ‘Aaswimah /Ar Riyaad1410 H.)[6] [7] Bihaarul Anwaar cha Al Majlisy (246/2)[8] (Jaamiur Ruwaat ) cha Muhammadil Ardiby Al Haairy (221/2) na (Kuliyyaat fii 'ilmir Rijaal ) cha Jaafar As Sabhaany (uk.26)[9] (Al Hadaaiqin Naadhira h) cha Yusuful Bahry(50/1) Bihaarul Anwaar  ccha Al mjlisy(250/2) [10] Angalia 9Aayatu tathiir cha 'Abdil Haadil Husseiny (uk. 20)[11] Sehemu ya Hadithi :aliyoismulia Muslim :Mlango wa fadhila za kukusanyika kwenye kisomo cha Qur-n ikatika Hadithi ya Abi Hureirah(ﷺ‬.a) nam. (2677)[12] Ameisimulia Hakim kwenye (mustadrak )( 120/2 ) na akasema (Swahihul Isnad) na Dhahaby akampinga kwenye (Talkhis ) .Na Muhaddith albany ameihukumu kwenye (As silsilati as Swahiha ) nam.(716 /nam 374)kuwa ni sahihi kutokana sanad zake na shahid .[13] Ameismulia At  Tirmidhy akasema (Hassanun  Swahihun  ) na (Ahmad ) (165/4), akadhoofishwa  pia na Muhadith Albaany . kwenye Silsialti Dhaiifah(446/2 nam .806 ).[14](Hakim kwenye Mustadrak) (325/3) (Swahihul Isnaad )   Ameismulia At  Tirmidhy[15] Imesimuliwa na Bayhaqy kwenye  (Sunanil Kubra) (101/7) kwa Sanad yake ni mpaka kwa shaaby toka kwa Nabii(s.a.w) kwa hiiyo.Na aksema:"Hii ni Mursal"[16] (Hakim kwenye Mustadrak) (196-209) na akasema (Swahihul Isnaad )  na akahukumui usahihi wake kwenye (Mukhtaararah ) Muhadith Albaany . kwenye (Swahiih Jaamii :3358 ) angalia Silsialt Swahiiha  (227/3 chini ya nam.1226) .[17] (Hakim kwenye Mustadrak) (312/3) na kusema (iko kwenye sharti la Muslim ) na kuafikiwa na Muhadith Albaany . kwenye (Silsialt Swahiiha) (226/3 chini ya nam.1226) . [18] Muttafaqun 'Alaihi [19] Angalia Aalil Bait wa (Hukuukuhum  Shariyyah ) cha Qadhi Swalih Darwiish (uk . 9-12 ).[20] (Manaaqib Amiiril Muuminiin (a.s) (116/2) na akaashiria hivi pia arbili kwenye Kashfil Ghummah na …. )[21] ()'Umdatu'uyuunSahhahil Akhbaar)cha Hully(6-7).[22]( Amaalit Tuusy ) uk. (191 ) na Bihaarul Anwaar cha Al Majlisy (288/22,44/287) [23] Swahihu muslim(Hadithi nam.2424)[24] Majmuu Fataawa )(487/4).[25] Akasema pia (ﷺ‬.a)[26] Imesimuliwa na Bukhary (3713) mlango wa sifa za Hassan na Hussein .[27] Angalia (As Sunanil Kubra) cha Bayhaqy 301/6,na (Bidaaya wan Nihaaya) cha Ibni Kathiir253/5.Akasema Ibni Kathiir :"Hii sanad yake ni sahihi ,yenye nguvu"[28]  Angalia Al Istiiaab cha Ibni 'Abdil Barri 387/4 na (Asmaal Matwaalib ) cha As Swalaaby 160.[29] (Muswannaf Ibni Abii Shaibah ) 567/14, na isnadi yake ni sahihi.[30] Tarekhe Dimashq cha Ibnl 'Asaakir 402/1 na Twabaqaat Ibn Saad  128/8.[31] Tarekheul Khulafaa cha as Suyuuty uk. 293.[32] Angalia Twabaqatil Kubraa  cha Ibni Saad 388/5[33] Siya'Umar cha Ibnil Jawzy 292.akiwa amenakili tokakwenye(Ad Dawlwtul Umawiyyah  cha Daktari As Swallaaby .)[34] "Al Bidaaya wa An Nihaaya " cha Ibni Kathiir 428/1[35] Sira ya Imama Ahmad cha Ibnil Jawzy. [36] " Hashia ya Al Bidaaya wa An Nihaaya " 284/11, na "Al 'Ibar fii Akhbaaril Ghubar " cha Ad Dhahaby 33/2[37] Angalia (As Siyari a'alaamin Nubalaa)  cha Adh Dhahaby 610/10[38] (As Siyari a'alaamin Nubalaa)  cha Adh Dhahaby 509 /18[39] Angalia Mpango wa uandishi wa historia ya Kiislamu  cha Muhammad Swamil as Salmy.[40] Watu muhuhimu[41] -“Al –Aghaan iy “wa A sSeiful Yamaaniy “ cha Mu hammadub ( رحمه الله )  [42] Toleo la “Daarul Wafaa -Misr” .Na angalia kwenye Tarjamati .Al Asfahaniilyowekwa pekee kwenye “Mu’jamil Mu-a-liffiin “ (234/2 chapa ya Ar  Risaalah) ,hapa tunaashiria kwenye darsa mbili kuhusiana na mtu huyu –isipokuwa  As Seiful Yamaaniy “ navyo ni vitabu viwili vya MuhammadA’hmad Khalaful Laahi  ,na Shafiiq Jabriy.[43] Angalia utangulizi wa uhakiki wa  “Al ‘Aqdil Fariid” (16/1) ,Maktabatu Ibni Taymiyyah , na pia angalia maneno ya Al ‘Allaama Muhammad Rashiidir Ridhaa kwenye Tafsiiril cManaar fiil Kitaab (85/5)  na Angalia pia : Kutubu ‘Haddhdh minhal ‘Ulamaa cha Mashhuur ‘Hassan Salmaan” ( 45/2 ) .[44] :  Taariikh Ibni Khulduun –Muqaddimah “(uk. 19)[45] “Rawdhwaatul Jannaat “ cha Alkhawansaary (20-21/5)[46] Angalia “Minhaaul Barraa’ah Sherhe Nahjul Balaagha “Mitrzaa H’biib  ullahil Al Khaw-i-y (14/1 chapa ya Daari I’hyaait Turaathil ‘Arabiy -Beruit ).[47] Angalia “Ummatu fii Rajuli Mu’hammad’Hussein Fadhlullahi “ cha MuhammadAl Jazaairy (uk. 219) [48] Angalia : Makala :” Fadhlullahi anaongoza Maspinduzi ya kitamaduni na anashuku ugaidi “ uk. 2/1/1999 M, naye Ustadh A’hmad il Kaatib anao utafiti muhimu wenye anwani “Ustwuura Madhluumiyyatuz Zahraa” nao ni utafiti makin iamezirekibisha habari zote na athari batili kuhusiana na jambo hili.[49] Tashiih ‘Aqiidatil Imaamiyyah”(uk.149/5 ) [50]“Ar Rijaal cha ibinl Ghadhwaairy uk.(119) (uk.119) tajamah ya Salim bin Qaisnam.193.[51] 2Al Madhuuaat fiil Athaar wal Akhbaar “Haashim Maaruuf al ‘Husseiny (uk.184) .[52] Muujamu”Rijaalil Hadiithcha Al Khau-i-y (142/2) .[53] Muqaddimatul Mufahrisa cha At Tuusisy (uk. 12)* Jerhe wa Taadiil :Sifa za kukubalika au ktokubalika kwa msimulizi .* Munkari ni Hadithi ambayo kwenye Isnadi yake yake yumo msimulizi mwenye makosa yaliyozidi  kipimo,sahau zake zimekuwa nyingi mno ,au madhambi yake makubwa  yamedhihiri [55] “Silsilati A’haadiith Dhwaiifah “ kwenye hHadithi 4972  Al Allaamatu Al Baaniy (رحمه االه )maeeleezea kwa kirefu hadithi hii.[56] Taariikhul Ya’quuby(168-171/ 2 ) .[57] Manhaj Kitaabatit Taariikhil Islaamy “(521)[58]  Ad Durarul Kaaminah (67-68).

التفاصيل