البحث

عبارات مقترحة:

السبوح

كلمة (سُبُّوح) في اللغة صيغة مبالغة على وزن (فُعُّول) من التسبيح،...

المجيب

كلمة (المجيب) في اللغة اسم فاعل من الفعل (أجاب يُجيب) وهو مأخوذ من...

الولي

كلمة (الولي) في اللغة صفة مشبهة على وزن (فعيل) من الفعل (وَلِيَ)،...

Maswali YaliyowaongozaVijana wa Kishia Kuingia Katika Haki

السواحلية - Kiswahili

المؤلف Sulaimani bin swalehe Alkharashiy
القسم كتب وأبحاث
النوع نصي
اللغة السواحلية - Kiswahili
المفردات الفرق المنتسبة للإسلام
Maswali YaliyowaongozaVijana wa Kishia Kuingia Katika Haki.

التفاصيل

Maswali Yaliyowaongoza Vijana wa Kishia Kuingia Katika Haki Utangulizi Hoja 1.     Aljaamiatu: 2.     Swahifa ya Annaamuusu (Ufunuo). 3.     Swahifa ya Al-ubaytwatu: 4.     Swahifa ya Dhuabatu Asseifu: 5.     Swahifa ya Ali: 6.     Aljifru: 7.     Msahafu wa Fatuma: 8.     Taurati, Injili na Zaburi: 9.     Katika maelezo haya kuna ushahidi wa yafuatayo: (1) – Mama wa Mahdiyi ni nani? (2) – Amezaliwa lini? (3) – Vipi ilivyobebwa mimba yake na mama yake? (5) – Alikua vipi? (6) – Anaishi wapi? (7) – Je, atarudi akiwa kijana au mzee? (8) – Ufalme wake utakuwa wa muda gani? (9) – Muda wa kughibu (kupotea) kwake ni muda gani?   Baada ya yote haya, ipo wapi taqiya ya Mashia?  Swali: Kabla ya Albaaqiru, Mashia walikuwa wanamwabudu Allah vipi?! Swali: Kwa nini hakupinga zile hadithi maudhui zilizomo ndani ya kitabu hicho?!   HITIMISHO  Maswali Yaliyowaongoza Vijana wa Kishia Kuingia Katika Haki UtanguliziSifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, aliyesema: {Na kwa hakika hii ndiyo Njia yangu Iliyonyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia yake…}. [Sura [6] Al-An‘aam 153]. Na Rehema na amani ziwe juu ya Mtume wake wa mwisho, aliyesema: "Kwa hakika Bani Israeli waligawanyika makundi sabini na moja, na umma wangu utagawanyika makundi sabini na tatu. Makundi yote yataingia motoni ispokuwa kundi moja." Akaulizwa: Ewe Mjumbe wa Allah, ni kundi gani hilo? Mtume (S.A.W.) akasema: Hilo ndilo kundi ambalo nimo mimi na Maswahaba zangu leo hii".([1])Ama baada ya haya:Kwa hakika Allah - kwa matakwa yake – ametaka Waislamu wagawanyike na kuwa makundi na madhehebu mbalimbali, wakifanyiana uadui na vitimbi wao kwa wao, kwa kufanya hivyo wanakhalifu amri ya Allah ya kurejesha tofauti zao katika kitabu cha Allah na Sunna za Mtume wake, Rehema na amani ziwe juu yake, pale Allah aliposema: {…Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.} [Sura [4] An-Nisa’59].          Na kwa sababu hii, imewajibika kwa kila mwenye kuunasihi umma wake, mpenda umoja na kuungana, ajitahidi kwa kadri ya uwezo wake kuunganisha umma "katika haki", na kuurejesha kama ulivyokuwa hapo zamani (kiitikadi, kisheria na kitabia), ili kufuata kauli ya Allah Mtukufu: {Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane…}. [Sura [3] Aal-‘Imran 103].          Miongoni mwa sababu muhimu zinazoharakisha jambo hili ni: Kuwapa mwangaza watu wa makundi yanayokhalifu wito wa Kitabu na Sunna, hasa katika yale wanayoyakosea, kuyakengeuka na kuwawekea kizuizi kati yao na uongofu wa kushikamana na jamaa ya Waislamu.          Na kutokana na hilo, imeibuka fikra ya kukusanya hoja na maswali haya yanayoelekezwa kwa vijana wa kundi la Shia Ithnasheria. Huenda yakachangia kuwarejesha katika haki wale wenye akili miongoni mwao, kama watazitafakari hoja na maswali haya, ambayo hayana upenyo wa kuyakwepa na kujitakasa nayo ila kwa kukubali wito wa kushikamana na Kitabu na Sunna visivyokuwa na kupingana. Kwa hakika yamenipendeza mno yale aliyoyafanya mmoja wa ndugu wa Kishia aliyeongoka na kuingia katika haki([2]) pale alipoeleza juu ya uzoefu alioupata kwa kuhama kutoka katika Upotevu kwenda katika uongofu, katika kitabu alichokichagulia jina mwafaka nalo ni: "Nimefaidika  na Maswahaba.. Wala sijahasirika na Aali Al-baiti"!          Kwa hakika amewafikishwa – Mola amthibitishe – katika uchaguzi huu. Kwa sababu Muislamu wa kweli haoni tabu kukusanya baina ya mapenzi ya Aali Al-baiti na Maswahaba – Mola awawie radhi wote.          Na huyu ndugu, kwa jambo lake hilo, ananikumbusha yule Mnasara aliyesilimu, na kutunga kitabu kwa anuani: "Nimefaidika Muhammad.. wala sijahasirika na Issa" Amani iwe juu yao.          Baada ya haya, napenda ijulikane kuwa mimi nimechagua aghlabu ya mswali na hoja hizi kutoka katika majukwaa ya wavuti – na hasa hasa jukwaa la kuihami Sunna. Kisha nikaongezea kiasi kikubwa cha hoja nilizozisoma katika vitabu vilivyozungumzia Mashia. Kisha nikazirekebisha na kuziweka pamoja kwa mtindo mmoja.  Nami sina lolote katika kazi hii zaidi ya kuikusanya na kuirekebisha, Huku namuomba Allah awanufaishe kwa kazi hii wale watakaoafikiwa miongoni mwa vijana wa Kishia, na aijalie iwe funguo ya heri kwao, na mwisho nawakumbusha kuwa: kurejea katika haki ni bora kuliko kung`ang`ania batili. Na kwa hakika mtu mmoja miongoni mwa Mashia akishikamana na Sunna, kuzifurahia na kuzinusuru, huenda akawazidi kimalipo na cheo maelfu ya Wasunni wanaofuata batili, wanaokengeuka na kuiacha dini yao, wanaopumbazika katika matamanio ya nafsi, au waliotumbukia katika shubuhati (utata wa kupoteza), Na Allah anasema: (Anayekufuru basi ukafiri wake utakuwa juu yake mwenyewe, na anayetenda mema, basi wanazitengezea nafsi zao). [Sura [30] Ar-Rum 44].Allah ndio mjuzi. Rehema na amani ziwe kwa Mtume wetu Muhammad, Aali zake na Maswahaba zake.Imeandikwa na / Abuu Musw-aabi  [email protected] Hoja1 – Mashia wanaitakidi kuwa Ali, Mungu amuwie radhi, ni Imamu maasumu (amekingwa hafanyi kosa), kisha tunamkuta – kwa kukiri kwao wenyewe Mashia – anamuozesha binti yake Ummu Kulthumi (dada wa Hassani na Huseini), kumuozesha Omari ibni Alkhatwaabi, Mungu amuwie radhi!!([3]) Na hili linawalazimisha Mashia moja ya mambo mawili na yote ni machungu:La kwanza: Ali, Mungu amuwie radhi, sio maasumu kwa sababu amemuozesha bintiye kwa kafiri!! Na jambo hili linapingana na msingi wa madhehebu yao, tena linapelekea kuwa Maimamu wengine nao sio maasumiina.La pili: Hakika Omari, Mungu amuwie radhi, ni Muislamu! Na Ali, Mungu amuwie radhi, amemridhia kuwa mkwe wake. Majibu mawili haya ni ya kutahayarisha.2 – Mashia wanadai kuwa Abuu Bakri na Omari, Mungu awawie radhi, walikuwa makafiri. Kisha tunakuta kuwa, Ali, Mungu amuwie radhi, naye ni Imamu maasumu kwa Mashia, ameridhia ukhalifa wao na kuwabaiyyi (kawavoti / kuwaunga mkono) mmoja baada ya mwingine wala hajajitoa katika kuwatii. Na hili linalazimisha kuwa Ali sio maasumu, kwa kuwa amewabaiyyi makafiri, waporaji na madhalimu, kwa kule kuwakubali. Na hili linaharibu umaasumi, pia ni kumsaidia dhalimu kutenda dhulma zake. Na hili katu, halitokei kwa maasumi au kitendo cha Ali ndicho kitakuwa sahihi!! Kuwa Omari na Abuu Bakri ni Makhalifa waumini wa kweli na waadilifu, kwa hiyo Mashia wanakuwa wameshamkhalifu Imamu wao katika kuwakufurisha, kuwatukaana, kuwalani Omari na Abuu Bakri na pia kutoridhia ukhalifa wao! Kwa hiyo tunatumbukia katika kutahayari: Imma tuchukue njia ya Baba Hassani, Mungu amuwie radhi, au tuchukue njia ya Mashia zake wanaoasi?!3 – Kwa  Ali, Mungu amuwie radhi, alioa wanawake kadhaa, baada ya kufariki Fatuma, Mungu amuwie radhi, Wanawake hao walimzalia watoto kadhaa, miongoni mwao ni: Abbasi bin Ali bin Abuu Twaalibu, Abdallah bin Ali bin Abuu Twaalibu, Jafari bin Ali bin Abuu Twaalibu, Athumani bin Ali bin Abuu Twaalibu. Mama yao ni: "Umm al-baniina binti Hizaami bin Daarimi".([4]) Pia, Ubaidillah bin Ali bin Abuu Twaalibu, Abuu Bakri bin Ali bin Abuu Twaalibu, Mama yao ni: "Layla bint Masoud Addaaramiyyatu".([5])Pia, Yahya bin Ali bin Abuu Twaalibu, Muhammad Al-Aswigharu bin Ali bin Abuu Twaalibu, Auni bin Ali bin Abuu Twaalibu. Mama yao ni: "Asmaa binti Umaysi".([6])Pia, Rukiya binti Ali bin Abuu Twaalibu, Omari bin Ali bin Abuu Twaalibu, ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka therathini na mitano. Mama yao ni: "Ummu HAbuubi binti RAbuuati".([7]) Pia, Ummu Hassani binti Ali bin Abuu Twaalibu, Ramlal Kubraa binti Ali bin Abuu Twaalibu, na Mama yao ni: "ummu Masoud binti Aruwati bin Masoud Atthaqaafiyyu".([8]) Swali: Je, Baba anaweza kumpa mtoto wake wa kumzaa jina la adui yake mkuu? Itakuwaje ikiwa baba mwenyewe ni Ali bin Abuu Twaalibu, Mungu amuwie radhi?Vipi Ali, Mungu amuwie radhi, awape watoto wake majina ya watu ambao mnadai kwamba walikuwa maadui zake?! Hivi mtu mwenye akili anaweza kuwapa wapenzi wake majina ya maadui zake?!Hivi mnajua kuwa Ali, Mungu amuwie radhi, ndiye Mkuraishi wa kwanza kuita majina ya Abuu Bakri, Omari na Athumani?4 – Mtunzi wa kitabu 'Nahju Albalaagha' nacho ni kitabu kinachotegemewa na Mashia, anasimulia kuwa: Ali, Mungu amuwie radhi, alisamehe ukhalifa na akasema: "Niacheni, na tafuteni mwingine"!([9]) Hili linajulisha kuwa madhehebu ya Shia ni batili. Vipi asamehe ukhalifa? Wakati kumsimikwa ukhalifa na Uimamu kwa Ali, Mungu amuwie radhi, ni amri iliyofaradhishwa na Allah nayo ni lazima – kwenu Mashia – ilipasa auchukue kutoka kwa Abuu Bakri?! 5 – Mashia wanadai kuwa Fatuma, Mungu amuwie radhi, ambaye ni kipande cha mwili wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, amedhalilishwa katika zama za Abuu Bakri, Mungu amuwie radhi, akavunjwa mbavu, amechomewa moto nyumba yake na kuavwa mimba yake ya mtoto ambaye walimuita Almuhsinu!Swali: Ali, Mungu amuwie radhi, alikuwa wapi, wakati yakitokea yote haya? Jambo hili linamtuhumu vibaya mno Ali kuwa ni mwanamume mwenye ushujaa mdogo mno (yaani mwoga). Kwa nini hakutetea haki ya Fatuma? Wakati Ali ni shujaa mwenye kuyakabili mapambano?!6 – Kwa hakika, tunakuta Maswahaba wengi wameoleana na Aali baiti Nabii, Rehema na amani ziwe juu yake, na hasa hasa Sheikhain (Abuu Bakri na Omari), Jambo hili limekubaliwa na wanahistoria na wanukuzi habari miongoni mwa Masunni au Mashia.  Kwa hakika Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake:-       Amemuoa Aisha binti Abuu Bakri, Mungu amuwie radhi.-       Amemuoa Hafsa binti Omari, Mungu amuwie radhi.-       Amewaozesha binti zake wawili (Rukiya kisha Ummukulthuumu) kwa khalifa wa tatu miongoni mwa makhalifa waongofu, ambaye ni mkarimu, mwenye haya, Athumani bin Afaani, Mungu amuwie radhi, na kwa ajili hiyo akapewa jina la Mwenye nuru mbili.-       Kisha mtoto wa Athumani ambaye ni Abaanu bin Athumani alimuoa Ummukulthuumu binti Abdullah bin Jafari bin Abuu Twaalibu.-       Na Marwani bin Abaani bin Athumani alimuoa Ummuqaasimu binti AlHassani bin AlHassani bin Ali bin Abuu Twaalibu.-       Kisha, Zaidi bin Amru bin Athuman alimuoa Sakina binti AlHuseini.-       Na Abdullah bin Amru bin Athumani bin Affaani alimuoa Fatuma binti AlHuseini bin Ali. Tunatosheka na kuwataja makhalifa watatu miongoni mwa Maswahaba, bila kuwataja Maswahaba wema wengine, ambao, vilevile, walioleana na Ahli albaiti, ili kubainisha kuwa: Kwa hakika Ahli albaiti walikuwa wanawapenda watu hao, ndio maana kukawepo huku kuoleana na kutangamana.([10])Pia tumekuta kuwa Ahli albaiti walikuwa wakiwaita watoto wao kwa majina ya Maswahaba wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake. Jambo hili limekubaliwa na wanahistoria na wanukuzi habari miongoni mwa Masunni au Mashia.Na huyu ni Ali, Mungu amuwie radhi, kama alivyoelezwa katika vyanzo vya Kishia, Anampa mmoja wa watoto wake kwa mkewe Layla binti Masoudi Alhandhaliyyatu, jina la Abuu Bakri, na Ali bin Abuu Twaalibu, Mungu amuwie radhi, ndio mtu wa mwanzo aliyempa mtoto wake jina la Abuu Bakri kati Ukoo wa banii Haashimu.[11] Vilevile Hassani bin Ali aliwapa watoto wake majina ya: Abuu Bakri, Abdulrahmani, Twalhatu na Ubeidillah.([12])Vilevile Hassani bin Hassani bin Ali.([13])Musa Alkaazim naye alimuita binti yake jina la Aisha.([14]) Pia kuna wale waliokuwa wakiitwa kwa jina la kupanga la Abuu Bakri wakati sio jina lao rasmi. Mfano wa hao ni Zaini Al-aabidiina bin Ali,([15]) na Ali bin Musa (Alrridhwaa).([16])Ama wale waliowapa watoto wao majina ya Omari Mungu, amuwie radhi. Miongoni mwao ni Ali, Mungu amuwie radhi, ambaye alimwita mtoto wake kwa jina la Omar Al-akbaru na mama wa mtoto ni Habiba binti RAbuuatu, Na kwa hakika huyu mtoto aliuliwa akiwa na nduguye Hassani, Mungu awawie radhi, katika Altwafu. Na mtoto mwingine ni Omari Al-asw-gharu, na mamaye ni Asswahbaau Attagh-libiiyyatu, Na huyu Omari wa pili aliishi na kuwarithi ndugu zake.([17])Vilevile Hassani bin Ali aliwapa watoto wake majina ya Abuu Bakri na Omari.([18])Vilevile Ali bin Hassani bin Ali.([19])Vilevile Ali bin Zaini Al-aabidiina.Vilevile Musa Alkaazim.Vilevile Hassani bin Zaini Al-aabidiina bin ALi.Vilevile, Is-haqa bin Hassani bin Huseini.Vilevile Hassani bin Ali bin Hassani bin Huseini bin Hassani.Na wenginewe wengi. Ila tunatosheka na kiasi hiki tu cha wale wa mwanzoni miongoni mwa Ahli baiti tukiogopea kurefusha mno.([20])Amma wale waliowaita mabinti zao kwa jina la Aisha ni: Musa Alkaazim,([21]) na Ali Alhaadi.([22]) Tunatosheka na Masheikh wawili Mungu awawie radhi pamoja na Aisha Mungu amuwie radhi.7 – Alkiliiniyyu katika kitabu Alkaafii, ametaja kuwa: "Kwa hakika Maimamu wanajua watakufa lini, na hawafi ila kwa hiari zao".([23]) Kisha Almajlisiyyu katika kitabu chake (Bihaaru Al-anuwaari) anataja hadithi isemayo: "Hakuna Imamu aliyekufa ila ameuliwa au amepewa sumu"([24]) Ikiwa Imamu anajua Ghaibu kama alivyosema Alkiliiniyyu na Alharri Al-aamiliyyi basi atakijua kile anacholetewa miongoni mwa vyakula na vinywaji na ikiwa kina sumu ataijua na kujiepusha nayo, na kama hajajiepusha nacho basi atakuwa amejiua, kwa kuwa anajua kuwa chakula kina sumu! Kwa hiyo anakuwa ni mwenye kujiua mwenyewe, huku Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, Maswahaba zake na watu wake ameeleza kuwa: Mwenye kujiua anaingia Motoni! Je, Mashia wanaridhia haya kwa Maimamu?!8 – Kwa hakika Hassani bin Ali, Mungu amuwie radhi, alimuachia na kumkabidhi Muaawiya, Mungu amuwie radhi, (ukhalifa), katika wakati ambao Maansari na Majeshi walikuwa wamejikusanya pamoja na Hassani jambo ambalo linamuwezesha Hassani kuendeleza vita. Na mkabala wa hilo nduguye ambaye ni Huseini Mungu amuwie radhi alitoka akiwa na watu wachache ili kupambana na Yazidi, wakati huo alikuwa anaweza kutulia na kusalimika.Mmoja wa wawili hao (Hassani au Huseini) haiepukani kuwa alikuwa katika haki, na mwingine katika batili, kwa kuwa, ikiwa kuacha kwa Hassani huku akiwa na uwezo wa kupambana (ndio haki) basi itakuwa kutoka kwa Huseini akiwa hana Silaha tena ana uwezo wa kufanya amani (ni batili). Na ikiwa kutoka kwa Huseini pamoja na udhaifu wake (ni haki) itakuwa kuacha Hassani pamoja na (nguvu zake) ni batili!  Na hili linawaweka Mashia katika wakati mgumu wasioutarajia, kwa kuwa kama wakisema: Wote wawili wapo katika haki, watakuwa wamekusanya vinyume viwiwli, na kauli hii inaangamiza misingi yao. Na kama watasema kuwa kitendo cha Hassani ni batili watalazimika waseme Uimamu wake nao ni batili, na kubatilika kwa Uimamu wake kunabatilisha Uimamu wa baba yake na umaasumu wake, kwa kuwa alimuusia. Na Imamu maasumu hausii ila kwa Imamu maasumu kama yeye kwa mujibu wa madhehebu yao. Na wakisema kuwa kitendo cha Huseini ni batili itawalazimu waseme ubatilifu wa Uimamu wake na umaasumu wake, na kubatilika kwa Uimamu wake na umaasumu wake kunabatilisha Uimamu na umaasumu wa kizazi chake chote, kwa kuwa yeye ndiye asili ya Uimamu wao na kwa njia yake umepitia Uimamu. Na ikibatilika asili yanabatilika yale yaliotokana na asili hiyo.(Baadhi ya Mashia wamejaribu kukwepa hoja hii kwa kutofautisha baina ya ukhalifa na uamiri! Yaani kule kuachia kulikuwa kwa ukhalifa na sio uamiri, na ukwepaji huu, unachekwa na wenye akili!) 9 – Alkiliiniyyu katika kitabu Alkaafii, ametaja kuwa: "Jamaa zetu wengi wametusimulia kutoka kwa Ahmadi bin Muhammad, kutoka kwa Abdillah bin Alhajjaali, kutoka kwa Ahmad bin Omari Alhalabiyyu, kutoka kwa Abuu Baswiiru amesema: Nimeingia kwa Abuu Abdillah (amani iwe juu yake) nikamwambia, niwe fidia yako, kwa hiyo nakuuliza maswali je, hapa kuna mtu anayesikia maneno yangu, akasema: Abuu Abdillah (amani iwe juu yake) alinyanyua pazia iliyoko baina yake na nyumba nyingine kisha akamtokea kisha akasema: Ewe Abaa Muhammad, uliza yale yaliyokudhihirikia. Akasema: Nikamuuliza: nimefanywa fidia yako…. Kisha akanyamaza kitambo kidogo, kisha akasema: Kwa hakika tuna Msahafu wa Fatuma (Mungu amuwie radhi) na nini kinawajulisha msahafu wa Fatuma (Mungu amuwie radhi) ni kitu gani? Akasema: nikamuuliza ni nini Msahafu wa Fatuma (Mungu amuwie radhi)? Akasema: huo ni msahafu ndani yake una Qur'an kama hii yenu kwa mara tatu, Wallahi yale yaliyo katika Qur'an yenu ni herufi moja, akasema: Nikamwambia: Wallahi hii ni elimu, akasema: Hakika hii ni elimu na Qur'an hiyo sio hii". Mwisho. Je, Mtume Rehema na amani ziwe juu yake, alikuwa unaujua msahafu wa Fatuma?! Ikiwa haujui, vipi Ahli beiti waujue na yeye haujui wakati yeye ndiye Mjumbe wa Allah?! Na ikiwa anaujua, kwa nini aliuficha umma?! Na Allah anasema: "Ewe Mtume! Fikisha uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake…." Sura [5] Al-Ma’idah 67.10 – Katika kitabu Alkaafii cha Alkiliiniyyu, juzuu ya kwanza, kuna majina ya watu waliosambaza hadithi za Mtume Rehema na amani ziwe juu yake, Aali zake na Maswahaba zake, kwa njia za Mashia, pia walitawanya kauli za Ahli Baiti. Miongoni mwa majina hayo ni haya yafuatayo:Mufadhalu bin Omari, Ahmadi bin Omari Alhalbiyyu, Omari bin Udaini, Omari bin abdilaziizi, Ibrahimu bin Omari, Omari bin Handhalatu, Musa bin Omari, Al-Abbaasi bin Omari na Kinachoyaunganisha majina haya ni jina Omari! Sawa sawa liwe jina la mpokezi au jina la baba yake. Kwa nini watu hawa waitwe Omari?!11 – Allah Mtukufu anasema: "Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanaosubiri, Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea. Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao Mlezi na rehema. Nao ndio wenye kuongoka. " Sura [2] Al-Baqarah 155 – 157".Na Allah Mtukufu anasema: "… na wanaovumilia katika shida na dhara na wakati wa vita…" Sura [2] Al-Baqarah 177.          Katika Nahju Albalaagha imetajwa kuwa: Ali Mungu amuwie radhi amesema, baada ya kufa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, nilikuwa namwambia Mtume Rehema na amani ziwe juu yake: Lau usingekataza kusikitika mno na ukaamrisha subira, tungemaliza maji ya machozi kwa ajili yako"([25])            Vilevile, ametaja: (Kwa hakika Ali, amani iwe juu yake, amesema: atakayepiga mkono wake katika paja lake wakati wa msiba, amali zake zimeshaporomoka.)([26])          Kwa hakika Huseini alimwambia dada yake ambaye ni Zainabu huko Karbalaa kama ilivyopokelewa na mwenye kitabu ((Muntahaa Al-aamaali)) kwa Kifarsi – Kiirani – na tafsiri yake kwa Kiarabu :([27])          ((Ewe dada yangu nakuapia kwa Allah, shikamana na kiapo hiki, nikiuawa usipasue mifuko ya nguo, kwa ajili yangu, wala usiparure uso wako kwa makucha yako, wala usiombee maangamizi na kuharibikiwa kwa ajili ya kufa kwangu kishahidi)).          Na Abuu Jafari amepokea toka kwa Amiri muuminiina (Ali), Amani iwe juu yake, amesema miongoni mwa yale aliyowafundisha Maswahaba zake: ((Msivae nyeusi kwani hayo ni mavazi ya Firauni)).([28])          Katika "Tafsiri Alswaafiyyu" kumekuja ufafanuzi wa aya: (wala hawatakuasi katika jambo jema), Sura [60] Al-Mumtahinah 12.) kuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake aliwabaiyi wanawake ya kuwa, wasivae nguo nyeusi, wala wasipasue maguo yao, wala wasiombe midua ya kujiangamiza.          Na katika kitabu "Furuu Alkaafii" cha Alkiliiniyyi" imetajwa kuwa: Kwa hakika Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, amemuhusia Fatuma, Allah amuwie radhi, kwa kumwambia: "Nikifa usijeruhi uso, wala usiziachie nywele (bila kuzichana nk) kwa ajili yangu, wala usiombe midua ya kujiangamiza, wala usinifanyie maombolezo".([29])          Na huyu ni Sheikhe wa Kishia, Muhammad bin Huseini bin Baabuuyah Alqummiyyu aliyepewa jina la Aswadduuqu na Mashia, anasema: "Miongoni mwa matamko ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, ambayo hayajapatapo kutanguliwa ni:           "Kulilia maiti ni miongoni mwa matendo ya zama za Jahiliya".([30])          Pia wanazuoni wao akiwemo Almajlisiyyu, Annuuriyyu na Alburuujurdiyyu  wamepokea kutoka kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake na Ahli zake, amesema: "Sauti mbili ni zenye kulaaniwa na kubughudhiwa na Allah; Kulia wakati wa msiba, na sauti wakati wa kuimba; yaani kulilia sana maiti na kuimba"([31])          Swali, baada ya riwaya zote hizi ni kwamba:          Kwa nini Mashia wanaenda kinyume na haki iliyokuja?! Tumsadikishe nani: Je, tumsadikishe Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake na Ahli Baiti wake au tumsadikishe Almalaaliyyu?!12 – Ikiwa tatwibiiru,([32]) yaani kulia sana na kujipiga vifuani, kuna malipo makubwa kama wanavyodai Mashia,([33]) Kwa nini Almalaaliyyu hafanyi tatwibiiru?13 – Ikiwa Mashia wanadai kuwa: Wale waliohudhuria GHADIRU KHAM ni maelfu ya Maswahaba ambao wote walisikia usia wa ukhalifa kwa Ali bin Abuu Twaalibu, Mungu amuwie radhi, baada ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake. Kwa nini hajatokea hata mmoja katika hao maelfu ya Maswahaba na kukasirika kwa ajili ya Ali bin Abuu Twaalibu. Hajajitokeza yoyote hata Amaaru bin Yaasir, Mikidad bin Amru wala Salmaan Alfaarisiyyu, Mungu awawie radhi, aje aseme: Ewe Abuu Bakri kwa nini unapora ukhalifa kutoka kwa Ali wakati wewe unajua yaliyosemwa na Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, siku ya GHADIRU KHAM?! 14 – Ali, Mungu amuwie radhi, kwa nini hakuongea lolote, pale Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, kabla ya kufa kwake, alipotaka kuwaandikia maandishi ambayo kamwe hawatapotea wakiwa na maandishi hayo baada ya kufa kwake? Huku Ali akiwa ni shujaa asiyeogopa ila Allah?! Pia anajua kuwa: Mtu anayenyamaza na kuacha kusema haki ni shetani bubu!! 15 – Je, Mashia hawasemi kuwa riwaya nyingi za Alkaafiyyu ni dhaifu?! Na kuwa wao hawana kitu sahihi ila Qur'an tu.Sasa, kwa nini baada ya yote haya,– kwa uongo na uzushi – Mashia wanadai kuwa: Tafsiri ya Qur'an kutoka kwa Mungu ipo katika kitabu ambacho riwaya zake nyingi ni dhaifu tena kwa kukiri kwao wenyewe?!  16 – Hakuna kuabudu ila kumwabudu Allah peke yake, Allah Mtukufu anasema: (Bali muabudu Mwenyezi Mungu tu….) Sura [39] Az-Zumar 66. Iweje Mashia wanajiita Abdul Huseini "mja wa Huseini", Abdul-Ali, Abudl-Azzahraa na Abdul-Imaam?! Kwa nini Maimamu hawajawaita watoto wao kwa majina ya Abdul-Ali na Abudl-Azzahraa? Je, inasihi maana ya Abdul Huseini iwe ni (mtumishi wa Huseini) baada ya Huseini Mungu amuwie radhi kufa shahidi? Je, inaingia akilini kuwa anapelekewa chakula, vinywaji na kumiminiwa maji ya udhu ndani ya kaburi lake!!! Ili kuwa mtumishi wake? 17 – Ikiwa Ali Mungu amuwie radhi anajua, kuwa yeye ndiye Khalifa aliyeandikwa na Allah. Kwa nini aliwabaiyyi Abuu Bakri, Omari na Athuman, Mungu awawie radhi?! Mkisema: Alikuwa hana uwezo. Basi, Asiye na uwezo hafai kuwa Khalifa, kwa kuwa ukhalifa haufai ila kwa mwenye kuweza mikiki mikiki yake. Na mkisema alikuwa anaweza lakini hakufanya, basi hii ni khiana (usaliti). Na msaliti hafai kuwa Imamu! Wala haaminiwi kuongoza raia. – Allah amemuepusha Ali na yote haya – je, jibu lenu ni nini ikiwa mna jawabu sahihi?18 – Ali Mungu amuwie radhi, alipotawalia ukhalifa hatujamuona akienda kinyume na makhalifa waongofu waliomtangulia, wala hajawaletea watu Qur'an kinyume na ile waliyokuwa nayo, wala hajakana kitu cha Swahabaa yoyote. Kinyume chake, tunakuta kauli yake iliyopokewa na wengi (mutawaatiru) akiwa katika membari: "Mtu mbora kabisa katika umma huu baada ya Nabii ni Abuu Bakri kisha Omari". Ali hukuweka sheria ya ndoa ya kuoa kwa muda (Mutaa), wala Fatuma arithi ardhi Fadaki, wala hajawajibisha watu wafanye mutaa katika Hija, wala hajaieneza kauli isemayo "Njooni katika amali bora" wakati wa adhana, wala hajafuta msemo "Swala ni bora kuliko usingizi".Abuu Bakri na Omari, Mungu awawie radhi, kama wangelikuwa ni makafiri, na wamempora Ali ukhalifa – kama mnavyodai – kwa nini Ali hakubainisha hayo, wakati utawala ulikua mikononi mwake?! Bali kinyume na hivyo, tunamkuta  amewasifu na kuwapongeza.          Mfungukiwe kama alivyofungukiwa Ali, au mlazimike kusema kuwa Ali ameufanyia khiana umma, kwa kuwa hajaubainishia jambo hilo. Allah amuepushe Ali na jambo hilo. 19 – Mashia wanadai kuwa makhalifa waongofu walikuwa makafiri, kama ni hivyo, vipi Allah aliwapa nguvu na kujaalia katika wakati wao kukombolewa miji kadhaa, na Uislamu ukawa una nguvu na kuhofisha, kwa kiasi ambacho hakuna Mwislamu aliyeona zama ambazo Allah ameupa nguvu Uislamu kuliko zama za makhalifa waongofu?          Je, hili linaafikiana na taratibu za Allah zilizohukumu kuwa Allah anawadhalilisha makafiri na wanafiki?!          Katika mkabala na hilo tumeona kuwa, katika zama za Huyo asiyekosea (Maasumu) na ambaye utawala wake umefanywa na Allah uwe rehema kwa watu – kama msemavyo – umma umefarikiana na kupigana vita, hadi maadui wakaingiwa na tamaa dhidi ya Uislamu na watu wake. Je, ni rehema gani iliyopatikana kwa umma kutokana na utawala wa Maasumu?! Ikiwa mna akili…?!          20 – Mashia wanadai kuwa: Kwa hakika Muawiya – Mungu amuwie radhi – alikuwa kafiri, kisha tunamkuta Hassani bin Ali, Mungu amuwie radhi, amemwachia ukhalifa – na huyo Hassani ni Imamu Maasumu – hapa inawalazimu wajue kuwa Hassani ameuacha ukhalifa kwa kafiri, na hili linapingana na Umaasumu wake, au inawalazimu wajue kuwa Muawiya ni Mwislamu!           21 – Je, Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake alisujudu juu ya udongo wa Huseiniyya? Udongo wanaousujudia Mashia?!           Wakisema ndio. Tunasema huu ni uongo! Tunaapa kwa Mola wa Kaaba.          Wakisema hajasujudu. Tunasema: kama ni hivyo, Je, nyinyi mmeongoka zaidi kuliko Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake?          Pia inafaa ijulikane kuwa riwaya zao zinataja kuwa Jibrilu alimjia Mtume na gao la mchanga wa Karbalaa.           22 – Mashia wanadai kuwa Maswahaba wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake waliritadi baada ya kufa kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, na wakamgeuka.          Swali: Je, Maswahaba wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, – kabla kifo chake – "walikuwa Mashia Ithnasheria", kisha baada ya kifo cha Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, wakabadilika na kuwa "Ahlu sunna"?          Au – kabla ya kifo cha Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, – walikuwa "Ahlu Sunna" kisha baada ya kifo cha Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, wakabadilika na kuwa "Mashia Ithnasheria"? kwa sababu neno kubadilika "inqilaabu" maana yake ni kuhama kutoka hali moja kwenda nyingine…?!          23 – Jambo linalojulikana ni kuwa Hassani, Mungu amuwie radhi ni mwana wa Ali, na mama yake ni Fatuma, Mungu awawie radhi, naye ni katika watu wa "Alkisaa" kwa Mashia,([34]) Naye ni miongoni mwa Maimamu Maasumiina, akiwa sawa sawa na nduguye Huseini Mungu, amuwie radhi, kwa nini Uimamu umekatika kwa upande wa watoto wake na ukaendelea katika upande wa Huseini?! Baba yao ni mmoja, mama yao ni mmoja, na wote wawili ni mabwana, na Hassani anamzidi Huseini katika jambo moja, nalo ni kuwa Hassani alikuwa Imamu kabla ya Huseini. Anamzidi Huseini kwa miaka pia Hassani ni mtoto wa kwanza kwa baba yake.          Je, kuna jibu la kukinaisha?24 – Kwa nini Ali bin Abuu Twaalibu – Mungu amuwie radhi – hajawasalisha watu hata sala moja katika siku za ugonjwa aliofariki nao Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, wakati yeye ndiye Imamu baada ya Mtume kama mnavyodai?! Kwa hakika Uimamu mdogo ni dalili ya Uimamu mkubwa.25 – Nyinyi mnasema: Kwa hakika sababu ya kupotea kwa Imamu wenu wa kumi na mbili katika njia ya chini ya ardhi (Sirdabu) ni kuhofia dhuluma, sasa kwa nini huku kupotea kuliendelea ingawa hatari ya kuhofia hiyo dhuluma ilitoweka kwa kusimikwa baadhi ya nchi za Kishia katika historia, kama Al-Abdiyiin, Albuuyihiin, Alswafuuyiin na la mwisho ni dola la Irani la sasa?! Kwa nini hatokei sasa hivi? Na hali ya kuwa Mashia wanaweza kumnusuru na kumlinda katika dola yao?! Na idadi yao ni mamilioni, na wao wanamfidia kwa kujitolea roho zao asubuhi na jioni…!!26 – Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, aliongozana na Abuu Bakri Siddiiqi katika hijira yake na hivyo ni kumbakisha awe hai. Na mkabala wa hilo alimuweka Ali bin Abuu Twaalibu, Mungu amuwie radhi, katika mazingira ya kifo na kuangamia katika kitanda chake… Ingekuwa Ali ndio Imamu aliyeusiwa na ni khalifa aliyesimikwa, je, kwa nini awekwe katika kuangamizwa na kubakishwa Abuu Bakri wakati hata kama angekufa kusingekuwa na madhara kwa Imamu wala msururu wa Uimamu kwa kufa kwake… Na hapa linaibuka swali: Nani afadhali abakie hai, asichomwe na mwiba, wala asiwekwe katika kitanda cha umauti na kuangamia…?Mkisema kuwa Ali anajua ghaibu, sasa kuna ubora gani alale hapo?!27 – Kwa hakika taqiya (mtu kudhihirisha kinyume na yale anayoyaficha) hakutokei ila kwa sababu ya hofu. Na hofu zipo aina mbili: Mosi: Hofu ya kuiogopea kuiogopea nafsi (kufa).Pili: Hofu ya matatizo, maumivu ya mwilini, matusi, shutuma na kuvunjiwa heshima.Ama hofu ya kuiogopea nafsi, haipo kwa Maimamu kwa njia mbili: Mosi: Kwa hakika kawida ya kifo kwa Maimamu wa Ithnasheria kinakuwa kwa hiari zao – kama mnavodai.Pili: Maimamu wanajua yalikuwepo na yatakayokuwepo, wanajua kifo chao kitakuwa vipi na lini kwa kujipangia – kama mnavyodai.Kwa hiyo kabla ya wakati wa kifo kamwe hawataogopea nafsi zao, wala hawana haja ya kufanya unafiki katika dini yao na kuwaghururisha Waumini wa kawaida.Ama kipande cha pili cha hofu, nacho ni hofu ya matatizo, maumivu ya mwilini, matusi, shutuma na kuvunjiwa heshima. Hakuna shaka kuwa kuvumilia na mambo haya na kuyasubiria ni kazi ya wanazuoni, na Ahli baiti wa Nabii ni bora kutendo haya.Sasa kwa nini kuwe na taqiya?28 – Kwa hakika imepasa kumsimika Imamu maasumu – kwa Mashia – kwa lengo la kuondosha dhulma na shari kwa miji na vijiji vyote, na kuweka uadilifu na usawa.Swali: Hivi mnasema kuwa kila mji na kijiji kilichoumbwa na Allah Mtukufu kina Imamu maasumu anayezuia dhulma dhidi ya watu? au hakuna?!Mkisema kuwa: kuna maasumu.Mtaambiwa: Huku ni kukuza mambo kuliko wazi kabisa, Je, katika miji ya kikafiri miongoni mwa washirikina na Ahli Kitabu yupo maasumu? Je, huko Shamu katika zama za Muawiya, Mungu amuwie radhi, kulikuwepo na Maasumu?Na mkisema: lakini sisi tunasema huyo ni mtu mmoja, na ana manaibu katika kila mji na kijiji. Mtaambiwa: Je, ana manaibu katika miji yote ardhini au katika baadhi ya miji tu?  Mkisema: katika miji na vijiji vyote duniani.Mtaambiwa: Huku ni kukuza mambo kama vile mwanzo!Mkisema: Yeye ana manaibu katika baadhi ya miji na vijiji. Mtaambiwa: miji na vijiji vyote vina shida moja ya kutaka maasumi. Sasa kwa nini mtofautishe?!29 – Alkiliiniyyu ameweka mlango maalumu katika kitabu Alkaafii wenye anuani (Kwa hakika wanawake hawarithi maekari ‘mali zisizohamishika’), akiwa amepokea kauli kutoka kwa Abuu Jafari isemayo: “Wanawake hawarithi ardhi yoyote wala mali zisizohamishika.([35])Naye Twuusiyyu amepokea katika Attahadhiibi ([36]) kutoka kwa Maysiri kauli isemayo: “Nilimuuliza Abuu Abdallah, amani iwe juu yake, kuhusu wanawake wana nini katika mirathi? Akasema: Wanawake wanapata thamani ya matofali, jengo, mbao na pau. Ama ardhi na mali zisizohamishika hawarithi” Na kutoka kwa Muhammad bin Muslim, kutoka kwa Abuu Jafari, Amani iwe juu yake, amesema: “Wanawake hawarithi ardhi yoyote wala mali zisizohamishika.” Na kutoka kwa Abdil Maliki bin A-ayuni, kutoka kwa mmoja wa wawili hao Amani iwe juu yao, amesema: “Wanawake hawapati nyumba wala mali isiyohamishika”. Katika riwaya hizi hakuna kuhusisha wa kuwepa pingamizi si kwa Fatuma, Mungu amuwie radhi, wala mwinginewe. Kwa kuzingatia haya, Fatuma, Mungu amuwie radhi, hana haki ya kuomba mirathi ya kumrithi Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, (kwa mujibu wa riwaya za madhehebu ya Kishia). Vilevile, kila kilichokuwa cha Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, ni cha Imamu. Kutoka kwa Muhammad bin Yahya, kutoka kwa Ahmadi bin Muhammad ameinyanyua, kutoka kwa Amru bin Shamaru, kutoka kwa Jaabiri, kutoka kwa Abuu Jafari, amani iwe juu yake, amesema: Mtume wa Allah, Rehema na amani ziwe juu yake, amesema: “Mungu amemuumba Adamu na akamkatia kipande cha ardhi, kile kipande kilichokuwa cha Adamu, amani iwe juu yake,  ni cha Mtume wa Allah, Rehema na amani ziwe juu yake, na kile kilichokuwa cha Mtume wa Allah, hicho ni cha Maimamu miongoni mwa Ahli Muhammad”([37]). Na Imamu wa kwanza baada ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, kwa mujibu wa itikadi za Kishia ni Ali, Mungu amuwie radhi, na kwa hiyo, mwenye haki ya kuidai ardhi ya Fadaki ni Ali, Mungu amuwie radhi, sio Fatuma, Mungu amuwie radhi, na hatujamuona Ali akifanya jambo hilo, lakini amesema: “Lau ningetaka ningeelekea katika njia ya kwenda katika asali safi, punje nzuri za ngano, na nyuzi za hariri, lakini huko ni mbali mno. Matamanio ya nafsi yangu na uroho kuniongoza kwenye kupendelea vyakula. Huenda huko Hijazi na Yamaamatu hakuna mtu asiye na tamaa ya vipande vya mikate, wala asiyewahi kushiba. (kama Ali)”([38]) 30 – Kwa nini Abuu Bakri, Mungu amuwie radhi, aliwapigavita walioritadi, na kusema: Lau wangeninyima kamba ya kufungia mnyama waliyokuwa wakiitoa kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, ningewapigavita kwa sababu ya kamba hiyo, na huku Mashia wanasema kuwa Ali, Mungu amuwie radhi, hakuutoa Msahafu aliouandika kutoka kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, kwa kuogopea watu wasiritadi!! Wakati yeye ndiye khalifa, akiwa na sifa na kuungwa mkono na Mungu, kama wanavyodai Mashia, pamoja na haya, anapinga kuutoa Msahafu kwa kuogopea watu wasiritadi, na anaridhia kuwaacha watu katika upotevu, huku Abuu Bakri anawapiga vita walioritadi kwa ukamba wa kufungia ngamia!!31 – Kwa hakika wamekubaliana Ahlu sunna waljamaa na makundi yote ya Mashia, kuwa Ali bin Abuu Twaalibu, Mungu amuwie radhi, ni shujaa asiye na dosari, na kwa hakika haogopi kwa ajili ya Allah lawama ya mwenye kulaumu. Na ushujaa huu haukukatika hata mara moja tangu kuanza maisha yake hadi alipouliwa na Ibnu Maljamu. Na Mashia, kama inavyojulikana, wanatangaza kuwa, kwa hakika Ali bin Abuu Twaalibu ni Aliyehusiwa awe khalifa baada ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, bila kutenganisha.Je, ushujaa wa Ali, Mungu amuwie radhi, baada ya kufa kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, ulikuwa wapi hadi ikafikia kumpa baiyyi Abuu Bakr Swiddiiq, Mungu amuwie radhi?! Kisha baadaye moja kwa moja akambaiyyi Alfarouku Omari bin Alkhatwaabu, Mungu amuwie radhi?! Kisha akambaiyyi Dhuu nuurayin Othumani bin Al-Affaan, Mungu amuwie radhi?!Je, – Mungu amuepushilie mbali jambo hili – Ali, Mungu amuwie radhi, alishindwa kupanda membari ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, walau mara moja tu katika kipindi cha ukhalifa wa mmoja kati ya watatu hao, na kutangaza huku akiashiria kuwa ameporwa ukhalifa?! Na kuwa yeye ndiye mwenye haki ya ukhalifa kwa kuwa yeye ndiye Waswiyyu?!Kwa nini hakufanya jambo hilo na kudai haki yake, na yeye, wamjua ni nani? Ni shujaa wa mstari wa mbele?! Huku akiwa na watu wa kumkinga wanaompenda.32 – Hadithi ya guo jeusi iliwajumuisha watu wane miongoni mwa nyumba ya Ali, Mungu amuwie radhi, kuwa walitwaharishwa.([39]) Sasa, kuna ushahidi gani wa kuwaingiza watu wengine wasiokuwa hao katika kutwaharishwa?!33 – Mashia wanapokea kutoka kwa Imamu Jafari Asswaadiq – mwanzilishi wa madhehebu ya Jafariyyu kwa mujibu wa itikadi zao – kauli yake ya kujifaharisha: (Abuu Bakri amenizaa mara mbili)([40]) kwa sababu nasabu yake inaishia kwa Abuu Bakri kwa njia mbili:Mosi: Kwa njia ya mama yake, Fatuma binti Qasimu bin Abuu Bakri.Pili: Kwa njia ya bibi yake kwa mama ambaye ni Asmaa bin Abdilrahmani bin Abuu Bakri, bibi ambaye ni mama wa Fatuma binti Qasimu bin Abuu Bakri.Kisha tunawakuta Mashia wanapokea kutoka kwa Asswaadiq riwaya za uongo zinazomshtumu babu yake ambaye ni Abuu Bakri, Mungu amuwie radhi! Swali: Vipi Asswaadiq ajifaharishe na babu yake kwa upande mmoja kisha anamtuhumu kwa upande mwingine?! Kwa hakika maneno haya huenda yanatoka kwa watu wa masokoni (wasema ovyo) walio wajinga, lakini hayawezi kutoka kwa Imamu anayezingatiwa na Mashia kuwa ni mwanachuoni mkuu na mchamungu kuliko marafiki na watu wa zama zake. Na hajalazimishwa na yoyote amsifu au amkosoe. 34 – Msikiti wa Aqswaa ulikombolewa katika zama za Omari, Mungu amuwie radhi, kisha katika zama za Kiongozi wa Kisunna, ambaye ni Swalahudini Al-Ayuubiyyu, Mungu amrehemu.Mafanikio ya Mashia yapo wapi katika kipindi chote cha historia? Je, wameshakomboa japo shibri ya ardhi au wamewafanya maadui wajisalimishe na kusilimu?!35 – Mashia wanadai kuwa Omari, Mungu amuwie radhi, anambughudhi Ali, Mungu amuwie radhi – kisha tunamkuta Omari anampa Ali uwalii wa Madina pale Omari alipotoka kwenda kupokea funguo za Baiti Maqdisi?! Huku ikijulikana kuwa, Ali, Mungu amuwie radhi, atakuwa khalifa wa Waislamu endapo Omari, Mungu amuwie radhi, atatokezewa na tatizo baya! Bughudha iko wapi?!36 – Mashia wanadai kuwa Mahdiyyu wao pindi atakapodhihiri, atatawala kwa mtindo wa utawala wa watu wa Daudi! Haulizi ushahidi. Ikowapi sheria ya Muhammad, Rehema na amani ziwe juu yake, iliyofuta sheria zilizotangulia, na ambayo imeandika ulazima wa kudhihirisha Ushahidi wakati wa kuhukumiana?!37 – Kwa nini Mahdiyyu wa Kishia akitokea atasuluhishana na Mayahudi na Manasara na kuwapiga vita Warabu na Makureishi?! Je, Muhammad, Rehema na amani ziwe juu yake, si miongoni mwa Makureishi na Warabu? Vilevile Maimamu wa Kishia – kwa mujibu wa kauli zenu?38 – Mashia wanaitakidi kuwa Maimamu zao wanabebwa mimba ubavuni mwa mama zao, na wanazaliwa kutoka katika paja la kulia!!([41]) Je, Muhammad sio mbora wa Manabii wote na mbora wa watu wote? Mbona yeye amebebwa mimba katika tumbo la mama yake na ametoka katika fuko la uzazi la mama yake?!  39 – Mashia wanapokea kutoka kwa Abuu Abdallah – Jafari Asswaadiqi – ya kuwa amesema: “Mwenye jambo hili ni mtu ambaye jina lake haitwi mtu mwingine ispokuwa kafiri…”([42])Mashia wanapokea kutoka kwa Muhammad Hassani Al-Askariyyu kuwa amemwambia Ummu Almahdiyyu: "Utashika mimba ya mwana wa kiume jina lake Muhammad naye ndiye atakayesimamia baada yangu…"([43])Je, huku sio kupingana?! Mara mnasema: Atakayemwita kwa jina lake basi huyo ni kafiri, mara mnasema kuwa Hassani Al-askariyyu alimwita Muhammad! 40 – Alkiliniyyu amepokea katika kitabu Alkaafii, kutoka kwa Ahmadi bin Muhammad, hadithi aliyoinyanyua hadi kwa Abuu Abdallah, amani iwe juu yake, amesema: "Weusi unachukiwa ila katika mambo matatu nayo ni: Khofu, kilemba na shuka la Alkisai"([44]) Na vilevile, kutoka kwake, katika kitabu Azziyyu, hadithi iliyonyanyuliwa hadi kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, amesema:  Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake na Ahli zake, alikuwa anachukia weusi ispokuwa katika viyu vitatu: khofu, guo la Kisau na kilemba".([45])Na Huru Al-aamiliyyu amepokea katika wasaili yake, kutoka kwa Swaduuqi, kutoka kwa Muhammad bin Selemani, hadithi Mursalu, kutoka kwa Abuu Abdallah, Amani iwe juu yake, amesema: Nilimwambia: "Je, nisali na kofia nyeusi? Akasema: Hapana, usisali nayo kwa sababu kofia nyeusi ni vazi la watu wa motoni"([46]) Pia imepokea kutoka kwa Swaduuqi katika kitabu cha Alfaqiihu, kutoka kwa Amiri Muuminiina, ikiwa ni hadithi Mursalu, pia katika Al-ilalu Walkhiswaalu kama ilivyo katika Alwasaailu, kutoka kwake,   Amani iwe juu yake, ikiwa ni Musnadu, ya kuwa amewaambia Maswahaba zake: Msivae kitu cheusi kwani kitu cheusi ni nguo ya Firauni. Pia amepokea kwa Isnadi yake kama ilivyo katika Alwasaailu kutoka kwa Hudhaifa bin Mansuri amesema: Nilikuwa kwa Abuu Abdallah, Amani iwe juu yake, katika Alhiirat na akajiwa na mjumbe wa Abuu Abasi Khalifa akimwita, akaomba mimtwara, na mimtwara ni nguo ya sufu inavaliwa wakati wa mvua ili kujikinga na mvua kama ilivyoelezwa katika (kamusi ya Lisani).([47])Pia zimekuja habari kutoka kwao zinazobainisha kua nguo nyeusi ni vazi la bani Abasi ambao ni maadui zao: Kama ilivyopokewa kutoka kwa Swaduuqi katika kitabu cha Alfaqiihu, ikiwa ni hadithi Mursalu, amesema: imepokewa kuwa Jibrilu, Amani iwe juu yake, alimjia Mtume wa Allah, Rehema na amani ziwe juu yake na Aali zake, akiwa na nguo aina Qubaa nyeusi (nguo ya kujitandia) na mshipi ukiwa na jambia, Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake na Ahli zake, akasema: Ewe Jibrilu ni vazi gani hili? Akasema: Vazi la mtoto wa ami yako Abasi. Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake na Ahli zake, akatoka kumwendea Abasi na kumwmabia: Ewe ami yangu, ole wake mwanangu kutokana na mwanao. Akasema: Ewe Mjumbe wa Allah, Je, niikate nafsi yangu? Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake na Aali zake, akasema: Kalamu imeshapita na yale iliyokuwa nayo. Ni dhahiri hapa kuwa: makusudio ya watu wa motoni katika baadhi ya habari zilizopita hao ni wale wanaoadhibiwa na moto huo, watakaokaa humo milele siku ya kiama, nao ni Firauni na yeyote atakayeenenda mwenendo wa Firauni na kumfanya ndiye kigezo chake miongoni mwa makundi yanayochupa mipaka, wakandamizaji miongoni mwa wale wanaofanana na Makhalifa wa Abasia na wengineo miongoni mwa makafiri wa umma huu, umma uliorehemewa, na nyumati zilizotangulia, zilizojitwalia nguo nyeusi kuwa ndio mavazi yao.([48])Na miongoni mwa maelezo hayo ni yale aliyoyapokea Swaduuqi katika Alfaqiihu kwa isinadi yake kutoka kwa Ismaili bin Muslim, kutoka kwa Asswaadiqu, Amani iwe juu yake, amesema: Allah amemfunulia Nabii miongoni mwa Manabii wake, Amani iwe juu yao: "Waambie Waumini wasivae nguo za maadui zangu wala wasile katika vyakula vya maadui zangu wala wasienende mienendo ya maadui zangu, (vinginevyo) watakuwa maadui kama walivyo maadui zangu.([49])  Katika kitabu Uyuunu Al-akhbaari Alaa Maa Fii Alhadaaiqi, baada ya kunukuu hiyo habari kwa isinadi nyingine kutoka kwa Ali bin Abuu Twaalibu, Amani iwe juu yake, kutoka kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake na Aali zake, kwa kunukuu kutoka kwa mtunzi, Mungu amuwie radhi: Kwa hakika nguo za madui ni nyeusi, na vyakula vya maadui ni mvinyo, vileo, mapovu, udongo, na kukimbilia samaki, ng`ombe pori, mbegu za mzumayru, na twaafiyyu, na kila kisicho na magamba miongoni mwa samaki, sungura... hadi aliposema: Na mienendo ya maadui ni mambo za kutuhumiwa, vikao vya kunywa pombe, vikao vya starehe, vikao vya kudharau waumini na Maimamu, amani iwe juu yao, vikao vya watu wenye maasi, dhulma na ufisadi. Imeisha kwa muhtasari.([50]) Na baada ya habari zote hizi ambazo ni nyingi, zinazojulisha shutuma ya Maimamu dhidi ya nguo nyeusi, na kuwa hayo ni mavazi ya maadui wa Kishia: Sasa kwa nini Mashia wanavaa nguo nyeusi na kuzitukuza? Na kuzijaalia ndio mavazi rasmi ya Wakuu wao…?!41 - Mtu Kama anataka kuwa Mshia, afuate madhehebu gani? Miongoni mwa jumla ya madhehebu ya kishia ambayo ni mengi?! Miongoni mwayo ni: Imamia, Ismailiya, Naswiiriya, Zaidiya, Duruzi, nk. Na yote yanadai kuwa yananasaba na Ahli baiti, na yanakiri Uimamu, na yanawafanyia uadui Maswahaba?! Na Yote yanaitakidi Uimamu wa Ali bin Abuu twalibi, Mungu amuwie radhi. Uimamu ni nguzo na Ali ni khalifa bila kipambanuzi, na asili ya dini ipo pamoja nao wao…..!!42 – Je, kumeteremshwa vitabu vingine kwenda kwa Mtume wa Allah, Rehema na amani ziwe juu yake, visivyokuwa Qur'an na kuhusishwa vitabu hivyo na Ali, Mungu amuwie radhi?!Mkisema: Hapana, mnajibu nini kwa Riwaya zenu zifuatazo: 1.     Aljaamiatu: Kutoka kwa Abuu Baswiiru, kutoka kwa, Abuu Abdallah amesema: Mimi ni Muhammadi, na kwa hakika sisi tuna Aljaamiatu, na nini kinawajulisha wao ni nini Aljaamiatu?Akasema: nikamwambia: nijaaliwe fidia yako Al-Jaamiatu ni nini?Akasema: ni swahifa (kitabu) urefu wake ni dheraa sabini kwa dheraa za Mtume wa Allah, Rehema na amani ziwe juu yake, na Mtume ameijaza kwa vipande vya mbao, na akapiga mstari upande wa kulia yake, na ndani ya kurasa hizo kuna kila la halali na haramu, na kila wanachokihitajia watu, mpaka mpasuko katika mchuno…hadi mwisho.([51])Zingatia: "na ndani ya kurasa hizo kuna kila wanachokihitajia watu".Kwa nini kimefichwa? Na tukanyimwa hicho kitabu na yaliyokuwemo?!Kisha, Je, huku sio kuficha elimu?! 2.     Swahifa ya Annaamuusu (Ufunuo).kutoka kwa Ridhwaa, Mungu amuwie radhi, katika hadithi ya alama za Imamu, amesema:"Na atakuwa na swahifa, na ndani yake kuna majina ya Mashia zao (wafuasi zao) hadi siku ya Kiama, na sahifa nyingine, ndani yake kuna majina ya maadui zao hadi siku ya Kiama".([52]) Tunasema: Ni Swahifa gani hizi, amabazo zinakusanya majina ya Mashia hadi siku ya Kiama?!Kwa mfano, lau yangesajiliwa majina ya Mashia wa Iran wa sasa tu, hilo lingehitaji, kwa uchache mijaladi mia moja!! 3.     Swahifa ya Al-ubaytwatu:Kutoka kwa Amiri Muuminiina, Mungu amuwie radhi, amesema: Naapa kwa Allah, kwa hakika nina swahifa (vitabu) nyingi, miongoni mwa mambo ya heri aliotuachia Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake na Aali zake, na Ahli baiti zake. Na kwa hakika ndani yake kuna swahifa iitwayo Al-ubaytwatu, na yaliyokuja ndani yake kuhusiana na Warabu ni makali mno, miongoni mwa hayo ni: Kwa hakika katika swahifa hizo kuna makabila ya kiarabu ya hovyo yapatayo sitini, hayana fungu lolote katika dini ya Allah.([53])          Tunasema: Kwa hakika riwaya hizi, hazikubaliki wala hazingii akilini, ikiwa idadi hii ya makabila haina fungu katika dini ya Allah, maana yake ni kuwa, hakuna Mwislamu hata mmoja mwenye fungu katika dini ya Allah!           Kisha tazameni: Kuyahusisha makabila ya Kiarabu na hukumu hii iliyokali mno na ambayo ina harufu ya ubaguzi wa utaifa.    4.     Swahifa ya Dhuabatu Asseifu:Kutoka kwa Abuu Baswiiri, kutoka kwa Abuu Abdallah, Mungu amuwie radhi. Katika Dhuabatu Asseifi ya Mjumbe wa Allah, Rehema na amani ziwe juu yake na Aali zake, kulikuwa na swahifa ndogo, ndani yake kuna herufi ambazo kila moja katika herufi hizo inafungua herufi elfu moja.Abuu Baswiiri akasema: Abuu Abdallah amesema: Mpaka sasa hakuna kilichotoka katika swahifa hizo ispokuwa herufi mbili tu.([54])Tunasema: Ziwapi hizo herufi nyingine?!Hivi, kwa nini zitolewe hizo herufi ili Mashia wa Ahli baiti wafaidike nazo?!Au hizo herufi zitabakia zikiwa zimeandikwa mpaka asimame mwenye kusimama?! Huku vizazi kwa vizazi vinaangamia na dini ikiwa imefungwa katika Sirdaabu…?! 5.     Swahifa ya Ali:Ni swahifa nyingine iliyokutikana katika Dhuabatu Asseifui:Kutoka kwa Abuu Abdallah, Mungu amuwie radhi amesema:Katika Dhuabatu Seifi ya Mtume wa Allah, Rehema na amani ziwe juu yake na Aali zake, imekutwa swahifa, na tahamaki ndani yake imeandikwa: Kwa jina la mwenyezi Mungu Mwenye kurehemu Mwingi wa Rehema. Kwa hakika mtu muovu zaidi mbele ya Allah siku ya Kiama ni yule anayempiga vita mtu asiyempiga vita, anayempiga asiyempiga, na anayewafanya vipenzi wasio mawalii wa Allah. Basi mtu huyo ameshayakufuru yale yaliyoteremshwa na Allah Mtukufu kwa Muhammad, Rehema na amani ziwe juu yake, na Aali zake. Vilevile mtu mwenye kuzusha jambo, au kumpokea mzushi, Allah hatamkubalia mtu huyo siku ya Kiama mali wala chochote cha kikomboleo.([55])  6.     Aljifru:Nazo zipo za aina mbili: Aljifru nyeupe na Aljifru nyekundu:Kutoka kwa Abuu Alaa amesema: Nimemsikia Abuu Abdallah, Mungu amuwie radhi akisema: Kwa hakika nina Aljifru nyeupe. Akasema: nikauliza: Kuna nini ndani yake?Akasema: Zaburi ya Daudi, Taurati ya Musa, Injili ya Issa na suhufi za Ibrahimu, Amani iwe juu yao, pia kuna halali na haramu.., Pia nina Aljifru nyekundu.          Nikauliza: Kuna nini katika Aljifru nyekundu? Akasema: Kuna silaha, kwa hakika hiyo Aljifru nyekundu, inafunguliwa kwa damu inayofunguliwa na mwenye upanga wa kuulia.Abdalah bin Abuu Alyaafuuri akamwambia: Mungu akufanye mwema, Je, haya yanajulikana na Banuu Hassani?        Akasema: Naapa kwa Allah, wanayajua kama wanavyoujua usiku kuwa ni usiku na mchana kuwa ni mchana, lakini hasadi na kutafuta dunia kunawafanya kuipinga na kuikana, na lau wangelitafuta haki kwa hakika, ingekuwa bora kwao.([56])Tunasema: Zingatia: Zaburi ya Daudi, Taurati ya Musa, Injili ya Issa na Sahifa za Ibrahimu, Amani iwe juu yao, pia kuna halali na haramu, zote katika Aljifru hii?Kwa nini mnaificha? 7.     Msahafu wa Fatuma: A – Kutoka kwa, Ali bin Said, kutoka kwa Abdallah, Mungu amuwie radhi amesema: Wallahi tuna msahafu wa Fatuma, kile kilichomo ndani yake ni aya katika kitabu cha Allah, na kwa hakika ni imla ya Mtume wa Allah, Rehema na amani ziwe juu yake, na Aali zake, kwa hati ya mkono wa Ali, Mungu amuwie radhi.([57])          B – Kutoka kwa Muhammad bin Muslimu, kutoka kwa mmoja wao, Mungu amuwie radhi:(Fatuma ameacha Msahafu ambao si Qur'an, lakini ni maneno miongoni mwa maneno ya Allah aliyoyateremsha kwake, ikiwa ni matamko ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake na Aali zake, hati ni za Ali, Mungu amuwie radhi).([58])           C – Kutoka kwa Ali bin Abuu Hamza, kutoka kwa Abuu Abdallah, Mungu amuwie radhi:          Sisi tuna msahafu wa Fatuma, amani iwe juu yake, Wallahi, hakuna ndani yake herufi miongoni mwa herufi za Qur'an, lakini wenyewe ni imla ya Mtume wa Allah, Rehema na amani ziwe juu yake, na Aali zake, na hati ni za Ali, Mungu amuwie radhi.([59])          Ikiwa hicho kitabu ni matamko ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake na Aali zake, na hati ni za Ali, kwa nini wanauficha umma?!          Allah Mtukufu amemwamrisha Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, awafikishia kila alichomteremshia. Allah Mtukufu amesema: {Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake..} Sura [5] Al-Ma’idah 67.           Baada ya maelezo haya, Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, atawezaje kuwaficha Waislamu wote hiyo Quran?! Na vipi iwe sawa kwa Ali, Mungu amuwie radhi, na Maimamu wa baada yake waifiche, wasiwape Mashia (wafuasi) wao?!Je, hii sio hiana ya amana?!  8.     Taurati, Injili na Zaburi:Kutoka kwa Abuu Abdallah, Mungu amuwie radhi: kwa hakika alikuwa anasoma Injili, Taurati na Zaburi kwa Lugha ya Kisuriani.([60])Tunasema: Amiri Muminiina na Maimamu wa baada yake wanaifanyia nini Zaburi, Taurati na Injili? Huku wakipeana wao kwa wao na kuisoma kwa siri. Na maandiko ya Kishia yanadai kuwa Ali pekee ndiye aliyepata Qur'an kamili na kupata vitabu na suhufi zote hizo na vinginevyo kwa mujibu wa madai yenu. Sasa ana haja gani na Zaburi, Taurati na Injili?!          Hasa hasa tukijua kuwa, vitabu hivyo ni mansukhu kwa kuteremka Qur'an?          Baada ya yote haya tunasema: Sisi tunajua kuwa Uislamu hauna vitabu ispokuwa kimoja tu nacho ni Qur'an Tukufu. Ama kuwa na vitabu vingi hili ni jambo linalowahusu Wayahudi na Manasara kama ilivyowazi katika vitabu vyao ambavyo ni vingi.43 – Mtume Rehema na amani ziwe juu yake, kwa nini hakujipiga pale alipokufa mwanawe ambaye ni Ibrahimu?!Ali, Mungu amuwie radhi, kwa nini hakujipiga pale alipokufa Fatuma, Mungu amuwie radhi?!44 – Wanazuoni wengi wa Kishia, na hasa hasa huko Irani hawajui lugha ya Kiarabu, nao ni watu Waajemi wa kilugha. Vipi wataweza kutoa hukumu kutoka katika kitabu cha Allah Mtukufu na Sunna za Nabii wake, Rehema na amani ziwe juu yake?! Huku ikijulikana kuwa kujua lugha ya Kiarabu ni moja ya vitu vya lazima kwa Elimu (ya Kiislamu).45 – Mashia wanaitakidi kuwa aghlabu ya Maswahaba walikuwa wanafiki na Makafiri ispokuwa wachache mno! Ikiwa ni hivyo: Kwa nini hawa Makafiri walio wengi hawakuwamaliza wale wachache waliokuwa na Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake?! Mkisema kuwa hao wengi waliritadi baada ya kufa kwa Mtumem, Rehema na amani ziwe juu yake, ispokuwa saba tu, kwa nini, hao wengi hawajawamaliza hao Waislamu wachache na kurejesha mambo kama yalivyokuwa kwa baba zao na babu zao?! 46 – Mashia wanasema kuwa: Abuu Jafari Muhammad bin Hassani Atwusiyyu katika utangulizi wa kitabu chake "Taadhibu Al-ahkaami"([61]) Nacho ni moja ya vitabu vyao vine: "Shukurani njema za Allah, Mlinzi wa haki anayestahiki hilo, Na Rehema na amani ziwe juu ya Mbora wa viumbe wake Muhammad, Rehema na amani ziwe juu yake, Baadhi ya marafiki wale ambao haki zao ni wajibu kwetu, Allah awatakase, wamenitajia hadithi za maswahiba wetu Allah awatie nguvu na rehema za Salafu miongoni mwao. Hadithi zenye mambo yenye khilafu na kutofautiana, kupingana na kwenda kinyume, hata inakaribia kuwa hakuna habari inayoafikiwa, bali katika kila habari mkabala wake kuna inayoipinga. Wala haisalimiki hadithi ispokuwa katika mukabala wake kuna inayoikanusha hadi ikawafanya wanaotukhalifu wawe ndio watiaji dosari wakubwa wa madhehebu yetu…". Na Sayyid Daldari Ali Alkahnuwiyyu Mshia Ithnasheria anasema katika Asaasu Al-usuli:([62]) Kwa hakika "Hadithi zilizopokelewa kutoka kwa Maimamu zinakhitilafiana sana, haikaribii kupatikana hadithi, ispokuwa katika mkabala wake kuna inayoikanusha, wala hakuna habari iliyoafikiwa sipokuwa kuna ya kinyume chake, hadi hiyo ikawa ndio sababu ya kurejea baadhi ya waliopungukiwa…" Na mwanazuoni, mhakiki, mwenye hekima, mwangalifu na sheikhe wao Hassani bin Shihabu Dini Alkurkiyyu katika kitabu chake "Hidaayatul Abraari Ilaa Twariiqi Al-aimmati Al-atwhaari":([63]) "Hilo ndilo lengo alilolitaja mwanzoni mwa Attahdhiib ya kuwa amekitunga kitabu hicho ili kuondosha kupingana baina ya habari zetu kwa yale yaliyomfikia kuwa, baadhi ya Mashia wamerejea na kuyaacha madhehebu kwa ajili ya jambo hilo". Tunasema: Kwa hakika wanazuoni wa Kishia wamekiri kuwa madhehebu yao yana kupingana,([64]) Na Allah anasema kuhusiana na batili: {…Na lau kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangelikuta ndani yake khitilafu nyingi}. Sura [4] An-Nisa’ 82.47 – Mashia wanaitakidi kuwa Ali bin Abuu Twaalibu ni mbora kuliko mwanawe ambaye ni Huseini, Ikiwi ni hivyo, kwa nini hawamlilii Ali katika kumbukumbu ya kuuawa kwake kama wanavyomlilia mwanawe?! Kisha, je, Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, hakuwa mbora kuliko hao wawili? Kwa nini hammlilii kupita mnavyowalilia hao waliotangulia?!48 – Ikiwa utawala wa Ali bin Abuu Twaalibu, Mungu amuwie radhi, na utawala wa watoto wake baada yake ni nguzo ambayo haithibitiki imani ya mtu ila kwa kuamini nguzo hiyo na asiyeiamini ameshakufuru na anastahiki Jehannamu hata kama atashuhudia kuwa Hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allah na hakika Muhammad ni mjumbe wa Allah, na kudumisha sala, kutoa zaka, kufunga Ramadhani, kuhiji Nyumba Tukufu ya Allah – kama wanavyoitakidi Mashia.Kwa nini hatukuti kutajwa kwa uwazi kwa hii nguzo kuu ndani ya Qur'an Tukufu?!Kwa hakika, tunaikuta Qur'an imetaja wazi wazi nguzo nyingine zisizokuwa hiyo pamoja na mambo ya wajibu yaliyo chini ya nguzo hiyo, kama Swala, Zaka, Funga, Hijah. Pia imetaja baadhi ya mambo ya halali kama kuwinda… Ipo wapi hiyo nguzo kuu yenye uzito mkubwa…?! 49 – Jamii ya Maswahaba ingekuwa kama inavyoelezwa na Mashia, ni jamii yenye bughudha, kuhusudiana, na kila mmoja anajaribu kuupata ukhalifa. Jamii ambayo hakuna waliobakia katika imani miongoni mwa watu wake ila watu wachache! Lakini hatupati zama katika Uislamu zama ambazo Uislamu ulifikia mafanikio ya kukomboa miji mingi, na maelfu ya watu kuingia dini ya Kiislamu ispokuwa katika zama za Maswahaba, Mungu awawie radhi.Kwa nini Mashia wengi wanaiacha swala ya Ijumaa. Swala ambayo imeeletewa amri ya wazi ya kuitekeleza katika Sura Al-Jumu‘ah: {Enyi mlioamini! Ikiadhiniwa Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara. Hayo ni bora kwenu, lau kama mnajua}. Sura [62] Al-Jumu‘ah 9.           Wakisema: Sisi tunaiacha hadi atokee Almahdiyyu Anayesubiriwa!          Tunasema: Je, huko kumsubiri kunahalalisha kuchelewesha jambo hili tukufu?! Kwani malaki ya Mashia wameshakufa, kama si zaidi, hali ya kuwa hawajaitekeleza ibada hii tukufu miongoni mwa ibada za Kiislamu, kwa sababu ya udhuru huu wa kisheitwani ulio wa kipuuzi.          51 – Mashia wanaitakidi kuwa kwa hakika Qur'an imefutwa na kubadilishwa baadhi ya aya zake na Abuu Bakri na Omari Mungu awawie radhi!          Na wanapokea kutoka kwa Abuu Jafari kuwa aliulizwa: Kwa nini Ali aliitwa Amiiri Muminiina?          Akasema: Allah Amempa jina hilo. Na hivi ndivyo alivyoteremsha katika Kitabu chake: (Na pale Mola wako Mlezi alipowaleta katika wanadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao, na akawashuhudisha juu ya nafsi zao, akawaambia: Je, Mimi si Mola Mlezi wenu? Na hakika Muhamad ni Mjumbe wangu na Ali ni Amiri Muminiina?)!([65])          Na Alkiliiniyyu anasema katika kutafsiri aya ifuatayo: (Basi wale walio muamini yeye,) yaani Imamu {na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyoteremshwa pamoja naye - hao ndio wenye kufanikiwa}. Sura [7] Al-A‘raaf 157.          Yaani: Wale wanaojiepusha na kuabudu Jibti na twaghuuti: ambao ni fulani na fulani!([66])Almajlisiyyu amesema (Makusudio ya Fulani na Fulani ni Abuu Bakri na Omari)([67])Na kwa ajili hii Mashia wanawazingatia wawili hao kuwa ni Masheitwani – Mungu atukinge na hilo.Katika ufafanuzi wao wa kauli ya Allah mtukufu {…Msizifuate nyayo za Shet'ani…} Sura [24] An-Nur 21. Wamesema: Tunaapa kwa Allah, nyayo za Shet'ani ni utawala wa Fulani na Fulani.([68]) Wamepokea kutoka kwa Abuu Abdallah amesema: {Atakayemtii Allah na Mtume wake katika utawala wa Ali na utawala wa Maimamu wa baada yake, kwa hakika ameshafaulu kufaulu kukubwa.} Akasema: Hivi hivi ndivyo ilivyoshuka.([69])Kutoka kwa Abuu Jafari amesema: Jibrilu, amani iwe juu yake, alimteremkia Muhammad na aya hii ikiwa kama hivi {Ni mabaya zaidi yale waliyoyanunua kwa nafsi zao, kwa kuyapinga yale yaliyoteremshwa na Allah kwenda kwa Ali, hali yakuwa mnachupa mipaka.}([70]) Kutoka kwa Jabiri amesema: Jibrilu, amani iwe juu yake, alimteremkia Muhammad na aya hii ikiwa kama ifuatavyo: {Mkiwa mnashaka kwa yale tuliyomteremshia mja wetu kuhusiana na Ali, leteni sura moja inayofanana nayo}.([71]) Kutoka kwa Abuu Abdallah, amani iwe juu yake amesema: Jibrilu aliteremka kwa Muhammad na aya hii ikiwa kama ifuatavyo: {Enyi mliopewa vitabu aminini yale tuliyoyateremsha kuhusu Ali yakiwa ni nuru yenye kuangaza}([72]).Kutoka kwa Muhammad bin Sinaani, Kutoka kwa Alridhwa Amani iwe juu yake, amesema: {Ewe Muhammad, Washirikina wanahisi tabu mno kwa kile unachowaitia kuhusu kutawala Ali}. Hivi ndivyo ilivyo katika kitabu cha mswada.([73]) Kutoka kwa Abuu Abdallah, amesema: {Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayotokea, Kwa wanopinga utawala wa Ali - ambayo hapana awezaye kuizuia} akasema: Wallah! Jibrilu amani iwe juu yake ameiteremsha hivi hivi kwa Muhammad, Rehema na amani ziwe juu yake na Aali zake.([74]) Kutoka kwa Abuu Jafari amesema: Jibrilu amani iwe juu yake ameteremsha aya hii kwa Muhammad, Rehema na amani ziwe juu yake na Aali zake kama ifuatavyo: {Lakini waliodhulumu haki ya Aali wa Muhammad waliibadili kauli isiyokuwa waliyoambiwa. Kwa hivyo tukaiteremsha juu ya wale waliodhulumu haki ya Aali wa Muhammad adhabu kutoka mbinguni kwa sababu ya walivyokuwa wamepotoka}.([75])          Kutoka kwa Abuu Jafari amesema: Jibrilu amani iwe juu yake ameteremsha aya hii kama ifuatavyo: {Hakika wale waliodhulumu haki ya Aali wa Muhammad Mwenyezi Mungu hawasamehi wala kuwaongoa njia ila njia ya Jehannam}. Kisha akasema {Enyi watu, amekujieni Mtume kwa haki kutoka kwa Mola wenu kuhusiana na utawala wa Ali kwa hiyo aminini ni bora kwenu na kama mkiupinga utawala wa Ali, Kwa hakika ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini}.([76])          Mashia wanadai kuwa aya hizi zinajulisha kwa uwazi kabisa Uimamu wa Ali Mungu amuwie radhi, lakini Abuu Bakri na Omari Mungu awawie radhi walizipotosha kwa mujibu wa madai ya Mashia.           Na haya ni maswali mawili yanayowatatiza sana Mashia:          Swali la kwanza: Maadamu Abuu Bakri na Omari wamezipotosha aya hizi, kwa nini Ali baada ya kuwa khalifa wa Waislamu hakuweka wazi jambo hili?! Au kwa uchache kuzirejesha aya hizi katika Qur'an kama ilivyoteremshwa?!          Hatujamkuta Ali Mungu amuwie radhi akifanya hivyo, lakini Qur'an ya zama zake ilibakia kama ilivyokuwa zama za makhalifa wa kabla yake, na kama ilivyokuwa katika zama za Mtume Rehema na amani ziwe juu yake, kwa kuwa Qur'an imehifadhiwa kwa hifadhi ya Allah aliyesema: {Hakika Sisi ndio tulioteremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutaoulinda}. Sura [15] Al-Hijr 9. Lakini Mashia hawajui.          Swali la pili: Baadhi ya aya hizi walizozipotosha ili zithibitishe utawala, Uimamu na ukhalifa wa Ali, kwa uwazi kabisa, zinatueleza kuwa jambo hilo kamwe halitotokea!!          Zingatieni aya ifuatayo, amabayo wameshaipotosha, Aya hiyo yazungumzia Wayahudi nao wameinasibisha na Waislamu!:           {Lakini waliodhulumu haki ya Aali wa Muhammad waliibadili kauli isiyokuwa waliyoambiwa. Kwa hivyo tukaiteremsha juu ya wale waliodhulumu haki ya Aali wa Muhammad adhabu kutoka mbinguni kwa sababu ya walivyokuwa wamepotoka}.          Kwa mujibu wa upotoshaji wao, aya hii inaongelea jambo litakalotokea  wakati ujao, na kuwa Ali anajua jambo hilo.          Sasa kwa haki gani, inamfanya Ali na Ahli baiti wake wadai haki yao iliyoporwa na hali Qur'an inawaeleza kuwa jambo hilo litatokea? Na kuwa Waislamu kamwe hawatokubali utawala wa Ali wala wasia na wala hatokuwa khalifa baada ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake?!           Kisha, lini imetokea adhabu iliyoshushwa na Mungu kwenda kwa wale waliodhulumu haki ya Aali wa Muhammad kuhusu ukhalifa?!           Kila mtu anajua kuwa hayo kamwe hayajatokea, lakini ni upotoshaji wa kijinga uliofichuliwa!           52 – Mashia wanapokea kutoka kwa Abuu Hassani kuhusiana na kauli ya Allah Mtukufu: {Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao...} "Wanataka kuuzima utawala wa Amiri muuminina" {…Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake…} Sura [61] As-Saff 8. Anasema: Allah ni mwenye kuutimiza Uimamu, na Uimamu ndio nuru", na hiyo ndio kauli ya Allah Mtukufu Aliyetukuka: {Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Nuru tuliyoiteremsha…}. Sura [64] At-Taghabun 8. Abuu Hassani amesema: "Wallahi, Nuru ni Maimamu miongoni mwa Aali Muhammad, Rehema na amani ziwe juu yake na Aali zake siku ya Kiama".([77])          Swali: je, Allah ametimiza nuru yake kwa kuusambaza Uislamu au kwa kuwapa utawala, wasia na ukhalifa, watu wa Ahli baiti?!          53 – Kwa mujibu wa ufahamu wenu – tumekuta – Maimamu  wawili tu ndio waliotawalia ukhalifa miongoni mwa Maimamu wote, nao ni Ali na mwanawe Hassani, Mungu awawie radhi! Sasa kuko wapi kutimizwa kwa nuru kwa Maimamu kumi waliobakia? Na nasu ya hadithi ya Mtume Rehema na amani ziwe juu yake, wanaikariri kwa kutolea hoja juu ya Maimamu zao kumi na wawili! Ndani ya nasu hiyo kuna: "Kwa hakika hao ni "Makhalifa" au "Mawalii amri – Wasimamizi" au Viongozi (maamiri), sasa upo wapi  ukhalifa au uamiri wa hao kumi waliobakia?!  54 – Baadhi ya vitabu vya Kishia vimepokea kutoka kwa Jafari Aswaadiqu kuwa amemwambia mwanamke aliyemuuliza kuhusu Abuu Bakri na Omari: Je, niwafanye watawala wangu?! Akamjibu: wafanye watawala wako. Akauliza: Je, nimwambie Mola wangu pindi nikikutana naye kuwa wewe umeniiamrisha kuwafanya watawala wangu?! Akamwambia: Ndio.([78])Na imepokewa kuwa: Mtu mmoja miongoni mwa watu wa Albaaqri alishangazwa pale aliposikia wasifu wa Albaaqri kumsifu Abuu Bakri, Mungu amuwie radhi, ya kuwa ni mtu Asswiddiiq (msadikisha, mkweli), Yule mtu akasema: Je, unamsifu kwa sifa hiyo? Albaaqri akasema: ndio ni Asswiddiiq na yoyote asiyemwita Asswiddiiq, Allah hatosadikisha kauli ya mtu huyo huko akhera.([79])          Je, mtazamo wa Mashia ni upi kuhusiana na Abuu Bakri, Allah amuwie radhi?          55 – Abuu Alfaraji Al-Aswfahaaniyyu katika kitabu Muqaatilu Attwaalibuna,([80]) Arbaliyyu katika Kashfu Alghummat,([81]) na Majlisiyyu katika Jalaau Aluyuuni,([82]) wametaja kuwa: Kwa hakika Abuu Bakri bin Ali bin Abuu Twaalibu alikuwa ni miongoni mwa wale waliouliwa huko Karbalaa akiwa pamoja na nduguye ambaye ni Huseini, Mungu awawie radhi, pia aliuliwa pamoja nao mtoto wa Hassani na jina lake ni Abuu Bakri! (na Muhammad mdogo aliyepewa jina la Abuu Bakri).          Mashia kwa nini wanaficha jambo hili?! Na kutilia mkazo kuuliwa Huseini tu?           Sababu ni kuwa jina la nduguye Huseini, na mtoto wake ni: (Abuu Bakri)!!          Mashia hawataki wafuasi wao walioghafirika wala Waislamu wajue hilo, kwa kuwa hilo linafichua uongo wao wa kudai uadui kati ya Ahli Baiti na Maswahaba wakubwa wakiongozwa na Abuu Bakri, Mungu amuwie radhi. Kwa sababu, lau angekuwa kafiri aliyeritadi na kupora haki ya Ali na Aali zake – kama Mashia wanavyodai – tusingeona Ahli baiti  wakijiita kwa jina lake!          Pia huu ni ushahidi wa mapenzi kwa mwenye kutafakari. Mashia kwa nini hawamuigi Ali na Huseini Mungu awawie radhi na kuwapa watoto wao jina la (Abuu Bakri)?! 56 – Imani ya kuamini kuwa Mtume Muhammad, Rehema na amani ziwe juu yake, ni Nabii wa mwisho inatufikisha katika makusudio ya Uimamu katika uhai wake na baada ya kufa kwake, na yeyote atakayethibitisha kuwa, kwa hakika Muhammad, Rehema na amani ziwe juu yake, ni mjumbe wa Allah, na kumtii ni wajibu, na akajitahidi kumtii kwa uwezo wake, ikisemwa kuwa mtu huyo anaingia Peponi, basi atakuwa hana haja na maswala ya Uimamu wala halazimiki kumtii asiyekuwa Mtume Muhammad, Rehema na amani ziwe juu yake. Na pakisemwa kuwa hakuna mtu atakayeingia Peponi ila kwa kumfuata Imamu hilo litakua ni kinyume na maandiko ya Qur'an Tukufu, kwani Allah Mtukufu Aliyetukuka amewajibisha Pepo kwa mwenye kumtii Allah na Mtume wake katika sehemu zaidi ya moja ndani ya Qur'an, na wala hajashurutisha kuingia Peponi kwa kumtii Imamu au kumwamini. Mfano wa hayo ni kauli ya Allah Mtukufu: {Na wenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume, hao wapo pamoja na wale aliowaneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na Masiddiqi, na Mashahidi, na Watu wema. Na uzuri ulioje kuwa pamoja na watu hao!}. Sura [4] An-Nisa’ 69. {…Na anayemt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Yeye atamtia katika Pepo zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.} Sura [4] An-Nisa’ 13. Uimamu ungekuwa ni Asili ya imani au kufuru, au ungekuwa ni nguzo kuu kabisa miongoni mwa nguzo za dini, nguzo ambayo, Allah hakubali matendo ya mja ispokuwa kwa nguzo hiyo kama wasemavyo Mashia, Allah Mtukufu aliyetukuka angeutaja Uimamu katika aya hizo na kuusisitiza. Kwa kuwa anajua kuwa kutakuwepo ukhalifa kwa nguzo hiyo hapo baadaye. Sidhani kama kuna mtu atakuja na kutwambia kuwa Uimamu katika aya hizo umetajwa pamoja na kumtii Allah na Mtume. Kwa sababu kusema hivyo ni kulazimisha tafsiri – ufafanuzi, lakini inatosha kubatilisha madai hayo tukisema kuwa kumtii Mtume ni kumtii Mola aliyempeleka, lakini Allah Mtukufu Aliyetukuka hakutaja kutiiwa yeye peke yake na kujaalia kumtii Mtume kumeambatanishwa chini ya kumtii yeye lakini ameitaja ili athibitishe nguzo mbili za muhimu sana katika itikadi ya Kiislamu (Kumtii Allah, na kumtii Mtume), Na kwa hakika, imewajibika kutaja twaa ya Mtume baada ya twaa ya Allah ikiwa ni sharti la kuingia Peponi. Kwa sababu Mtume ni mfikishaji kutoka kwa Allah na kumtii yeye vilevile ni kumtii aliyemtuma. Na kwa kuwa haijathibiti kwa yeyote baada ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake na Aali zake, kuwa anafikisha ujumbe kutoka kwa Allah, basi kwa hakika Allah Mtukufu Aliyetukuka, amefungamanisha kufaulu na kufanikiwa kuingia Peponi na kumtii Mtume wake na kulazimika kutii amri zake na wala sio amri za watu wengine.Katika zama za Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake na Aali zake na Maswahaba zake, kulikuwa na watu, wanamuona mara moja tu kisha wanaenda majumbani kwao, bila shaka hawajasikia, utawala wa Ali bin Abuu Twaalibu, watoto na wajukuu zake, Mungu awawie radhi wote. Na hasa hasa Mashia wanadai kuwa jambo la Utawala limetokea mwanzoni mwa Daa'wa – wito, huko Makka, wakitoa hoja ya Hadithi ya Nyumba. Je, Uislamu wa watu hao ni pungufu?!Mkisema: ndio. Tunasema: ingekuwa hivyo, basi Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, ndio mbora zaidi wa kusahihisha Uislamu wao na kuwabainishia jambo la Uimamu. Wala hatujakuta kuwa, Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, amefanya jambo hilo.58 – Katika kitabu (Nahju Albalaagha) imekuja kuwa, yale wanayoyathamini Mashia ni yafuatayo: (Ali amani iwe juu yake, miongoni mwa aliyomwandikia Muawiya ni:Kwa hakika, watu walionibaiyyi mimi ni wale waliombaiyyi Abuu Bakri, Omari na Athumani kwa kile walichowabaiyyi. Mtu aliyekuwepo hakuwa na uchaguzi wala mtu asiyekuwepo hakuweza kukataa. Kwa hakika hiyo ni shura kwa Muhajirina na Maanswari. Wakiungana pamoja kwa mtu na kumtaja ni Imamu hilo linakuwa lenye radhi za Mungu. Na mtu akitoka nje ya jambo lao kwa kukosoa au kuzusha wanamrejesha katika kile alichokitoka na akikataa wanamuua kwa kuwa amefuata njia isiyo ya Waumini na Allah anampelekea kwa yale aliyoyafuata. Nakuapia, ewe Muawiya lau ungetazama kwa akili zako pasi na matamanio yako utanikuta mimi ni mtu niliyetakasika mno kuliko watu wote na damu ya Athumani, na inapasa ujue, kuwa mimi nilikuwa nimejitenga naye ila kama utadai kuwa mimi nimefanya dhambi basi utachuma dhambi kwa kile kitakachokudhihirikia, Wassalaam).([83])  9.     Katika maelezo haya kuna ushahidi wa yafuatayo:1-    Imamu anachaguliwa na Muhajirina na Maanswari, hana mafungamano yoyote na nguzo ya Uimamu kwa Mashia!2-    Kwa hakika Ali alibaiyyiwa kwa njia ile ile waliyobaiyyiwa Abuu Bakri, Omari na Athumani, Mungu awawie radhi wote.3-    Kwa hakika shura kwa Muhajirina na Maanswari, na hili linajulisha ubora wao na daraja zao za juu kwa Allah, na linapinga na kukhalifu picha wanayoiakisi Mashia kwa Maswahaba.4-    Hakika kukubali, kuridhia na kubaiyyi kwa Muhajirina na Maanswari kwa Imamu wao kunakuwa kwa radhi za Allah, hakuna kupora haki ya Uimamu kama wanavyodai Mashia, na kama si hivyo, vipi Allah aridhie jambo hilo?!5-    Kwa hakika Mashia wanamlaani Muawiya, Mungu amuwie radhi, wala hatujapatapo kuona kuwa Ali, Mungu amuwie radhi, akimlaani katika risala zake!59 – Mashia hawawezi kukanusha kuwa Abuu Bakri, Omari na Athumani, Mungu awawie radhi wote, walimbaiyyi Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, chini ya mti. Na Allah ameeleza kuwa: amewaridhia na amejua yaliyokuwa mioyoni mwao,([84]) Iweje kwa Mashia baada ya haya wayakufuru maelezo ya Allah Mtukufu, na kudai kinyume chake?! Kama vile wanasema: (Ewe Mola, Wewe huwajui kwa yale tunayowajua sisi)! – Tujikinge kwa Allah!60 – wakati tunawakuta Mashia wanajikurubisha kwa Allah kwa kuwatukana Maswahaba wakubwa, wakiongozwa na Makhalifa watu Waongofu: Abuu Bakri, Omari na Athumani, Mungu awawie radhi, humkuti Msuni hata mmoja akimtukana yoyote miongoni mwa Ahli baiti! bali wanajikurubisha kwa Allah kwa kuwapenda.Na haya ndio wasiyoyaweza kuyapinga Mashia, japo kwa uongo.  61 – Wakati Mashia wanakariri mauaji ya Huseini, Mungu amuwie radhi, katika vitabu vyao ya kuwa amekufa kwa kiu katika uwanja wa mapambano, kwa hiyo utawaona wanaandika katika matenki ya kuhifadhia maji ibara ifuatayo (Kunywa maji na kumbuka kiu ya Huseini)!           Swali: kwa kuwa Maimamu – kwa ufahamu wa Mashia – wanajua ghaibu:Je, Huseini hakujua kuwa ana haja ya maji wakati wa vita, na atakufa akiwa na kiu, na kwa hiyo anaweza kukusanya kiasi kikubwa cha maji kinachotosha katika vita?! Kisha: Je, kujiandalia maji kwa ajili ya vita hakuingii katika mlango wa kuchukua tahadhari?! Na Allah anasema: {Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi waliofungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu…}. Sura [8] Al-Anfaal 60.62 – Dini ya Kiislamu imekamilika katika zama za Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, kwa kauli ya Allah Mtukufu: {…Leo nimekukamiliishiani Dini yenu…} Sura [5] Al-Ma’idah 3. Lakini madhehebu ya Kishia yamedhihiri baada ya kufa kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake?!63 – Allah – Mtukufu Aliyetukuka, ameteremsha utakasifu wa bibi Aisha, Mungu amuwie radhi, katika kisa cha Ifki kilicho mashuhuri, na kumtakasa na ubaya huo, kisha tunawakuta baadhi ya Mashia wanaendelea kumvurumishia bibi Aisha kuwa ametembea nje ya ndoa!!([85]) Mungu atukinge – Na katika jambo hilo kuna kumtia dosari Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, pia kuna kumtia dosari Allah Mtukufu Aliyetukuka Anayejua ghaibu, eti hajamwambia Mtume wake kuwa mkewe amemwendea kinyume?! Allah amemwepusha Aisha na hayo.Kwa hakika madhehebu mabaya zaidi ni yale yanayotia dosari wake za mbora wa wanadamu, ambao ni mama za waumini.64 – Ikiwa Ali na Watoto wake wawili, Mungu awawie radhi, wana hali za kimaajabu zinazosimuliwa na vitabu vya Kishia. Mashia wananufaika na Ali pamoja na watoto wake wawili hadi sasa wakiwa ni wafu – kama wanavyodai – kwa nini hawakuzinufaisha nafsi zao walipokuwa hai?!Tumemkuta Ali, Mungu amuwie radhi, kuwa hakutulia na utawala, kisha akafa kwa kuuawa, na tukamkuta Hassani hivyo hivyo, amelazimika kuachia utawala kwa Muawiya, na tukamkuta Hussein, akipatwa kibano kisha kauawa wala hakupata ayatakayo… na hivyo hivyo kwa Maimamu wa baada yao!  Sasa zipo wapi hizo hali za kimaajabu walizokuwa nazo?Mashia wanadai kuwa ubora wa Ali umepokewa kwa tawaatiru (na watu wengi) kwa njia za Mashia, vilevile maandiko ya Uimamu wake. Inasemekana kuwa: Mashia ambao si Maswahaba, hao hawajamuona Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, wala hawajasikia maneno yake. Kwa hiyo nukuu zao ni Mursalu (kurusha maneno, kusema maneno ya mtu ambaye hujamsikia wala hakuwa katika zama zako) pia ni Munkatiu (zimekatikiwa isinadi, hazijapokelewa mtu na mtu kuna watu hawakutajwa) kama hawajayaegemeza kwa Maswahaba kwa hiyo hayatokuwa sahihi, na Maswahaba wanaowakubali Mashia ni wachache mno ni kama kumi na ushei hivi, na Tawaatiru haithibiti kwa kunukuu watu wachache kama hawa! Idadi kubwa ya Maswahaba walionukuu fadhila za Ali wanatiwa dosari na Mashia na kuwatuhumu kuwa ni makafiri!Kisha kama watajuzisha kuwa Maswahaba wengi waliosifiwa na Qur'an, huku wao wakiwaona kuwa ni waongo na wafichaji. Sasa inawalazimu wajuzishe hilo hilo kwa hao wachache kwa kujuzisha hilo kwa wachache ni bora zaidi!66 – Mashia wanadai kuwa: Abuu Bakri, Omari na Athumani, Mungu awawie radhi, walikuwa na lengo la utawala na ufalme, wakadhulumu wengine kwa sababu ya utawala. Basi wanaambiwa kuwa: Hawa Maswahaba hawajapambana na Mwislamu kwa ajili ya utawala, bali waliwaua walioritadi na makafiri, na wao ndio waliovunja Kasri la Kisraa na Kaisari, na kuikomboa miji ya Farsi (maeneo ya Irani na kuusimika Uislamu, Na wakaupa nguvu Uislamu na Waislamu na kudhoofisha Kufru na watu wake. Na Athumani ambaye ana nafasi ya chini kicheo kuliko Abuu Bakri na Omari, Watu wa machafuko walitaka kumuua alipokuwa katika utawala wake, naye hajawaua Waislamu wala hakuuliwa Muislamu katika utawala wake.Kama Mashia wanajuzisha kwa Maswahaba hawa kuwa ni madhalimu katika utawala wao, pia ni maadui wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, basi itawalazimu waseme maneno hayo kwa Ali, Mungu amuwie radhi!! 67 – Makadiani wamekufuru kwa kudai kwao Utume wa kiongozi wao, sasa tofauti ipo wapi kati yao na Mashia wanaodai kuwa Maimamu wao wana sifa za Mitume na zaidi?!Je, haya sio mambo yanayopelekea katika kukufuru? Au watutajie tofauti za msingi kati ya Imamu na Mtume?! Je, Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, amekuja kutubashiria Maimamu kumi na wawili wenye kauli kama kauli zake, matendo kama matendo yake, wamekingwa na maasi kama alivyokingwa Mtume, sawa kwa sawa…?68 - Iweje Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, azikwe katika chumba cha Aisha, Mungu amuwie radhi?! Na nyinyi mnamtuhumu kuwa ni Kafiri na mnafiki, Mola atukinge na hayo?! Je, huu si ushahidi wa kuwa Mtume  anampenda Aisha na kumridhia?!69 - Mfano wa hilo: Vipi Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, azikwe katikati ya Abuu Bakri na Omari, na wawili hao – kwa mtazamo wenu – ni makafiri?! Hivi Allah hukumuhifadhi asizikwe jirani na makafiri wawili alipokufa – kwa mujibu wa madai yenu.Kisha, Ali yupo wapi, wakati yanatokea yote hayo?! Kwa nini hakupinga jambo hili la hatari?!Inakulazimikieni kuwa: Abuu Bakri na Omari, Allah awawie radhi, ni Waislamu, Allah amewapa utukufu wa kuzikwa jirani na Mtume kwa kuwa watu hao ni watukufu kwa Allah na kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake. Na hii ndio haki. Au iwe Ali, Mungu amuwie radhi, amewapaka mafuta dhidi ya dini yake (alikuwa anawafanyia unafiki wa kuwasifu kuwa ni wazuri kumbe ni wabaya)!! Ali ameepukana na hilo. Kama si hivyo, iweje, Mtume aliyeteuliwa azikwe pamoja na Makafiri Waovu kama mnavyodai? 70 – Mashia wanadai kuwa: maandiko juu ya Uimamu wa Ali, Mungu amuwie radhi, na kustahiki kwake kuwa khalifa yamethibiti katika Qur'an lakini Maswahaba wameyaficha. Madai haya ni batili kwa kuwa tumekuta kuwa Maswahaba, Allah awawie radhi, hawajaficha zile hadithi ambazo Mashia wanazitolea ushahidi wa Uimamu wa Ali. Mfano hadithi ya: "Wewe kwangu mimi una nafasi ya Haruna kwa Mussa" na hadithi nyinginezo zinazofanana na hii, kwa nini hawakuzificha na hadithi hizi?!71 – Khalifa wa haki baada ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, ni Abuu Bakri Swiddiiq. Na ushahidi wa hili ni: (1) – Makubaliano ya Maswahaba juu ya kumtii na kutekeleza amri zake na kuacha makatazo yake, na hawakumpinga. Na lau asingekuwa khalifa wa kweli wasingemuacha katika hali hiyo wala wasingemtii. Na wao ni watu walioipanyongo dunia, wachamungu, wenye dini, walikuwa hawajali lawama za mwenye kulaumu katika amri ya Allah. (2) – Ali, Mungu amuwie radhi, Hajamkhalifu Abuu Bakri wala hajampiga vita. Hapa hapakosi kuwa; Ali ameacha kupambana naye kwa kuogopa fitina, shari na kwa sababu ya kushindwa, au Ali anajua kuwa haki ipo na Abuu Bakri.Haiwezekani kuwa: kuacha kwake kuwe kwa ajili ya kuzuia fitina na kuogopa shari. Kwa kuwa alipambana na Muawiya. Mungu amuwie radhi, na wakauliwa katika vita hivyo viumbe vingi, akapambana na Twalhat na Zuberi, Mungu awawie radhi, pia akapambana na Aisha, Mungu amuwie radhi, pale alipojua kuwa haki ni yake wala hakuacha kwa kuogopea fitina!Na haiwezekani kuwa alishindwa! Kwa kuwa wale waliokuwa upande wake wakati wa Muawiya, walikuwa waumini siku ya Assaqiifatu na siku ya kutawala Omari na siku ya Shura, na kama wangejua kuwa haki ni ya Ali, wangemnusuru dhidi ya Abuu Bakri, Allah amuwie radhi, kwa kuwa kumpiga vita Abuu Bakri ni bora zaidi kuliko kumpiga vita Muawiya.Kwa hiyo imethibitika kuwa Ali ameacha jambo hilo kwa vile alikuwa anajua fika kuwa haki ipo pamoja na Abuu Bakri, Allah amuwie radhi!72 – Mashia wanadai kuwa Muawiya, Allah amuwie radhi, alikuwa kafiri aliyeritadi! Mambo yakiwa kama wanavyosema basi inawalazimu wamtie dosari Ali na mwanawe ambaye ni Hassani, Allah awawie radhi, kwa ufafanuzi huu: Ima Ali awe ameshindwa na walioritadi. Na Hassani amewapa walioritadi mambo ya kutawala Waislamu. Huku tunamkuta Khalidi bin Alwaliidi aliwapiga vita walioritadi wakati wa Abuu Bakri na kuwatenza nguvu, na ushindi wa Mwenyezi Mungu kwa Khalidi dhidi ya makafiri ulikuwa mtukufu mmno kuliko alivyomnusuru Ali! Na Allah Mtukufu Aliyetukuka ni Mwadilifu hadhulumu mtu miongoni mwao, kwa hiyo anakuwa Abuu Bakri ni mbora mbele za Allah kuliko Ali, Pia jeshi la Abuu Bakri, Omari, Athumani na manaibu wao yalikuwa yakinusuriwa dhidi ya makafiri, huku Ali anashindwa kupambana na walioritadi! Vilevile, Allah Mtukufu Aliyetukuka anasema; {Wala msilegee, wala msihuzunike, kwani nyinyi ndio wa juu mkiwa ni Waumini} Sura [3] Aal-‘Imran 39.  Pia anasema: {Basi msilegee na kutaka suluhu, maana nyinyi ndio mtakaoshinda. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi, wala hatakunyimeni malipo ya vitendo vyenu} Sura [47] Muhammad 35. huku Ali, Allah amuwie radhi, amemwita Muawiya kutaka suluhu mwishoni mwa jambo hilo aliposhindwa kumtimua kumtoa katika mji wake. Na akataka kila mmoja kati yao abakie kama alivyo. Na kama ikiwa wafuasi ni waumini na hao wengine ni walioritadi – kama Mashia wanavyodai – italazimika wafuasi wa Ali wawe washindi, lakini hilo ni kinyume na uhalisia! 73 – Hakika Mashia wanashindwa kuthibitisha imani ya Ali na uadilifu wake, wala hawatoweza kutimiza hilo ila wawaendee Wasunni. Kwa kuwa, kama Makhawariji na wengineo miongoni mwa wanaompinga au kumuona Ali ni fasiki watawaambia Mashia: "Hatukinaiki kuwa Ali alikuwa muumini, lakini alikuwa kafiri au dhalimu – kama wasemavyo Mashia kuhusu Abuu Bakri na Omari – Mashia hawatakuwa na ushahidi zaidi wa ule ule wa imani ya Abuu Bakri, Omari na Athumani kwa uzuri zaidi. Kama wataleta hoja ya yale yaliokuja kwa tawaatiru (watu wengi) juu ya kusilimu, hijra na jihadi zake. Kwa hakika mambo hayo yamepokewa kwa tawaatiru, yakiwahusu Abuu Bakri, Omari na Athumani. Pia Uislamu wa Muawiya, makhalifa wa banii Ummayya na banii Al-Abbasi umepokewa kwa tawaatiru, vilevile sala zao, funga zao na jihadi zao dhidi ya makafiri!Kama watadai kuwa mmoja wa watu hawa ni mnafiki, hilo litawawezesha Khawariji adai kuwa Ali ni mnafiki!Kama watataja vitu vya utata utatajwa utata ulio mkubwa kuliko huo! Wakisema yale wayasemayo wazushi nayo ni kuwa Abuu Bakri na Omari kisirisiri walikuwa wanafiki na maadui wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, wameifisidi dini yake kwa kadiri wanavyoweza. Hili linamwezesha Khawariji aseme hayo hayo kwa Ali, na kufafanua hayo kwa kusema kuwa Ali alikuwa anamfanyia husda mtoto wa Ami yake – na uadui kwa wanandugu – alikuwa anataka kuiharibu dini yake, hakuweza kutekereza hilo wakati wa uhai wa Mtume na uhai wa makhalifa watatu, hadi akahangaikia kumua khalifa wa tatu na kumwashia moto wa fitina. Hatimaye akafanikiwa kuwaua Maswahaba wa Muhammadi kwa chuki na uadui wake. Alikuwa mtu batwiniya (yaaani anayedai anajua mambo ya ndani wengine hawayajui) kwa wanafiki waliodai kuwa Ali ni Mungu na ni Mtume. Alikuwa anadhihirisha kinyume na yale anayoyaficha kwa kuwa dini yake ni taqiya kwa hiyo Wabatwiniya ndio walikuwa wafuasi zake na wao wana siri zake, nao wananukuu kutoka kwake mambo ya ndani na kufuata madhehebu hayo!Wakitaka kuthibitisha imani na uadilifu wa Ali kwa maandiko ya Qur'an yanayomuhusu. Wataambiwa: "Qur'an ni aamu" (yaenea) na inapomgusia yeye isidhaniwe kuwa yeye ndiye mkuu kuliko inavyowagusia wengine. Hakuna aya inasemwa kuwa ni maalumu kwa Ali, na kama itasemwa hivyo, basi inawezekana kudaiwa hayo hayo na zaidi kwa Abuu Bakri na Omari. Kwa hiyo mlango wa madai bila hoja unawezekana kufunguliwa. Na madai juu ya ubora wa Sheikhaini (Abuu Bakri na Omari) inawezekana zaidi kuliko ubora wa wasiokuwa wao. Wakisema: Hilo limethibiti kwa nukuu za mapokeo, basi nukuu na mapokeo kwa Abuu Bakri na Omari ni mashuhuri na nyingi zaidi. Wakidai kuwa nukuu zao zimekuja kwa tawaatiru, basi tawaatiru kwa hao wengine ndio sahihi zaidi. Wakitegemea nukuu za Maswahaba, basi nukuu za Maswahaba kuhusu fadhila za Abuu Bakri na Omari ni nyingi zaidi! 74 – Mashia wanadai kuwa Ali alikuwa ni mwenye haki ya kuwa Imamu kuliko watu wote kwa kuwa fadhila zake zimethibiti kuliko Maswahaba wote – kama wanavyodai – na kwa ajili ya wingi wa fadhila zake kuliko wengine. Tunawaambia: Hapa mmempata Ali, Mungu amuwie radhi, akiwa na fadhila zinazojulikana, kama kuwa wa mwanzo kusilimu, kupigana jihadi pamoja na Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, wingi wa elimu na kuipa nyongo dunia. Je, sifa kama hizo mmezipata kwa Hassani na Huseini, Mola awawie radhi, ukiwalinganisha na Saadi bin Abuu Wakaaswi, Abdulrahmani bin Aufi, Abdullahi bini Omari na wengineo miongoni mwa Muhajiriina na Maanswaari?!Hakuna yoyote miongoni mwao anayeweza kudai hilo kwa Hassani na Huseini. Kwa hiyo hakujabaki zaidi ya madai ya maandiko yanayowahusu. Na hili la madai ya maandiko halishindikani kwa yoyote mfano wake. Kwa mfano: lau Umawiyya ungejihalalishia kudhihirisha kwa uongo dai la maandiko linalomuhusu Muawiya ingekuwa jambo lao katika hilo lina nguvu zaidi kuliko jambo la Mashia. Kwa kauli ya Allah Mtukufu: {…Na aliyeuliwa kwa kudhulumiwa basi tumempa madaraka mrithi wake. Lakini asipite mpaka katika kuuwa. Kwani yeye anasaidiwa}. Sura [17] Al-Isra 33. Watasema: Aliyedhulumiwa ni Athumani bini Afaani. Na Allah amemnusuru Muawiya kwa vile amekuwa walii wa damu ya Athumani! 75 – Mashia wanadai kuwa Abuu Bakri na Omari wamepora ukhalifa kutoka kwa Ali na wakafanya njama dhidi yake ili wamzuie asiupate… hadi mwisho wa uzushi wao.Tunasema; Yale mlioyasema yangekuwa ni ya kweli, sasa nini kilichomfanya Omari amuingize Ali katika shura pamoja na wale aliowaingiza? Lau kama angemtoa kutoka katika shura kama alivyomtoa Saidi bini Zaidi, au angemkusudia mtu mwingine na kumtawalisha asingepingwa na yoyote kuhusu jambo hilo hata kwa neno moja?!Kwa hiyo ni sahihi yale tuliyoyasema nayo ni kuwa hiyo umma umemuweka katika nafasi yake bila ya kuzidiwa nguvu wala kufanya upungufu, Mungu awawie radhi wote, na kuwa umma huo umemtanguliza mtu anayestahiki zaidi kisha anayefuatia kwa ubora. Na wamewafanya wote ni sawa sawa katika mtazamo wao.Na haya yanathibitishwa na hoja zifuatazo: Kwa hakika Ali, Mungu amuwie radhi, alipotawala baada ya kuuliwa Athumani, Mungu amuwie radhi, makundi ya Muhajirina na Maanswari yalifanya haraka kumpa baiyyi. Je, kuna mtu miongoni mwao aliyetajwa kuwa alimuomba radhi Ali kwa yale yaliyopita ya kumbaiyyi Abuu Bakri, Omari na Athumani?! Je, kuna mtu miongoni mwao aliyetubu kwa kuwa alipinga maandiko ya Uimamu wa Ali?! Au aliyesema: Kwa hakika nimekumbuka maandiko haya niliyasahau kuhusiana na jambo la Ali?! 76 – Kwa hakika Maanswari, Mungu awawie radhi, walishindana na Abuu Bakri, Mungu amuwie radhi, na wakatoa wito wa kumbaiyyi Saadi bin Ubaadati, Mungu amuwie radhi. Na Ali, Mungu amuwie radhi, alikaa nyumbani kwake, hakuwa kwa hawa wala hawa, kwa hiyo kurejea kwa Maanswari wote na kumbaiyyi Abuu Bakri hakuepukani kulikuwa kwa moja sababu zifuatazo: (1) -  Kwa kutumia nguvu.(2) - Au kwa kudhihiri haki ya ukhalifa kwa Abuu Bakri. Kwa hiyo hilo likalazimisha kumtii na kumbaiyyi.(3) - Au walifanya hivyo bila ya maana yoyote. Kwa vyovyote vile hakuna jambo la nne. Kama Mashia watasema kuwa: kwa hakika wamembaiyyi kinguvu. Huo ni uongo kwa sababu hakukuwa na vita, mapigano, kutukanana, vitisho wala silaha. Ni muhali kutishika Maanswari na wakati wao ndio wengi zaidi, wakiwa na wapanda farasi elfu mbili, na wote ni mashujaa wa jamii moja. Wamedhihirisha ushajaa wao bila kuwa na lengo lolote lingine. Nao walidumu kwa miaka minane mfululizo wakipambana na Warabu wote katika maeneo ya miji yao. Wakiyaendea mauti, wakitokezewa na vita dhidi ya Kaisari wa Roma katika vita vya Mutaa na vinginevyo. Ni muhali kutishwa na Abuu Bakri na watu wawili tu aliokuja nao. Hawategemei jamii kubwa yenye mali, kundi wala mali. Vipi watamwendea huku wakimjua kuwa yeye ni batili! Lakini kinyume chake, wamembaiyyi bila ya kusitasita wala kurefusha muda kwa kuwa wamehakikisha kuwa ni khalifa halali.   Pia ni batili kuwa wametangua kauli yao na yale waliyoyaona kuwa ni haki yao ya kummbaiyyi mtoto wa ami yao. Ni muhali kwa idadi hii kubwa kukubaliana kwa matamanio yao, juu ya kile wanachokijua kuwa ni batili bila kuwa na hofu inayowalazimisha kufanya hivyo, tena bila tamaa ya kuharakisha kupata mali au vyeo. Kisha wanasalimisha yote hayo kwa mtu asiye na jamii, mtu wa kumkinga, kizuizi, walinzi wa mlangoni, jengo lenye ulinzi, wafuasi wala mali.  Na kama yote haya yamebatilika, basi hakuna kilichobaki zaidi ya kuwa Maanswari, Allah awawie radhi, wamerejea na kumbaiyyi Abuu Bakri, Mungu amuwie radhi, kwa ushahidi wa kweli uliothibitika mbele yao kutoka kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake. Wala sio kwa jitihada zao wala dhana kama zilivyodhana zao.Ikiwa ni batili kwa Maanswari kukamata ukhalifa na kwa hiyo ukhalifa ukawatoka. Nini kilichowapelekea wao wote kuanzia wa kwanza wao hadi wa mwisho wao wakubaliane kuyapinga maneno ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, yanayohusu ukhalifa wa Ali?! Ni muhali rai zao zote ziafikiane kumsaidia aliyewadhulumu na kuwapora haki yao!!  77 – Kwa vile Abuu Bakri na Omari, Mungu awawie radhi, wamefanikiwa kumwondoa Ali, Mungu amuwie radhi, kutoka katika ukhalifa – kama wanavyodai Mashia – Je, wamepata faida gani?!Kwa nini Abuu Bakri hakumwachia madaraka mmoja wa watoto wake kama alivyofanya Ali?!Kwa nini Omari hakumwachia madaraka mmoja wa watoto wake kama alivyofanya Ali?!78 – Tumekuta kuwa Muhammad bin Abdallah bin Amru bin Athumani bin Afaani, Mungu awawie radhi, mama yake ni Fatuma binti Huseini bin Ali bin Abuu Twaalibu, Mungu awawie radhi, bibi yake ni Fatuma, Mungu amuwie radhi, na babu yake ni Athumani bin Afaani, Mungu amuwie radhi! Hapa kuna swali linalowatatiza Mashia: Je, kwa Mashia, inasihi Fatuma, Mungu amuwie radhi, awe na mjukuu aliyelaniwa?! Kwa sababu Banii Ummaya, akiwemo huyo Muhammad tuliomtaja – kwa Mashia – ni katika (Ule mti uliolaniwa katika Qur'an)!([86]) 79 – Mashia wamewakusanyia Maimamu zao Al-iswima (kukingwa na dhambi) na taqiya. Na mambo mawili hayo ni vinyume viwili havitangamani. Kwa sababu, ni nini faida ya Al-iswima kwa Maimamu wenu ikiwa hamjui ukweli wa yale wanayoyasema na kuyatenda? Muda wa kuwa tisa ya kumi ya dini yenu ni taqiya?!  Kwa vile nyinyi Mashia mnajaalia thawabu na daraja ya taqiya kua ni sawa na sala, kiasi ambacho "mwenye kuiacha taqiya ni sawa na muacha sala"([87]) "Pia tisa ya kumi ya dini yenu ni taqiya"([88]) Hakuna shaka kuwa Maimamu wenu wameifanyia kazi hiyo tisa ya kumi yote! Na hili ni kinyume na Iswima inayodaiwa!  80 – Mashia wanajipinga wenyewe kwa wenyewe pale wanapotoa ushahidi wa Uimamu wa Maimamu zao kwa kutumia hadithi ya vizito viwili (thaqalayni).([89]) Kisha tunawakuta wakiwakufurisha wale wanaokosoa uzito mdogo nao ni Ahli baiti, tofauti na wanaokosoa uzito mkubwa nao ni Qur'an. Lakini Mashia wanasema kuwa: mwenye kukosoa Qur'an ni mujitahidi aliyekosea tu wala hawamkufurishi.81 – Mashia wanadai kuwa Maswahaba wote waliritadi ispokuwa idadi ndogo sana isiyozidi watu saba (kwa makadirio makubwa). Swali: wapo wapi Ahli baiti wengine? Kama watoto wa Jafari na watoto wa Ali na wengineo…? Je, waliritadi pamoja na wale walioritadi?! Hadithi ya Mahdiyi imekuja hivi: "Lau isingebakia kwa dunia ila siku moja. Allah angeirefusha siku hiyo hadi amlete katika siku hiyo mtu mmoja miongoni mwa Ahli baiti wangu, jina lake linaafikiana na jina langu, na jina la baba yake linaafikiana na jina la baba yangu."([90]) Na Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, jina lake linajulikana nalo ni: Muhammad bin Abdullah, Rehema na amani ziwe juu yake, na Mahdiyi wa Mashia, jina lake ni Muhammad bin Al-Hassani! Huu ni utata mkubwa!Kwa ajili hii, mmoja wa masheikhe wa Kishia ametatua utata huu kwa jawabu la kufurahisha! Pale aliposema: (Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, alikuwa na wajukuu wawili, Abuu Muhammad Al-Hassani na Abuu Abdallah Al-Hassani. Sasa hoja – yaani anayesubiriwa – alipokuwa ni katika kizazi cha Al-Huseini bin Abuu Abdallah, na jina lake la kuniya lilikuwa ni Al-Huseini Abuu Abdullah, Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, akaita jina la kuniya kwa kutumia tamko la jina, kwa ajili wa mlinganisho wa jina la baba yake. Na babu akamwita kwa neno baba)!!([91])83 – kupingana katika uhai wa Mahdiyi wa Kishia anayesubiriwa:  (1) – Mama wa Mahdiyi ni nani?Je, ni mjakazi jina lake ni Narjisi au ni mjakazi jina lake ni Swaqiilu, au ni mjakazi jina lake ni Mulaikatu, au ni mjakazi jina lake ni Khamtwu au ni mjakazi jina lake ni Hakiimatu, au ni mjakazi jina lake ni Raihaanatu au Sausanu, au ni muungwana jina lake ni Mariamu?! (2) – Amezaliwa lini?Je, amezaliwa baada ya kufa kwa baba yake kwa miezi minane? Au amezaliwa kabla ya kufa kwa baba yake mnamo mwaka (252)? Au amezaliwa mwaka (256)? Au amezaliwa mwaka (257)? Au amezaliwa mwaka (258)? Au amezaliwa mwezi 8 dhul-qaedati? Au amezaliwa mwezi 8 Shab'an? Au amezaliwa mwezi 15 Ramadhani?! (3) – Vipi ilivyobebwa mimba yake na mama yake?Je, mama yake alibeba mimba yake tumboni mwake kama wanavyobeba wanawake wengine? Au aliibeba ubavuni mwake kinyume na wanawake wengine?!(4) – Je, amezaliwa kutoka katika utupu wa mama yake kama wanavyozaa wanawake wengine?  Au kutoka katika paja lake ikiwa ni kinyume na kawaida ya wanawake wengine? (5) – Alikua vipi?Imepokewa kutoka kwa Abuu Al-Hassani: (Sisi kundi la Maauswiyaai tunakua kwa siku moja sawasawa na wanavyokuwa wengine kwa juma moja)!Na kutoka kwa Abuu Al-Hassani amesema: (Kwa hakika mtoto miongoni mwetu akifikia mwezi mmoja anakuwa kama aliyefikia mwaka mmoja)!Na kutoka kwa Abuu Al-Hassani amesema: (Sisi kundi la Maimamu tunakua kwa siku moja sawa sawa na wanavyokuwa wengine kwa mwaka mmoja)!([92]) (6) – Anaishi wapi?Mashia wamesema: Yupo Twibatu, kisha wakasema: yupo katika mlima Radhwaa huko Ruuhaau, kisha wakasema: yupo Makka katika Twuwaa. kisha wakasema: yupo Saamraau!Hadi ilifikia baadhi yao walisema:(Nastaajabu, wapi ulipotulizana kwako umbali… bali, ni ardhi gani iliyokuchukua? Je, ni Radhwaa au eneo lingine? Au katika Twuwaa?... Au Yemeni katika bonde la Shamruukhu? Au katika kisiwa cha Kijani?([93])  (7) – Je, atarudi akiwa kijana au mzee?Kutoka kwa Almufadhilu amesema: nilimuuliza Aswaadiqu: Ewe bwana, je, atarudi akiwa kijana au atadhihirika na mvi zake? Akasema: (Subahana Allah, - Ametakasika Mwenyezi Mungu - je, hilo linajulikana? Atadhihiri atakavyo na sura atakayo).([94]) Katika riwaya nyingine (Atadhihiri akiwa katika sura ya ujana unaoafikiana na kijana wa miaka thelathini na miwili).([95]) Katika riwaya nyingine (Atatokea akiwa na umri wa miaka hamsini na mmoja).([96])Katika riwaya nyingine (Atadhihiri akiwa katika sura ya ujana unaoafikiana na kijana wa miaka thelathini).([97]) (8) – Ufalme wake utakuwa wa muda gani?Muhammad Swadru amesema: (nazo ni habari nyingi lakini zinatofautiana kimadhumuni kwa kiasi kikubwa hadi ikawapelekea waandishi wengi watumbukie katika kutahayarii na kuchanganyikiwa).([98]) Imesemekana: (Ni mfalme atakayekaa na sisi miaka kumi na tisa 19) na katika riwaya nyingine: (miaka saba, Allah anamrefushia mchana na usiku hadi mwaka mmoja katika miaka yake unakuwa sawa na miaka kumi. Kwa hiyo miaka ya utawala wake inakuwa ni sabini 70 kwa miaka yenu).([99])Na katika riwaya nyingine (Atakayekaimu atakuwa mfalme kwa miaka (309) kama vile walivyokaa watu wa Kahfu – pangoni – ndani ya pango lao. (9) – Muda wa kughibu (kupotea) kwake ni muda gani?  Imepokewa kutoka kwa Ali bin Abuu Twaalibu kuwa amesema: (Mahdiyi atapotea na kutakuwa na tahayari. Na katika kipindi hicho kaumu zitapotea na wengine wataongoka. Na alipoulizwa: Muda gani utakuwa wa kutahayari? Akasema: Siku sita au miezi sita au miaka sita).([100]) Na kutoka kwa Abuu Abdallah amesema: (Baina ya kutokea kwa huyo msimamizi na kuuliwa kwa nafsi isiyo na kosa ispokuwa miusiku kumi na mitano), yaani katika mwaka (140 Hijiriya)!Muhammad Swadru amesema kuhusiana na habari hii: Ni habari inayoaminika, inawezekana kuthibitishwa kihistoria – kwa hesabu za mfumo wa kitabu hiki – imepokewa na Almufiidu katika Al-Irshaadu kutoka kwa Thaalabatu bin Maymuunu kutoka kwa Shuaibu Alhaddaadu kutoka kwa Salehe bin Muyattamu Aljamaalu, na wote hawa ni watu wanaoaminiwa na ni watukufu!([101])Kwa vile hakudhihiri kama ilivyosema riwaya iliyopita! Ikaja riwaya nyingine kutoka kwa huyo huyo akisema: (Ewe Thabiti kwa hakika Allah aliliwekea wakati jambo hili kwa sabini. Alipouliwa Huseini ghadhabu za Allah kwa watu wa ardhini zilizidi akalichelewesha hadi miaka mia na arobaini: tukakusimulieni kuwa atatokea mwaka mia na arobaini (140). mkaitawanya hiyo hadithi na mkaondoa kifuniko cha pazia. Mwenyezi Mungu hajatujalia wakati baada ya jambo hilo.)([102])  Kisha ikaja riwaya nyingine ikizikadhibisha (ikisema ni za uongo) riwaya zote zilizotangulia kutoka kwa Abuu Abdallah Jafari Asswaadiqu amesema: (Wawekao wakati wamesema uongo, kwani sisi watu wa Albeiti hatupangiwi wakati).([103]) 84 – Mashia wanapokea kutoka kwa Ali, Mungu amuwie radhi, kuwa: Alipowatokea maswahiba zake akiwa amehuzunika na kuhema, alisema: (Vipi nyinyi, na zama zimeshakupotezeni, sheria za Mungu zinakwamishwa na mali zinafanywa kinyang`anyiro? Na mawalii – wapenzi wa Allah – wanafanyiwa uadui, na maadui wa Allah ndio wanafanywa watawala?) wakasema: Ewe Amiri Muuminiina kama tutaiwahi zama hiyo tufanye nini? Akasema: (Kuweni kama watu wa Issa, Amani iwe juu yake: walipasuliwa na misumeno, na kusulibiwa kwa mbao. Kufa kwa kumtii Allah Mtukufu ni bora kuliko kuishi kwa kumuasi Allah.([104]) Baada ya yote haya, ipo wapi taqiya ya Mashia?85 – Nini kilichomlazimisha Abuu Bakri, Mungu amuwie radhi, awe pamoja na Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake katika Hijra?! Lau angekuwa mnafiki – kama wasemavyo Mashia – kwa nini autoroke umma wake wa kikafiri hali ya kuwa umma wake ndio unatawala ukiwa na nguvu katika mji wa Maka?! Unafiki wake ungekuwa kwa maslahi ya kidunia. Maslahi gani aliyoyatarajia akiwa pamoja na Mtume katika muda huo? Huku Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, ni mpweke anayefukuzwa?! Vilevile, Abuu Bakri, alipatwa na majaribio ya kuuliwa na Makafiri waliokuwa hawajamsadiki! 86 – Allah Mtukufu Aliyetukuka amewasifu Maswahaba katika sehemu nyingi ndani ya kitabu chake kitukufu. Allah Mtukufu amesema: {Na utuandikie mema katika dunia hii na katika Akhera. Sisi tumerejea kwako}. Pia amesema: {Adhabu yangu nitamsibunayo nimtakaye. Na rehema yangu imeenea kila kitu. Lakini nitawaandikia khasa wanaomchamungu, na wanaotoa Zaka, na wale ambao wanaziamini Ishara zetu, Ambao kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiyesoma wala kuandika, wanayemkuta kaandikwa kwao katika Taurati na Injili, anayewaamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na anawaharimishia viovu, na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyokuwa juu yao. Basi wale waliomuamini yeye, Na wakamhishimu, Na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyoteremshwa pamoja naye – hao ndio wenye kufanikiwa.} Sura [7] Al-A‘raaf 156 – 157. Pia amesema: {Waliomwitikia Mwenyezi Mungu na Mtume baada ya kwishapatwa na majaraha – kwa waliofanya wema miongoni mwao na wakamchamungu utakuwa ujira mkubwa. Walioambiwa na watu: Kuna watu wamekukusanyikieni, waogopeni! Hayo yakawazidishia Imani, wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosha, naye ni mbora wa kutegemewa.} Sura [3] Aal-‘Imran 172 – 173.Pia amesema: {Na wakitaka kukukhadaa basi Mwenyezi Mungu atakutosheleza. Kwani Yeye ndiye aliyekuunga mkono kwa nusura yake na kwa Waumini. Na akaziunga nyoyo zao. Na lau wewe ungelitoa vyote viliomo duniani usingeliweza kuziunga nyoyo zao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaunganisha. Hakika Yeye ndiye Mtukufu Mwenye nguvu na Mwenye hikima.} Sura [8] Al-Anfaal 62 – 63.Pia amesema: {Ewe Nabii! Mwenyezi Mungu anakutoshelezea wewe na Waumini waliokufuata.} Sura [8] Al-Anfaal 64.Pia amesema: {Nyinyi mmekuwa bora ya umma waliotolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu…} Sura [3] Aal-‘Imran 110. Na aya nyingine nyingi.Mashia wanakubali kuwa Maswahaba waliamini wakati wa uhai wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, lakini wanadai kuwa Maswahaba hao hao waliritadi bada ya hapo! Ajabu ilioje! Vipi Maswahaba wote wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, wawafikiane kuritadi bila sababu baada ya kufa kwake? Kwa nini?Vipi walimnusuru Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, wakati alipokuwa na shida na matatizo, na kumtolea fidia kwa nafsi na mali zao. Kisha wanaritadi baada ya kufa kwake bila sababu?! Labda mseme kuwa kuritadi kwao ni kwa sababu ya kutawala kwa Abuu Bakri, Mungu amuwie radhi. Mtaambiwa: Kwa nini, Maswahaba wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, wawe na ijimai ya kumbaiyyi Abuu Bakri, Mungu amuwie radhi. Walikuwa wanaogopa nini kutoka kwa Abuu Bakri? Je, Abuu Bakri, Mungu amuwie radhi, alikuwa na nguvu sana na ubabe juu yao na kuwalazimisha wambaiyyi kinguvu?! Kisha kwa hakika Abuu Bakri, Mungu amuwie radhi, ni wa ukoo wa Banii Tamiimu katika Maquraishi, nao ndio idadi ndogo zaidi miongoni mwa Maquraishi. Huku wingi wa idadi miongoni mwa Maquraishi ulikuwa kwa Banii Haashimi na Banii Abduddaari na Banii Makhuzuumi.Kama Abuu Bakri hakuweza kuwalazimisha Maswahaba wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, wambaiyyi. Kwa nini hao Maswahaba, Mungu awawie radhi, wapoteze juhudi zao, imani zao, juhudi zao, mambo yao yaliyopita, dini yao na akhera yao kwa bahati ya mwingine. Naye ni Abuu Bakri, Mungu amuwie radhi?!87 – Kama Maswahaba wameritadi baada ya kufariki kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, kama mnavyodai – kwa nini waliwapiga vita wale walioritadi miongoni mwa watu wa Musailamati, Twulayhatu bin Khuwailidi, Aswadu Al-Ansaa, Sajahi na wengineo, kisha wakawarejesha katika Uislamu!? Kwa nini hawakuwasaidia? Au hawakuwaacha? Maadamu wao ni kama wao kwa kuritadi – kama mnavodai?!88 – Tabia za ulimwengu na sheria zinathibitisha kuwa Maswahaba wa Mitume ndio wafuasi bora wa dini zao. Kwa hakika lau kama watu wa kila dini wataulizwa kuhusiana na wabora miongoni mwa wafuasi wa dini hiyo wangesema: Maswahaba wa Mitume.Lau watu wa Taurati wangeulizwa kuhusu wale waliobora miongoni mwa wafuasi wa dini hiyo, wengesema ni Maswahaba wa Mussa, Amani iwe juu yake, na lau watu wa Injili wangeulizwa kuhusu wale waliobora miongoni mwa wafuasi wa dini hiyo basi wengesema Maswahaba wa Yesu, Amani iwe juu yake, na hivyo watu wa Mitume mingine. Kwa sababu Maswahaba wa Mitume wapo karibu zaidi na ufunuo na wanaufahamu kwa kina. Na ujuzi wa Maswahaba juu ya utume na Mitume, Amani ziwe juu yao, ni mkubwa na wenye kuaminika.Kwa hiyo, waonaje kwa Mtume wetu Muhammad, Rehema na amani ziwe juu yake, Mtume aliyehusishwa na Allah kwa ujumbe wa milele wenye kukusanya kila kitu. Na sheria nyepesi iliyokamilika, Mtume aliyebashiriwa kuja kwake na Manabii waliomtangulia. Amebashiriwa na vitabu vya mbinguni vilivyotangulia. Kwa madai yenu – Maswahaba zake waliomwamini, kumnusuru, kumpa nguvu na kumuheshimu kisha wakamkufuru. Kuna maana gani ya kusema ujumbe huu wa Muhammadi ndio utakaobakia? Sheria hii ya Mwenyezi Mungu mnaipa uzito gani, baada ya kuachwa na Maswahaba wa Muhammad walio mahususi, nao wakaritadi na kurejea nyuma ya visigino vyao?! Basi wale waliokuja baada yao ndio wanafaa zaidi kumkufuru na kurejea na kukhasirika kuliko wale waliotengana na watu wao na nchi zao kwa ajili ya kumnusuru Mtume, wakapigana vita dhidi ya wazee na ndugu zao, baada ya kufa kwa Mtume, wamezikomboa nchi na miji. Kwa kutumia elimu na Qur'an na Tibiyaani, kisha  kwa upanga na zana za kivita.  89 – Tumekuta kuwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, hajaifanyia kazi taqiya tena akiwa katika hali ngumu kabisa, huku Mashia – kama ilivyotangulia – wanadai kuwa: Hii taqiya ni tisa ya kumi ya dini yao! Na Maimamu zao wameitumia sana. Kwa nini hawakuwa kama babu yao amabaye ni Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake?! Pia wangekuwa kama wake zake ambao ni mamama wa waumini?!90 – Tumekuta kuwa Ali, Mungu amuwie radhi, hajawakufurisha wagomvi wake, hata Makhawariji waliompiga vita, kumuudhi na kumkufurisha. Kwa ni Mashia hawamuigi?! Mashia ndio wanaowakufurisha Maswahaba bora wa Muhammad, Rehema na amani ziwe juu yake, pia wakeze ambao ni mamama wa waumini?!91 – Kwa Mashia Ijimai pekee si hoja, ila kuwe na sababu ya kuwepo Maasumi – kama wasemavyo ([105]) – na huku ni kuweka maneno mengi. Kwa kuwa haina maana, na kama ni hivyo hakuna haja ya ijimai. 92 - Tumekuta Mashia wanawakufurisha Wazeidiyya. Pamoja na kuwa Mazeidiyya ni wafuasi wa Ahli baiti. Kwa hapa tukajua kuwa kinachotegemewe kwa Mashia ni baadhi ya Maswahaba na Salafu Wema wala si mahaba ya kuwapenda watu wa Ahli baiti kama wanavyodai.([106]) 93 – Mashia wanadai kuwa Ali anastahiki ukhalifa baada Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, kwa hadithi: "Wewe kwangu mimi ni kama nafasi ya Haruna kwa Mussa"([107]) Kisha tunakuta kuwa Haruna Hakuwa khalifa baada ya Mussa – Amani iwe juu yao! Lakini aliyekuwa khalifa wa Mussa ni Yoshua bin Nuun!94 – Mashia wamewafanya wafuasi zao watende makosa makubwa ya kuangamiza kwa madai kuwa (mapenzi ya Huseini ni wema, maasi hayadhuru kitu kukiwa na mapenzi ya Huseini). Madai haya yanakadhibishwa na Qur'an. Qur'an ambayo katika aya zake nyingi inaonya kutotenda uhalifu na makatazo kwa madai yoyote yale. Na inasisitiza kuwa {Si kwa matamanio yenu, wala matamanio ya Watu wa Kitabu! Anayefanya ubaya atalipwa kwalo, wala hatajipatia mlinzi wala wa kumnusuru, isipokuwa Mwenyezi Mungu.} Sura [4] An-Nisa’ 123.95 – Mashia wanaitakidi itikadi ya (ALBADAA), kisha wanadai kuwa Maimamu zao wanajua ya ghaibu! Je, Maimamu ni wakuu kuliko Mungu?! Vyovyote watakavyojaribu kutafsiri itikadi hii amabayo inamnasibisha Allah Mtukufu na ujinga. Habari zao nyingi zinapingana na tafsiri zao hizo.([108])96 – Historia inatueleza kuwa Mashia walikuwa wakiwanusuru maadui wa Kiislamu miongoni mwa Wayahudi, Wanasara na Washirikina katika matukio mengi. Yaliyo makuu ni: Kuporomoka kwa Baghdadi chini ya Almaghooli. Kuporomoka kwa Qudsi kwa Manasara… Je, Mwislamu wa kweli anafanya waliyoyafanya? Na anazikhalifu aya zinazokataza kuwafanya mawalii Wayahudi na Wanasara?! Je, Ali au mmoja wa watoto zake, Mungu awawie radhi, alifanya hivyo?!  97 – Tumewakuta Mashia wengi wanatumbukia makosani kuhusiana na Hassani bin Ali, Mungu amuwie radhi, na kumshtumu pamoja na kizazi chake, ingawa ni moja wa Maimamu zao, na ni miongoni mwa Ahli Baiti.([109])  98 – Mwenye kuwatafakari Mashia atakuta madhehebu yao yamegawanyika sana. Na wanapingana na kukufurishana sana wao kwa wao kwa nyakati zilizokaribiana. Na mfano wa wazi kabisa juu ya hilo ni: Sheikh wao Ahmadi Al-Ahsaaiyyu ameanzisha kikundi kilichokuja kujulikana kwa jina la Al-Shaukhiyatu, kisha mwanafunzi wake ambaye ni Kazim Alrashtiy akaja na kuanzisha kikundi cha Alkaashafiyyatu. Kisha mwanafunzi wake ambaye ni Muhammad Kariim Khaani akaanzisha kikundi cha Alkarmakhaaiyyatu. Na mwanafunzi wake mwingine Quratu Ayuni, alianzisha kikundi kilichojulikana kwa jina la Alquratiyyatu. Na Mirza Ali Shiirazi alianzisha kikundi cha Al-Baabawiyyatu. Na Mirza Huseini Ali alianzisha kikundi cha Al-Bahaaiyyatu. Tazama namna vilivyochimbuka vikundi vyote hivi vya Kishia katika zama moja, na nyakati zinazokaribiana. Amesema kweli Allah Mtukufu aliyesema: {…wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia yake...} Sura [6] Al-An‘aam 153.99 – Tumekuta watu wa fitina waliochupa mipaka, wakati walipoizingira nyumba ya Athumani bin Afaani, Mungu amuwie radhi, Ali, Mungu amuwie radhi, aliihami nyumba ya Athumani na kuwafukuza watu hao watoke. Ali aliwatoa watoto zake Hassani na Huseini na mtoto wa ndugu yake Abdallah bin Jafari.([110]) Lakini Athumani, Mungu amuwie radhi, aliazimia kuwataka watu waache silaha zao na wabakie majumbani mwao. Hili linajulisha kubatilika kwa madai ya Mashia eti Ali na Athumani wanabughuziana na kufanyiana uadui.100 - Omari, Mungu amuwie radhi, alikuwa anapokea ushauri wa Ali, Mungu amuwie radhi, katika mambo mengi na hiyo ni kwa makubaliano ya Masunni na Mashia.([111]) Lau kama Omari angekuwa dhalimu – kama mnavyodai – hasingetaka ushauri kwa watu wa haki, kwa sababu dhalimu hataki haki!101 – Imethibitika kwa maafikiano kuwa, Salmaani Alfaarisiyyu, Mungu amuwie radhi, alikuwa amiri wa Almadaaini katika zama za ukhalifa wa Omari.([112]) Na Ammaaru bin Yaasiru alikuwa amiri wa Kuufatu.([113]) Na wawili hao ni miongoni mwa wale wanaodaiwa na Mashia kwamba walikuwa wanamnusuru Ali na Mashia zake, Mungu amuwie radhi. Lau Omari angekuwa ni murtadi au dhalimu mwenye kuchupa mipaka dhidi ya Ali kwa mtazamo wao, wasingekubali hilo. Vipi wasaidie dhuluma na walioritadi?! Na Allah anasema: {Wala msiwategemee wanaodhulumu, usijeukakuguseni Moto…} Sura [11] Hud 113.102 – Mashia wanadai kuwa kwa hakika Maimamu zao wamezuiwa na makosa (hawakosei). Na kuwa Mahdi wao yupo, anawasiliana na baadhi ya maulamaa wa madhehebu yao. Imesemekana hao maulamaa wapo therathini. Je, baada ya madai haya, vipi kuwe na khitilafu na kutofautiana katika madhehebu yao, kiasi ambacho imefikia kuwa hakuna kundi miongoni mwa makundi yote linalolingana na Mashia. Hadi inafikia kuwa kila mujitahidi au tegemeo miongoni mwa maulamaa wa madhehebu yao ana madhehebu yake?! Ingawa wanadai kuwa ni wajibu kuwepo Imamu anayesimamisha hoja kwa watu. Naye ni Mahdiyyu anayesubiriwa. Sasa kwa nini Mashia wawe ni miongoni mwa watu wenye kutofautiana sana duniani licha ya kuwepo Imamu wao na wasimamizi wake na kuwasiliana naye?! Kisha mnasema, Majlisiyyu ametaja hadithi ya kuwa Imamu aliyeghibu haonekani, na atakayedai kuwa amemuona Imamu Mahdiyyu ameongopa kisha tunasoma kuwa maulamaa wenu wamemuona Imamu Mahdiyyu mara kibao.  103 – Mashia wanaambiwa: Nyinyi mnasema kuwa haisihi kuwa na zama isiyo na msimamizi wa Allah kwa hoja naye ni Imamu. Sasa kama taqiya – iliyopo kwenu – ni tisa ya kumi ya dini. Na hiyo taqiya ni nzuri kwa Imamu, nayo ni sunna, ubora na fadhila, kwa kuwa Imamu ni mcha Mungu kuliko watu wengine, sasa vipi itatimia hoja ya Imamu huyo kwa viumbe?! (Wakati anafanya taqiya)?104 – Mashia wanadai kuwa: kuwajua Maimamu ni sharti la kusihi kwa imani. Sasa watasemaje kwa wale waliokufa kabla ya kukamilika Maimamu kumi na wawili?! Jawabu ni nini kama ikiwa mfu ni Imamu?! Wakati baadhi ya Maimamu zao walikuwa hawajui nani atakuwa Imamu baada yake! Kwa nini amejaalia hilo liwe sharti la imani?!105 – Mwenye "Nahju Albalaagha" anasimulia kuwa Ali alipofikiwa na habari kuwa Maanswari wanadai kwamba Uimamu ni wa kwao alisema: "Je, mmewapa hoja ya kuwa Mtume wa Allah, Rehema na amani ziwe juu yake, amewahusia kuwa wafanyiwe ihsani na makosa yao yasamehewe? Wakasema: katika hili kuna hoja gani kwao? Akasema: Lau Uimamu ungekuwa ni wa kwao kusingekuwa na wasia kuwahusu wao"([114]) Mashia wanaambiwa: Pia Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, amewahusia Ahli baiti kwa kauli yake: "Nakukumbusheni Allah juu ya Ahli baiti wangu". Lau Uimamu ungekuwa ni haki mahususi kwao pasi na wengineo wasingehusiwa?!  106 – Lau kama utaambiwa kuwa kuna mtu anaongoza naye ni muumini, mwema, mcha Mungu anawatawala watu ambao baadhi yao ni waumini na wengine ni wanafiki. Na kwa fadhila za Allah kwa mtu huyo, anawajua watu wanafiki kwa kauli zao. Pamoja na haya, Mtu huyo aliwatenga watu wema, kisha akawachagua wanafiki na kuwapa vyeo vya kuongoza na kuwatawala watu wakati wa uhai wake. Pia alijikurubisha na hao wanafiki na kuwafanya baadhi yao ni wakweze na akafa akiwa amewaridhia. Je, unasema nini kuhusu mtu huyu?!Basi haya ndio wanayoyaitakidi Mashia kwa Mtume wa Allah, Rehema na amani ziwe juu yake! 107 – Mwanazuoni wa Kishia Alhurru Al-Aamiliyyu anasimulia kutoka kwa Abuu Jafari katika kutafsiri kauli ya Allah Mtukufu: {…Wala msiwaweke wanawake makafiri katika kifungo cha ndoa zenu…} Sura [60] Al-Mumtahinah 10. Amesema: Mwenye kuwa na mwanamke kafiri, yaani aliye katika dini isiyo Uislamu. Na huyo mwanamume ni Mwislamu. Amtangazie Uislamu huyo mkewe. Akiukubali basi huyo ni mkewe na akiukataa basi huyo yupo huru si mkewe. Allah amekataza kumuweka mwanamke kafiri katika kifungo cha ndoa.([115])Mama wa waumini Aisha, Mungu amuwie radhi, lau kama angekuwa kafiri aliyeritadi – Allah atukinge na hilo – kama wanavyosema Mashia, ingekuwa ni wajibu kumtaliki kwa mujibu wa kitabu cha Allah. Au kama Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, hakujua unafiki wake na kuritadi kwake. Na Mashia ndio waliojua hilo! 108 – Kundi la Khatwaabiyyatu miongoni mwa Mashia linafuata mwelekeo kuwa Imamu baada Jafari Swaadiqu ni mwanawe Ismaili. Wakajibiwa na maulamaa wa Kishia: "Ismaili alikufa kabla ya Abuu Abdallah, juu yake amani, na maiti hawi khalifa wa watu hai…" hadi mwisho.([116]) Mashia wanaambiwa: Nyinyi mnatoa hoja ya utawala wa Ali kwa kwa kutumia kauli ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake: "Wewe kwangu mimi una nafasi ya Haruna kwa Mussa" Ni jambo linalojulikana kuwa Haruna alikufa kabla ya Mussa – Amani iwe juu yao! na maiti hawi khalifa wa watu hai kwa kukiri kwenu!109 – Mashia wanatoa hoja ya kuthibitisha Uimamu wa Maimamu zao kumi na wawili kwa kutumia hadithi: "Amri haitoacha kuwa ni azizu hadi kwa makhalifa kumi na wawili. Wote ni Wakuraishi" na katika riwaya nyingine "Watakuwa maamiri kumi na wawili" na katika riwaya nyingine "Amri ya watu haitoacha kuendelea muda wa kuwa wametawaliwa na watu kumi na wawili"([117])Inasemwa: Hiyo hadithi kwa mapokeo yake yote, ipo wazi kuwa hao kumi na wawili watakuwa ni "Makhalifa" na "Maamiri" kwa watu. Ni jambo linalojulikana kuwa Maimamu wa Kishia hakuna aliyetawalia ukhalifa na uamiri ukitoa Ali na mwanawe Hassani. Kwa hiyo hii hadithi ipo katika bonde na Mashia wapo katika bonde lingine. (yaani ipo mbali nao). Hizo riwaya hazijawataja hao makhalifa hata mmoja wao!  110 - Mashia wanadai kuwa: Kama inavyojulikana – ya kwamba Maswahaba waliritadi baada ya kufa kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, ispokuwa wachache tu. Wanaambiwa mwenye kuritadi kwa hakika anaritadi kwa shubha au matamanio ya nafsi. Ni jambo linalojulikana kuwa Shubuhaatu za mwanzoni mwa Uislamu zilikuwa zina nguvu sana. Wale waliokuwa imani zao kama milima wakati Uislamu ulipokuwa dhaifu. Vipi itakuwa imani yao baada ya kudhihiri bendera ya Uislamu na kuenea kwa beramu (bendera) zake?!Ama matamanio ya nafsi: Wale waliotoka majumbani mwao na kuacha mali zao, na wakaacha utukufu kwa ajili mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Kwa kutii kwao wala sio kwa kulazimishwa, vipi wadhaniwe kuwa wameritadi kwa ajili ya matamanio ya nafsi, waliyokwishayaacha?! Huku tukijua kuwa kuritadi walikonasibishwa nako ni katika nguzo muhimu sana kwa Mashia nayo ni Uimamu.111 – Mashia wanaitakidi kuwa Maswahaba wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, si waadilifu. Lakini tunakuta katika vitabu vyao, mapokeo yanayojulisha uadilifu huu bila ya shaka! Miongoni mwa hizo ni zile zilizopokewa kutoka kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, ya kuwa amechumbia katika Hija ya kuaga huku akisema: "Allah anamnawirisha mja aliyesikia maneno yangu na kuyatia akilini, kisha akayafikisha kwa wale wasiyoyasikia…"([118]) Na kama Maswahaba si waadilifu vipi Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, ampe yoyote miongoni mwao, amana ya kufikisha maneno yake kwa wasioyasikia?! 112 - Mashia mmoja aliulizwa: Hivi Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, hakutulingania tuchague mke mwema? Pia tujitwalie wakwe wakarimu miongoni mwa watu?Akajibu: Ndio ametuamrisha hivyo, bila shaka yoyote.Akaambiwa: Je, wewe mwenyewe unaridhia kuwa na mkwe mtoto wa zinaa?Akasema: Najikinga kwa Mwenyezi Mungu na hilo!Akaambiwa: Ahaa, nyinyi mnadai – uongo – kuwa Omari bin Alkhattwaabu, Mungu amuwie radhi, kuwa yeye ni mtoto wa mwanamke mzinifu jina lake ni (Swuhaaku)!([119]) Mwanazuoni wenu, Niimatu Llaahi Aljazaairiyyu anadai kwa uovu kabisa kuwa Omari alikuwa hatulii ispokuwa kwa maji ya wanamume ([120]) – Mungu atukinge. Pia mnadai kuwa binti wa Omari ambaye ni Hafsa alikuwa mnafiki na ni khabithi kama baba yake, vilevile ni kafiri!Je, waonelea kuwa, Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, amemfanya mkwe mtoto wa zinaa?!Au, je, Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, anaridhia awe na mke fasidi mnafiki?!Wallah kwa hakika nyinyi mnamzushia Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, na Maswahaba zake, kisha mnaridhia wawe na vitu ambavyo nyinyi wenyewe hamridhiki kuwa navyo. 113 – Ikiwa wanafiki na wanaoritadi miongoni mwa Maswahaba wamefikia wingi huu wanaoudai Mashia, uislamu ulienea vipi?! Wafarsi (Wairani) na Warumi tawala zao ziliporomoka vipi? Vipi ilikombolewa Baiti Maqdisu?! 114 – Mwanazuoni wa Kishia, Muhammad Kaashifu Alghutwaau anasema kumhusu Ali, Mungu Amauwie radhi: "Pale Ali alipowaona makhalifa wawili wa kabla yake – yaani Abuu Bakri na Omari – wakitoa juhudi kubwa sana katika kueneza neno la kumpwekesha Mungu, na kuandaa majeshi, na kupanua maeneo yaliyokombolewa, hawakujipendelea wala hawakufanya ukandamizaji, kwa hiyo akawabaiyyi na kuwapa amani"([121])Kwa hiyo: Abuu Bakri na Omari walieneza neno la kumpwekesha Mungu, na kuandaa majeshi kwa ajili ya njia ya Allah, na kukomboa miji – kwa kukiri kwa mmoja wa wanazuoni mkubwa wa Kishia – kwa hiyo, kwa nini wanawatuhumu kuwa wao ndio vichwa vya ukafiri, unafiki na kuritadi?!  Kupingana gani huku?!115 – Mashia wanatoa ushahidi wa kuritadi kwa Maswahaba baada ya kufa kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, kwa kutumia hadithi: "Itatokea kwa watu ninaowajua na wanaonijua, wanafukuzwa kutoka katika hodhi, nami nitasema: Maswahaba wangu! Maswahaba wangu!  Itasemwa: kwa hakika wewe hujui walichokizusha baada yako"([122]) Mashia wanaambiwa kuwa: hadithi hiyo ni (Aamu) ya wote wala hajatajwa yoyote pasi na mwingine, hakuvuliwa Amaaru bin Yaasiri, wala Almikdadi bin Al-As`wadu wala Abuu Dhari wala Salmaanu Alfaarisiyyu miongoni mwa wale wasioritadi kwa mtazamo wa Kishia! Pia Ali bin Abuu Twaalibu mwenyewe hakuvuliwa! Kwa nini wameihusisha kwa baadhi pasi na wengine?! Kwa hakika kila mwenye chuki moyoni mwake dhidi ya yeyote miongoni mwa Maswahaba anaweza kudai kuwa hadithi hii inamuelezea Swahaba huyo!  116 – Maliki bin Al-Ashtaru mmoja wa wafuasi wakubwa wa Ali, Mungu amuwie radhi, naye ni miongoni mwa wanaoadhimishwa na Mashia anasema: "Enyi watu, hakika Allah Mtukufu Aliyetukuka amekuleteeni Mtume Muhammad, Rehema na amani ziwe juu yake, akiwa ni mbashiri na muonyaji. Na amemteremshia kitabu, ndani yake kumefafanuliwa halali, haramu, faradhi na sunna. Kisha akamchukua kwake akiwa ameshatekeleza yale yaliyompasa. Kisha Allah akamuweka Abuu Bakri awe khalifa wa watu, naye akaenenda kwa mwenendo wa sunna ya Mtume, na Abuu Bakri akamuweka Omari naye akaenenda mwendo kama huo."([123]) Huyu Maliki bin Al-Ashtaru anawasifu Abuu Bakri na Omari kwa yale wanayostahiki. Pamoja na hayo kwa nini, Mashia – Mungu awaongoze – wanajitia upofu na hawaoni sifa hizi wala hawazitaji katika vikao vyao na Huseiniyaati zao ambazo haziachi kuwajeruhi watu wawili hao!117 – Ibni Hazmi anasema kuhusiana na Ali, Mungu amuwie radhi, akiwalazimisha Mashia – kwamba "Ali alimbaiyyi Abuu Bakri baada miezi sita ya kuchelewa kumbaiyyi (na hili) haliepukiki kwa lazima kuwe na moja ya pande mbili: Imma Ali awe amepatia katika kuchelewa kwake na amekosea pale alimpombaiyyi. Au Ali awe amepatia katika kumbaiyyi kwake na amekosea pale alipochelewa kumbaiyyi!"([124])118 – Kama Mashia wataambiwa: Kwa nini Ali, Mungu amuwie radhi, alinyamaza na kuacha kutetea ukhalifa baada ya kufa kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake – na ukhalifa kama wanavyodai Mashia – umeandikwa uwe wa Ali. Wakisema; Kwa sababu Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, amemuhusia asiutumbukize umma katika fitina wala kunyanyuliana mapanga baada ya Mtume! Wataambiwa: Kwa nini mapanga yalinyanyuliwa kwa watu wa Jamali na Swaffaini?! Katika vita hivyo walikufa maelfu ya Waislamu?! Je, nani anastahiki upanga? Je, dhalimu wa kwanza, au wa nne au wa kumi… nk?! 119 – Mashia hawataji tofauti kubwa iliyopo baina ya Mitume na Maimamu, hadi Shehe wao Almajlisiyyu alisema kuhusiana na Uimamu: "Wala hatujui upande wa kutosifika kwao kiutume ispokuwa kwa kumchunga Mtume wa mwisho. Wala haiingii akilini mwetu tofauti kati ya Utume na Uimamu."([125])Swali: Kama ni hivyo, ni nini umuhimu wa itikadi ya Mtume wa mwisho?! Kama kazi na mambo yanayowahusu Mitume pasi na watu wengine yakiwemo kwa maasumiina, kufikisha ujumbe kutoka kwa Allah, kufanya miujiza na mengineyo hayajasimama kwa kufa kwa Mtume wa mwisho Muhammad, Rehema na amani ziwe juu yake, lakini yanaendelea baada yake kwa watu kumi na wawili?! 120 – Mashia wanadai kuwa: Wajibu wa kuwasimika Maimamu unarejea katika msingi wa "Upole."([126]) Jambo la kushangaza, ni kwamba Imamu wao wa kumi na mbili amejificha akiwa mdogo wala hajatokea hadi leo! "Upole" gani huo kwa Waislamu kwa kusimikwa kwake Uimamu?! 121 – Mashia wanadai kuwa: Maimamu wao ni maasumiina.([127]) Kwa hakika yamepokewa kwa makubaliano yale yanayopingana na hili. Chukua mfano:          (A) – Hassani bin Ali alikuwa anamkhalifu baba yake Ambaye ni Ali pale alipotoka kupambana na wanaotaka haki ya damu ya Athumani. Mungu amuwie radhi. Hapana shaka kuwa mmoja wa wawili hao amepatia na mwingine amekosea. Na wote wawili ni Maimamu walio maasumu kwa Mashia!(B) – Huseini bin Ali alimkhalifu Hassani nduguye katika kadhia ya suluhu na Muawiya, Mungu amuwie radhi. Hapana shaka kuwa mmoja wa wawili hao amepatia na mwingine amekosea. Na wote wawili ni Maimamu walio maasumu kwa Mashia!(C) – Baadhi ya vitabu vya Kishia vimesimulia kauli ya Ali: "Msitosheke na maneno yangu kuwa ni haki, au ushauri wa uadilifu, kwa hakika mimi si mwenye kusalimika na kukosea."([128]).122 – Mashia wa zama hizi wameshambulia sana wanazuoni wa Kisunni katika miji ya Maka na Madina kwa sababu ya fatuwa zao za kujuzisha kutaka msaada kwa makafiri "kukiwa na dharura" ili kupambana na wachafuzi na walioritadi. Kisha tumekuta kuwa shehe wao mashuhuri Ibnu Almutwaharu Alhuliyyu ananukuu katika kitabu chake "Muntahaa Attwalabi fii Tahqiiki Almadh-habi"([129]) ananukuu ijimai ya Mashia – ispokuwa shehe wao Attuusiyyu – kuwa inajuzu kuwataka msaada "Ahli Dhimmati katika kuwapiga vita waliochupa mipaka"!! Eeh! Kujipinga gani huku?!123 – Miongoni mwa misingi ya Mashia ni kuwa Uimamu unathibiti kwa mwenye kudai kuwa ni Imamu miongoni mwa watu wa Ahli baiti kisha akadhirisha mambo ya kinyume na kawaida yanayojulisha ukweli wake. Na Mashia hawakuthibitisha Uimamu wa Zaidi bin Ali ijapokuwa amedai kuwa yeye ni Imamu, na mkabala wake wamethibitisha Uimamu wa Mahdi wao aliyeghibu na ambaye hajadai kuwa yeye ni Imamu wala hajadhihirisha kitu kwa kughibu kwake akiwa mdogo – kama wanavyoitakidi.124 – Iliposhuka kauli ya Allah Mtukufu {Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mzirudishe amana kwa wenyewe…} Sura [4] An-Nisaa’ 58. Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, aliwaita Banii Shaibatu na akawapa ufunguo wa Kaaba na akasema: "Uchukueni enyi banii Twalhatu uwe kwenu milele na milele hadi siku ya Kiama, hatokunyang`anyeni ispokuwa mtu dhalimu"([130]) Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, anasema haya katika jambo ambalo halihusu kingine ispokuwa utumishi wa Kaaba.Kwa nini hakusema maneno kama hayo katika jambo la ukhalifa wa Ali? Nalo ni jambo muhimu kwa Waislamu wote na lina maslahi ya wengi?!125 – Mashia wamezusha hadithi isemayo: "Allah amemlaani yule asiyeshiriki katika jeshi la Usama."([131]) Wanakusudia kumlaani Omari, Mungu amuwie radhi! Na imewapita kuwa jambo hilo linawalazimu wao mambo mawili:(A) – Ali awe ameshiriki. Na huku ni kiukiri kwao Uimamu wa Abuu Bakri. Kwa sababu Ali ameridhia kuamrishwa na Amiri aliyesimikwa na Abuu Bakri!(B) – Au waseme kuwa Ali hakushiriki katika jeshi hilo, na hapo inampata kile walichokiongopa!126 – Mashia wanadai kuwa Ali, Mungu amuwie radhi, ana nakala ya Qur'an iliyopangwa kulingana na kuteremka kwake! Patasemwa: Ali, Mungu amuwie radhi, alitawala ukhalifa baada ya Athumani, Mungu amuwie radhi, kwa nini hakuutoa huo msahafu uliokamili wenye kusalimika?! Kwa vile misahafu yetu ya sasa ni ile ilipokewa kutokana na riwaya za Ali, Mungu amuwie radhi, wala haijapangwa kulingana na kuteremka kwa Qur'an.Mashia wanadai kuwapenda Ahli Baiti na kizazi cha Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, lakini sisi tunakuta kwa Mashia mambo yanayopingana na hayo mapenzi. Kiasi ambacho wamekanusha nasaba za baadhi ya hicho kizazi. Kama Rukia na Ummu Kulthuumi mabinti wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake! Na Abbasi amabaye ni ami wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, walimtoa pamoja na wanawe wote. Na zuberi bin Swafiyyatu shangazi wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake. Pia Mashia hawawathamini sana baadhi ya watoto wa Fatuma, Mungu amuwie radhi, kama Zaidi bin Ali, na mwanawe Yahya, Ibrahimu na Jafari watoto wa Mussa Alkaazimu. Mashia wanawatukana Jafari bin Ali ndugu wa Imamu wao Hassani Al-Askariyu. Na wanaitakidi kuwa Hassani bin Hassani (Almuthannaa), na mwanawe Abdallah (Almahdhu), na mwanawe Muhammad (Annafsu Azzakiyatu) waliritadi! Na hivyo hivyo, Mashia wameitakidi kuhusu Ibrahimu bin Abdallah, Zakariya bin Muhammad Albaaqiru, Muhammad bin Abdallah bin Huseini bin Hassani, Muhammad bin Qaasimu bin Huseini na Yahya bin Omari… nk. Madai ya kuwapenda Ahli baiti yapo wapi?! Na hilo linashuhudiwa na maneno ya mmoja wao: "Banii Hassani bin Ali wengine walikuwa na matendo mabaya wala hayachukuliwi kuwa ni taqiya."([132]) Pia kuna makubwa kuliko haya na mabaya zaidi.128 – Kwa hakika Mashia wanawakufurisha Ahli baiti wote wa karne ya mwanzo!! Pale ilipokuja katika habari na vyanzo vyao vya kutegemewa: ya kwamba watu wa baada ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake waliritadi ispokuwa watatu tu (Salamani na Abuu Dharri na Mikidadi) na baadhi ya Mashia wanawafikisha watu saba. Katika saba hao hakuna hata Ahlu baiti mmoja)([133]) Kwa hiyo wamewahukumu wote kuwa ni makafiri na wameritadi – Mungu atukinge. 129 – Hassani, Mungu amuwie radhi, – licha ya wingi wa wafuasi wake – alisamehe ukhalifa kwa Muawiya, Mungu amuwie radhi, wakati ambapo Huseini nduguye, Mungu amuwie radhi, – licha ya uchache wa wafuasi wake – alipambana na Yazidu bin Muawiya na kumtokea. Na wote wawili – Hassani na Huseini – ni Maimamu maasumu kwa Mashia! Kama kitendo cha Hassani ni haki na ni sawasawa kusamehe pamoja na kuwepo wafuasi, basi kitendo cha Huseini cha kutoka bila ya wafuasi ni batili. Na kinyume chake ni sahihi! Pia hakika Mashia wameweka wazi kuwakufurisha baadhi ya Ahli baiti! Kama Abbasi ami wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake. Waliomdaia kuwa: Kauli ya Allah Mtukufu imeshushwa kwa ajili yake: {Na aliyekuwa hapa kipofu, basi atakuwa kipofu Akhera, na atakuwa aliyeipotea zaidi Njia.} Sura [17] Al-Isra’ 72.[134]Pia mtoto wake ambaye ni Ibni Abbasi mtaalamu wa umma na mfasiri wa Qur'an. Katika Alkaafii yamekuja yale yanayokusanya kumkufurisha na kuwa yeye ni mjinga mpumbavu wa akili!([135])Katika Rijaalu Alkashiyyu: "Ewe Mola walaani wanangu wawili, fulani na fulani, watie upofu macho yao kama zilivyopofuka nyoyo zao…"!([136]) na haya yamefafanuliwa na shehe wao Hassani Almustafawiyyu aliposema: "Wawili hao ni Abdallah bin Abbasi na Ubaidullah bin Abbasi"([137])Pia mabinti wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake – ispokuwa Fatuma – wamefikwa na chuki za Mashia, lakini pia baadhi ya Mashia walikanusha kuwa hao si mabinti wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake!([138]) Yapo wapi mahaba yanayodaiwa kwa Ahli baiti?!130 – Katika zama za ukhalifa wa Abuu Bakri, Mungu amuwie radhi, – Ali, Mungu amuwie radhi,  alishiriki katika vita vya walioritadi, na akajitwalia mjakazi miongoni mwa mateka wa (Banii Haniifatu), baadaye akamzalia mtoto aitwaye (Muhammad bin Alhanafiyyati). Na hili linalazimisha kwamba Ali haoni kama utawala wa Abuu Bakri ni batili. Na kama si hivyo, basi kilichojengwa juu ya batili nacho ni batili.131 – Maneno yaliyonukuliwa kutoka kwa Jafari Asswaadiqu yanatofautiana katika mambo mengi. Kwa mfano hutapata jambo – la kifiqihi – ispokuwa litakuwa na kauli mbili au zaidi zinazopingana. Mfano: Kisima kilichoingiwa na najisi, mara amesema kuwa kisima ni bahari hakinajisiki na kitu, kisha akasema mara nyingine, maji yake yote yanatolewa. Na mara nyingine akasema, zinaondoshwa kutoka katika kisma hicho ndoo saba au sita. Na mmoja wa wanazuoni wa Kishia alipoulizwa: kunatokeka vipi katika kupingana kama huku? Akasema: mwenye kujitahidi anajitahidi baina ya kauli hizi na anaitia nguvu kauli moja na kauli nyingine anazichukulia kuwa ni "taqiya"! Akaambiwa: Je, kama mujitahidi mwingine akajitahidi na kuipa nguvu kauli isiyo ile iliyotiwa nguvu na mujitahidi wa kwanza, aseme nini kwa kauli za  mujitahidi mwingine? Akasema: Anasema kitu hicho hicho, ya kwamba hiyo ni taqiya! Akaambiwa: Je, kama yatapotea madhehebu ya Jafari Asswaadiqu!! Kwa sababu hakuna jambo alilonasibishwa nalo ispokuwa linategemewa kuwa ni taqiya, kwani hakuna mafungamo ya kupambanua baina ya yale ya taqiya na yale yasiyo ya taqiya! 132 – Vitabu vya hadithi vinavyotegemewa kwa Mashia ni: "Alwasaailu" cha Alhurru Al-Aamiliyyu, aliyekufa mwaka 1104 Hijiriya, "Albihaaru" cha Almajlisiyyu aliyekufa mwaka 1111 Hijiriya na "Mustadraku Alwasaailu" cha Atwabrisiyyu aliyekufa mwaka 1320 Hijiriya vyote ni vya mwishoni! Ikiwa wamekusanya hadithi hizo kwa njia ya sanadi na mapokezi vipi akili iamini mapokezi ambayo hayakusajiliwa kwa muda mrefu wa kipindi cha karne kumi na moja au kumi na tatu?! 133 – Kuna riwaya na hadithi nyingi zilizopo katika vitabu vya Kishia kutoka kwa Ahli Baiti zinazoafikiana na zile zilizopo kwa Masunni. Sawa sawa kiitikadi na kukanusha bidaa au mengineyo. Lakini Mashia wanazitoa kutoka katika udhahiri wake kwa kuwa haziafikiani na matamanio yao kwa madai ya kuwa hizo ni taqiya!134 – Mwenye kitabu "Nahju Albalaagha" – nacho ni miongoni mwa vitabu tegemeo kwa Mashia – ananukuu namna Ali alivyomsifu Abuu Bakri na Omari, Mungu awawie radhi wote. Mfano aliposema kuhusu Abuu Bakri "Dhahabu safi, nguo yenye dosari ndogo, heri zake zimepatia na shari zake zimepita, ametekeleza twaa ya Allah, na kumcha kwa haki."([139]) Mashia wanatahayari kwa sifa kama hizi zinazokhalifu itikadi zao za kuwatia dosari Maswahaba. Na wanazibebesha kauli hizi "utaqiya"!! Na hakika si jinginelo, Ali alisema maneno kama hayo kwa ajili ya kuwarekebisha wale wanaoitakidi kuwa ukhalifa wa Mashehe wawili ni sahihi pia kuzivutia nyoyo zao. Yaani Ali alitaka kuwahadaa Maswahaba! Hili linawalazimisha Mashia kuwa Ali alikuwa mnafiki muoga anayedhihirisha yale anayoyaficha. Na hili linatofautiana na yale wanayoyasimulia kuhusu Ali, kwamba yeye ni shujaa wa kusema haki... nk. 135 – Mashia wanadai Umaasumu wa Maimamu zao – kama inavyojulikana – na hili limewatatiza Mashia wengi kwenye riwaya nyingi zenye kusema Maimamu ni kama watu wengine, inajuzu kwao kupatwa na kusahau na kukosea…, hadi mwanazuoni wa Kishia Almajlisiyyu amekiri kuwa: "Mambo yanatatiza mno, kwa sababu ya ushahidi wa habari na aya nyingi zinazojulisha kutokea kwa kusahau kwa Maimamu…"([140]) 136 – Hassani Al-Askariyyu Imamu wa Kumi na moja wa Kishia amekufa bila ya kuacha mtoto (wa kiume), na ili nguzo za madhehebu ya Shia Imamiya isiporomoke jamaa mmoja jina lake ni "Athumani bin Saidi" amedai kuwa Al-Askariyyu ana mtoto wa kiume aliyejificha akiwa na umri wa miaka mine. Na huyo mtoto ndio wakili wake.Ajabu ilioje! Kwa Mashia! Wanadai kuwa wao hawakubali ispokuwa kauli ya maasumu. Haya! Hapa wanakubali madai ya mtu mmoja asiye maasumu katika jambo la itikadi yao muhimu sana!!137 – Mashia wanamshambulia Marwani bin Alhakamu na kumpachika kila ovu. Kisha wanajipinga na kusimulia katika vitabu vyao: Ya kuwa Hassani na Huseini, Mungu awawie radhi, walikuwa wakisali nyuma yake!([141])Ajabu ni kwamba huyu Muawiya bin Marwani amemuoa mjane wa mtoto wa Ali, mungu amuwie radhi!! Kama walivyoeleza watu wa nasaba.([142]) Pia Zainabu binti Hassani "Almuthanaa" Aliolewa na mjukuu wa Marwani: Walidi bin Abdilmaliki.([143]) Pia Walidi alimuoa: Nafisa binti Zaidi bin Hassani bin Ali.([144])138 – Mashia katika visa vyao vingi juu ya Mahdi aliyeghibu – wanadai ya kwamba huyo Mahdi alipozaliwa "Ndege kutoka angani walimteremkia na kupangusa mabawa yao katika kichwa na uso na sehemu nyingine za mwili wake kisha wakaruka! Alipoulizwa baba yake alicheka na kusema: Hao ni malaika wa mbinguni wameshuka kumbariki mtoto huyu, nao ni walinzi wake atakapotoka."([145]) Swali: Maadamu Malaika ndio maanswari wake, kwa nini kuwe na hofu na kuingia katika Sirdabu?!139 – Mashia wameweka shuruti kadhaa kwa Imamu: Miongoni mwazo: Awe mtoto mkubwa kwa baba yake, asioshwe ispokuwa na Imamu, na Guo la Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, liwe linamtosha, awe mjuzi kuliko watu wote, asipatwe na janaba, wala haoti, na anajua ghaibu! nk. Lakini – baadaye – wametumbukia katika tatizo kwa masharti haya!! Kwa sababu tumekuta kuwa baadhi ya Maimamu hawakuwa wakubwa kuliko ndugu zao, kama Mussa Alkaazimu na Alhassani Al-Askariyyi. Na baadhi yao hawakuoshwa na Imamu, kama Ali Ridhwaa hakuoshwa na mwanawe Muhammad Aljawaadi kwani umri wake hakufikia miaka minane kwa wakati huo. Vilevile Mussa Alkaazimu hakuoshwa na mwanawe ambaye ni Ali Ridhwaa kwa kuwa alijificha kwa wakati huo. Pia Huseini bin Ali hakuoshwa na mwanawe Ali Zeini Al-Aabidiina kwa kuwa alikuwa kitandani (mgonjwa) vilevile kwa kuzuiwa na maaskari wa Ibni Ziyaadi wasifanye hilo.Na baadhi ya Maimamu Guo la Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, haliwatoshi, mfano: Muhammad Al-Jawaadi ambaye hakuvuka umri wa miaka minane wakati anakufa baba yake. Pia mwanawe amabaye ni Ali bin Muhammad Ambaye alikufa akiwa mdogo. Na baadhi ya Maimamu hawakuwa wajuzi kuliko watu wote. Kama wale waliokuwa watoto. Na baadhi yao, maandiko yamekuja na kuwahusu – miongoni mwa habari za Kishia – kwamba anaota na kupatwa na janaba. Kama Ali na watoto zake wawili Hassani na Huseini, Mungu awawie radhi, pale waliposimulia kuwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Si halali kwa yoyote awe na janaba katika msikiti huu ispokuwa mimi, Ali, Fatuma, Hassani na Huseini."([146]) Ama elimu ya ghaibu huu ni uongo Allah ameshaurudi katika kitabu chake.140 – Mashia wanadai kuwa Imamu lazima awe ametajwa katika "maandiko". Kama ni hivyo, tusingekuta tofauti nyingi baina ya makundi ya Kishia kuhusu suala la Uimamu, kila kundi linadai "lina maandiko" juu ya Imamu wake! Sasa nini kinafanya kundi hili liwe bora kuliko lingine?! Kwa mfano kundi la Alkaysaaniyyatu linadai kuwa Imamu wa baada ya Ali, Mungu amuwie radhi, ni mwanawe "Muhammad bin Al-Hanafiyyatu", na hivyo hivyo. 141 – Baadhi ya Mashia wanamzushia Aisha, Mungu amuwie radhi, na wanamtuhumu kwa yale waliyomtuhumu watu wa Ifki – Mungu atukinge na hayo – kama ilivyotangulia. Wanaambiwa: mambo yakiwa kama mnavyozusha, kwa nini Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, hakumtekelezea adhabu naye Mtume ndiye aliyesema "Naapa kwa Allah, lau Fatuma binti Muhammad angeiba ningemkata mkono wake."?!([147]) Kwa nini Ali hakumtekelezea adhabu, na Ali haogopi lawama za mtu kwa ajili ya Allah?! Kwa nini Hassani hakumtekelezea adhabu pale alipotawala?!142 – Mashia wanaitakidi kuwa elimu imehifadhiwa kwa Maimamu zao. Na hao Maimamu wamerithi kitabu na elimu wasiyoirithi watu wengine. Wao wana: "Swahifatu Aljaamia" (kitabu chenye kukusanya kila kitu) na "Kitabu cha Ali" na "Al-Abaytwatu" na "Diwani Alshiia" na "Aljifru". Na vitabu hivyo vya kizushizushi ndani yake kuna kila wanachokihitaji watu. Nini faida ya vitabu hivi vilivyojificha tangu kughibu kwa Mahdiyyu?!Pia panaulizwa: Vipo wapi "vyanzo hivyo" leo hii? Anangoja nini "huyo mngojewa wao" hadi atokee kwa watu? Je, watu wanamuhitaji kwa ajili ya dini yao? Kama wanamuhitaji, tangu kujificha kwa Imamu kunakodaiwa kwa zaidi ya karne kumi na moja kwa nini umma unabaki mbali na vyanzo vya kuongoka kwake? Nini dhambi ya vizazi vyote hivi hadi vinanyimwa hazina hizo? Na kama umma hauna haja na vyanzo hivyo, sasa madai yote haya ya nini? Kwa nini Mashia wanaoepushwa na chanzo cha uongofu wao wa kweli? Nacho ni kitabu cha Allah na Sunna ya Mtume wake, Rehema na amani ziwe juu yake?!143 – Mashia katika vitabu vyao wanataja mwendo wa Huseini hadi kwa watu wa Alkufa kisha wakamdhalilisha na kumuua na hiyo ndio iliyokuwa sababu ya watu kuritadi ispokuwa watu watatu. Kwa hiyo, kama angekuwa anajua yajayo – kama wanavyodai – kwa nini aliwaendea?!144 – Mashia wanadai kuwa sababu za kufichikana kwa Imamu wa kumi na mbili ni hofu ya kuuwawa. Wanaulizwa: Kwa nini Maimamu wa kabla yake hawakuuwawa?! Nao walikuwa wakiishi katika dola za makhalifa, nao ni wakubwa, vipi auliwe naye ni mtoto mdogo?! 145 – Mashia wanadai kuwa wao wanategemea hadithi "zilizosahihi kwa njia ya Ahli Baiti"([148]) Na hili ndani yake kuna kuzuga na kuhadaa, kwa kuwa wao wanamchukulia kila mmoja katika Maimamu wao kumi na wawili kuwa ni kama Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, hatamki kwa matamanio ya nafsi yake, na maneno yake ni kama maneno ya Allah na Mtume wake. Kwa hiyo, ni mara chache kuona maneno ya Mtume katika maandiko yao. Kwa sababu wao wametosheka na yale yaliokuja kutoka kwa Maimamu zao. Vilevile: sio sahihi kwamba wao wanayategemea yale yaliokuja kwa njia ya Ahli baiti (wote), kwa hakika, wanategemea njia ya Maimamu wao tu. Kwa mfano, hawawategemei wajukuu wa "Hassani".146 - Pia wanaulizwa: nyinyi mnategemea yale yaliokuja kwa njia ya "Maimamu zenu wa Ahli baiti" kama mnavyodai. Inajulikana kuwa, hata mmoja miongoni mwa Maimamu zenu hajakuwa na Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, huku huyo Imamu akiwa ni mwenye umri wa kufahamu mambo ispokuwa Ali bin Abuu Twaalibu, Mungu amuwie radhi, Je, Ali ataweza kunukuu kila sunna ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, kwa vizazi vya baada yake?! Kivipi? Na Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, alikuwa akimfanya Ali kuwa khalifa wake kwa baadhi ya nyakati au akimtuma – tena kwa kukiri kwenu? Kwani Ali hakuwa ni mwenye kuongozana na Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, kwa wakati wote.  Vilevile, vipi Ali, Mungu amuwie radhi, aweze kunukuu hali za Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, hali ambazo wakeze ndio wamehusika kuzinukuu? Kwa hiyo, Ali peke yake hawezi kunukuu Sunna zote za Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, kukufikishiani nyinyi!147 – Inasemekana kuwa: Miji mingi ya Kiislamu imefikiwa na elimu kuhusu Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, si kwa njia ya Ali, Mungu amuwie radhi, na wengi wa wale waliofikisha juu ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, si kwa njia ya Ahli baiti wake! Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, alimpeleka As-adu bin Zuraaratu kwenda Madina akawalinganie watu katika Uislamu, na kuwafundisha Maanswari Qur'an, na dini. Akampeleka Al-Alaa bin Alhadhramiyyu Bahreini kwa kazi kama hiyo, Muaadhi na Abuu Mussa kawapeleka Yemeni. Itaabu bun Usaidi kampeleka Maka. Uwapi wito wa Kishia wa kwamba hakuna anayefikisha juu ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, ispokuwa Ali au mtu miongoni mwa Ahli baiti wake?!148 – Mashia katika vitabu vyao wanakiri kuwa wao hawakufikisha elimu ya halali na haramu, matendo ya hija ila kwa njia ya Abuu Jafari Albaaqiru. Na hili linamaanisha kuwa Abuu Jafari Albaaqiru hajawafikishia kitu kutoka kwa Ali! Vitabu vya Kishia vinasema: "Kabla ya kuwepo Abuu Jafari. Mashia walikuwa na matendo ya hija yao, halali na haramu, hadi alipokuja Abuu Jafari na kuwafungua na kuwabainishia matendo ya hija yao, halali na haramu hadi watu wakawa wakimtolea hoja baada ya kuwa wanapata hoja kwa watu.([149]).  Swali: Kabla ya Albaaqiru, Mashia walikuwa wanamwabudu Allah vipi?!149 – Mashia wanapingana wenyewe kwa wenyewe na wanamuhukumu yule anayedai kuwa amemuona Mahdi wao Anayesubiriwa kuwa mtu huyo ni mwadilifu na mkweli. Shehe wao Almumqaanii anasema: "Mtu anapata utukufu kwa kumuona huyo hoja – Allah awahishe kutokea kwake na ajaalie awe kikomboleo chetu dhidi ya kila machukizo! - baada ya kughibu kwake. Tunatolea ushahidi jambo hilo kuwa mtu huyo yupo katika daraja ya juu zaidi ya daraja ya uadilifu ya lazima"([150]) Wataulizwa: Kwa nini hamuipitishi hukumu hii kwa yule aliyemuona Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake?! Na huyo ni mtukufu wa daraja na ni mbora zaidi kuliko huyo hoja wenu?!150 – Mashia wanapingana wenyewe kwa wenyewe na kuzikataa riwaya za mwenye kumpinga Imamu miongoni mwa Maimamu zao, kwa hiyo wanazikataa riwaya za Maswahaba kwa ajili hii. Kisha tunawakuta hawatekelezi jambo hilo hilo kwa Mashia ambao waliotangulia pale wale waliowapinga baadhi ya Maimamu zao! Shehe wao Alhurru Al-Aamiliyyu amesisitiza kuwa Maimamia wamezifanyia kazi habari za "Alfutwahiyyatu"([151]) na habari za "Alwaaqifiyatu"([152]) na habari za "Annaawuusiyyatu"([153]) Makundi yote haya matatu yanapinga baadhi ya Maimamu wa Kishia wale kumi na wawili, licha ya hivyo, wanayazingatia makundi hayo kuwa ni miongoni mwa watu wa kutegemewa (thikaatu).([154]) Wala hawafanyi kitu kama hicho kwa Maswahaba wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake!151 – Kundi kubwa la wanazuoni wa Kishia wanaitakidi kuwa kitabu chao "Alkaafii" cha Alkiliiniyyu kina hadithi sahihi, dhaifu na Maudhui. Na ni jambo lililokubalika miongoni mwa Mashia kuwa kitabu hiki kimeonyeshwa kwa Mahdi wao aliyeghibu – kama wanavyodai – naye akasema kuwa "Kinawatosha Shia wetu"([155]).  Swali: Kwa nini hakupinga zile hadithi maudhui zilizomo ndani ya kitabu hicho?!  152 – Shehe wa Kishia Almuhammadaniyu anasema katika kitabu Misbaahu Alfaqiihi: "Wigo wa kukubali hoja ya ijimai ni kile kilichokubaliwa na maoni ya waliokuja baadae si kwa kukubaliana wote, wala kukubaliana katika zama moja, lakini kwa kuona maoni ya maasumu kwa njia ya fikra ya moja kwa moja…"([156]) Kwa hiyo wao wanajua rai ya wale walioghibu miongni mwao inayounga mkono ijimai kwa njia ya fikra ya moja kwa moja ambayo inaweza kukosea. Wakati huo huo wanaikataa ijimai iliyothibiti kihisia! Tazama kupingana huku!153 – Mashia wanakiri kuwa mmoja wa wanazuoni wao mkubwa ni Ibnu Baabawiyah Alqummiyu mwenye kitabu "Man laa yahdhuruhu Alfaqiihu" (Asiyefikwa na mwanazuoni) moja ya vitabu vinne vinavyofanyiwa kazi na Mashia. Wanakiri kuwa huyu mwanazuoni "anadai ijimai katika jambo na kudai ijimai katika jambo lingine lililokinyume na la kwanza"([157]). Hadi mmoja wa wanazuoni wao alisema "Kwa njia yake hii ya kudai ijimai, vipi atategemewa na kuaminiwa yale anayoyanukulu"([158]). 154 – Miongoni mwa maajabu ya Mashia ni kuwa, wanapokhitalafiana katika jambo na ikawa moja ya kauli mbili inajulikana msemaji wake na nyingine hajulikani msemaji wake, basi ya kweli kwao wao ni ile kauli iliyosemwa na mtu asiyejulikana msemaji wake! Kwa kuwa wao wanadai kuwa huenda hiyo ikawa ni kauli ya Imamu maasumu! Hadi pale shehe wao Alhurru Al-Aamiliyyu alipowakosoa na kusema kwa mshangao: "Na kusema kwao kuwa ni sharti kitu kisichojulikana nasaba kuingia kwa Maimamu ni jambo la kushangaza sana na geni mno. Je, lina ushahidi gani? Vipi litajulikana ni maasumu au ni dhana yake."([159]). 155 – Shehe wa Kishia Almajlisiyyu anasema: Kulielekea kabri ni jambo la lazima hata kama halijaafikiana na kibla"([160]) na hiyo ni wakati wa kutekeleza rakaa mbili za kutembelea makaburi yao!!Cha kushangaza ni kuwa makatazo ya kuyafanya makaburi kuwa ni misikiti na kibla yamekuja katika vitabu vyao kutoka kwa Maimamu zao wa Ahli baiti, lakini wao wanachukulia makatazo hayo kwa njia ya taqiya – kama ada yao katika kila kisichoafikiana na matamanio yao!156 – Mara nyingi Mashia wanairudia rudia hadithi ya "Alghadiiru" na kauli ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, katika tukio hilo, "Nakukumbusheni Mwenyezi Mungu juu ya Ahli baiti wangu" huku wakisahau kuwa wao ni wa mwanzo kuukhalifu usia huo wa Mtume. Pale walipowafanyia uadui watu wengi miongoni mwa Ahli baiti! 157 – Mashia wanaambiwa: Kama Maswahaba wangeficha maandiko ya Ali, Mungu amuwie radhi, basi wengeficha fadhila na ubora wake wala wasingenukuu chochote katika hayo. Na hili ni kinyume na uhalisia. Kwa hiyo imejulikana kuwa lau kama kungekuwa na kitu kama hicho (andiko) wangelinukulu. Kwa kuwa andiko la ukhalifa ni tukio kubwa, na tukio kubwa linapasa kuwa mashuhuri sana. Na kama lingepata umashuhuri huo wangelijua wanaolipinga na wanaoliafiki. 158 – Mashia wanasimulia kuwa Hassani Al-Askariyyu baba wa Imamu anayesubiriwa aliamrisha kuzuiwa habari za "msubiriwa" ispokuwa kwa watu wa kuaminika, kisha wanajipinga na kudai kuwa asiyemjua Imamu kwa hakika anamjua na kumwabudu asiyekuwa Allah! Na kama atakufa kwa hali hiyo, amekufa kifo cha kikafiri na unafiki!([161]) Kwa nini baba yake amejikalifisha na kuweka ahadi hii kwa Mashia?!159 – Mashia wanaodai kuwa, Allah amempa Mahdi wao anayesubiriwa" mamia ya miaka, kwa sababu viumbe na ulimwengu wote vinashida naye! Wanaambiwa kuwa: Kama Allah angekuwa ni mwenye kurefusha umri wa mwanadamu yoyote kwa ajili ya haja ya viumbe kwa mtu huyo angeurefusha umri wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake.160 – Mashia hawakubali kauli ya Jafari nduguye Hassani Al-Askariyyu baba wa "Imamu wao aliyeghibu" aliposema kuwa: "Nduguye Hassani hajazaa mtoto, kwa kuwa – kama wanavyosema – yeye si maasumu,([162]) kisha wanakubali madai ya Athumani bin Saidi, katika kuthibitisha kuwa Hassani ana mtoto. Naye pia – si maasumu – kupingana kulioje huku?!161 – Miongoni mwa itikadi za Mashia zilizomashuhuri ni: itikadi ya "udongo" – kama ilivyotangulia katika utangulizi – kwa ufupi ni kuwa Allah Mtukufu Aliyetukuka amewaumba Mashia kwa udongo maalumu na kuwaumba Masunni kwa udongo maalumu! Kisha ukachanganywa udongo wa makundi mawili kwa aina maalumu, kwa hiyo yale yote yaliyokuwepo kwa Mashia miongoni mwa maasi na maovu ni athari ya kuathirika na udongo wa Kissuni! Na yale yaliyopo kwa Masunni miongoni mwa wema na kuaminika yote hayo ni kwa sababu ya kuathirika na udongo wa  Kishia! Na siku ya Kiama maovu na machafu ya Mashia yatakusanywa na kuwekwa kwa Masunni! Na mema ya Masunni yanakusanywa na kupewa Mashia!Mashia wamepitikiwa kuwa, itikadi hii ya kizushi, inapingana na madhehebu yao katika Kadhaa na Kadari na matendo ya waja. Kwa sababu muktadha wa itikadi hii ni kuwa mja amelazimishwa kutenda matendo yake wala hana hiari. Kwa kuwa matendo yake ni kwa mujibu wa "udongo", licha ya kuwa madhehebu yao ni kuwa mja anaumba matendo yake kama yalivyo madhehebu ya muutazila!162 – Wanazuoni wa Kishia Ithnasheria wanataja sana mapenzi ya Maanswari kwa Ali bin Abuu Twaalibu, na kwamba maanswari walikuwa wengi katika jeshi la Ali katika vita vya Swaffaini. Wanaambiwa: Kama mambo ni hivyo, kwa nini hawakumkabidhi ukhalifa na wakaukabidhi kwa Abuu Bakri?! Hutopata jibu la kukinaisha na kutuliza moyo wako.Kwa hakika mtazamo wa Maanswari na kabla yao Muhaajiriina ni wa upeo wa mbali na sahihi kuliko sisi sote. Hili kundi lenye imani lilikuwa linatofautisha baina ya ukhalifa na mafungamano ya kihisia ya kuwa na ukaribu na Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake.Kwa hiyo, tumeona vitabu vya Kishia vinavyowasifu hawa Maanswari kwa kuwa pamoja na Ali katika vita vya Swaffaini ndio vitabu hivyo hivyo vinavyowashambulia eti ni wenye kuritadi na kurejea nyuma katika vita vya Assaqiifa! Mizani ya ajabu wanayopimiwa Maswahaba wa Mtume wa Allah, Rehema na amani ziwe juu yake, kama wakiwa na Ali katika jambo moja, wanakuwa ni watu bora, ama msimamo wao ukiwa upo pamoja na wale walio kinyume na Ali au sema ukiwa haupo katika mwelekeo alioutaka Ali wameshakuwa wenye kuritadi na wapenda maslahi na wanafiki! Wakisema tumewahukumu kuwa ni wenye kuritadi na kurejea nyuma katika visigino vyao kwa sababu wamepinga andiko juu ya Ali bin Abuu Twaalibu. Wataambiwa kwa kuwashangaa: je, sio Mashia Ithnasheria wanaotaja kuwa hadithi ya Alghadiiru ni mutawaatiri na kuwa mamia ya Maswahaba wameipokea? Sasa kupinga kupo wapi?Nikisema kwa ulimi wangu kuwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake alimwambia Ali "Mtu atakayekuwa maula wangu (kipenzi changu) basi na Ali ni maula wake" Sasa kukowapi huko kupinga andiko?!Ikisemwa: Wamepinga maana. Wataambiwa watu hao: Nani kasema kuwa kile mnachokifuata katika tafsiri yenu ya hadithi hiyo ndio haki?! Je, nyinyi ndio mnaofahamu zaidi na wenye akili sana kuliko Maswahaba wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, waliokuwepo katika kipindi hicho na kuisikia hadithi hiyo kwa masikio yao?! Au nyinyi mnafahamu zaidi Kiarabu kuliko wao hadi mmekuwa mnafahamu katika hiyo hadithi kuliko waliyoyafahamu?!([163]). 163 – Mbele yetu kuna makundi mawili: kundi moja linakosoa kitabu cha Allah likidai kuwa kimetiwa upotoshaji na kubadilishwa. Wakiongozwa na Annuuriyyu Altwabrisiyyu – mtunzi wa kitabu Al-mustadraki – moja ya misingi minane ya hadithi kwa Mashia Ithnasheria – na ametunga kitabu kwa jina (Faswlu Alkhitwaabu Fii Ithibaati Tahriifu Kitaabu Rabbi Al-Arbaabi) anasema ndani ya kitabu hicho kuhusu Qur'an na kutokea kwa kupotoshwa maandiko yaake ni: (miongoni mwa ushahidi wa kupotoshwa ufasaha wa Qur'an ni kuwa baadhi ya vifungu vyake vimefikia upeo wa muujiza na vingine ni vya kijinga)!([164]). Bwana Adnani Albahreniyyu amesema: (Habari amabzo hazihesabiki kwa wingi wake zimepindukia upeo wa tawaaturi, katika kunukuliwa kwake hakuna faida baada ya kuenea kwa kauli ya kupotoshwa na kubadilishwa baina ya makundi mawili. Na kuwa hicho ni kitu kinachokubalika bila kupingwa kwa Maswahaba na Mataabiina pia na ijimai ya makundi ya haki na kuwa hilo ni miongoni mwa mambo ya lazima katika madhehebu zao na kwa hiyo zimeshikamana habari zao.)([165]).Yusufu Albahreniyyu amesema: (Hakuna kujificha katika habari hizi kwa kuwa kuna ushahidi wa wazi na makala fasaha ya yale tulioyachagua na uwazi wa yale tuliyoyasema, lau kama kutaletwa kukoselewa katika habari hizi licha ya wingi na kuenea kwake, imewezekana kuzitia dosari habari za sheria yote, kama ilivyo kuwa haifichikani. Kwani msingi ni mmoja na vilevile njia na wapokezi, mashehe na kunukuu. Naapa kuwa, kauli ya kusema kuwa hakuna mabadiliko na kubadilishwa haitoki katika kuwadhania vizuri Maimamu wa uovu, na kwamba wao hawajafanya khiana katika Uimamu mkubwa licha kudhihiri khiana yao katika amana nyingine ambazo zina madhara makubwa katika dini)([166]).Kundi hili limeikosoa Qur'an kwa uwazi kabisa likisema kuwa kumetokea upotoshaji!Na kundi la pili: (nao ni Maswahaba wa Mtume wa Allah) ambao kosa lao ambalo halisamehewi na Mashia Ithnasheria ni kuwa wameukabidhi ukhalifa kwa Abuu Bakri badala ya Ali! Kundi la kwanza lililokosoa kitabu cha Allah. Wanazuoni wa Kishia Ithnasheria wanatoa udhuru kwa kundi hili na upeo wa wakisemacho ni neno (wamekosea), (wamejitahidi na kutafsiri wala hatuwaafiki kwa yale waliyoyafuata), Nywele zangu zimesisimuka kwa ajabu, lini imekuwa mambo ya kuhifadhiwa kwa kitabu cha Allah au kupotoshwa kwake ni kitu cha kujitahidi?! Je, kuna kujitahidi gani katika kauli ya muovu huyu kuwa eti kuwa: (Katika Qur'an kuna aya za kijinga)! Wallah huu ni msiba mkuu. Tuchukulie mfano wa mtazamo wa wanazuoni wa Kishia Ithnasheria kwa wale wasemao huko kupotoshwa:Bwana Ali Almailaaniyyu – ni miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa Kishia Ithnasheria kwa sasa – anasema katika kitabu chake (Adamu Tahriifu Alquraani uk 34). Akimtetea (Almiirza Nuuriyyu Altwiirisiyyu): (Almiirza Nuuriyyu ni miongoni mwa watu wakubwa wa hadithi, (Kwa hakika sisi tunamuheshimu Almiirza Nuuriyyu. Almiirza Nuuriyyu ni miongoni mwa wanazuoni wetu wakubwa, wala hatuwezi kumfanyia uadui kwa kitu kidogo, wala haijuzu, na hilo ni haramu, kwani yeye ni mtu mkubwa wa hadithi miongoni mwa wanazuoni wetu)!!([167]). Tafakari huku kupingana.164 - Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Fuateni mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola Mlezi wenu, wala msifuate rafiki au walinzi wengine badala yake. Ni machache mnayoyakumbuka}. Sura [7] Al-A‘raaf 3. Hili ni andiko la kubatilisha kumfuata mtu kinyume na Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake. Kwa hakika shida ya kufaradhishia Imamu ili atekeleze ahadi ya Allah Mtukufu iliyotujia kwa yale ya mwenye kuabudu tu sio kuwaletea watu yale wasiyoyaweza kuyajua miongoni mwa mambo ya dini aliyokuja nayo Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake. Tumemkuta Ali, Mungu amuwie radhi, pale alipoitwa kwenda katika kuhukumiwa kwa Qur'an alikubali, na kueleza kuwa kuhukumiwa kwa Qur'an ni haki. Na kama Ali alipatia katika hilo basi hiyo ndio kauli yetu. Na kama ameitikia batili basi hiyo si sifa yake, Mungu amuwie radhi. Na kama kuhukumiwa kwa Qur'an haijuzu kunapokuwepo Imamu basi Ali angesema wakati huo: Vipi mnataka kuhukumiwa kwa Qur'an, na mimi ndio Imamu mfikishaji kutoka kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake?Kama watasema: Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, amekufa, kwa hiyo hakuna budi ya kuwepo Imamu anayefikisha dini.Tunasema: hilo ni batili na ni madai bila ushahidi, pia ni maneno yasiyo na dalili ya kusihi kwake. Kwa hakika kile wanachokihitaji watu wa ardhini kutoka kwa Mtume wa Allah, Rehema na amani ziwe juu yake, ni uchambuzi wake na kufikisha tu, sawa sawa katika hilo, kwa mwenye kuwa naye, au kuwa mbali naye, au atakayekuja baada yake. Kwani Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, hana faida kama hajaongea kwa wazi juu ya vitu vya dini. Makusudio ya kuwepo Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, ni kuwepo maneno yake yanayobaki milele, anayoyafikisha kwa watu wote waliomo ardhini.Pia, lau kama yale waliyoyasema ya kuwa na haja ya kuwa na Imamu milele. Basi hilo liingekuwa linapingana na wao juu ya yule aliyekuwa hayupo mbele ya Imamu miongoni mwa miji ya ardhi hii. Kwani hakuna njia ya kumuona Imamu kwa watu wote wa ardhini ambao wapo mashariki na magharibi miongoni mwa mafakiri, wadhaifu, wanawake, wagonjwa, wenye kazi kwa kutafuta maisha yake ambayo yatapotea kama akiyapuuzia, kwani ni lazima kufikisha.Kama ni lazima Imamu afikishe, basi ufikishaji wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, ni bora zaidi kufuatwa kuliko ufikishaji wa yule wa chini yake. Na kwa hili hawana namna ya kujitenga nalo ([168]).165 – Kuna riwaya zilizothibiti na sahihi kwa sanadi za Mashia zinazoshutumu na kulaani kundi la watu waongo ambao dini ya Mashia imesimama kwa riwaya zao. Hizo riwaya zinawashutumu watu wao kwa majina yao. Mashehe wa Kishia hawakukubali shutuma zilizokuja kuwahusu watu hao (kwa sababu, kama watazikubali watakuwa ni miongoni mwa Masunni na hivyo wataachana na ushazu wao) wakakimbilia taqiya ili kukabiliana na shutuma hizo, na hili halina tafsiri zaidi ya kupinga kauli ya Imamu kwa njia ya kuficha. Kama mpingaji wa andiko la Imamu ni kafiri katika madhehebu ya Kishia, kwa hiyo watu hao, kwa jambo hili wameshatoka kichwa chini kutoka katika dini!Muhammad Ridhwaa Almudhwaffaru – naye ni mmoja wa mashehe na maaya zao wa kisasa – amekiri kuwa: Riwaya zao nyingi zimenukuu shutuma kutoka kwa Maimamu zilizonukuliwa na vitabu vya Mashia wenyewe. Almudhwaffar ameelezea shutuma zilizokuja kumuhusu Hishaam bin Saalimu Aljuwaaliiqiyi kwa kusema: "Umekuja ukosoaji mwingi kumuhusu Hishaam bin Saalimu, kama ulivyokuja kuwahusu wengine miongoni mwa Maanswari na marafiki wa Ahli baiti waaminifu. na jawabu juu ya hilo ni la wote na ni lenye kufahamika"([169]). (Yaani sababu maarufu inayotumika kwa Mashia ni taqiya). Kisha akasema: "Itasihi vipi, kwa watu watukufu kama hawa watiwe dosari? Hivi dini ya kweli na jambo la Ahlu baiti haikusimama na kudhihiri kwa hoja zao za nguvu"([170]). Tazama, namna taasubi (ubaguzi) inavyowafanya watu wake: Wao wanawatetea hawa walioshutumiwa na Maimamu wa Ahlu baiti. Na wanatoa maandiko yaliopokewa na wanazuoni wa Ahlu baiti kuhusiana na kuwakosoa watu hao na kuonya dhidi yao, yanayonukuliwa na vitabu vya Kishia. Kana kwamba wao kwa jambo hili, wanawakadhibisha Ahlu baiti, lakini pia wanasadikisha yale yanayosemwa na waongo hawa. Huku  wakidai kuwa watu hao wamewashutumu Maimamu  kwa njia taqiya. Wao hawawafuati Ahlu baiti katika kauli zao zinazoafikiana na nukuu za Maimamu. Ispokuwa wanafuatilia athari za maadui zao na kuchukua kauli zao na kukimbilia taqiya katika kuzirudi kauli za Maimamu.166 – Kwa njia ya tawaaturi, imejulikana kuwa, Abuu Bakri, Omari na Athuman, Mungu awawie radhi, walikuwa na nafasi kubwa mbele ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake. Pia walikuwa ni watu wa karibu zaidi na Mtume. Wote wameoleana na Mtume. Mtume alikuwa anawapenda na kuwasifu. Kwa hiyo, ima walikuwa katika msimamo wa wazi na wa siri katika uhai na baada ya kufa kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, au walikuwa kinyume na hivyo katika uhai na baada ya kufa kwake. Na kama walikuwa hawana msimamo licha ya ukaribu huu na Mtume, basi moja ya mabo mawili lazima liwepo: Ima Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, hakujua hali zao, au alikuwa anawapaka mafuta kwa mgongo wa chupa, na lolote kati ya mawili hayo ni baya mno kwa haki ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake. Kama ilivyosemwa: Kama ulikuwa hujui basi huo ni msiba * na kama ulikuwa unajua huo ndio msiba mkuu.            Kama Abuu Bakri, Omari na Athuman, Mungu awawie radhi, wamekengeuka baada ya kuwa walikuwa na msimamo, basi hiyo ina maana Mungu kamdhalilisha Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, kwa watu wake wa karibu mno, Maswahaba zake wakuu, na kwa wale aliowaahidi kuwa atafanya dini yake ishinde dini zote. Vipi watu wa karibu yake wawe ni murtadiina? Mambo haya na yaliyo kama haya ni mambo makuu ambayo Mashia wanatia dosari kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, kama alivyosema Abuu Zar-aa Alraazi: Kwa hakika, hawa jamaa walitaka kumtia dosari Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, ili aseme msemaji kuwa: Mtume ni muovu alikuwa na wafuasi waovu. Lau kama angekuwa mtu mwema wafuasi wake wangekuwa wema. 167 – Mashia wanasema kuwa: "Uimamau ni wajibu kwa kuwa Imamu ni naibu wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, katika kuhifadhi sheria ya Kiislamu, kuwawepesishia Waislamu njia iliyonyooka, kuhifadhi na kutunza hukumu zisizidishwe wala kupunguzwa"([171]) Pia wanasema kuwa: "hapana budi kuwepo Imamu msimikwa na Allah Mtukufu. Na haja ya ulimwengu unataka kuwepo kwa Imamu, asiye na uharibifu. Kwa hiyo, ni wajibu kuwepo maandiko (nasu)…"([172]) Na kuwa imewajibika kuwa na Imamu kwa kuwa ni huruma… na kwa hakika jambo hilo ni huruma, kwa sababu watu wakiwa na kiongozi anayetiiwa, anayeongoza, anayekemea madhalimu wasidhulumu, anayewapeleka watu katika heri, na kuwakemea waache maovu. Hao Maimamu watakuwa wapo karibu zaidi na uongofu, na watakuwa mbali mno na ufisadi, na hiyo ndio huruma yenyewe."([173]). Mashia wanaambiwa: Kwa hakika Maimamu zenu kumi na wawili – ukimtoa Ali, Mungu amuwie radhi, hawajashika uongozi wa kuongoza watu wote katika mambo ya kidini na kidunia, wala hawakumiliki nguvu za kukemea madhalimu waache dhuluma zao, wala kuwapeleka watu katika heri, au kuwakemea waache maovu! Iweje mnawadaia madai ya kufikirika ambayo hayana uhalisia kabisa?! Na lau kama mngezingatia, basi haya yanatengua Uimamu wao – kwa mujibu wa ufahamu wenu – kwa kuwa huruma mnayoidai haijapatikana kutoka kwao!168 – Katika kitabu cha Nahju Albalaagha kumekuja kuwa: Ali, Mungu amuwie radhi, alikuwa akimuomba Mola wake kwa dua hii: "Ewe Mola nisamehe yale unayoyajua kuhusu mimi, na kama nikirejea, basi nirejeshee msamaha, kwa yale niliyoahidi ([174]) mimi mwenyewe na hujanikuta kuwa nimeyatekeleza. Ewe Mola nisamehe kwa yale niliyokukaribia kwayo kwa ulimi wangu kisha yakazoeleka na moyo wangu, Ewe Mola nisamehe makonyezo ya ncha za macho na kutereza kwa matamshi na kujisahau kwa moyo na  kuropoka kwa ulimi."([175]). Ali, Mungu amuwie radhi, anamuomba Allah amsamehe dhambi zake kutokana na kusahau na mengineyo. Na haya yanapingana na yale mnayomdaia kuwa amekingwa na madhambi!169 – Mashia wanadai kuwa hakujawahi kuwa na Nabii yoyote ispokuwa amewalingania watu kuhusu uwalii wa Ali!([176]) Na kwamba, Allah amechukua ahadi ya Manabii juu ya uwalii wa Ali!([177]) Vilevile kutia chumvi na kukuza mambo kwao kumefikia upeo hadi Shehe wao Altwahraaniyyu amedai kuwa uwalii wa Ali "Ulitangazwa kwa vitu vyote, na kitu kilichoukubali kimefaulu na kisichoukubali kimefisidika"!([178]) Mashia wanaambiwa: Wito wa Mitume, amani iwe juu yao, ulikuwa ni upwekeshaji na kuitakasa nia kwa Allah. Wala sio uwalii wa Ali kama mnavyodai. Allah Mtukufu amesema: {Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipokuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu}. Sura [21] Al-Anbiya. Kama uwalii wa Ali, kama mnavyodai, eti umeandikwa katika sahifa zote za Mitume. Kwa nini iwe Mashia peke yao ndio wanaonukuu habari hizo wala hakuna watu wengi wanaoijua?! Kwa nini watu wa dini nyingine wasijue habari hizo?! Huku wengi wao wamesilimu wala hawajataja huo uwalii. Pia haukusajiliwa katika Qur'an wakati Qur'an ndio inakusanya vitabu vyote?! 170 – Je, Maimamu walifanya mutaa?! Watoto wao kwa njia ya mutaa ni akina nani?! 171 – Mashia wanasema kuwa: Kwa hakika Maimamu wanajua yaliyopita na yatakayokuja, na kuwa hakuna kinachofichikana juu yao. Na kwa hakika Ali bin Abuu Twaalibu ni mlango wa elimu – iweje asijue hukumu ya Madhii, na matokeo yake anamtuma mtu aende kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, ili amfundishe hukumu zinazohusiana na jambo hilo?!172 – Kwa hakika uovu uliofanywa na Maswahaba kwa mujibu wa Mashia ni kukengeuka kwao na kuacha uwalii wa Ali, Mungu amuwie radhi, na wakaacha kumkabidhi ukhalifa, kwa hiyo, matendo yao haya, yameporomosha uadilifu wao kwa mujibu wa Mashia. Je, kwa nini hawakufanya hivyo hivyo kwa makundi mengine ya Mashia yaliyopinga baadhi ya Maimamu. "Kama "Alfatw-hia" na "Alwaaqifatu" na wengineo?! Lakini utawakuta wanatolea hoja kauli za watu hao na kuwafanya ndio waadilifu!([179]) Kwa nini kupingana huku?!173 – Vyanzo vya Kishia vinaafikiana juu ya Maimamu na watu wengine katika kuifanyia kazi taqiya – kama ilivyotangulia – nayo ni kuwa Imamu anadhihirisha kinyume na yale anayoyaficha. Huenda akasema mambo yasiyo ya haki. Na mtu anayetumia taqiya ataongopa. Na uongo ni maasi!174 – Alkiliiniyyu ananukuu kuwa: baadhi ya wanaomnusuru Imamu Ali, Mungu amuwie radhi, walimtaka Ali arekebishe yale yaliyofisidiwa na Makhalifa waliomtangulia, naye akakataa huku akitoa hoja kuwa yeye anaogopea jeshi lake lisitengane naye ([180]) licha ya kuwa tuhuma walizotuhumiwa Makhalifa wa kabla yake (Abuu Bakari, Omari na Athumani, Mungu awawie radhi) zinajumuisha kuikhalifu Qur'an na Sunna. Je, Ali kuacha makosa ya kukhalifu mambo hayo yawe kama yalivyo, yananasibiana na "Kukingwa kuwa hafanyi kosa" kunakodaiwa na Mashia kua Ali yupo hivyo?!175 – Omari, Mungu amuwie radhi, alichagua watu sita ili wafanye shura baada ya kufa kwake, kisha watu watatu wakajitoa, kisha akajitoa Abdulrahmani bin Aufi, na wakabakia Athumani na Ali, Mungu awawie radhi, kwa nini tangu mwanzo, Ali hakutaja kuwa yeye amehusiwa awe khalifa?! Je, alikuwa anaogopa mtu yoyote baada ya kufa kwa Omari?! 176 – Katika mambo ya ajabu sana ni kuwa Mashia wametunga riwaya zinazotaja mrorongo wa majina ya Maimamu baada ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, hadi Mahdi wao. Licha ya hivyo, rejeo lao kuu katika zama hizi linakanusha na kudai kuwa hakuna andiko linalotaja hao Maimamu! Pale Alkhuuiyyu anaposema: "Riwaya zilizokuja kwa tawaaturi ambazo zimetufikia kutokana na njia ya (Masunni na wengineo) zimeainisha Maimamu, amani iwe juu yao, kuwa wapo kumi na wawili kiidadi. Wala hawajaainishwa kwa majina yao mmoja mmoja, amani iwe juu yao" ([181]).177 – Mashia wanadai kuwa Maswahaba wengi waliritadi baada ya kufa kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, kama inavyojulikana. Kisha tunawakuta Mashia hao hao wakijipinga wenyewe kwa wenyewe pale wanapotaka kuwajibu wale wanaowaambia: Ali, Mungu amuwie radhi, kwa nini hajajiombea mwenyewe baada ya kufa kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, ikiwa ameandikwa kuwa yeye ndiye walii? Mashia wanadai kuwa, Ali hakufanya hivyo kwa kuchelea kuritadi kwa Maswahaba na kuuacha Uislamu!! Katika Alkaafii kutoka kwa Albaaqiri amesema: Kwa hakika watu walipofanya yale waliyoyafanya, pindi walipombayyi Abuu Bakri, hakuna kilichomzuia Amiri Muuminiina (Ali) asijitangaze nafsi yake ispokuwa mtazamo wake kwa watu, na kawaogopea wasije wakaritadi na kuuacha Uislamu na kurejea katika kuabudu masanamu ([182]).178 – Mashia kama ilivyotangulia – wanadai kuwa kuna andiko juu ya Maimamu zao. Lakini sisi tunakuta katika vitabu vyao riwaya nyingi sana zinazokanusha madai haya. Ustadhi Faisal Nuru amezikusanya na kuzithibitisha katika kitabu chake "Al-Imaamatu Wannaswu", Anayetaka kujua uhakika na akirejee kitabu hicho. HITIMISHONamuomba Allah awanufaishe vijana wa Kishia kwa maswali haya, na ayajaalie haya maswali yawe ufunguo wa heri kwao, uwajulishe haki, na kuwahimiza waitafute na kushikamana nayo, wakiwa hawaogopi katika jambo hilo lawama za mwenye kulaumu. Kwa wale watakaopata hoja ambayo sijaitaja katika maswali yaliyotangulia, napenda wailete ili kuiongeza katika chapa zifuatazo – Inshaallah. Allah ni Mjuzi. Na Rehema na amani ziwe juu yake Nabii wetu Muhammadi pamoja na Aali zake na Maswahaba zake.         *       *       *[1]  Sahihi Al-Tirmidhiyyu ya Albani (2129). Pia tazama maelezo juu ya hadithi hii kiriwaya na kidiraya katika risala ya Sheikh Sulaim Al-Hilaaliyyu "Dar`u al-irtibaabi an hadiith maa anaa alayhi wal-asw`haabu" Kuondoa shaka juu ya hadithi – (..ambalo nimo mimi na Maswahaba zangu kwa sasa). [2]  Huyo ni ndugu mbora: Abuu Khalifa Al-Qudhaybiyyu, kutoka Falme ya Bahraini. Na kwa hakika amenikirimu kwa kutembelea nyumba yangu mjini Riadhi.[3]  Ndoa hii imethibitishwa na masheikh wa Kishia wafuatao: Alkiliiniyyu katika kitabu Alkaafii filfuruui (115/6), Atwusiyyu fii Tahdhiibi Al–ahkaami (Babu adadu annissaai juzuu ya 8 uk 148), na katika (380/2), na katika kitabu chake: Al–Istibswaaru (356/3). Almaazindaaraaniyyu katika manaaqibu Aali Abuu Twaalibu, (162/3),  Al–aamiliyyu katika Masaaliki Al–afhaami, (1/Kitaabu Annikaahi),  Murtadha ilmu alhudaa fii Alshaafii, (uk 116, ibni Abuu Alhadiith katika Sharhu Nahju Albalaagha, (124/3), Al-ardibiiliyyu katika Hadiiqatu Asshiatu, (uk 277), Alshuushtariyyu katika majaalish almuuminiina. (uk 76/82), Almajlisiyyu  fii bihaari Al–anwaari, (uk 621). Kwa ziada tazama: Risaalatu "ndoa ya Omari bin Alkhatwaabi, kumujoa Ummu kulthuumi binti Ali bin Abuu Twaalibu – ni hakika sio uzushi" cha Abuu Muaadhi Al-ismaaiiliyyi.[4]  Kashful-ghumma fii maarifatil- Aimmati.[5]  Rejeo lililotangulia, na "Al-irshaadu" uk 167, "Muujamul- khuuiyyi" (66/21).[6]  Rejeo lililotangulia.[7]  Rejeo lililotangulia, na "Al-irshaadu" uk 167, "Muujamul- khuuiyyi" (45/13). [8]  Kashful-ghumma fii maarifatil- Aimmati,  Ali Al-Arbaliyyi (66/2). Ili kujua marejeo mengine ya Kishia yaliyothibitisha majina yaliyopita ya watoto wa Ali Mungu amuwie radhi, tazama: "Al-Imaamatu wannaswu" cha Ustaadhi Faysali nuuri, uk 683-686.  [9] ((Nahju Albalaagha)), uk 136, pia tazama: uk 366 – 367, na uk 322. [10]  Anayetaka kuzamia katika masuala ya kuoleana kati ya Maswahaba na Ahli baiti na arejee katika kitabu (Al-ddurru Al-mandhuuru min turaathi Ahli albaiti) cha mwanazuoni imaamiyyi Alaa`a Al-diini Al-mudarrisu. Kitabu hicho kinatosheleza na ziada ya yale tuliyoyataja.[11] Tazama: Al-Irshaadu Lilmuffid uk 354, na Muqaatilu AtTwaalibuna LiAbuu Alfaraji Al-Aswfahaaniyyu Al-shii`iyyu, uk 91, na Taarikhu Al-Yaaquubiyyu Al-shii`iyyu, juzuu 2 uk 213.[12] Attanbiihi wal-Ishraafu lilmasoudiyyi Asshiiyyi, uk 263.[13]  Muqaatilu AtTwaalibuna LiAbuu Alfaraji Al-Aswfahaaniyyu Al-shii`iyyu, uk 188, chapa ya Daru Almaarifa.[14] Kashful-ghumma fii maarifatil- Aimmati,  Ali Al-Arbaliyyi (3/26). [15]  Kashful-ghumma fii maarifatil- Aimmati,  Ali Al-Arbaliyyi (3/217).[16] Muqaatilu AtTwaalibuna LiAbuu Alfaraji Al-Aswfahaaniyyu Al-shii`iyyu, uk 561 - 562, chapa ya Daru Almaarifa.[17] Tazama: Al-Irshaadu Lilmuffid uk 354, Muujamu rijaali Al-hadiithi lil-khuuliyyi, juzuu 13 uk 51, Muqaatilu AtTwaalibuna LiAbuu Alfaraji Al- Aswfahaaniyyu Al-shii`iyyu, uk 84, chapa ya Beiruti, Umdatul-Twaalibu uk 361, chapa ya Najafu na Jalau Al-uyuuni uk 570. [18] Al-Irshaadu Lilmuffid uk 194, Muntahaa Al-aamaali juzuu 1 uk 240, Umdatul-Twaalibu uk 81, Jalau Al-uyuuni lilmajlisiyyi uk 582, Muujamu rijaali Al-hadiithi lil-khuuliyyi, juzuu 13 uk 29, namba (8716), na Kasfu Al-ghummati 3/201.   [19] Al-Irshaadu Lilmuffid 3/155, na Kasfu Al-ghummati 3/294.[20]  Ufafanuszi wa hili upo katika ((Muqaatilu AtTwaalibuna)) na vyanzo vingine miongoni mwa vyanzo vya Imaamiyyayu, kwa mfano tazama: (Al-durru Al-manthuuru) cha Alaadiini Al-muddarrisu uk 65 – 69.[21] Al-Irshaadu uk 302, Al-fusuulu Al-muhimmatu 242, na Kasfu Al-ghummati juzuu 3 uk 26.[22] Al-Irshaadu Lilmuffid 3/312.[23]  Tazama: usulu Al- Kaafii Lil-Kiliiniyyi, 1/258, na Kitabu: Al- fusuulu Al- muhimmatu Lilharri Al-Aamiliyyi, uk 155.[24]  43/364.[25]  Nahju Albalaagha, uk 576. Pia tazama: Mustadiriku alwasaaili. 3/445.[26] Tazama ((Alkhiswaalu)) llil- Swadduuqi uk 621, na ((Wasaailu Asshiiati)) 3/27.[27]  (1/248)[28]Man laa Yahdhuruhu Al-faqiihu, LiAbuu Jafari Muhammad bin Baabuuyah Al-Qummyiyyu (1/232), imepokelewa na Al-hurr Al-aamiliyyu katika "Wasaailu Al-Shiiati'' (2/916). [29]  (5/527).[30] Imepokewa na Swaduuqu katika Man laa Yahdhuruhu Al-faqiihu, (4/271 – 272). Pia imepokewa na Alhurru Al-aamiliyyu, katika Wasaaili Ashiiati (2/915), Na Yusuf Al-bahreiniyyu, katika Al-hadaaiqi Al-nnaadhirati, (4/149). Na Al-hajji Huseini Al-Baruujardiyyu katika Jaamiu Ahaadiithu Ashiiati, (3/488). Pia imepokewa na Muhammad Baaqir Al-Majlisiyyu kwa tamko la: "Kulilia maiti ni matendo ya kijahiliya" Bihaaru Al-anwaari (82/103).   [31]  Imetolewa na Al-Majlisiyyu katika Bihaaru Al-anwaari (82/103). Na Mustadiraku Al-wasaaili (1/143-144) pia Jaamiu Ahaadiithu Ashiiati, (3/488) na Man laa Yahdhuruhu Al-faqiihu, (4/271).[32]  Tatwibiiru ni kujitoa damu kichwani. Kitendo kinachofanywa na Mashia katika siku ya Ashuraa. Tazama siratwa al-nnajaati” cha Attibriiziyyi (1/432).[33]   Tazama “Irshadu Assaailu” (uk 184).[34]  Hadithi ya Alkisaa, ufupisho wake ni kuwa: Mtume Rehema na amani ziwe juu yake, mara moja alitoka akiwa na nguo (kisaa) ya manyoya meusi, akaja Hassani, na Mtume akamuingiza katika Alkisaa, kisha akaja Huseini, akamuingiza, kisha akaja Fatuma, akamuingiza,   kisha akaja Ali, akamuingiza, kisha Mtume akasoma: {…Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu, enyi Watu wa Nyumba ya Mtume, na kukusafisheni baarabara} Sura [33] Al-Ahzaab 33. Imepokewa na Muslimu katika fadhaaili asswahaabati.[35]  Tazama: “Furuu Alkaafiyyi” cha Alkiliiniyyu. (7/127).[36]  (9/254).[37]  Usulu Alkaafii cha Alkiliiniyyi, Kitabu Alhijati – babu : kwa hakika ardhi yote ni ya Imam, amani iwe juu yake, (juzuu ya 1 uk 476).[38]  Nahju Albalaagha (1/211).[39]  Nao ni: Ali, Fatuma, Hassani na Huseini – Mungu awawie radhi – kama ilivyotangulia.[40]  Kasfu al-ghummat, cha Al-ribaliyyu. (2/374).[41] “Ithibati Al-waswiyyat” Al-Masoudiyyu. (uk 196).[42] Al-Anuari Annumaaniyya (2/53).[43] Al-Anuaru Annumaaniyat, (2/55).[44]  Swaahib Al-wasaail ameipokea Imepokewa kutoka kwake. (juzu ya 3 uk 278) hadithi (1), pia tazama: "Furuu Alkaafii" cha Alkiliiniyyi (6/449).  [45]  Ameipokea katika Alkaafii(juzuu ya 2 uk 205) mlango wa kuvaa vyeusi, chapa ya Tehrani ya mwaka 1315 hijiriyya, ispokuwa katika kitabu hicho kuna: Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake na Aali zake, alikuwa anachukia weusi ispokuwa katika vitu vitatu: kwa kutanguliza kiremba kabla ya guo la Kisau.[46]  Imepokewa katika Alwasaailu (juzuu 3 uk 281 mlango wa 20 hadithi ya 3 katika milango ya nguo za  kusalia), Pia Assuduqi ameipokea katika Alfaqiihi (2/232): Amesema: Mkweli Rehema na amani ziwe juu yake aliulizwa vipi kuhusu kofia nyeusi? Akasema: Usisali nayo kwa hakika kofia nyeusi ni miongoni mwa nguo za watu wa motoni. Pia tazama: Wasaailu Shiat, (3/281).[47] Ameipokea katika: Man laa yahdharhu Alfaqiihu (juzu 1 uk 251), na mwenye Alwasaaili ameinukuu kutoka kwake katika (juzu 3 uk 278) katika milango ya mavazi ya msaliji. Na riwaya ya pili katika Alwasaaili katika (juzuu 3 uk 279 hadithi ya 7 katika milango ya mavazi ya msaliji ). Na imepokewa na Alfaqiihu (juzuu 2 uk 252) na Alkaafii (juzuu 2 uk 205). [48]  Au katika Al-ilalu Walkhiswaalu, kama ilivyo katika Alwasaailu, na ameipokea katika Alfaqiihu (juzuu 2 uk 252).[49] Ameipokea Alfaqiihu (juzuu 1 uk 252), Pia tazama: "Wasaailu Shiat" (4/384), na "bihaaru Al-anuaari" (3/291), (28/48).[50] Hayo yametajwa katika (1/26) katika uyuunul akhbaari. [51] Tazama: "Alkaafii" (1/239). [52]  Bihaaru Al-anuaari (26/37).[53]  Bihaaru Al-anuaari (26/37).[54]  Bihaaru Al-anuaari (26/56).[55]  Bihaaru Al-anuaari (27/65).[56]  "Usulu Alkaafii" (1/24).[57] Bihaaru Al-anuaari (26/41). [58] Albihaaru (26/41).[59] Albihaaru (26/48).[60]  Tazama "Usulu Alkaafii" (1/227).[61]  (1/45).[62]  (uk 51) chapa ya Lakhanu India.[63]  (uk 164) chapa ya kwanza 1396 Hijiriya.[64]  Tazama: Usuli Madh habu shia al-imaamia al-Ithnasheria, cha al-iqaariyyu. (1/418 na ya baada yake).[65]  "Usulu Alkaafii" (1/412).[66]  Marejeo yaliyotangulia (1/429).[67]  (Bihaaru Al-anuaari) (23/309).[68]  Tafsiri ya Al-ayyaashiyyu, (1/214), Tafsiri ya Asswaafiyyu (1/242).[69]  Tazama: Kitabu "Usuulu Alkaafii" (1/414).[70] Rejeo lililotangulia. (1/422).[71] Sharhu Usuuli Alkaafii" (7/66).[72]  Rejeo lililotangulia.[73] Rejeo lililotangulia. (5/301).[74] Tazama: Kitabu "Usuulu Alkaafii" (1/414).[75] Rejeo lililotangulia. (1/423).[76] Rejeo lililotangulia. (1/424).[77]   "Alkaafii" (1/149).[78]  Raudhatu Alkaafii (8/237).[79]  Kashfu Alghummati (2/360).[80]  Ukurasa wa 88, 143 na 188, chapa ya Beiruti.[81]  (2/66).[82] Ukurasa wa 583.[83] Tazama kitabu "swafwatu sherhu nahju Albalaaghat" (uk 593). [84] Allah Mtukufu amesema: {Kwa hakika Mwenyezi Mungu amewapa radhi Waumini walipofungamana nawe chini ya mti, na alijua yaliyomo nyoyoni mwao. Basi akateremsha utulivu juu yao, na akawalipa kwa Ushindi wa karibu.} Sura [48] Al-Fath 18.[85]  Tazama: "Tafsiri Al-Qummiyyi" (2/377), na "Alburhaanu" ya Albahraaniyyu" (4/358),[86]  Tazama: "Alkaafii" (5/7), "Kitabu cha Sulaimu bin Qabsi" (uk 362).[87] "Bihaaru Al-Anwaari" (75/421).[88] "Bihaaru Al-Anwaari" (75/421). "Mustad-raku Al-wasaali" (12/354).[89] Nayo ni kauli ya Mtume (SAW): "Kwa hakika nimekuachieni mazito mawili: kitabu cha Allah na Ahli baiti wangu." Imetolewa na Tirmiziy (5/328 – 329).[90] Imetolewa na Abuu Daudi (4/106) , na imesahihishwa na Albaniy katika Swahiihu Al-jaamii" (5180). Na Mashia wanatolea ushahidi hadithi hii. Lakini wamenda mchomo katika jina kama itakavyofuata![91] Kashfu al-ghummati fii Maarifati Al-aimmati" cha Arbaliyyi, (3./228), Amaaliyyu Atwuusiyyu" uk 362, "Ithibaatu Al-hudaatu" (3/594- 598).[92] Tazama "Alghaibatu", cha Atwuusiyyu, (uk 159 – 160).[93] Bihaaru Al-Anwaari (103/108).                                [94] Bihaaru Al-Anwaari (53/7).[95] Kitabu Taariikhu maa baada A-dhuhuri (uk 30).[96] Kitabu Taariikhu maa baada A-dhuhuri (uk 361). [97] Kitabu Alghaibatu cha Atwuusiyyu, (uk 420).[98] Taariikhu maa baada A-dhuhuri (uk 433).[99] Taariikhu maa baada A-dhuhuri (uk 436).[100] Alkaafii (1/338).[101] Taariikhu maa baada A-dhuhuri (uk 185).[102] "Usulu Alkaafii" (1/368). "Al-ghaibatu" cha Annuumaaniyyu (uk 197), "Alghaibatu", cha Atwuusiyyu, (uk 263). Bihaaru Al-Anwaari (52/117). [103] "Usulu Alkaafii" (1/368). "Alghaibatu" cha Annuumaaniyyu (uk 198),[104]  Nahju Assaadatu, (3/639).[105] Tazama: Tahdhiibu Al-wusuuli cha ibni Al-Mutwahar Al-huliy. (uk 70), na Al-Marji-iya Al-Diiniyyati Al-Uliyaa, cha Huseini Maatuuqi, (uk 16).[106]  Kwa faida tazama: Risaalatu "Takfiiru Shiia liumuumi Al-Muslimiina" ya Sheikh Al-Amaariyyu, Ametaja maandiko ya wazi mengi yanayowahusu Mashia wakiwakufurisha wasiokuwa wao. Na miongoni mwa wakufurishwa ni Wazeidiyya. [107]  Imepokewa na Bukhariyyu na Muslimu.[108]  Itazame katika "Usuulu Madhabu Al-sshiia Al-Imaamiyati" cha Sheikh Al-Qaffaariy (2/1131 – 1151). [109]  Tazama: "Aabadi Al-Shiia" (1/26), na kitabu "Sulaymu bin Qaysi" (uk 288). Na Biharu Al-Anwaaru" (27/212).[110] Tazama: Sherhu Nahju Albalagha cha ibni Abuu Al-Hjadiidu (juzuu ya 10 uk 581) chapa ya Irani, na Taariikhu Al-masuudiyyu Al-Shiiyy (juzu ya 2 uk 344) ya beiruti. [111] Tazama: Nahju Albalagha. Uk 325 – 340). Kimehakikiwa na Subhi Swaalihu.[112] "Sayri Aalaamu An-nubalaau" ya Ad-dhahabiyyu, (1/547).[113]  Rejeo lililotangulia (1/422).[114] Nahju Albalaagha, (uk 97).[115]  Wassaailu Asshiatu, (20/542).[116]  Kamaalu Addiini wa Tamaamu An-niimatu, (uk 105).[117] Imepokewa na Bukhariyyu na Muslmu[118] Alkhiswaalu, (uk 149 – 150), hadithi namba 182.[119] Alkashkuulu cha Al-Bahreiniyu (3/212), na kitabu  "Laqad Shayyaanii Al-Huseiniu" (uk 177). [120] Al-Anuwaaru An-nuumaaniyyatu, (1/63).[121] [122] Imepokewa na Bukhariyyu.[123] Maaliki bin Al-Ashtaru – Khutubatu Waaraauhu, (uk 89), na "Al-Futuuhu) cha Ibni Aathamu, (1/396). [124]  Al-Fiswalu fii Al-Milalu Wal`ahawaau Wannihalu, (4/235).[125] Bihaaru Al-Anuwaaru (26/28).[126] Yaani UImamu – kwa Mashia – ni kama Utume, nao ni upole kutoka kwa Allah. Kwa hiyo ni lazima katika kila zama kuwe na Imamu mwongozaji anakuwa khalifa wa Mtume katika kazi za kuongoza watu, kuwapa maelekezo na kupanga mambo yao na maslahi yao…. hadi mwisho. Tazama: "Al-Imaamatu wa Annaswu" cha Ustadhi Faisal Nuru, uk 290.[127] Na kuwa Maasumi kwa Mashia ina maana kuwa: (Imamu amekingwa na madhambi madogo na makubwa, haterezi katika fatwa wala hakosei katika kujibu, haghafiliki, hasahau, hafanyi upumbavu kwa chochote katika mambo ya kidunia". Kama ilivyo katika kitabu Mizani Al-Hikmati (1/174). Pia tazama: "Aqaaidu Al-Imaamiyati" (uk 51), na "Bihaaru Al-Anwaari" (25/350 – 351). [128] "Alkaafii" (8/256), "Bihaaru Al-Anwaari" (27/253).[129]  (2/985).[130] Imepokewa na Attwabaraaniyyu katika AlkAbuuru na katika Al-Auswatu (Majmaa Azzawaaidu 3/285).[131]  Tazama: "Al-Muhaddhabu" cha Ibni Al-Buraaju (1/13), (Al-Iidhwaahu" cha Ibni Shaadhaani (uk 454), "Wuswulu Al-Akhbaaru) cha Al-Aamiliyyu (uk 68).[132] Tanqiihu Al-Maqaali (3/142).[133]  Tazama: kitabu cha Sulaimu bin Qaisi  Al-Aamiriyyu, (uk 92). Na kitabu Al-Rawadhwatu min Alkaafii (8/245). Na "Hayaatu Al-Quluubi" cha Al-Majlisiyyu – Faarisiyyu – (2/ 640). [134] "Rijaalu Alkashiyyu", (uk 53).[135]  Usuulu Alkaafii, (i/247).[136] Rijaalu Alkashiyyu, (uk 53), "Muujamu Rijaali Al-Hadithi" cha Khuwaaiyyu, (12/81).[137] Rejeo lililotangulia, la Alkashiyyu. [138] Kashfu Al-Ghitwaai, cha Jafari Annajafiyyu, (uk 5), na Daairatu Al-Maarifu Al-Shi-iyyati cha Muhsini Al-Amiinni, (1/27).[139] Nahju Albalaagha, (uk 350), Tahakiki ya: Subhiyyu Al-Swaalihu.[140]  Bihaaru Al-Anwaaru, (25/351").[141] Bihaaru Al-Anwaari, (10/139). Annaaadiru cha Al-Ruwaandiyyu (uk 163).[142] Nasabu Quraishi cha Muswaa bin Azzubeiriyyu, (uk 45). Na Jamharatu Ansaabu Al-Arabu cha Ibni Hazmi (uk 87).[143] Nasabu Quraishi, (uk 53). Na Jamharatu Ansaabu Al-Arabu (uk 108).[144] Umdatu Twaalibu fii Ansaabu Aali Abuu Twaalibu, cha Ibni Anbatu Al-Shiiyyu, (uk 111), na twabakaatu ibn Saadi, (5/34).[145] Rawdhatu Al-Waahidhiina, (uk 260).[146] Uyuuni Akhibaari Al-Ridhwaa. (2/60).[147]  Imepokewa na Bukhariyyu.[148]  Aslu Al-Shia Wa Usuuluhaa, cha Muhammad Huseini Aalu Kaashifu Al-Ghatwaau. (uk 83).[149] Usulu Alkaafii, (2/20), Tafsiri Al-Abaashiyyu, (1/252 – 253), Al-Burhaanu, (1/386), Rijaalu Alkashiyyi, (uk 425).[150] Tanqiihu Al-Maqaali, (1/211).[151] Hao ni wafuasi wa Abdallah "Al-Aftwahu" bin Jafari Al-Swaadiq.[152] Hao ndio wale amabao walioishia kwa Musa bin Jafari na hawakukubali uImamu wa wale wa baada yake.[153] Wafuasi wa mtu aitwaye Naawuusu au ibni An-naawuusu. Nao wanasema kuwa Jafari bin Muhammad hajafa, naye ndiye Mahdiyu.[154] Kwa mfano: tazama: Rijaalu Alkashiyyu, (kurasa: 563, 565, 570, 612, 616, 597, 615).[155] Utangulizi wa Alkaafii, na Huseini Ali, "uk 25), raudhwaatu Al-jannaatu cha Alkhuwansaariyyu, (6/109), Asshia cha Muhammad Swaadiqu Asswadru, (uk 122).[156] Misbahu Al-faqiihi, (uk 426), Al-Ijitihadi wa At-qliidu, (uk 17).[157] Jaamiu Al-Maqaali fiimaa yataalaqu biahwaaali Al-hadiithi warrijaali, Al-Twariihiyyu, (uk 15).[158] Rejeo lililotangulia.[159]  Kutoka kwa: Muqtabisu Al-Athari, (3/73).[160] Bahaaru Al-Anwaaru, (101/369).[161] Usuulu Alkaafii, (1/181 – 184).[162] Tazama: Al-ghaibatu, (uk 106 – 107).[163] Thumma Abswartu Al-haqiiqata, Muhammad Saalim Alkhudhwaru, (uk 291 – 292).[164] Faswlu Alkhitwaabu fii Ithibaati Tahriifu Kitaabu Rabbi Al-Arbaabi (uk 211).[165]  Mashaariqu Al-Shumuusu Al-Duriyyatu (uk 126).[166] Adduraru Annajafiyatu cha Yusuf Al-Bahreniyyu, Muasasatu Aali al-beiti liihyaai Atturaathi (uk 298).[167] Thumma Abswarat Al-Haqiiqatu, (uk 294). [168] Al-Faswilu fii Al-Milali Wal-Ahwaau Wannihali (4/159 – 160).[169]  Al-Imaamu Al-Swaadiqi cha Muhammad Al-Hussein Al-Mudhwaffar. (uk 178).[170] Chanzo kilichotangulia katika ukurasa huo huo.[171]  Mashia katika historia, (uk 44 – 45).[172]  Minhaaji Alkaraama, (uk 72 – 73).[173]   Aayaani Al-Shiia, (1/3/uk 6).[174] Waaytu: Yaani niliyoahidi. Na Waayu yaani ahadi.[175] Nahju Albalaagha (Sherhe ibni Abuu Al-Hadiidi, 6/176).[176] Tazama: "Bihaaru Al-Anuwaari" (11/60), "Al-Maalimu Al-Zalfiyu" (uk 303).[177] "Al-Maalimu Al-Zalfiyu" (uk 303).[178] Wadaaiu Annubuwati" cha Al-Twahraaniyyu, (uk 155).[179]  Kwa mfano tazama: "Rijaalu Alkashii" (uk 27, 219, 445, 465), na "Rijaalu Annajaashiyyu" (uk 28, 53, 76, 86, 95, 139), na "Jaamiu Al-Ruwaatu" cha Al-Dibiiliyyu (1/413). [180]  "Al-Rawdhwatu cha Alkiliiniyyu), (uk 29).[181]  Swiraatu Annajaati, (2/452). Pia tazama "Al-Imaamatu wannaaswu" cha ustaadhi fayswalu Nuuru, uk  306.[182]  Alkaafii (8/295), pia taqzama  "Al-Bihaaru" (28/255) na "amaaliyyu Al-Twuusiyyu", uk 234.

المرفقات

2

Maswali YaliyowaongozaVijana wa Kishia Kuingia Katika Haki
Maswali YaliyowaongozaVijana wa Kishia Kuingia Katika Haki