البحث

عبارات مقترحة:

الشاكر

كلمة (شاكر) في اللغة اسم فاعل من الشُّكر، وهو الثناء، ويأتي...

البارئ

(البارئ): اسمٌ من أسماء الله الحسنى، يدل على صفة (البَرْءِ)، وهو...

القدير

كلمة (القدير) في اللغة صيغة مبالغة من القدرة، أو من التقدير،...

Nimefaidika kuwa na Maswahaba na wala sijapata hasara ya kuwakosa Aalbeiti

السواحلية - Kiswahili

المؤلف Aly bin muhammad Al Qudhwayby
القسم كتب وأبحاث
النوع نصي
اللغة السواحلية - Kiswahili
المفردات تفسير طبقة الصحابة
Nimefaidika kuwa na Maswahaba na wala sijapata hasara ya kuwakosa Aalbeiti Utangulizi Ukumbusho Imamu Al-Khuuiyu aonekana mwezini...!! Mambo yaliyonisumbua sana katika dhehebu hili... Kuwatusi na kuwalaani Maswahaba: Ndoa ya mutaa: Migongano inayoendelea ndani ya dhehebu hili... Na mchawi hafanikiwi popote afikapo…! Baadhi ya Taasubi (ubaguzi/chuki) zinaua! Historia ya Aalibeiti inakana itikadi ya Imaamiya kwa maandiko Mahdi anayesubiriwa Jina Mtu wa zama limenitikisa! Kwa hakika ni mshtuko mkubwa! Hiyo ni siku ya kulipiza kisasi! Kisa tumekiamini kwa kuwa hatutaki kufikiri Kwa nini wanamshambulia Al-Marjiu Muhammad Husein Fadhlullah?! (Swalaahu Al-Kaazimiy) na hofu ya kifo Ameenda hija akiwa Shia… na kurudi kutoka katika hija akiwa Sunni… Hitimisho  Nimefaidika kuwa na Maswahaba na wala sijapata hasara ya kuwakosa AalbeitiMiongoni mwa maneno ya Imamu Ali, Amani iwe juu yake: Kwa hakika nimewaona Maswahaba wa Muhammad, Rehema na amani ziwe juu yake, na wala sijapata kumuona mtu anayefanana nao. Nywele ziliwatimka na mavumbi kuwapata. Na usiku walikuwa wakisimama na kusujudu, wanajipumzisha kwa kulalia mbavu na mashavu yao. Wanasimama kama kaa la moto kwa kutajwa marejeo yao. Baina ya macho yao ni kama vile magoti ya mbuzi kwa kusujudu sana. Akitajwa Allah, macho yao yanabubujikwa na machozi hadi shingo za kanzu zao zinaloa. Wanayumbayumba kama miti inavyoyumba katika siku yenye kimbunga wakiogopa adhabu na kutarajia thawabu… hotuba namba (97)   katika Nahju Al-Balaagha. Abuu Khalifa Ali bin Muhammad Al-Qudhwaibiyu    Utangulizi Sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu. Sifa zenye uzuri na baraka.  Sifa zilizojaa mbinguni na Ardhini, na kujaa kila kitu kingine akitakacho Mola wetu. Rehema na amani  zimwendee chaguo la viumbe vyake, Mtume wake wa mwisho Muhammad. Pia, Rehema na amani ziwe juu ya Aali zake, Maswahaba zake na waliowafuatia kwa wema hadi siku ya Kiama.Ama baada ya haya:          Karatasi hizi tumeziandika kwa ajili yako wewe msomaji. Hizi ni miongoni mwa kurasa zilizonipitia maishani mwangu… Ndani yake nimejumuisha fikra na maswali yaliyoniongoza kufikia pale nisipopapangia hata siku moja. Kwa hakika huu ni mvutano mgumu katika maisha ya mwanadamu… ni mvutano baina ya haki na batili, ni mvutano baina ya itikadi za kurithi na uhakika uliowazi.Huo ni uzoefu, kwa mara ya kwanza, unaweza kuonesha utu wa mtu. Lakini sio hivyo, huu ni uzoefu wangu, wako na watu wengi, kwa wale waliozaliwa na kulelewa katika imani na ufahamu, walioutolea muhanga na kujitahidi kuulinda. Kisha waje kutambua kuwa haki ni kinyume chake, na kwamba ung`ang`anizi na unazi kwa itikadi ya jamaa, ndugu, ukoo, na ya mtoto huko ni kubadilisha kitu cha heri kwa kitu duni. Na yaliyo kwa Allah ndio bora na ndio yanayobakia.Abuu Khalifa Ali Al-Qudhwaibiyu27 / 3 / 2005 UkumbushoNimelelewa katika nyumba ya Kishia. Najikurubisha kwa Allah Mtukufu kwa kuyatumikia madhehebu yangu, kielimu na kiibada.Baba yangu alikufa nikiwa bado mdogo, mjomba wangu akabeba jukumu la kunilea mimi na wadogo zangu. Naye ni shehe mvaa kilemba,  amesomea katika moja ya madarasa ya elimu katika eneo la (Jadu Hafswi), nchini Baharein, kisha akakamilisha masomo yake katika mji wa (Quum) uliopo Iran.Alikuwa mwangalifu sana kwetu... akijitahidi tusichanganyike na marafiki wabaya, na wala tusifuate mkumbo wa mambo yatakayo tuharibia sifa na maadili yetu, na kumkasirisha Mola wetu, Mtukufu aliyetukuka... hadi kufikia kwamba, wakati alipojua kuwa nimenuia kujiunga na chuo cha muziki nitakapomaliza sekondari, ili niwe mwalimu wa muziki. Alikasirika sana na akanipinga akisema: Kwa  hakika udogoni mwangu sikuwa na mtu wa kuninasihi na kuniongoza, na nimeishi maisha magumu sana, kwa hiyo sikia nasaha zangu.Naweza kusema kuwa: Mjomba wangu alikua na nafasi kubwa sana katika kubadilisha mawazo haya ya muziki kichwani mwangu... na kwa kuongezea sababu nyingine, zilinizuia nisielekee mwelekeo huo.Ama mama yangu alikuwa akifanya bidii zote katika kushiriki kwenye matukio ya kidini (ya majonzi au ya furaha). Anafanya hivyo kwa kutarajia malipo na thawabu... kwa kuwa anamtumikia Imamu Husein.Hata magonjwa hayakuwa kikwazo kwake cha kuacha kushiriki. Alikuwa akiamini kwamba, kutoshiriki kwake ni maasi, na kushiriki kwake ndio kupona maradhi yake na ni baraka.Ama babu yangu (mzaa mama) katika maisha yake alikuwa akitengeneza ngoma za kimila zinazotumika katika kuandaa matembezi ya kujipigapiga na kujijeruhi katika misafara ya Huseiniya, na katika matembezi ya sherehe za mausiku ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani yanayoitwa (Usiku wa kuagana).Na wala hainipiti nikaacha kuashiria kuwa familia yangu yote nikiwemo na mimi mwenyewe, wakati huo tulikuwa wafuasi wa bwana Al-Khuuiyu.Na kwa vile mimi ni zao la mazingira haya ya kiwalii nilikuwa napenda kuhudhuria (maombolezo ya Haji Abbas) katika wilaya ya (Hamamu) mjini Manama tangu utotoni.Utotoni mwangu nilikuwa napupia sana kwenda mapema katika maombolezo ya kila tukio, ili nijihakikishie kuibeba bendera ambayo kikawaida inabebwa katika msafara wa Huseiniya, kabla haijachukuliwa na wenzangu. Na nilipokua kidogo, nikawa nashiriki katika msafara wa tanzia ya maombolezo hayo hayo kwa kujipiga (minyororo) ya mgongo.Shuleni nilikuwa na marafiki zangu tukipupia sana sherehe za kidini. Sherehe za kidini zilikuwa ni mashindano makubwa kwetu kuliko mambo ya shuleni. Kwani utoro wa kutoroka shule ulikuwa unakithiri sana katika matukio kama haya. Kwa hoja ya kushiriki katika matukio hayo, na hasa hasa, shule nilizosomea ni za Kishia. hatukuwa tukiulizwa juu ya utoro,  lakini tulikuwa tunapata uungwaji mkono kutoka kwa walimu.Na kwa huzuni kubwa, vijana wengi walikuwa wanafurahia kufika kwa matukio hayo. Kwa sababu walikuwa wakiona hiyo ndio nafasi ya dhahabu ya kutongoza wasichana. Kwa sababu ya wepesi wa kuchanganyika katika matukio haya. Na hakuna mwenye uwezo wala mwenye nguvu ispokua Allah...! Na kwa upande wa familia yangu, umuhimu wa nadhiri ulipewa kipaumbele kwa kiasi kikubwa. Shangazi yangu (dada ya baba yangu) daima, mimba zake zilikuwa zikiharibika. Afe mtoto kabla ya kuzaliwa, au afe baada ya kuzaliwa tu. Hali hii ilimrudia rudia mara nyingi, hadi ndugu zangu wakihisi kukata tamaa. Wakaweka nadhiri kwa imamu Ali kama atamjalia kupata mtoto na kumkinga na mabaya yote([1]) basi watakuwa wakimleta mtoto huyo, kila asubuhi ya siku ya Ashuuraa ya kila mwaka, wakiwa pamoja na msafara wa kujipiga na kujijeruhi. Huku mtoto huyo atakuwa akivaa sanda (yaani kitambaa cheupe) na damu za watakaoshiriki katika msafara wa kujipiga na kujijeruhi zitakuwa katika sanda hiyo. Kisha watampandisha farasi anayefanana na farasi wa imamu shahidi. Shangazi yangu akazaa mtoto na kumwita jina la (Uqaili)([2]). Kisha huyo Uqaili hakupitisha muda mrefu katika kutekeleza ile nadhiri, akatambua kuwa, hakuna kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allah pekee, na kuwa Imamu Ali ni mtu, na haifai kwa ibada kuelekezwa kwake wala kwa mtu mwingine, si kwa dua, wala kuomba msaada, wala kuweka nadhiri. Akamkinaisha baba yake uharamu wa nadhiri kama hii. Kwa hiyo suala hili likawa kumbukumbu ya hekaya za kujifurahisha akiwa pamoja na wenzake.Nami nina kisa kinafurahisha kama kisa cha (Uqaili). Nilipokuwa mtoto, nilifanyiwa upasuaji wa operesheni shingoni. Kisha kidonda hakikuchukua muda mrefu na baada ya siku chache kilifura/kilivimba na nikafanyiwa upasuaji wa pili.Mama yangu anasema: Hali yako ya kiafya ilikuwa mbaya sana... ulikuwa baina ya kuishi na kufa.Kwa ajili ya kuogopea nisije nikapatwa na tatizo, na kwa vile yeye ni mtu wa kawaida, mama yangu alikubali nasaha za mmoja wa Mamullah, za kumtaka aende katika maziara/makaburi yaliyopo Manama katika kitongoji cha Sakiya, aweke nadhiri maalumu kwa ajili yangu ili nipate afueni kutokana na maradhi yangu. Akiamini kama Mashia wengine wanavyoamini kuwa: Atabaati, makaburi, na watu waliozikwa ndani ya makaburi hayo wanaleta manufaa na kuondoa madhara. Kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake, mama yangu hakuweza kutimiza ahadi yake ya nadhiri hadi nikakua.Na pale nilipobadilika na kujiunga na itikadi ya Ahli Sunna waljamaa kwa uongofu wa Allah. Kisha watu wote wakajua kuhusu hilo,  ndugu zangu walitaka kunipa hoja za kuthibitisha kuwa, kubadilika kwangu na kujiunga na Ahli Sunna ni kuwakosea na kuwadhulumu Aalibeiti! Walinikumbushia ile nadhiri ya mama yangu na kuniambia kiwazi wazi: Kama si Aalibeiti usingepona ugonjwa wako na wala usingekuwa mzima hadi leo. Kisha haukupita muda, wakanionya nisipuuzie lile suala la nadhiri. Wakinihimiza niende nao kule makaburini kutekeleza ile nadhiri... ili nisije nikapatwa na mabaya au kupoteza uhai.Mara nyingi walijalibu kunikinaisha, niende nao kule makaburini. Pia walijaribu kunikinaisha nirudi katika Ushia, lakini majaribio yao hayakufanikiwa.La kuchekesha katika tukio hili ni kwamba, baada ya miaka mingi ya kulitukuza kaburi hilo na kumuomba msaada na kumwekea nadhiri mwenye kaburi hilo. Iligundulika kwamba, yote yaliyoibuliwa kuhusu kaburi hilo ni upotofu juu ya upotofu.([3]) Kwani baadaye, eneo lote hilo lilivunjwa, na Allah ndiye mwenye kustahiki kushukuriwa. Imamu Al-Khuuiyu aonekana mwezini...!!Baada ya kufa kwa imamu Al-Khuuiyu, naye ndio tegemezi kubwa na ni kiongozi katika maswala ya kielimu katika mji wa (Najafu). Baada ya kumaliza matembezi kwa ajili yake, ambapo tulibeba jeneza linalofanana na jeneza lake. Washiriki wa matembezi hayo walishtushwa na habari zilizotujia kutokea eneo la Al-Makhaariqatu zikiripoti kuonekana picha ya Al-Khuuiyu mwezini! Ingawa sisi hatukuiona picha hiyo, lakini baadhi ya watu wa Manama walilithibitisha hilo. Na haraka haraka uvumi huo ukaenea, na watu wengi wakausadiki na hasa hasa wanawake.Tulishangazwa na watu tuliokuwa nao katika msafara wakiashiria mwezini huku wakidai jambo hilo hilo. Rafiki yangu Ali akaniuliza: Je, unaona kitu? Nikamjibu: Hapana, akaniambia hata mimi sioni kitu. Kwa nini unadai pamoja nao ya kwambia unaiona picha ya Al-Khuuiyu wakati  huioni?! Akaniambia: Je, huoni hamasa waliyokuwa nayo?! Naogopa wasije wakanipiga! Tukacheka kutokana na tukio hilo.Mmoja wa wakazi wa Manama alikuwa na maelezo sahihi kuhusiana na hii habari ya uvumi wa ajabu. Siku hiyo alisema: Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, alipokufa hakuonekana mwezini, vipi aonekane Al-Khuuiyu?! Mambo yaliyonisumbua sana katika dhehebu hili...Kwa kuanzia na kabla ya kitu chochote, sijidai eti mimi nimefikia upeo wa juu wa tabia njema, upeo unaoweza kufikiwa na mwanadamu. Lakini kwa vyovyote vile, mwanadamu atakavyokuwa mnyenyekevu katika utamaduni wake au katika dini yake au kuwa na tabia za Kiislamu, kwa hakika kuna mistari mekundu ambayo haruhusiwi kuivuka. Na kama si hivyo, huyo mwanadamu atakuwa ameshajivua na kuacha maumbile sahihi na tabia njema.Mgongano wa hakika wa kwanza baina yangu na dhehebu nililokuwa nalifuata ulikuwa katika upande wa tabia.Mwazoni nilikuwa nikiipoza nafsi yangu, ya kwamba vitendo vya mtu binafsi ninavyoviona, havihusiani na dhehebu si kwa karibu au kwa mbali, hadi ikafika siku ambayo nilikuja kugundua ukweli na kuporomoka ile pazia iliyokuwa ikiuficha ukweli huo nisiujue.Mambo yaliyokuwa yakinisumbua sana katika dhehebu hili ni matatu:·        Kuwatusi Maswahaba na kuwalaani.·        Ndoa ya mutaa (ndoa za kustarehe kwa muda, sio za kudumu).·        Kumuomba asiyekuwa Allah na kushikamana na viumbe pasi na Allah aliyehai asiyekufa.Mambo matatu haya ndio yaliyokuwa utambi uliowasha mwanzo wa kubadilika kwangu kikweli kweli... kutoka katika akida/itikadi ya Imamiya niliyokulia na kulelewa katika dhehebu hilo, na kwenda katika akida ya Ahli Sunna na jamaa, ambao nililelewa kwa kuwachukia na kuwatazama kwa jicho la kuwachukia na kuwabughudhi. Kuwatusi na kuwalaani Maswahaba:Nilikuwa nikiwabughudhi Maswahaba, Allah awawie radhi, nikiamini kwamba wao wamewadhulumu Aalibeiti. Lakini jambo hilo halikunipelekea niwe nawatukana na kuwalaani.  Maswala haya kwa upande wangu niliyachukulia kuwa ni ya kimaadili bila kujali maoni yangu kuhusu Maswahaba wakati huo.Nilikuwa nikidhani kuwa matendo kama haya kamwe hayawezi kuwa ni wito wa kidini.  Sijawahi kusikia dini yoyote inawahimiza wafuasi wake wawatukane maiti na kuburudika kwa kuwalaani hadi wanapokwenda chooni – Allah atuepushe na hayo, – kama anavyosema (Umdatu Al-Muhaqiqiina Muhammad Al-Tuusiri Kani) katika kitabu chake “La-Aaliu Al-Akhbaari” (4/92): “Elewa kwamba, maeneo, nyakati na hali bora zaidi na yenye kufaa sana kuwalaani – lana ziwe juu yao – ni pale unapokuwa chooni. Sema kwa kila moja wao, wakati wa kuvua nguo, kujitakasa, na kujisafisha kwa kurudia rudia kwa moyo wako usiojali: Ewe Mola mlaani Omari kisha Abuu Bakari na Omari kisha Othumani na Omari kisha Muawiya na Omari... Ewe Mola mlani Aisha na Hafsa na Hindu na Umu Al-Hakami, na walani wale wote wanaopendezewa na matendo yao mpaka siku ya Kiama”!!!Lakini nilishangazwa kwamba, yale matendo niliyokuwa nikiyaona ni ya kinyaa na kuyakosoa ndani ya nafsi yangu, kwa hakika ni matunda ya fikra ya uchochezi dhidi ya Maswahaba wa Mtume wa Allah. Mapokeo yetu yaliachangia kwa uwazi kabisa kutuchokoza na kuchochea hisia zetu dhidi ya Maswahaba na yanayofungamana nao. zilianza kwa kuwakufurisha Maswahaba na kusema kuwa wameritadi. Kisha zikaja kuwalaani na kujiepusha nao. Yote haya yameandikwa na kuwekwa katika vitabu vyetu vile vya zamani na vya sasa kama inavyojulikana.Miongoni mwa haya ni yale yaliyokuja katika “Rijaalu Al-Kaashiyi”: ... kutoka kwa Hanani bin Sadayri, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abuu Jafari, Amani iwe juu yake, amesema: Watu walikuwa ni wenye kuritadi baada ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake ila watu watatu. Nikamuliza: hao watatu ni akina nani? Akasema: Hao ni Miqdad bin Al-Asuad, na Abuu Dhari Al-Ghaffaari, Salman Al-Faarisiyu, kisha baadaye kidogo, watu wakafahamu. Akasema: Hawa ndio wale waliosagwa na jiwe la kusagia nafaka na wakakataa kumpa baiyi Abuu Bakari hadi wakaletewa Amiiri Muuminiina kwa kulazimishwa naye akam`baiyi”([4]). Na riwaya nyingine zinasema: watatu hawa wameungana na wengine wanne, kwa hiyo idadi ya waumini – kama wanavyodai – katika kipindi cha Maswahaba ilifikia saba, lakini hawajavuka idadi hiyo.Na haya ndio yanayozungumzwa na riwaya kwa kusema: “kutoka kwa Al-Haarithi bin Al-Mughira Al-Nasriyi, amesema: nimemsikia Abdulmalik bin Aayuni! Akimuuliza Abdallah, Mungu amuwie radhi,  na hakuacha kuendelea kumuuliza hadi akamwambia: Kwa hiyo, watu wameangamia([5])! Akasema: Ee Wallahi ewe ibni Aayuni! Watu wote wameangamia, nikauliza: Je, watu wa mashariki na wa magharibi?! Akasema: Amesema: kwa hakika umefunguliwa kwa upotofu. Ee Wallahi wameangamia ispokuwa watu watatu kisha Abuu Saasaani akaungana nao”([6]). Madua dhidi ya  masanamu mawili ya Kiquraish na madua mengine yaliyojaa laana za kuwalaani mashehe wawili: Abu Bakari na Omari, na kuwafananisha na masanamu, Al-jibtu na Twaghuuti, hayako vingine ila ni matunda miongoni mwa matunda ya fikra hii ya uchochezi dhidi ya Maswahaba wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake.Nilisimama sana katika maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: [Na wale walio tangulia, wa kwanza, katika Wahajiri na Ansari, na walio wafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhika naye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa] [Tawba 100]. Nikaikuta aya hii ina andiko la wazi ya kwamba Allah Mtukufu amewaridhia Muhaajirina, Maanswari na wale waliotangulia kuamini, miongoni mwa hao kwa sifa za kipekee ni, Abuu Bakari, Omari, Athumani, Twalhata, Zuberi, Saadi bin Abuu Waqaasi, Abdallah bin Masoud na Saadi bin Muaazi, Allah awawie radhi... Wahesabu uwatakao miongoni mwa majina yanayolaaniwa na Mashia leo hii.Nikajiuliza: vipi mtu mwenye akili aone sawa kusema kwamba: Maswahaba wamemdhulumu Ali, Allah amuwie radhi, na kuupora ukhalifa. Wakati ambapo, Mola Mtukufu anatuambia katika aya hii kwamba yeye yupo radhi nao na amewaandalia Pepo zenye neema?! Ikiwa Maswahaba, wakiongozwa na makhalifa watatu: Abuu Bakari, Omari, Athumani, Allah awawie radhi. Na Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake alikufa akiwa radhi nao, na aya za kuwasifu zimeshuka na zinasomwa. Kisha wakarudi nyuma kwa kutumbukizwa katika fitina baada ya kufa kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake. Pia walituhumiwa kuwa wameipotosha Quran na kubadilisha hukumu za dini. Je! Allah alikuwa anajua kama Maswahaba hao watarejea nyuma baada ya kufa kwa Mtume wake au alikuwa hajui? Kama alikuwa analijua hilo, nalo ni jambo ambalo kila Muislam analielewa ya kwamba Allah Mtukufu anayajua yaliyokuwepo, yaliyopo na yatakayokuwepo. Kwa hiyo, ni nini hukumu ya aya zinazosomwa na ndani yake zinawasifia hao Maswahaba, wakati Maswahaba hao wamekuwa wanafiki na walioritadi kwa itikadi ya Mashia?!Je, Allah Mtukufu, aliyetakasika na kila dosari na upungufu, - Allah  anisamehe kwa kauli hii – alitaka kumhadaa Mtume wake kwa kuwasifu na kuwaridhia hao Maswahaba katika Quran pia, kuoleana kwao na Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, na namna Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake,  alivyowaamini, kisha waje kubadilika baada ya kufa kwake?!Je, fikra kama hii si aina ya upuuzi usiofaa kwa haki ya Allah Mtukufu nao ni kufuru?!!.Kwa nini Allah Mtukufu hakuzitaja ndani ya Quran sifa zao za hakika na namna watakavyokuwa baada ya kufa kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake?!Sikupata jibu la kunikinaisha, isipokua kusema kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyewaridhia na kuwabashiria pepo katika Quran na kwa ulimi wa Mtume wake, Rehema na amani ziwe juu yake, anajua kuwa wataendelea katika uongofu na sunna za Mtume wake, Rehema na amani ziwe juu yake: (Kwa hakika Mwenyezi Mungu amewapa radhi Waumini walipofungamana nawe chini ya mti, na alijua yaliyomo nyoyoni mwao. Basi akateremsha utulivu juu yao, na akawalipa kwa Ushindi wa karibu). [Al-Fat-hi 18]. (Na wale tulioambiwa ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alijua  yaliyomo katika nyoyo zao, na akawaridhia, na kuwashushia utulivu katika nyoyo zao. Kwa hiyo, si halali kwa mtu yoyote kusita katika mambo yao wala kuwatilia shaka kabisa)”.([7])  Ndoa ya mutaa:Ama ndoa za mutaa ijapokuwa ni halali – bali ni jambo linalopendeza – kwetu sisi kama Mashia. Lakini, kwa hakika, katika nafsi yangu kulikuwa na kitu tangu mwanzoni, kabla ya macho yangu kuona ushahidi unaoharamisha ndoa hizo, kwani ndoa hizo nilikuwa nikizipinga. Na nilipokuwa nikimsikia mtu anajadili ili kuzihalalisha, nilikuwa naona aibu kujiunga naye katika mazungumzo, na huwa namuuliza tu: Je, utakubali dada yako aolewe kwa ndoa hiyo?? Anajibu kwa kuona haya "hapana" na wakati mwingine jibu liliambatana na hasira.Kwa hakika kuhalalishwa ndoa ya mutaa kulikuwa kwa muda maalum tena kwa dharura.([8]) kisha Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, akaiharamisha hadi siku ya kiama katika hadithi sahihi na za wazi... na jambo la kushangaza ni kukuta katika urithi wa Kishia riwaya za maimamu wa Aalibeiti zikielezea kwa uwazi uharamu na ubaya wa ndoa za mutaa. Kisha hautapata mwitiko kutoka kwa kaumu yetu kuhusiana na riwaya hizi.Kutoka kwa Abdallah bin Sinaani amesema: "Nilimuliza Abaa Abdallah, Amani iwe juu yake, kuhusiana na mutaa. Akasema: usiichafue nafsi yako kwa ndoa hiyo".Na kutoka kwa Ali bin Yaqtiini amesema: "Nilimuliza Abaa Al-Hasan, Amani iwe juu yake, kuhusiana na mutaa. Akasema: Wewe inakuhusu nini ndoa hiyo, wakati Allah ameshakutosheleza na huna haja nayo?!”Na kutoka kwa Hishamu bin Al-Hakamu kutoka kwa Abdallah, Amani iwe juu yake, amesema: "Hakuna anayeifanya ndoa hiyo kwetu ispokua waovu"([9]). Ama Al-Tuusiyu amepokea katika "Al-Istibswaaru" (3/142) kutoka kwa Amru bin Khalid kutoka kwa Zaid bin Ali kutoka kwa baba zake kutoka kwa Ali amesema: “Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, ameharamisha nyama ya punda kihongwe na ndoa za mutaa".Hawakupata pa kutokea, katika riwaya hii zaidi ya kusema: "Ufafanuzi wa riwaya hii, ni kuichukulia kuwa ni taqiya[10], kwa sababu inakubaliana na madhehebu ya Al-aammati”![11] Kaikana kwa kuwa inaafikiana na msimamo wa Masunni, ingawa ni sahihi kwake yeye!  Migongano inayoendelea ndani ya dhehebu hili...          Tangu utotoni tulijifunza kuyahuisha yale mausiku ya Ashuraa kwa kijipiga piga na kupiga kelele huku tunataja yaliyompata Abuu Abdallah, Amani iwe juu yake. Lakini nani katika sisi aliyefikiri japo kidogo kuhusu haya tunayoyafanya. Je, yana mandiko ya sheria ya dini kutoka katika Quran na Sunna au ushahidi unalaani yale tunayoyafanya?!... Hakuna hata mtu mmoja...! Miaka mingi ya umuri wangu imepita na mimi nikiwa katika hali hiyo hadi yakanitokea mabadiliko yalionipelekea katika Usunni.Katika maisha yangu yote, sidhanii kama nimeishi kwa makosa, kuliko nilivyoishi katika kipindi hicho.Mwanazuoni mtegemewa Al-Tabriiziyu anaulizwa kuhusu matendo ya ibada ya Husseiniya: ushahidi wake ni nini kisheria? Anajibu kwa kusema: “Mashia wa wakati wa maimamu walikuwa wakiishi kwa taqiya. Ama kutokuwepo kwa matendo ya ibada hizi katika wakati wao ni kwa sababu hakukuwa na uwezekano wa hilo. Na hili halijulishi kwamba matendo haya si ya kisheria katika zama hizi. Lau kama Mashia wa wakati huo wangekuwa wanaishi kama tunavyoishi sisi katika zama hizi, ambapo kuna uwezekano wa kudhihirisha matendo ya ibada hiyo na kuitekeleza, wangeifanya kama tunavyoifanya. Kama vile kusimika bendera nyeusi katika milango ya Husseiniyaati, vilevile nafasi ya kuonesha huzuni”.[12]Haya masuala ni ya kuonwa mazuri na baadhi ya wanazuoni wa dhehebu hili. Wala hakuna andiko la Quran au sunna linallojulisha kuwa haya masuala yanayofanywa katika siku tukufu kwa jina la “Kuhuisha matendo ya ibada ya Allah Mtukufu” ni ya kisheria. Wakati ambapo mwenye kutazama katika riwaya nyingi za maimamu wa Aalibeiti na maneno ya wanazuoni wa zamani wa Kishia anapata kitu kingine. Ibn Babaweih Al-Qummiyu ametaja katika "Man la Yahdhuruhu Al-Faqiihi" (4/376), kuwa miongoni mwa maneno ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, ambayo hayajatanguliwa ni "Kulia kwa kupiga kelele ni miongoni mwa matendo ya zama za kijinga".Al-Nuuriyu Al-Twabrisiyu amepokea katika "Mustadiraku Al-Wasaili" (1/143 – 144) kutoka kwa Ali, Amani iwe juu yake, amesema: “Mambo matatu ni miongoni mwa matendo ya zama za kijinga, watu hawataacha kuendelea nayo hadi kusimama kwa kiama: kuomba mvua kwa kuzielekea nyota, kuaibishana kwa nasaba, na kulilia maiti kwa makelele".Muhammad Baaqiru Al-Majlisiyu amepokea katika "Bihaari Al-Anwaari" kutoka kwa Ali, Amani iwe juu yake, amesema: Wakati Ibrahim mtoto wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, alipokufa. Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, aliniamrisha nikamwosha naye akamvika sanda na kumpaka marashi. Kisha akaniambia: "Ewe Ali mmbebe" nikambeba hadi nikamfikisha Baqii. Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake,  akamswalia... na alipomuona amewekwa kaburini alilia na waumini wakalia kwa kulia kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, hadi sauti za wanaume zikapaza kuliko sauti za wanaake.  Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, aliwakataza vikali, na kusema: “Macho yanatoa machozi,  Moyo unahuzunika, wala hatusemi yale yanayomchukiza Mola. Sisi kwa  hakika kwako wewe Ibrahim tumepata msiba na kwa hakika, kwa ajili yako, sisi ni wenye kuhuzunishwa...)([13]).     Tazama msimamo wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, na msimamo wa Imamu Ali, Amani iwe juu yake, dhidi ya kulia kwa kelele...  Pia tazama namna katazo la kukataza kulia kwa makelele na kuelezwa kuwa jambo hilo ni miongoni mwa matendo ya kijinga kisha likageuka na kuwa na hukumu ya (kuhalalishwa)?!Na kwa sababu ya uwazi wa maandiko yanayokemea kulia kwa kelele, Al-Tuusiyu na Ibnu Hamza wameharamisha kulia kwa makelele. Huku Al-Tuusiyu akieleza kuwa kuna Ijimai (Makubaliano ya wanazuoni wote) wa zama zake, kuwa jambo hilo ni haramu([14]).Riwaya zimeeleza kuwa kupiga uso na kifua ni bidaa([15]) mbaya sana isiyoridhiwa na Allah Mtukufu wala Mtume wake, Rehema na amani ziwe juu yake, wala Maimamu wema. Imamu Al-Baaqir  amesema: “Kukosa subira kuliko kukubwa kabisa ni kulia kwa makelele ya kuomba shari, kupayuka, kupiga uso na kifua, na kukata nywele za utosi. Na mwenye kulia kwa makelele, ameshaacha subira na amefuata njia ya kinyume chake”([16]).Imepokewa kuwa Imamu Husein amemwambia Zainabu, “Ewe dada yangu, mche Mwenyezi Mungu, na uomboleze kama anavyotaka Allah. Pia fahamu kwamba, vya ardhini vinakufa, na vya mbinguni havibaki. Na kila kitu kitaangamia ispokuwa Allah Mtukufu aliyeumba viumbe kwa uwezo wake, navyo vitarejea kwake. Na Allah ni mmoja wa pekee. Baba yangu ni mbora kuliko mimi, mama yangu ni mbora kuliko mimi, na kaka yangu ni mbora kuliko mimi. Na mimi ni kigezo kwa kila Muislam anayemkubali Mtume wa Allah.” Akamsubirisha kwa mtindo huu, kisha akamwambia: “Ewe! dada yangu, Nimekuapia, kwa hiyo nitakase na kiapo changu, pindi nikiuliwa, usipasue nguo kwa ajili yangu, wala usijeruhi uso wako kwa ajili yangu, wala usijiombee shari na kuangamia kwa ajili yangu”([17]). Kwa ajili hii, Muhammad bin Makkiyu Al-Aamiliyyu “Asshahiidu Al-Awwalu” amenukuu kutoka kwa Al-Tuusiyu akisema: “Ni haramu kujipiga, kujichuna na kukata nywele kwa mujibu wa ijimai. Ameyasema hayo katika kitabu “Al-Mabusuutwu” kwa vile matendo hayo ni kuchukia hukumu ya Allah”([18]). Ama kuvaa nguo nyeusi, inakutosha kauli ya Imamu Ali, Amani iwe juu yake, “Msivae nguo nyeusi, kwani hizo ni nguo za Firauni”([19]).Mbele ya riwaya hizi zinazoharamisha kulia kwa kupiga kelele, kujipiga na kuvaa nguo nyeusi, nilitahayari, sijui nifanyeje baina ya riwaya hizi na hali halisi inayoumiza niliyolelewa nayo, huku nikidhani kuwa yale ninayoyafanya yaelezea mapenzi yangu kwa Aalibeiti. Wala sikuwa najua kuwa yale tuliyokuwa tunayafanya katika maadhimisho ya Al-Huseiniya na matanga ni ukiukwaji wa wazi wa usia na maneno ya Aalibeiti na maneno ya babu yao Mustafa, Rehema na amani ziwe juu yake. Na mchawi hafanikiwi popote afikapo…!Katika eneo letu la Al-Qudhwaibiya([20]) kuna mtu mashuhuri kwa kutibu wagonjwa na kuondoa matatizo ya watu kwa kutumia Quran na dua zinazokubalika kisheria. Baada kujibadili na kuingia katika itikadi ya Ahlu Sunna Waljamaa, huku ndugu zangu, marafiki zangu na wengineo wakishindwa kunirejesha katika Ushia. Wakaeneza uvumi wa kichochezi kunihusu mimi, ili wanibane na kuniporomosha.Basi huyo mtu mashuhuri aliyekuwa akidhaniwa na Mashia kuwa ni miongoni mwa wanazuoni na ni mwema alijitolea kunikinaisha niache maamuzi yangu, kwa hiyo akanikaribia, na kwa njia za kidiplomasia akanitajia kuwa baba yake alikuwa ni rafiki wa baba yangu Allah amrehemu. Kisha akaanza kutaja mambo kadhaa. Miongoni mwayo, alinifungulia msahafu bila ya kukusudia sehemu maalum huku akisema maneno nisiyoyajua. Kisha akaniambia: Soma aya hii nami nikaisoma... Tahamaki nikakuta ni aya, ambayo kwa madai ya mtu huyo, eti aya hiyo inanionya niache niliyokuwa nayo!!Akaniambia: aya hii ni rehema... nayo ni heri kwako kama utaitekeleza, na utaisikia zaidi ya mara moja usiku huu huu ili kuhakikisha heri yako!Na kama alivyosema... punde tu nilipopanda gari yangu na kufungua redio idhaa ya Quran Tukufu... tahamaki naiskia aya ile ile!Akatabasamu huku akisema: Hakika Allah anakupenda! Na utafanikiwa maishani mwako kama utaitekeleza aya hii.Na nilipofika nyumbani nilifungua Tv na kushangazwa na aya ile ile!Nikafikiria aliyoyasema... na haraka haraka nilifungua msahafu niliokuwa nao hapo nyumbani na kwa mtindo wa kufungua ovyo ovyo, nikashangazwa kwa kuikuta aya ile ile!Usiku huo sikulala... sio kwa kumhofia au kuhofia yale anayoyatoa ila yale yaliyonitokea yameteka fikra zangu, nikajilaza huku nafikiria: “Vipi kauli yake imekuwa kweli katika hili na lile?! Vipi initokezee hivi na vile, vipi? vipi?” Baada ya siku chache, rafiki yangu wa Kishia wa maeneo hayo hayo alinishtua kwa kuniambia: Nimewasikia watu wa eneo hili wakisema kuwa eti fulani – akikusudia yule mtu mashuhuri kwa usomi na wema – amewaambia kuwa ametabiri kwamba hivi karibuni (Al-Qudhaibiyu) atarejea katika Ushia kama alivyokuwa zamani. Nikacheka na kusema: Je, huyu mtu wetu anajua ghaibu (yaliyofichikana) au ni mchawi?!Na hapo hapo nikaanza kufikiria yale niliyosema. Ndio... Kwa nini asiwe mchawi?!Niliunganisha baina ya maneno ya rafiki yangu na maneno yake alipokuwa nami na ile aya iliyokuwa ikinirudia rudia.Nikajiuliza: Mtu huyu anataka nini hasa kutoka kwangu?Nikamuulizia kwa rafiki yangu mwingine wa eneo hilo hilo, naye akaniambia kuwa huyo mtu Mashuhuri si mwema kama wanavyomdhania watu wa eneo hilo. Lakini mtu huyo anatumia majini. Siku zilipita huku yule mtu akijaribu kunikinaisha kuwa ananitakia heri. Na kwamba heri ipo katika kufuata dhehebu la Aalibeiti. Allah awatakase Aalibeiti waepukane na mtu huyo na wale walio mfano wake.Nikapenda nimjaribu ili nitoe yaliyo ndani yake. Nakajiingiza katika kujadiliana naye kuhusu tauhidi na shirki katika vikao vingi. Nikamuona anashindwa kujibu maswali niliyomuuliza na hoja nilizomuelekezea.Na katika kikao kimojawapo kilichokusanya idadi kubwa ya Mashia na baadhi ya Ahlu Sunna wa eneo hilo. Nilimpa baadhi ya maswali yanayofungamana na shirki, nikamtajia yale aliyonifanyia usiku ule uliopita. Hakuweza kujibu, ispokuwa aliwaduwaza watu wote kwa kukimbia kikao. Uhakika wake ukafichuka na akafedheheka.Wakati huo nikakumbuka kauli ya Allah Mtukufu: “...Namchawi hafanikiwi popote afikapo…” (Twaha 69)   Na kauli ya Allah Mtukufu Aliyetukuka: “... Hakika hila za Shetani ni dhaifu”. (Annisaai 76).Lakini yule jamaa yetu hakutosheka na hayo, na akatoa juhudi zake zote ili awaepushe watu wa eneo hilo waepukane nami. Ili wasiathirike nami, akidai eti mimi nina nia mbaya!Lakini majaribio yake yaalishindwa, na akafedheheka na watu wakajua uhakika wake. Na tangu siku hiyo akwa hatoki sana nyumbani kwake, na akajulikana pale kitongojini kwa jina la “Mchawi” na kila anapokutana na mtu wa eneo hilo alijaribu kujitafutia sababu za kujisafisha huku akidai kuwa, kile kilichompelekea kufanya aliyoyafanya ni kwa lengo la kutaka heri.Sijui huyu mtu anajiweka wapi na aya na hadithi za wazi wazi zinazolaani uchawi na wachawi na kueleza kuwa watu hao ni makafiri!!Kisha ni haki gani anayoitetea kwa kutumia uchawi na mazingaombwe badala ya hoja na ushahidi?!Hii hapa ni riwaya yetu inasema: Kwa hakika Mtume wa Allah, Rehema na amani ziwe juu yake amesema: “Jiepusheni na mambo saba yenye kuangamiza”, wakauliza: Ni yepi hayo? Akasema: “Shirki na Uchawi...”[21]Kutoka kwa Imamu Jafari Asswaadiqu, amani iwe juu yake, kutoka kwa babu yake ambaye ni Ali, Amani iwe juu yake amesema: “Mwenye kujifundisha chochote miongoni mwa uchawi, iwe kidogo au mwingi ameshakufuru”.[22] Na kutoka kwa Imamu Ali, Amani iwe juu yake amesema: “Atakayemwendea mpiga ramli na kumsadiki yale anayosema, ameshayakufuru yaliyoteremshwa kwa muhammad”([23]). Baadhi ya Taasubi (ubaguzi/chuki) zinaua!Taasubi zinapofikia upeo wa juu zinaondosha upole na utu kutoka kwa watu, na kuonesha matukio ya kuchekesha na kuliza kwa wakati mmoja.Nataja matukio mawili miongoni mwa matukio hayo: mojawapo limenitokezea mimi mwenyewe baada ya kuingia Usunni na lingine limentokea mtoto mdogo asiyeelewa chochote katika mambo yetu ya kibaguzi na chuki zilizoangamiza vibichi na vikavu. Nilikuwa nje ya msikiti baada ya kumaliza swala ya laasiri. Ghafla mwanamke wa Kishia anayeitwa (Mama Ibrahimu) ambaye ni mzee, na ananijua na kuwajua ndugu zangu vizuri sana, aliniona.Alikuwa amebeba mfuko mkononi ukiwa na mahitaji ya nyumbani. Baada ya kumsalimia, aliniuliza ajue hali yangu na hali ya babu yangu, mama yangu na ndugu zangu. Kisha nikampokea ule mfuko ili nimsaidie kuubeba na kuufikisha nyumbani kwake ambako ni karibu na msikitini. Tulipofika nymbani kwake akaniuliza: Hivi umetokea wapi? Nikamjibu huku nikiashiria msikitini bila kujijua: “Natoka msikitini”. Akanikasirikia na kunitemea mate usoni huku akisema: Allah autie weusi uso wako! Nimeambiwa kuwa: ummebadilika na kuingia Ahli Sunna, lakini sikuwasadiki!Ama kisa cha mtoto (Omari bin Ali) nimesimuliwa na mmoja wa ami zake kwa kusema: Bibi wa (Omari) ambaye ni mzee (ni miongoni mwa wakazi wa Al-Qudhwaibiya, ana mahusiano makubwa na wanawake wa Kishia katika eneo hilo, kiasi cha kufikia wakati mwingine alikuwa anakaa nao katika matanga.Siku moja bibi huyo alikaa nao huku akiwa na mjukuu wake ambaye jina lake ni (Omari). Na (Omari) alikuwa na umri mdogo hawezi hata kutamka jina lake kwa sababu ya udogo wake. Omari alikuwa anacheza uani katika matanga hayo pamoja na watoto wengine na alipoanguka alilia. Mmoja wa wanawake (wa moja ya maeneo ya jirani na eneo letu) alijaribu kumbembeleza ili atulie na aache kulia. Akamuuliza: Jina lako nani ewe mwanangu? Yule mtoto akamjibu kwa kusema: Umalu, yaani (Omari). Akamuuliza tena kwa vile hakumfahamu anachokusudia kwa sababu ya matamshi yake. Yule mtoto akarejea jibu lile lile. Na hapo bibi ya mtoto akamjibia – na hilo lilikuwa mbele ya wanawake – huku akisema: jina lake ni (Omari). Bibi akapigwa bumbuwazi na yule mwanamke, alipomsukuma yule mtoto huku akimwambia yule mtoto: Tokaa... Allah akulani na amlani Omari na aliyekupa jina la Omari na yoyote anayemwita mtoto wake kwa jina la Omari...![24] Hapo yule bibi akatoka matangani bila ya kurejea tena.  Historia ya Aalibeiti inakana itikadi ya Imaamiya kwa maandikoMwenye kutazama kwa makini katika urithi wa historia ya Shia atakuta kuwa, itikadi ya Uimamu inayofuatwa na Mashia na kuwafanyia wengine uadui kwa ajili ya itikadi hiyo, leo hii, kwa hakika haikukamilika wala haikuwa na alama za wazi kwa Mashia wenyewe hadi alipokufa Imamu Alhassan Al-Askariyu na matokeo yake kugawanyika kwa Mashia na kuwa makundi mengi baada ya kifo chake. Miongoni mwayo ni Imaamiya, Ithnaashariya na Ismailiya. Fikra ya kimapinduzi dhidi ya Al-Umawiyiina na Al-Abbasiyiina, na fikra ya haki ya Al-Alawiyiina kuwa makhalifa ndio zinazotawala kwa Mashia wote. Na hizo ndio cheche zilizoanzisha kila kundi la Kishia kwa wakati huo bila kuanisha idadi ya majina ya maimamu kumi na wawili.Kwa hiyo Mashia wengi walikuwa hawatofautishi maimamu wa Aalibeiti, ispokuwa Mashia walikuwa wanajichanganya katika kila vuguvugu linaloanzishwa na Imamu au mwanamapinduzi yoyote. Kama ilivyotokea katika vuguvugu la Imamu Zaidi bin Ali na vuguvugu la Dhii An-nafsi Al-zakkiya na wengineo. Na tukitazama kwa kina katika kipindi cha baada ya mauaji ya Husein, Amani iwe juu yake, kwa sifa ya kipekee, tunaona kuwa Ali bin Hassan (Zeini Al-Aabidiina), Amani iwe juu yake, ni Imamu wa nne kwa Ithnaashariya – Imamu huyu amejitenga na siasa za Kishia na kuacha uongozi uchukuliwe na mmoja wa maimamu wa Aalibeiti wa zama zake, ili awaongoze Mashia na kuyashughulikia matatizo na mapinduzi yao. Naye akajishughulisha kwa ibadi na akajulikana kuwa yeye ni mwenye kuipa nyongo dunia na ni mwingi wa kuswali... hadi Al-Mufiidu na Al-Arbiliyu wametaja kuwa (Zeini Al-Aabidiina alikuwa anaswali kila siku rakaa elfu moja).[25]  Na jumla ya yanayotajwa kumuhusu huyu Imamu mcha Mungu ni mawaiza, dua na baadhi ya hukumu za kisheria zinazotolewa fat-waa na wanazuoni.Pengo hili lililowazi linalohusu namna Zeini Al-Aabidiina alivyoacha kuchukua Uimamu limewafanya wanazuoni wa Kishia wa Ithnaashariya wapupie kuliziba pengo hilo kwa kutaja visa na miujiza ya Imamu huyu, huku wakimsifu kwa lengo la kumthibitishia Uimamu. Ingawa hali halisi ya Mashia wa wakati huo ilikuwa ikiashiria namna wanavyomuheshimu na kukiri elimu yake na ubora wake. Na sio kwa vile yeye ni kiongozi wa kisiasa au ni Imamu.[26] Kwa ajili hii Zaidi bin Ali, Amani iwe juu yake, alipofika Kufa, alishtushwa na nadharia (Muumin altwaaqi) na wale waliokuwa pamoja naye. Nadharia hiyo inasema kuwa Imamu ni baba wa Zaidi ambaye ni Ali bin Husein (Zeini Al-Aabidiina), Zaidi bin Ali akamwambia Muumin altwaaq, alipokuwa akiongea naye: “Ewe Abuu Jafari, nilikuwa nakaa na baba – Ali bin Husein – katika meza, naye alikuwa akinilisha nyama iliyonona, na akinipozea tonge la moto hadi linapoa na hiyo ni kwa ajili ya kunihurumia. Je, baba huyo hajanionea huruma mimi niepukane na moto, kwa kukwambia wewe mambo ya dini na kuacha kuniambia mimi mambo hayo?!” Muumin altwaaqi akamjibu huku akisema: “Nimefanywa fidia yako! Kutokana na upole wake kwako usiingie motoni hajakueleza, ameogopea usije ukayakataa na matokeo yake utaingia motoni ndio maana akanieleza mimi... Na kama nikiyakubali nitaokoka, na nisipoyakubali hajali endapo nitaingia motoni. Kama Yaqubu alivyowaficha ile ndoto watoto wake”!![27]Tazama wazo hilo...! mtoto wa Imamu hajui uimamu wa baba yake wala hajamsikia baba yake katika zama zake akieleza fikra za kuutetea uimamu kisha anakuja (Muumin altwaaqi) na walio mfano wake miongoni mwa watu wa Kuufa wakileta madai kama haya baada ya kufa kwa baba yake (Zeini Al-Aabidiina)!Upande huu wa historia ya Ushia haupaswi kupuuzwa, pia kuna pande nyingine nyingi ambazo zinatosha kutengua Uimamu wa maandiko.Kuna hadithi nyingi za Kishia zinazoelezea wazi wazi kuwa kuna uwezekano kwa Mashia kutomjua Imamu wao. Na riwaya hizo zinawawekea Mashia msimamo wa kuufuata katika hali kama hizo. Na jambo hili haliingii akilini katika itikadi ya Uimamu kwa maandiko, itikadi ambayo inamuwajibisha kila Shia aamini Maimamu kumi na wawili na kuwajua majina yao, pamoja na watoto zao.Al-Kiliiniyu amepokea katika “Al-kaafii” kuwa mtu mmoja alimuuliza baba Abdallah, Amani iwe juu yake, kwa kusema: nikiamka asubuhi na kufika ijioni nami simuoni imamu wa kumfuata nifanye nini?... Akasema: “Mpende unayempenda, na mbughudhi unayembughuzi mpaka Allah Mtukufu Aliyetukuka akudhihirihishie” ([28]).Na Al-Swaduuq amepokea kutoka kwa Imamu Al-Swaadiq kauli ifuatayo: “Mtakuwaje endapo mtakaa muda mrefu katika umri wenu na hamumjui imamu wenu?... Akaulizwa: Kama itakuwa hivyo tufanye vipi? Akasema: Shikamaneni na wa mwanzo hadi mbainishiwe”.[29]     Al-Kiliiniyu, Al-Swaduuq na Al-Mufiidu wamepokea kutoka kwa Issa bin Abdallah Al-Alawiyu Al-Amriyu kutoka kwa Abuu Abdallah Jafari bin Muhammad, Amani iwe juu yake, amesema: “Nilimwambia: Niwe fidia yako! Endapo kutatokea la kutokea, na ikaja siku, Allah hanioneshi – kwa hapo nimfuate imamu gani? Akasema: Akasema: Akaashiria kwa Musa. Nikasema: Je, Musa akiondoka nimfuate imamu gani? Akasema: mfuate mwanawe, nikamuuliza: Huyo mwanawe akiondoka huku ameacha  kaka mkubwa na mtoto wake mdogo, hapo nimfuate imamu gani? Akasema: mfuate mwanawe, kisha ndio hivyo hivyo milele. Nikamuuliza: Kama sitomjua na sitojua sehemu alipo nifanyeje?... Akasema: Sema: Allahu mimi namtawalisha yule aliyebakia miongoni mwa hoja wako katika kizazi cha Imamu aliyepita...! Kwa hakika hilo linakutosha”!!Kuna riwaya nyingine kutoka kwa Zuraara bin Aayuni na Yaqubu bin Shaibu na Abdi Al-Aalaa zinaeleza kuwa wao walimuuliza Imamu Al-Swaadiq: Endapo tukio litamtokea imamu watu wafanye nini? Akasema: wawe kama Allah alivyosema: “...Lakini kwa nini hawatoki baadhi katika kila kundi miongoni mwao, wakajifunze vyema Dini, na kisha waje kuwaonya wenzao watakapo warejea, ili wapate kujihadharisha” (Tawba 122).Nikamuuliza sasa watakuwa na hali gani? Akasema: hao wana udhuru. Nikamwambia, niwe fidia yako! Wanaongoja hadi warejee wanazuoni watakuwa na hali gani? Akasema: Allah akurehemu! Hivi hujajua kuwa baina ya Issa na Muhammad kulikuwa na miaka mia tano na watu walikufa wakiwa katika dini ya Issa huku wakisubiri dini ya Muhammad na Allah akawapa malipo yao mara mbili?! Nikasema: Je, kama tukihama na baadhi yetu wakafia njiani? Akasema: “Na anayetoka nyumbani kwake kuhama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kisha yakamfika mauti njiani basi umethibiti ujira wake kwa Mwenyezi Mungu. (An-nisaai 100).Nikasema: tukafika Madina na kumkuta mwenye jambo hili akiwa amefungiwa mlango na kulegezewa paziwa. Akasema: Jambo hili haliwi ila kwa maamrisho ya wazi. Naye ndio yule ambaye ukiingia Madina sema: Fulani ameusia nani? Wakasema: kwa fulani.[30]Pia kuna riwaya nyingi zinazoashiria kuwa maimamu wenyewe hawana maarifa ya kujua uimamu wao au uimamu wa watakaokuja baada yao ispokuwa wakati wa karibu na kufa kwao. Zaidi ya hayo Mashia Imamia wenyewe walikuwa wakitumbukia katika tahayari na hitilafu baada ya kufariki kila Imamu. Mashia Imamiya walikuwa wakimuomba kila Imamu awaainishie imamu atakayemfuatia baada ya kufa kwake na amtaje kiwazi wazi ili wasife hali ya kuwa hawamjui Imamu mpya. Na kwa hakika mara nyingi walikuwa wanatumbukia katika tahayari.Katika kitabu “Baswaairu Al-darajaati” cha Abuu Jafari Muhammad Al-Swaaghiru – bwana huyu ni miongoni mwa watu wa Imamu Al-Hassan Al-Askariyu – kuna mlango wenye anuani ifuatayo: “Mlango kuhusu Maimamu kuwa wanamjua yule wanayemuhusia awe Imamu kabla ya kufa kwao kwa vile wanavyojulishwa na Allah” ([31]). Ndani ya kitabu hicho ametaja riwaya nyingi miongoni mwa riwaya hizo ni ile aliyoipokea Abdulrahman Al-Khazaazu kutoka kwa Abuu Abdallah, Amani iwe juu yake, amesema: Ismaili bin Ibrahim alikuwa na mtoto mdogo akimpenda sana, na matamanio ya Ismaili yalikuwa kwa mtoto huyo, lakini Mwenyezi Mungu amekataa jambo hilo, akasema: Ewe, Ismaili huyo ni fulani, na Mwenyezi Mungu alipohukumu kifo cha Ismaili, ukaja usia wake na kusema: ewe mwanangu yakija mauti fanya kama nilivyofanya. Kwa ajili hiyo, hafi Imamu ispokuwa Allah anampa habari za atakayemuhusia!Pia katika “Baswaairu Al-darajaati” kuna mlango wenye anuani: “mlango kuhusu Imamu (As) ya kuwa anajua atakayekuwa baada yake kabla ya kufa kwake”!Haya yakiwa ni matokeo ya kawaida ya utata unaoizonga akida ya Uimamu wa maandiko – huku Imamu mwenyewe hajui imamu wa baada yake ni nani hadi kabla kidogo ya kufa kwake – Mashia wote wamehangaika baina ya Imamu huyu na yule. Katika hili, pia wamo wapokezi wakubwa na watu wa Maimamu!   Zuraara bin Aayuni – mmoja wa wafuasi wakubwa wa Maimamu wawili: Al-Baaqir na Al-Swaadiq – alikufa bila ya kumjua Imamu wa baada ya Imamu Al-Swaadiq!Zuraara alimpeleka mwanawe ambaye ni Ubeidillah kutokea Kufa aende Madina ili amtafutie habari za imamu mpya. Lakini kifo kilimkumba. Akaweka Quran katika kifua chake na kusema: “Ewe Mola, mimi ninashuhudia kuwa ninamfuata imamu yule aliyethibitishwa uimamu wake na msahafu huu” ([32]).Lau kama ingekuwa inajulikana kwa Mashia na wengineo miongoni mwa watu wa Maimamu, kwamba imamu wa baada ya Jafari Al-Swaadiq ni Musa bin Al-Kaazim Allah amuwie radhi wangeuamini uimamu wake bila ya kuwa na shida ya kuuliza au kuwa na shaka.Al-Ssufaaru, Al-Kiliiniyu, Al-Mufiidu na Al-Kabshiyu wametaja kuwa wale wafuasi muhimu wa Maimamu, kama vile Hisham bin Saalim Al-Juwaaliiqiyu na Muhammad bin Nuuman Al-Ahwali – Mwanzoni – walifuata msimamo wa kuwa imamu ni Abdallah Al-Aftwahu baada ya baba yake ambaye ni Jafari Al-Swaadiq na hayo ni kutokana na riwaya ya Abuu Abdallah amesema: “kwa hakika Uimamu ni wa mkubwa kama hana dosari”, na Ammaaru Al-Sibaatwiyu – naye ni miongoni mwa wafuasi wa maimamu wawili Al-Baaqir na Al-Swaadiq ameshikilia msimamo wa kusema kuwa imamu ni Abdallah Al-Aftwahu hadi mwisho wake![33]Hishamu bin  Saalim Al-Jawaliqiyu anasema kuwa, aliingia kwa Abdallah Al-Aftwahu akiwa pamoja na kikundi cha Mashia. Hao Mashia walimuuliza Abdallah Al-Aftwahu baadhi ya mambo ya kifiqihi. Naye hakuwajibu kwa usahihi. Jambo hilo liliwafanya watilie shaka uimamu wake na wakatoka kwa tahayari, na kwa kupotea...) Tukakaa katika vichochoro vya Kufa huku tukilia kwa tahayari hatujui tuelekee wapi wala tumkusudie nani. Tukasema: Twende dhehebu la Murjia?! Zaidiya? Muutazila? Khawaariji? Tukiwa katika hali hiyo ghafla nikamuona mzee ambaye simjui, akiniashiria kwa mkono wake... Akaniambia: Ingia Allah akurehemu! Nikaingia. Tahamaki nikamuona Abuu Al-Hassan Musa, akaanza kwa kuniambia: usiende kwa Murjia, wala Qadaria, wala Zaidiya! Wala Khawaariji! Njoo kwangu, njoo kwangu! Nakamwambia, niwe fidia yako! Je, baba yako ameshapita? Akasema ndio. Nikauliza: Je, tumfuate nani baada yake? Akasema: Allah akipenda kukuongoza anakuongoza. Nikasema: niwe fidia yako! Je, wewe ndiwe huyo? Akasema: Hapana sisemi hivyo. Nikasema nafsini mwangu: sijapatia njia ya hili jambo. Kisha nikamwambia: Niwe fidia yako! Je, imamu ni juu yako? Akasema: Hapana. Nikaingiwa na kitu ambacho hakuna anayekijua ispokuwa Allah! Na hiyo ni kwa ajili ya kumtukuza na haiba yake” ([34]).Katika riwaya hii, Hishamu anasema kuwa watu walijumuika  - kwa uchache mwanzoni - juu ya uimamu wa Abdallah Al-Aftwahu. Na vigogo wa Imaamiya walikuwa hawajui andiko lolote la uimamu wa Kaazim ambaye hakuwa tayari kuutangaza huo uimamu mbele za watu. Ni sawa, ikiwa Hishamu bin Saalim na wenzake walirejea nyuma na kuacha kauli ya kusema imamu ni Abdallah Al-Aftwahu alipokuwa hai au hawajarejea. Kwa hakika Al-Aftwahu alikufa baada kupita siku sabini tu baada ya kufariki baba yake wala hakuacha mtoto ili uimamu uendelee katika kizazi chake. Hili likazua mtafaruku mpya katika safu za Maimamiya wa wakati huo. Kukatokea makundi, kundi moja lilirejea na kuacha kauli ya kusema kuwa imamu ni Abdallah Al-Aftwahu na kulifuta jina lake katika orodha ya maimamu. Na likaamini imamu mpya (Musa bin Jafari) Nao ndio Al-Muusawiya. Na kundi lingine, akiwemo Abdallah bin Bakiiri na Ammaaru bin Musa Al-Sibaatwiyu walichukua kauli ya kusema kuwa imamu ni nduguye Musa baada yake. Na hawa walijulikana kwa jina la Al-Fatwihiya. Nao walikuwa ni wanazuoni wakuu wa imamu Al-Swaadiqu na Maimamu wengine waliomfuatia.Ewe msoma usilete taswira kuwa mambo yalitengemaa baada ya mvurugiko huo na kuyumba huko, lakini kabla ya nadharia ya uimamu kuvuta pumzi baada ya tatizo la usia kwa Ismaili na kujua kuwa yeye ndiye hasa. Na tatizo la Abdallah Al-Aftwahu na kufariki kwake bila kuacha imamu wa baada yake. Kisha likatokea tatizo la kuuthibitisha uimamu wa Kaazim. Tatizo jipya likaibuka, nalo ni kifo cha utata cha Imamu Kaazim katika jela ya Haruna Rashidi mjini Baghdadi mwaka (183 H). Na kauli ya Mashia wote wa (Al-Muusawiya) wa wakati huo inasema kuwa Imamu huyo ametoroka jela na kujificha!Kifo cha Imamu Al-Kaazim kilikuwa tata sana kiasi ambacho kiliwachanganya wengi miongoni mwa watoto wake,  wanafunzi wake na wafuasi wake. Miongoni mwao ni baadhi ya watu wa Ijimai na wapokezi wa kutegemewa kama Ali bin Abuu Hamza, Ali bin Al-Khatwaab, Ghaalibu bin Athumani, Muhammad bin Jariiri, Musa bin Bakri, Wahiibu bin Hafsi Al-Jariiriyu, Hahya bin Husein bin Zaidi bin Ali bin Husein, Yahya bin Al-Qaasim Al-Hidhaau (Abuu Baswiiri), Abdulrahman bin Al-Hajjaaji, Rifaatu bin Musa, Yunusi bin Yakubu, Jamiilu bin Duraaji, Hammaadu bin Issa. Ahmadi bin muhammad bin Abuu Nasri, Aalu Mahraan na wengineo miongoni mwa wafuasi wake wa kutegemewa.[35]  Sababu kuu ya Mashia Al-Muusawiya (kuishia) kwa imamu Kaazim na kukataa kuukubali uimamu wa mwanawe Ali Al-Ridhwaa, Amani iwe juu yake, ni kuwepo kwa riwaya nyingi zinazoelezea kuwa Kaazim ni Mahdiyu na kuwa kabla ya kufa kwake atasimamia umahadiyu. Al-Twuusiyu katika kitabu chake “Al-Ghaibatu” ameashiria baadhi ya riwaya hizo na kuzijadili ([36]).  Shaka na maswali kuhusu namna Ali Al-Radhwaa, Amani iwe juu yake, alivyojua kuhusu kifo cha baba yake ziliendelea kufululiza... Amejua lini? Lini amejijua kuwa yeye Al-Radhwaa amekuwa imamu anayemrithi baba yake... Je, kulikuwa na kitenganishi baina ya kifo cha Kaazim na kujua kwa mwanawe ambaye ni Al-Ridhwaa na kwa hiyo akatawalia uimamu baada yake?([37])Mashia (wa wakati huo) walizidisha shaka juu ya imamu Al-Radhwaa, na hadithi ambayo ilikuwa imeenea kwao wao ni: (Kwa hakika imamu haoshwi na yoyote kinyume na imamu mwingine). Wakasema: kwa hiyo vipi Ali aliyopo Madini amuoshe baba yake aliyefia Baghdadi?!!([38])Andiko juu ya imamu Ali bin Musa Al-Ridhwaa sio tu lilikuwa tata kwa Mashia wa kawaida tu, lakini pia, lilikuwa tata kwa watoto wa imamu Kaazim na mkewe bibi Al-Athiiratu (Ummu Ahmadi) kama Historia inavyoeleza ([39]).Moja ya riwaya inasema: Mashia wa Madina waliposikia habari ya kifo cha Imamu Kaazim walijikusanya katika mlango wa (Ummu Ahmadi) na Kumbaiyi Ahmadi bin imamu Al-Kaazim awe imamu naye akapokea baiya yao ([40]).Wakati Maimaamiya walipokuwa wanajaribu kuuthibitisha uimamu wa Al-Ridhwaa kwa maandiko na miujiza, Imamu Al-Ridhwaa alikufa huko Kharasan mwaka (203 H). Na mwanawe (Muhammad Al-Jawaadu) akiwa na umri wa miaka saba. Hilo lilisababisha kutokea tatizo jipya katika safu za Mimaamiya. Na likaleta changamoto kubwa kwa nadharia ya mtoto. Kwani haikuwa ikiingia akilini Allah Mtukufu amsimike mtoto awe kiongozi wa Waislamu wakati mtoto anazuiwa kujichukulia maamuzi, hana haki ya kutumia mali zake mwenyewe, halazimiki kisheria, wala hakupata nafasi ya kujifunza kutoka kwa baba yake aliyemwacha huko Madina akiwa na umri wa miaka minne ([41]). Jambo hilo limepelekea kugawanyika kwa Mashia Imaamiya na kuwa makundi mengi: a.      Kundi lilirudi nyuma na kusimama kwa imamu Kaazim, likaacha imani yake ya uimamu wa Al-Ridhwaa na kukataa kukubali uimamu wa Al-Jawaadu.b.     Kundi lilienda kwa ndugu wa imamu Al-Ridhwaa (Ahmadi bin Musa) aliyekuwa na mtazamo wa kukubali rai ya dhehebu la Zaidiya. Alitoka pamoja na Abuu Al-Saraaya huko Kufa. Na huyu Ahmadi alikuwa ni mtu wa kuheshimika na kupendwa na nduguye Al-Ridhwaa. Pia alikuwa na elimu na ucha Mungu kama anavyomuelezea Al-Mufiidu katika “Al-Irshaadu”([42]) Kundi hili lilidai kuwa Al-Ridhwaa amemuhusia Ahamadi na kuweka andiko la kumsimika uimamu ([43]). c.      Kundi lingine miongoni mwa Mashia lilishikamana na Imamu Muhammadi bin Al-Qaasimu bin Omari bin Ali bin Al-Husein bin Ali bin Abuu Twaalibi aliyekua naishi Kufa. Alikuwa maarufu kwa kufanya ibada sana na kuipa nyongo dunia, kunyenyekea, elimu na fiqihi. Akalipua mapinduzi ya kumpinga Khalifa Al-Muutaswim huko Al-Twaaliqaani mwaka (218 H) ([44]). d.     Kundi lingine likasema kuwa imamu ni Al-Jawaadu, lakini likakumbana na tatizo lingine. Kwani tatizo la umri mdogo wa imamu Al-Jawaadu liliendelea kwa mara nyingine tena kwa mwanawe Ali Al-Haadi. Kwani Al-Jawaadu alikufa akiwa bado kijana kwani alikufa akiwa hajatimiza miaka ishirini na mitano. Na watoto wake wawili wapekee Ali na Musa walikuwa wadogo na yule mkubwa hakuzidi miaka saba. Na kwa kuwa Al-Haadi alikuwa mdogo wakati wa kifo cha Al-Jawaadu, basi huyo baba yake alimuhusia na kumwamuru (Abdallah bin Al-Musiwaari) asimamie mali zake zikiwemo pesa, mashamba, matumizi ya watumwa kisha aje amkabidhi Al-Haadi atakapokua mkubwa!! Na shahidi wa hilo alikuwa ni Ahmadi bin Abuu Khaalidi maulaa wa Abuu Jafari.[45] Mambo haya yaliwapelekea Mashia wa wakati huo wajiulize: Ikiwa Al-Haadi – kwa mtazamo wa baba yake – hawezi kusimamia Mali, mashamba na matumizi kwa kuwa ni mdogo. Sasa ni nani imamu wa kipindi hicho?! Mtoto mdogo vipi atashika uimamu?! Swali hilo limetolewa na baadhi yao wakati alipofariki Imamu Al-Ridhwaa hapo kabla. Na hilo ni pale Al-Jawaadu alipokuwa mtoto mdogo. Na utata na kutahayari uliongezeka zaidi kwa ndugu wawili: Ali na Musa: Imamu ni yupi kati yao?           Al-Kiliiniyu na Al-Mufiidu wanatusimulia utata na tahayari hizo zilizowapata Mashia katika suala la Uimamu baada Al-Jawaadu. Wakuu wa Kishia hawakujua wasifu wa imamu mpya. Wakajikusanya kwa Muhammad bin Al-Faraji ili kuzungumzia jambo hilo. Kisha akaja mtu na kuwaambia usia aliopewa kwa siri na imamu Al-Jawaadu ya kuwa imamu ni Al-Haadi mwanawe ([46]).          Kutahayari huko pamoja na ule utata katika jambo la uimamu, vilipelekea kugawanyika kwa Mashia (Imaamiya) ambao ni wafuasi wa Al-Jawaadi na kuwa makundi mawili: -         Kundi moja linasema imamu ni Al-Haadi.-         Na lingine linasema imamu ni nduguye ambaye ni Musa Al-Mubarqaa ([47]). Lakini imamu Al-Hadii aliwashtua watu wote kwa kumteua mwanawe Muhammad awe khalifa wake. Kisha huyu mtoto naye akafa wakati wa uhai wa imamu Al-Haadi. Akamuusia mwanawe mwingine (Al-Hassan Al-Askariyu) na kumwambia: "Ewe mwanangu nahadithia kwa ajili ya kumshukuru Allah. Kwa hakika limekutokea jambo"!!          Al-Kiliiniyu, Al-Mufiidu na Al-Twuusiyu wamepokea kutoka kwa Hisham Daudi bin Al-Qaasim Al-Jafariyu amesema: Nilikuwa kwa Abuu Al-Hassan Al-Askariyu wakati anafariki mwanawe Abuu Jafari. Naye alikwishamuashiria na kumjulisha. Na kwa hakika mimi nafikiria nafsini mwangu na kusema: Hiki ni kisa cha Abuu Ibrahim na kisa cha Ismaili. Abuu Al-Hassan alinielekea na kusema: ndio ewe Abuu Haashim! Allah amedhihirihikiwa kwa Abuu Jafari. Na sehemu yake akawekwa Abuu Muhammad, kama  alivyodhihirihikiwa kwa Ismaili baada ya kumjulisha Abuu Abdallah na kumwekea andiko, na jambo hilo lipo kama nafsi yako ilivyokusimulia na limepingwa na watu wa batili… Abuu Muhammad bin Al-Khalaf ana kile wanachokihitaji. Pia ana nyenzo ya uimamu na sifa njema ni za Allah.([48]).          Kama ilivyotokea kwa (Ismailiya) waliopinga kifo cha Ismaili bin Jafari kwa andiko la Jafari Al-Swaadiq, Amani iwe juu yake, kundi mojawapo miongoni mwa Mashia wa Imamu Al-Haadi lilikana kifo cha mtoto wake ambaye ni Muhammad. Na wakang`ang`ania kusema kuwa uhai wake na kufichika kwake vinaendelea.  Na wakadai kuwa tangazo la Al-Hadi la kifo cha mwanawe lilikuwa ni aina fulani ya taqiya na kuufunika uhakika!!          Lakini kifo cha Hassani Al-Askariyu, Amani iwe juu yake, huko Saamiraa mwaka (260 H) bila ya kuwa na mrithi wake, kulilipua tatizo baya mno katia safu za Mashia Imaamiya waliokuwa wanaitakidi kuwa ni lazima kuendelea kwa Uimamu wa kiuungu baada ya Hassan Al-Askariyu. Kwa hiyo, wakagawanyika makundi kumi na manne kama anavyosema Al-Qummiyyu katika "Al-Maqaalaatu Walfiraqu",  Annuubakhtiyu katika "Firaqu Al-Shiati"  Ibnu Abuu Zainabu Al-Nuumaaniyu katika "Al-Ghaibatu",  Al-Swaaduuqu katika "Ikmaalu Al-Diini", Al-Mufiidu katika "Al-Irshaadu", Al-Twuusiyu katika "Al-Ghaibatu", na wengineo miongoni mwa wanazuoni wa Kishia.  Mahdi anayesubiriwaKwa hakika imani ya kuamini kutokea kwa Imamu Mahdi katika zama mwisho na kwamba huyo Mahdi atakuwa ni miongoni mwa Aalibeiti Nnabiyi (watu wa nyumbani kwa Mtume) Rehema na amani ziwe juu yake. Na ni miongoni mwa kizazi cha Fatuma Zahraa kwa sifa za pekee. Imani hii ni ya yakini wala haina shaka. Wala jambo hili halina mjadala baina ya Masunni na Mashia.          Nikiwa kama Shia yoyote yule, nimejifunza kushikamana na heba ya (Mtu wa zama), tangu utotoni nimejifunza kuwa imamu wangu ana majina mengi, yeye ni (Hoja wa Allah), (Mwenye kusimama), (Mtu wa zama), (Baba Salehe/mwema), (Mwenye amri), (Mtu wa zama hizi)… lakini sikutegemea kuwa mtu huyu niliyoshikamana naye tangu utotoni, pia matumaini yangu na furaha yangu zote zilishikamana naye, kuwa atakuwa ni mtu wa kubunika tu.          Mapenzi yangu kwa imamu huyo hayajanifanya nifikirie juu ya jambo hilo. Lakini utafiti huru umeniongoza kuufikia uhakika huu. Jina Mtu wa zama limenitikisa!Miongoni mwa mambo makubwa yaliyonishtua ni jina mtu wa zama lililotajwa na mwanazuoni Al-Nuuriyu Al-Twibrisiyyu katika kitabu chake “Al-Najmu Al-Thaaqibu fii Ahwaali Al-Imaamu Al-Hujjati Al-Ghaaibu.”           Mwanazuoni Al-Nuuriyu Al-Twibrisiyyu hana haja ya kutambulishwa. Inakutosha kuwa amesoma kwa (Shehe Abbasi Al-Qummiyi) na shehe (Aaghaa Bazraki Tehraaniyu) na (Shehe Muhammad Husein Aali Kaashifu Al-Ghatwaau) na (Al-Sayyid Abdulhusein Sharafu Al-Diini Al-Muusawiyyu) mtunzi wa “Al-Muraajaatu” huyu ni miongoni mwa wanafunzi wake.          Kwa hakika ametaja kuwa, miongoni mwa majina ya mtu wa zama (Khasiruu Majuusi)([49]) nalo ni jina la arobaini na saba la imamu huyo!  Kwa hakika ni mshtuko mkubwa!Vipi imamu wetu asifike kuwa ni (Khasiruu Majuusi)?! Majusi wanaingiaje kwa mtu wa zama?! Mtu wa zama atakuja kuwalipizia kisasi maadui wa Aalibeiti, hao maadui wakiongozwa na Abuu Bakar na Omari.. Hivi ndivyo tulivyojifunza. Omari bin Al-Khatwaabu ndio khalifa ambaye katika zama zake Iran ilikombolewa, Uislamu ukaingia, adhana ikapigwa, na swala ikasaliwa… kwa mara ya kwanza katika historia ya Iran… Nikaanza kuunganisha baina ya hili na lile.Lakini ukitaka kupigwa mshtuko mkubwa zaidi pamoja nami, soma riwaya hii kutoka katika “Bihaaru Al-Anuwaari” cha mwanazuoni Al-Majlisiyu.Al-Majlisiyu amepokea kutoka kwa Al-Nuushajaani bin Al-Buudamardaani amesema: Wafarsi walipotolewa Kaadisiya. Na Yazidijardi bin Shahrayaari akafikwa na habari zilizompata Rostom na namna Waarabu walivyomuondoa. Yazidijardi bin Shahrayaari akadhani kwamba Rostom ameangamia na Wafursi wote. Akaja mbio na kumueleza habari za siku ya Kaadisiya, uhamaji, na kuuawa kwa watu hamsini elfu. Yazidijardi akatorokea kwa watu wake na kusimama mlangoni mwa iwani (baraza) na akasema: Amani iwe juu yako ewe Iwani! Ni mimi hapa ninaondoka na kukuacha. Nitarejea kwako mimi au mtu miongoni mwa watoto wangu, zama zake bado hazijakaribia wala wakati wake haujafika.Suleimani Al-Daaylaamiyyu amesema: niliingia kwa Abuu Abdallah amani iwe juu yake, nikamuuliza kuhusu suala hilo kwa kumwambia: Anasema nini kuhusu kauli hii: “au mtu miongoni mwa watoto wangu”? Akasema: Huyo ndio mtu wenu atakayesimama kwa amri ya Allah Mtukufu Aliyetukuka, naye ni wa sita kutoka kwa mwanangu, amezaliwa na Yazidijardi naye ndiye mtoto wake.[50]  Hiyo ni siku ya kulipiza kisasi!Mtu wa zama ni mtoto wa Yazidijardi naye atalipiza kisasi cha baba zake Wafursi dhidi ya Waislamu walioikomboa Farsi. Hivi ndivyo inavyosema riwaya, na hivyo hivyo ndivyo anavyofahamika kwa jina la (Khasiruu Majuusi)!Allahu Akbaru (Mungu Mkubwa)…! Nilikuwa wapi sijauona uhakika huu?!Hata hivyo nina mengi ya kushangaza na kuathiri…Katika kitabu “Al-Ghaibatu” cha Muhammad bin Ibrahim Al-Nuumaaniyu (uk 234) kutoka kwa Abuu Abdallah, Amani iwe juu yake, amesema: “Huyo aliyesimama akitokea, basi hakutokuwa baina yake na Warabu na Makureishi ispokuwa upanga, na hakichukuliwi kitu ila kwa upanga”.Kwa nini, chuki zote hizi dhidi ya Warabu na Maqureishi kwa sifa ya kipekee?! Pia riwaya nyingine zinaeleza kuwa huyo aliyesimama “atamwaga damu ([51]) za makabila sabini miongoni mwa makabila ya Kiarabu” ([52]). Jaribu kuunganisha baina ya hili na yale niliyoyataja hapo kabla ya kwamba miongoni mwa majina ya mtu wa zama ni (Khaasiru Majuusi) na kwamba Yazidijardi ni babu yake. Naye amewaahidi Waislamu waliomtoa yeye na kundi lake kutoka katika kiti cha enzi yake, kwamba atakuja huyo mtu wa zama!!Uhakika huu ni sawa na pigo kubwa juu ya kichwa cha kila mwenye akili…! Kisa tumekiamini kwa kuwa hatutaki kufikiriTangu utotoni wamenifundisha kisa nilichokisadiki kwa vile nilikuwa mdogo tena bila ya kufikiria na kupima kwa mizani ya akili timamu.Mukhtasari wa kisa ni kwamba imamu Al-Askariyu alimwita (Bashari bin Suleiman Al-Nakhaasu) na kumwambia: Nitakutajia siri sitomtajia mtu yoyote Yule zaidi yako. Akamwandikia hati kwa lugha ya Kirumi na kuipiga muhuri wake. Kisha akampatia Dinari mia mbili na ishirini. Akamwambia: chukua pesa hizi na uende Baghdadi huko utakuta soko la watumwa ([53]).  Hapo kuna mtu jina lake (Omari bin Yazidu Al-Nakhaasi) na utaona miongoni mwa wajakazi alionao, mjakazi mmoja sifa zake ni kadha kadha – akamtajia sifa zake – huyo mjakazi anakataa wanaume, ukimuona muoneshe hati yangu hii. Bashari akaenda hadi Baghdadi na kuyakuta yale yaliyosemwa na imamu. Na alipompa hati yule mjakazi  alilia kilio kikubwa, akamwambia Omari bin Yazidi: yaani mwenye hati hiyo. Kisha Bashari alimuuliza yule mjakazi baada ya kumnunua, nini sababu ya kilio chake. Akamweleza kuwa (Yeye ni Mulaikatu binti Yashuuaa Sham`uuni bin Hamuuni bin Al-Swafaa)!!Kisha yule mjakazi akamtajia kisa cha ajabu kinachohusiana na Kaisari babu yake ambaye alitaka kumuozesha kwa mtoto wa ndugu yake. Na namna alivyomuona Muhammad, Rehema na amani ziwe juu yake, ndotoni akimjia Yesu, Amani iwe juu yake, akimuhutubia usia wa binti wa Shamuuni. Na namna yeye mwenyewe alivyomuona Fatuma Zahraa na Maryamu bint Imraana – Amani iwe juu yao – ndotoni, na sifa elfu moja miongoni mwa sifa za peponi. Na namna alivyomuona imamu Al-Hassan Al-Askariyu ndotoni, na kwamba huyo imamu amemweleza babu ya mjakazi huyo kuwa atapeleka jeshi kupigana vita na Waislamu katika siku fulani. Na huyo mjakazi anapaswa kujiunga na jeshi hilo akijificha kwa kutumia nguo za watumishi. Na namna alivyoangukia kuwa mateka baada ya tukio hilo.Hiki ndio kisa cha Mama wa mtu wa zama… Kisa kinafaa kutengezewa sinema, wala si cha itikadi ya Muislamu aliyejiwa na Quran ili ikomboe akili yake iepukane na khurafaati (mambo ya ovyo ovyo) na visa kama hivi…Ama mimba ya (Narjisu) kumbeba mtu wa zama, inakutosha usome riwaya iliyotajwa na Abbasi Al-Qummiyu katika "Muntahaa Al-Aamaali" na wengineo miongoni mwa wanazuoni wa madhehebu yangu yaliyotangulia.Riwaya hiyo inasema kuwa: Sisi kundi la watu tuliousiwa, mimba zetu hazibebwi matumboni . Hakika si jinginelo, mimba zetu zinabebwa mbavuni, wala hatutoki katika fuko la uzazi. Hakika si jinginelo, sisi tunatoka katika mapaja ya kulia ya mama zetu. Kwa kuwa sisi ni nuru ya Allah isiyopatwa na najisi!!Mitume wanazaliwa kutoka katika fuko la uzazi na Wausiwa wametakaswa na hayo. Uislamu gani huu unaoridhia maneno kama haya?!  Ama kuzaliwa kwa huyo mtu wa zama, riwaya zinamzungumzia kuwa: Huyo bwana, amani iwe juu yake, alipozaliwa nuru ing`aayo ilidhihiri kutoka kwake hadi ikafikia upeo wa mbingu. Na nikaona ndege weupe wakitua kutoka mbinguni na mbawa zao zikimpangusa kichwani, usoni na sehemu nyingine za mwili wake kisha wanaruka. Abuu Muhammad Al-Hassan amani iwe juu yake, alipiga kelele na kusema: Ewe shangazi, mchukue na umlete. Aliponiletea nilimkumbatia, na ghafla nikamuona ametakasika (ametahiriwa na kukatwa ukamba wa kitovu), msafi aliyesafishwa, na katika mkono wake wa kuume kumeandikwa: "Kweli imefika, na uwongo umetoweka. Hakika uwongo lazima utoweke" ([54]). Ama sheria atakayohukumu kwayo, huyo mtu wa zama ni sheria nyingine sio sheria ya Kiislamu.Ibnu Babaweihi Al-Qummiyu anaashiria katika kitabu chake "Al-Iitikaadaatu" kuwa Mahdiyu atakaporeja kutoka mafichoni mwake atafuta sheria ya Kiislamu inayohusiana na hukumu za mirathi, na akataja, kutoka kwa Al-Swaadiq, anasema kuwa: "Kwa hakika Allah ameunganisha roho katika kivuli kabla ya kuumba miili kwa miaka elfu moja, lau angesimama huyo msimamaji wetu sisi Aalibeiti basi ndugu aliyeunganishwa katika kivuli hicho anamrithi nduguye waliyeunganishwa naye wala hatomrithi nduguye kwa kuzaliwa"([55]).  Na mtu atakayefikia umri wa miaka ishirini na hajaelimika kidini anauliwa ([56]). Huyo mtu wa zama atahukumu kwa hukumu za (Aali Daudi) sio kwa hukumu za (Muhammad na Aali Muhammad). Riwaya za Mashia zinasema kuwa: "Akisimama huyo kaimu wa Aali Muhammad atahukumu kwa hukumu ya Daudi na Suleiman wala hatouliza ushahidi"([57]), na katika tamko lingine: "Akisimama huyo kaimu wa Aali Muhammad atawahukumu watu kwa hukumu ya Daudi, Amani iwe juu yake, wala hatohitaji ushahidi"([58]). Madhumuni ya fikra hii ni kuwa huyo Mahdiyu ataacha kuhukumu kwa Quran na badala yake atatumia kitabu kingine badala ya Quran. Jambo hili ndilo linaloashiriwa na riwaya ya Al-Nuumaniyi kutoka kwa Abuu Baswiiri amesema: Abuu Jafari, amani iwe juu yake, amesema: Huyo kaimu atasimama na jambo jipya, kitabu kipya na makadhi wapya”([59]). “Kana kwamba namtazama akiwa baina ya nguzo na maqaamu huku akiwabaiyi watu kwa kitabu kipya”([60]).Hata maeneo matakatifu ya Kiislamu hayatosalimika!Riwaya zinaeleza kuwa “Huyo kaimu atauvunja msikiti wa Maka hadi aurejeshe katika misingi yake, pia msikiti wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, hadi ufikie msingi wake. Na atairejesha nyumba katika eneo lake na kuijenga juu ya msingi wake” ([61]).  Kwa nini mtu wa zama ametoweka?Wanaoamini kuwepo kwa (mtu wa zama) wanalijibu swali hili kwa kusema: "Kuna sababu zinazozuia kudhihiri kwa mtu wa zama, na wakati wowote sababu hizo zitakapoondoka, basi mtu huyo atadhihiri". Kisha wanazibainisha sababu hizo zinazozuia kudhihiri kwa huyo Mahadiyyu kwa kusema: "Kwa hakika, hakuna sababu inayomzuia asidhihiri ispokuwa hofu ya kuuliwa. Kwani kama isingekuwa hivyo, basi hasingekuwa na sababu ya kujificha. Alikuwa anavumilia shida na maudhi. Na kwa hakika daraja za Mitume na Maimamu zinatukuzwa kwa kuvumilia kwao shida kubwa kwa ajili ya Allah".Historia za mababa zake zinajulikana na kila mtu, baba zake walikuwa wanachangamana na watu, wala hawakumwogopa mtu yoyote.Wale wanaoamini kuwepo kwa mtu wa zama wamepokea riwaya kadhaa zinazotaja kuwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, alijificha alipokuwa Maka, mwanzoni mwa Daawa [wito wa kuwalingania watu waingie Uislam], kwa kuogopea asiuawe. Kisha wanalinganisha kujifcha kwa mtu wa zama na kujificha kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake. Miongoni mwa riwaya hizo ni ile iliyopokewa na Al-Majlisiyu katika “Al-Bihaaru” (18/176) kutoka kwa Abuu Abdallah, Amani iwe juu yake, amesema: “Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, alijificha kwa sababu ya hofu, kwa muda wa miaka mitano, wala hadhihiri. Alikuwa pamoja na Ali na Khadija, kisha Allah mtukufu alimwamrisha adhihirishe yale anayoamrishwa, naye akalidhihirisha jambo lake.”Pia, imepokewa katika “Al-Bihaaru” (18/177) kutoka kwa Abdallah, Amani iwe juu yake, anasema: “Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, baada ya kujiwa na ufunuo kutoka kwa Allah Mtukufu, alikaa Maka kwa muda wa miaka kumi na mitatu. Miongoni mwayo miaka mitatu aliyojificha huku akiogopa wala hukudhihirika hadi pale Allah Mtukufu alipomwamrisha adhihirishe kila anachoamrishwa. Kwa kipindi hicho ndipo alipodhihirisha daawa.”          Kuna riwaya nyingine zinazofanana na hizi zinazoelezea maana hiyo hiyo, nimeziacha kwa ajili ya kufupisha.          Kwa hakika mlinganisho huu ulikuwa ni mlinganisho baina ya vitu vilivyotofautiana mno [Qiyaasi maa al-faariq], na hiyo ni kwa njia zifuatazo:Ya kwanza: Kwa hakika Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, hakujificha na macho ya walimwengu, ispokuwa alifanya daawa kwa siri.Ya pili: Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, alikuwa pamoja na watu, mkewe Khadija na Ali na wengineo. Lakini Al-Mahdiyu mnayomletea madai haya, hayupo hivyo.Ya tatu: Kwa hakika Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, alijificha hadi akadhihiri, na katika muda huo wa kujificha alikuwa anaandaa daawa, na kwa kweli, aliandaa wafuasi ili wamsaidie katika daawa. Ama Al-Mahdiyu, amejificha wala hana wafuasi, na kama Mashia Imaamiya ndio wafuasi zake – ni jambo linalojulikana kuwa wao ni wafuasi zake tangu anajificha – na kwa sasa wao wapo mamilioni, je, idadi hiyo haitoshi kumfanya huyo Al-Mahdiyu atokeze na awe katika amani akipigana jihadi pamoja nao?!!          Hapa napenda kueleza kuwa, siku moja nilishuhudia kipindi cha Luninga kinajadili mambo ya uwepo na uhakika wa Al-Mahdiyu na kisa cha kujificha kwake.          Mazungumzo yalikuwa kati ya pande mbili: Anayeaminii uwepo wake na mwingine asiyeamini uwepo wake na wote wawili ni Mashia.          Maelezo ya upande usioamini kuhusu mambo hayo, yalieleza hivi: kama tutaikubali kimjadala tu, kauli inayosema ni sahihi habari na riwaya zote zilizokuja kuhusiana na kisa cha Al-Mahdiyu na sababu ya kujificha kwake. Basi ni jambo linalojulikana katika habari hizo kuwa sababu ya kujificha kwake ni hofu ya kuuliwa na Al-Abbasiyiin [Watu wa ukhalifa wa Abbasiyiin] wa wakati huo. Lakini kwa nini Al-Mahdiyu hadhihiri sasa hivi katika Luninga, wakati tupo katika zama za madishi ya sataleiti na mtandao wa internet au kwa uchache adhihiri katika kanda ya video kwa sauti na picha kama wafanyavyo wanasiasa wengi wa upinzani waliokimbia  na kuwapiga vita viongozi – na kuzikabidhi hizo video mikononi mwa wale watu wanaodai mara kwa mara kuwa wamekutana naye. Na kwa hivyo, atauthibitishia ulimwengu – angalau kwa wale wasioamini uwepo wake, kwa uchache – kuwa yeye si mtu wa kudhanika tu, wala si mtu wa ngano wala si mtu wa uongo, na kuwahakikishia yale yaliyokuja katika habari na riwaya?! Kwa nini wanamshambulia Al-Marjiu Muhammad Husein Fadhlullah?!Anayetazama kwa makini uhalisia wa Kishia leo hii anatambua kuwa kuna mwamko na kuwa macho, kutoka katika usingizi mzito uliorefuka… lakini hautorefuka sana.Majina yameshajitokeza uwanjani yakiwa ndio ya wakosoaji wa ghuluwi [kuzidisha mno hadi kupotosha] iliyopo katika dhehebu hili. Majina hayo, yameanza kupekua na kufuatilia kwa kina riwaya wanazozipitia wasomi wa tanzia, mahatibu wa membari (majukwaa) za Al-huseiniya na wenye misimamo ya kibaguzi miongoni mwa watoto na mashehe wa dhehebu hili, wasiozitafiti wala kuzichunguza kwa kina riwaya hizo. Majina ya wakosoaji hao yameanza kuongezeka siku hadi siku.Juzi juzi, (Ayatu Allah Al-Udhmaa Abuu Al-Fadhli Al-Barqiyi) na (Ahmadi Al-Kisrawiyyu) na (Al-Allaama Al-Khuwainiyu) na (Al-Duktur Musa Al-Muusawiyu) na (Muhmmad Al-Yaasriyu) na (Ahmadi Al-Kaatibu) waliinukia, na leo hii, (Ayatu Allah Al-Udhmaa Muhammad Husein Fadhlullah) naye ameinukia. Bwana Fadhlullah – naye ni marejeo na mwanazuoni mkubwa mno miongoni mwa Mashia – ametambua kuwa badhi ya mapendekezo ya kiitikadi na kihistoria aliyokuwa akiyatetea alipokuwa mdogo, na kuyafasili na kuyapigia debe, kwa kweli mapendekezo hayo hayakuwa ya uhakika. Katka ngazi ya kihistoria Bwana Fadhlullah kwa kutumia utafiti wake na kutathimini yale yanayotajwa kuhusiana na tukio la kufanyiwa uovu Bibi Fatuma Zahraa, amefikia matokeo ya kuwa kila kinachotajwa kuhusiana na kupigwa kwa Zahraa na kuporomoka kwa mimba yake hakina uhakika hata kidodo.Kwa sababu ya maelezo haya, alipata maudhi na wagomvi wengi hadi zikatolewa fat`waa za kumuona ni mpotovu na huenda za kumkufurisha! Bwana Fadhlullah anasema akiyakosoa yale yanayotajwa katika kisa cha kumfanyia uadui Zahraa: “…Hivi wewe, kama atakujia mtu na kumshambulia mkeo na akataka kumpiga, je, utakaa ndani ya nyumba yako chumbani huku ukisema: Laa Haula walaa Quwata illa Billaah [Hakuna hila wala nguvu ispokuwa kwa Allah], au utamshambulia yule atakayekuja kumpiga mkeo?!Ali bin Abuu Twaalibi, Amani iwe juu yake, huyu mtu ndiye aliyepakaziwa kwa batili kuwa amewaacha hao jamaa wakimshambulia Zahraa kwa mtindo huu huku yeye mwenyewe akiwa amekaa chumbani akisema: Laa Haula walaa Quwata illa Billaah Al-Aliyyu Al-Adhiim?!Ni yupi miongoni mwenu anayekubali kufanya haya kwa nafsi yake? Hakuna wala mmoja” ([62]). Na Fadhlullah anaendelea kusema: kwa nini Zahraa afungue mlango… hivi wewe ukiwa upo nyumbani na mkeo yupo na mtu mmoja akagonga mlango, na hasa wakija polisi ili wakutie mbaroni, je, utamwambia mkeo: toka wewe?...Ina maana Imamu Ali ni mwoga, hana wivu?! Wanasema: Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, amemuusia asianzishe vita vya kugombea ukhalifa! Sio asimtetee mkewe” ([63]). Ama kwa kiwango cha kiitikadi, miongoni mwa maelezo makali aliyoyaeleza bwana Fadhlullah baada kufikiria na kuzingatia maandiko ya Quran na Sunna, ni kwamba uimamu si sharti la kusihi Uislamu au kukubaliwa matendo ya waja. Hakika si jinginelo, uimamu ni nadharia inayotiliwa nguvu na baadhi ya Waislamu na haitiliwi nguvu kwa Waislamu wengine. Na uimamu ni katika mambo yanayobadilika([64]) yanayohitaji kuthibitishwa na kudhoofishwa.Miongoni mwa mambo ambayo Bwana Fadhlullah ameyaendea kwa upande wa kuyasahihisha, ni pale alipokosoa kunasibishwa elimu ya ghaibu kwa maimamu.Katika tafsiri yake ya maneno ya Allah mtukufu: “Sema: Mimi sikwambiini kuwa ninazo khazina za Mwenyezi Mungu. Wala sijui mambo yaliyofichikana. Wala sikwambiini kuwa mimi ni Malaika. Mimi sifuati ila yanayofunuliwa kwangu. Sema: Je, wanakuwa sawa, kipofu na mwenye kuona. Basi hamfikiri?” Al-Anaam 50. Fadhlullah ametaja kuwa aya hii inajulisha kwa uwazi kabisa kuwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, hakuwa mwenye kumiliki elimu ya ghaibu, na kwa hakika Allah hakutaka Mtume awe mtu anayesimama mbele za watu ili awahadithie siri zilizofichikana vifuani mwao na yale yanayomngoja kila mtu miongoni mwa mambo ya wakati ujao. Kwa misingi ya elimu ghaibu aliyonayo kutoka kwa Allah. Kama inavyodhaniwa na wengi kuwa kazi ya Mtume ndio hiyo, kwa kumfanya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, kuwa sawa na kuhani [mtabiri] ([65]).Lakini mapendekezo haya, kwa masikitiko makubwa, hayakupata nyoyo za kuyasikiliza wala akili za kuyafikiria na kujadiliana na Bwana Fadhlullah kwa utulivu na uadilifu ili kuthibitisha hayo matokeo aliyoyafikia baada ya utafiti na uchunguzi. Ispokuwa Bwana Fadhlullah kwa sababu ya mapendekezo hayo, alipata mafuriko makubwa ya kumpakazia na kumtuhumu kuwa amepotea.Kwa hakika mimi ni mwenye kusamehe wenye kutubia na kuamini na kutenda mema kisha akaongoka.Kwa ajili ya haya yote, na hakika nyinginezo, hapa hapatoshi kuyataja, imenilazimu kuifuata haki. Nimefikia uhakika huu baada ya miaka mingi ya kupambana na nafsi yangu.Sikuweza kuikinaisha nafsi yangu kuwa inawezekana kwangu niseme: Mimi ni Mshia Ithnaasheria, na wakati huo huo siamini yale yanayoaminiwa na Ithnaasheria…! Ikanilazimu nichague… Uislamu haukubali rangi ya kijivujivu katika itikadi. Nifuate haki au niende katika msafara wa batili.Nilifikiri sana… Nitakosa nini kama nitabadilika kutoka katika itakadi niliyozaliwa nayo na kuingia katika itikadi nyingine inayopewa nguvu kwa ushahidi na hoja na kukubalika kimaumbile na kitabia?Kwa hakika nimeshachagua na wala sijapata hasara ya kitu chochote, ila nimefaidika!    Ndio… nimefaidika maswahaba na wala sijahasirika Aalibeiti, kwani nimejua kuwa, Maswahaba na Aalibeiti ni roho moja katika mwili mmoja. Sikuwa mtu wa pekee kuchagua njia hii, kuna wengi waliopita njia hii hii… wakitarajia rehema na radhi za Allah Mtukufu… Wakiichukua kauli ya Allah Mtukufu: “Na hakika Mimi ni Mwingi wa Kusamehe kwa anayetubia, na akaamini, na akatenda mema, tena akaongoka.” Twaha 82. Kuwa ndio taa yao maishani mwao. (Swalaahu Al-Kaazimiy) na hofu ya kifoNdugu zake walishtushwa pale hali yake ilipobadilika na kuwa sio ya kawaida, daima alikuwa anazungumzia kifo, hadi akajulikana kuwa anaogopa kufa. Na atakufa hivi karibuni huku yeye mwenyewe hataki kufa.Akawa analala kwa muda mchache mno, anakula kidogo tu, madaktari wameshindwa kumtibu, mashehe na Mamullah (mullah ni mwanazuoni) wa Kishia nao wameshindwa kumtibu, nao walikuwa wanadai eti amedhuriwa na jini. Akapata hasara kubwa kwa ajili ya kuwaridhisha mashehe na mamullah waliokuwa wakimtibia kwa madai yao. Ndugu (Swalaahu) anasema: matibabu yao yalikuwa kwa njia za ajabu sana, wengine walikuwa wakimtibu kwa Tawlatu [uchawi wa mapenzi], wengine kwa matalasimu, na kadhaalika. Lakini Quran haikupewa nafasi katika kumtibu.Kisha Shia mmoja alimpa pendekezo la kwenda kwa mashehe wa Ahlu Sunna Wal-Jamaa ili asomewe Quran, kwa kuwa pumzi za Masunni ni tiba kwa Mashia (hii ni kwa mujibu wa itikadi iliyoenea kwa Mashia kuwa shetani hatoki ila kwa kutumia shetani mwingine).  Akaenda msikiti wa Imamu Ahmadi bin Hanmbali uliojirani na nyumba yake. Na pale imamu wa msikiti huo alipomsomea Quran, na huyu ndugu (Swalaahu) akasikia aya, akahisi utulivu na kutulia na furaha ya moyoni.Huyo shehe akamaliza kusoma… ndugu (Swalaahu) akawa kimya kabisa… hakuongea wala kutamka herufi moja, zaidi ya kukaa msikitini bila kutoka kwa vile alikuwa anahisi raha kuwa katika hewa ya msikitini. Ulipofika wakati wa adhana na mwadhini akaadhini, ndugu (Swalaahu) alikuwa akitazama na kuwachunga wanaoswali wakiingia msikitini hadi swala ikakimiwa. Bila ya kusita sita akaingia kuswali pamoja nao. Na katika siku ya pili, imamu alishtushwa na kuhudhuria msikitini kwa ndugu (Swalaahu) wakati wa swala, na imamu huyo alipomuuliza hali yake ndugu (Swalaahu) alisema: Alhamdu lillah… Hali yangu ni njema sana.  Swalaahu ameona kuwa uhalisia wa Ahlu Sunna, wanajua zaidi na wapo karibu sana na Quran Tukufu. Ameona namna wanavyomtukuza Allah na Utukufu wake. Ameona wanavyotekeleza Swala kwa jamaa tena kwa wakati wake. Akaona kuwa hotuba zao za membarini zimejaa kumtukuza na kumsifu Allah. Kinyume na hotuba za membarini za Mashia Wanaotilia umuhimu kuwatukuza Aalibeiti na kuwaongelea maimamu na kukiacha Kitabu cha Allah.Swalaahu amenieleza kuwa, kwa hakika alikuwa anakaa msikitini kusoma matayasari ya Quran. Akanitajia namna moyo wake ulivyoshikamana na Kitabu cha Allah kwa kukisoma na kukizingatia, na kwamba imamu wa msikiti huo alikuwa na nafasi kubwa katika kuupandikiza upande huu wa kiiamani kwa Swalaahu.(Swalaahu) aliendelea kwenda msikiti huo… hadi baadhi ya Mashia wanaomjua wakaona jambo hilo, wakaazimia kumkinaisha aache jambo hilo. Lakini yeye hakuwakubalia. Siku zote alikuwa anawaambia: najisikia vizuri  na raha moyoni nikiswali pamoja na Ahlu Sunna. Na hasa hasa, ninaposikia kisomo cha imamu katika swala za jahariya.Kisha wakamletea baadhi ya mashehe wavaa vilemba wa Kishia ili wamkinaishe kuwa afanyalo ni kosa. Lakini yeye akaingia nao katika mjadala pale walipomfafanulia baadhi ya mambo. Wakaendelea nae zaidi ya kikao kimoja… hadi wakajifungulia mlango wa kutokea matawi ya mjadala… akawaingiza katika maswala ya kupotoshwa kwa Quran, na namna Mashia wasivyotilia umuhimu Quran na elimu zake ([66]) Akawathibitishia kutoka katika vyanzo vya Kishia kuwa wao wanawatuhumu Maswahaba, Allah awawie radhi, kuwa wameipotosha Quran ([67]) Kwa hiyo hawakuwa na kingine zaidi ya kukimbia na kukana jambo hilo bila ya ushahidi wala hoja.Ndugu wa bwana (Swalaahu) walishtushwa na kubadilika kwake na kuingia Ahlu Sunna. Kwa sababu hiyo, ndugu na marafiki zake wa Kishia walimghadhibikia sana. Lakini yeye alifadhilisha radhi za Allah Mtukufu kuliko radhi za watu. Na leo hii, yeye ni mwenye furaha kwa neema ya uongofu, na hizo ni fadhila za Allah anampa amtakaye.Abuu Abdirahmani (Swalaahu) leo hii amekuwa mtafuta elimu anayejitahidi. Allah amzidishie elimu na kumnyanyua.   Ameenda hija akiwa Shia… na kurudi kutoka katika hija akiwa Sunni…Alikuwa akiishi kitongoji cha (Jaddu Hafsi) kabla kwenda Manama mji mkuu wa Bahrein. Anajishughulisha na kuuza mboga mboga, ana mahusiano mazuri na jamaa watatu wa Kisunni. Safari moja yalitokea mazungumzo kati yake na hao marafiki zake. Mazungumzo yenyewe ni kuhusiana na namna Mashia wanavyomtukana na kumjeruhi, Aisha, Allah amuwie radhi, mke wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake. Hakuweza kuyapinga hayo, na akasema: kwa uwazi kabisa sisi Mashia tunambughuzi, kumchukia, kumtusi na kumlaani. Na huyo Aisha ni Naaswabiya ([68]). Nasi tunaitakidi kuwa yeye ni miongoni mwa watu wa motoni. Mmoja wa wale Masunni akamwambia: Hivi, hujasikia kauli ya Allah Mtukufu: “Nabii ni bora zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao. Na wake zake ni mama zao” [Al-ahzaabu 6] akamtafsiria aya hiyo na kumshereheshea… na kufikia hapo huyo Mshia alitahayari kutokana na kuisikia aya hiyo na maana yake, akauliza: Je, aya hii ipo katika Quran?... Kwa hakika hii ndio mara yangu ya kwanza kuisikia. Wakamfunulia kurasa za Quran hadi wakasimama katika aya hiyo waliyoitolea ushahidi. Akasema: sasa ndio nimejua kuwa Aisha, Mungu amuwie radhi, ni mama yangu na ni mama wa kila muumini, yeye na wake wengine wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake. Akasema: siwezi kusema maneno ya Allah ni uongo na kuyasadikisha maneno ya watu.Pia, akaambiwa: Allah Mtukufu amesema kuhusiana na wake za Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, “Ewe Nabii! Waambie wake zako: Ikiwa mnataka maisha ya dunia na pambo lake, basi njooni, nitakupeni kitoka nyumba, na kukuacheni mwachano mzuri. Na ikiwa mnamtaka Mwenyezi Mungu na Mtume wake na nyumba ya Akhera, basi Mwenyezi Mungu amewaandalia wafanyao mema, miongoni mwenu, malipo makubwa”. [Al-Ahzaabu 28 - 29].Mashia na Masunni wanaafikiana kuwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, amekufa bila kuwapa talaka wake zake tisa. Na hizi aya mbili ni amri kutoka kwa Allah kwenda kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, awaache wake zake kama watachagua mapambo ya dunia na kuwabakiza ikiwa watamchagua Allah na Mtume wake na nyumba ya Akhera.Je, kafiri na mnafiki wanachagua nyumba ya Akhera na kuacha mapambo ya dunia?! Jibu ameachiwa mwenye akili…!Ikiwa mama wa waumini bibi Aisha amedhamiria unafiki – Allah aepushe – je, huyo Allah si mwenye kujua yaliyo nafsini mwa Aisha na nafsi ya kila mtu? Kwa nini hakumbainishia Mtume wake, Rehema na amani ziwe juu yake, kuhusu jambo hilo hadi Mtume akafa akiwa na mkewe bibi Aisha akiongea kwa nafasi yake ya mama wa waumini?!Kwa hakika Mashia wanaitakidi kuwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, ni maasumu na madhambi makubwa na madogo, kukosea na kusahau. Je, wanazingatia ndoa yake na mama wa waumini Aisha, Allah amuwie radhi, ni kosa miongoni mwa makosa yake?! Kwa hapo alijiuliza: Vipi nimtukane mama wa waumini Aisha naye ni mama yangu na ni mama wa kila muumini?!Akawaendea baadhi ya wanazuoni wa Kishia na kuwauliza juu ya kauli ya Allah Mtukufu: “Nabii ni bora zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao. Na wake zake ni mama zao” [Al-ahzaabu 6] Baadhi yao walikacha kujibu swali hilo, na wengine walikiri kuwa ni kweli wake za Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, ni mama wa waumini, na hii ni heshima waliyopewa na Allah.Msimu wa hija ulipofika, akatoka kutoka nchini kwake kwenda hija. Na huko hija, Allah alimfungua kifua chake kuikubali haki. Akarejea kutoka katika hija akiwa Sunni na wengi walishtushwa kwa kurudi kwake kutoka katika hija akiwa Sunni.Alipata umashuhuri mkubwa kwa jambo hili huko ufalme wa Bahrein. Akawa ndio simulizi za mtaani. Naye ndiye mtu aliyeenda hija akiwa Shia na kurudi kutoka huko akiwa Sunni. HitimishoKwa ndugu zangu na majirani zangu…   Kwa wale ninaowapenda na wanaonipenda…Na kwa wale wanaowapenda Aalibeiti Nabii, Rehema na amani ziwe juu yake. Na wakapenda kuwafuata… Kwa wanaotaka uhakika wa mambo na nuru ing`aayo…Wito wa ukweli wa kutafakari na kufikiri… na kuitikia wito wa kimaumbile aliousema Allah Mtukufu:  Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini - ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu. Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo Dini iliyo nyooka sawa. Lakini watu wengi hawajui. [Al-Ruum].  Allah Mtukufu aliyetukuka amemkirimu binadamu kwa kumpa akili. Na kwa akili hiyo Allah amempa ubora binadamu kuliko viumbe wengine. Jambo la muhimu kwa mwanadamu aiheshimu neema aliyopewa na Allah. Kwa nini isiwe hivyo, wakati huyo mwanadamu anasoma kauli ya Allah Mtukufu katika kitabu chake: Basi hamfikiri? [Al- Anaam 50]. Na kauli yake:  Basi je, hamzingatii? [Al-Baqara 44]. Na kauli yake:  Basi je, hamwoni? [Al- Qaswasi 72]. zote zinahusika na kufikiri na kuzingatia na kuipa uhuru akili isiige kiupofu?!Mtu mwenye akili ajihadhari na kwenda katika kiza/dhulma cha matamanio ya nafsi na kuiga kiupofu ambako hakumletei chochote ila shari. Mwenye akili ajihadhari ili asiwe miongoni mwa aliowasema Allah Mtukufu: Na ikiwa hawakuitikii, basi jua kuwa wanafuata pumbao lao tu. Na nani aliye potea zaidi kumshinda anaye fuata pumbao lake bila ya uwongofu utokao kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu. [Al- Qaswasi 50].Mapenzi yetu kwa Aalibeiti, Allah awawie radhi, ni kwa jili ya ukaribu wao na Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, na cheo chao kinachotokana na ukaribu huo, vile vile Maswahaba, Allah awawie radhi, wamepata vyeo vyao kwa kufanya usuhuba na Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake. Kitu kinachowajumuisha wote hao ni Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake. Wale ni ndugu wa karibu na hawa ni Maswahiba zake… Atakayewapenda wote hao, anawapenda kwa kumpenda  na Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, aliyewapenda hao.Kwa ajili hii, na baada ya kuutambua uhakika huu, imenilazimu nisisite kuwapenda Maswahaba na ndugu wa karibu wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake. Ninasema kwa sauti inayosikika na wote: “Nimefaidika kuwa na Maswahaba na wala sijapata hasara ya kuakosa Aalibeiti, Allah awawie radhi wote”.Na mwisho wa dua zetu ni kumshukuru Allah, Mola wa viumbe vyote. Na Rehema na amani ziwe juu ya Nabii wetu, Muhammad na Aali zake na Maswahaba zake wote hadi siku ya Kiama.([1]) Wakati mwingine jambo lilowekwa nadhiri linasadifu kutokea kama alivyolitaka mwenye nadhiri. Na kutokea kwa nadhiri kama ilivyowekwa haina maana kuwa inasihi au kuruhusiwa kisheria kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allah Mtukufu. Kwa hakika Wakristo wanaweza kwenda kanisani na kumuomba Bikira Maria - Amani iwe juu yake – kupona au kupata riziki. Kisha wanapata wanachotaka kutoka kwa Allah ikiwa ni fitina kwa mtu huyo na ni majaribio ya Allah Mtukufu. Na hivyo hivyo kwa wafuasi wa imani zote ikiwemo Hindusi na wenye kuabudia masanamu, wale wenye kuomba kwa miungu yao, na Allah Mtukufu akawajalia kutokea wanchokitaka ili kuwajaribu kwa kuwahakikishia matakwa yao. Allah Mtukufu amesema: "Tutawapururia pole pole kwa namna ambayo wenyewe hawaijui" [Al-a'aarf 182]. Kuhusiana na jambo hili, Imamu Al-Swaadiq, kama ilivyo katika “Al-Kaafi” (2/452) akiitafsiri ayah hii anasema: "Huyo ni mja anayetenda dhambi huku Allah akiendelea kumpa neema. Hizo neema zinampumbaza kwa hiyo anaacha kuomba msamaha wa dhambi hiyo". Kumuomba asiyekuwa Allah Mtukufu si dhambi tu, bali ni dhambi kubwa kabisa. Na katika hadith iliyopokelewa na Al-Twubrusiyu katika “AL-Mustadiraku” (14 / 331): Kwa hakika Abdallah bin Masoud, Allah amuwie radhi, alimuliza Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake: Dhambi gani ndio kubwa kabisa? Mtume akasema: “Umjaalie Allah awe na mshirika wakati Allah ndiye aliyekuumba”.Na Muislamu anaamini kwa yakini kabisa kwamba dua ni ibada, na hakika ya ibada huwa haabudiwi ispokuwa Allah Mtukufu pekee. Kama Allah Mtukufu alivyosema katika kitabu chake kitukufu: (Na hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu.). [Sura  Al-jinn 18], pia kuweka nadhiri ni ibada, na hakika ya ibada huwa haabudiwi ispokuwa Allah Mtukufu pekee. Na kwa hivyo Annuuriyu Al-Twubrusiyu amepokea katika “AL-Mustadiraku” (16 / 82): Imamu Jafari Al-Swaadiq amekataza kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allah Mtukufu.  Aayatullah Al-Udhumaa Muhammad Amiin Zainidini katika kitabu chake “Kalimatu Al-taquwaa” (6 / 422) masuala namba (63) andiko lake ni: (Haifai kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allah ni sawa sawa awe Rasuli, Nabii, Walii, Malaika au Mja mwema. Na haifai kuweka nadhiri kwa Kaaba, makaburi, misikiti, maeneo ya ibada, na sehemu takatifu nyingine katika Uislamu”. Na Muislamu anaamini imani ya yakini kabisa kuwa Allah Mtukufu peke yake ndio anayemiliki kutoa manufaa, madhara, riziki na kuponya. Wala hakuna anayemiliki kutoa manufaa, madhara, riziki au kuponya, kutekeleza shida ispokuwa Allah Mtukufu. Allah Mtukufu amemwamrisha Mtume wake, Rehma na amani ziwe juu yake, - na huyo Mtume ndio mbora wa viumbe vyote - awafikishie watu kuwa yeye Mtume hamiliki kumnufaisha au kumtia madhara mtu yoyote. Sasa itakuwaje kwa asiye Mtume wa Allah, sawa wawe Manabii, maimamu na watu wema? Allah Mtukufu amesema katika [Sura Al-jinn 20 - 21] (Sema: Hakika mimi namwomba Mola wangu Mlezi, wala simshirikishi Yeye na yeyote * Sema: Mimi sina mamlaka ya kukudhuruni wala kukuongozeni).Mwenye akili asighururike na mapambo ya shetani. Msomaji aelewe ya kwamba kisa changu ni mfano wa hadithi hizi. Nacho ni kunukuu imani zilizojipenyeza kwa baadhi ya watu wa kawaida ambao si wasomi, kwa sababu ya udhaifu wao wa kuacha kushikamana na Allah Mtukufu, pia udhaifu wa imani yao kwake. Na kama si hivyo, ni akili gani inayokubali imani kama hizi, wakatika huyo mtu anasoma maneno ya Allah Mtukufu (Je! Mwenyezi Mungu si wa kumtosheleza mja wake?) [Surat   Azzumar 36]. Muisilamu anatosheka na Mola wake Mtukufu. Wakati aisyekuwa Muislamu hali yake inasema kama alivyosema Allah Mtukufu: (Na wengi katika wao hawamuamini Mwenyezi Mungu pasina kuwa ni washirikina) [Surat Yusuf 106]. [2] Naye ni Uqaili bin Abduljalili Ahmad.[3] Mnamo mfunguo sita mwaka (1425) Hijiria, - sawa na Mei (2004), yalionekana baadhi ya mabango  ya Kishia yaliyokuwa yakiashiria kuwa sehemu hiyo ni makaburi ya mawalii. Pia itikadi ya kuamini kwamba sehemu hii ina mabaki ya nyayo za Mahdiyu anayengojewa, na kwamba sehemu hii imebarikiwa, ilienea!.  [4] "Al-kaafi" (8/245), na “Al-Daraajatu Al-Rafiiat” (Uk 213).                                                                    [5] Yaani baada ya kufa kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, na watu kumchagua Abuu Bakari, Mungu amuwie radhi. [6] Al-Aradiiliyu amesema: Abu Sasani jina lake ni Al-Huswain bin Al-Mundhir, au inasemekana ni Abuu Sinani. kisha akaleta riwaya iliyotajwa na Al-Kishiyi "Jaamii Al-ruwaati" (2/387). [7] "Faslu" Ibn Hazmi Andalusi (4/225).[8] Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, aliihalalisha kwa muda wa siku tatu katika ukombozi wa Khaibari kuwaoa makafiri.  [9] "Al-Nawaadiru" cha Ahamad bin Issa Al-Qumiyi (uk 87). [10] Taqiya ni moja ya itikadi za Kishia na maana yake ni kuficha wanachokiamini na kudhihirisha kinyume na wanavyoamini kwa kuogopa madhara. Ama Sunni wanaona imani hii ni sawa na unafiki. [11] Al-aammatu ni neno lenye maana ya watu wa kawaida wasio wanazuoni au mashehe wa dini. Neno hili linatumiwa na Mashia kumaanisha Waislamu wasiokuwa Mashia,na hapa lina maana ya Masunni. Na Sunni hata kama atakuwa ni mwanazuoni na shehe katika dhehebu lake, bado Mashia wanamwita ni miongoni mwa Al-aammatu.[12] Kiambatisho katika juzuu ya pili ya “Swiraatwu Al-Najaati” cha Al-Khuuiyu (uk 562).[13] “Bihaaru Al-Anwaari” (82/ 100 – 101). [14]Tazama: “Al-dhikraa lisshahiidi al- awwali” (uk 72).[15] Bidaa ni uzushi, au kuzua kitu katika dini ya Kiislamu kisichokuwepo enzi za Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake wala zama za Maswahaba.[16] Imepokewa na Al-Kiliiniyu katika kitabu “Al-Kaafi” (3/222 – 223), na (Al-Faidhu Al-Kaashaanii fii Al-Waafi” (13 – 87), na Al-Huru Al-Aamiliyu katika “Wasaaili Al-Shiat” (2/915).[17] “Al-Malhuufu” cha Ibnu Twuusu (uk 50). Na “Muntahaa Al-Aamaali” cha Abbasi A-Qummi (1/481). [18] “Al-Dhikraa” (uk 72).[19] “Man laa yahdhuruhu Al-faqiihu” (1/163), na “Wasaailu Al-Shiat” (3/278).[20]Al-Qudhwaibiya: ni eneo mashuhuri huko Bahrein, na eneo hilo lipo katika mji wa Al-Manaama. Na hapo ndipo nilipozaliwa na vile vile mababu zangu. Na eneo hili zamani lilikuwa ni sehemu ya kupunzikia ya watu wa miji ya jirani wakati wa kiangazi  na hasa hasa watu wa Almahruuqu. Na hiyo ni kwa ajili ya uzuri wa hali ya hewa yake… kama walivyonieleza baadhi ya wazee akiwemo babu yangu mzaa mama.[21] “Wasaailu Al-Shiat” (15/330), na “Bihaaru Al-Anuwaaru” (78/113).[22] “Wasaailu Al-Shiat” (17/148), na “Bihaaru Al-Anuwaaru” (67/210).[23] “Mustadiraku Alwasaaili” (13/100).[24]Kwa kufanya hivi huyu mwanamke pia, tayari ameshawalaani (Aalibeiti) bila kujijua. Atwibrisiyyu ametaja katika “Iilaamu Alwaraa” (1/213) kuwa miongoni mwa watoto wa Imamu Hassan ni (Omari). Na Imamu Zeini Al-aabidiina amemwita mmoja wa watoto zake kwa jina la (Omari), kama alivyosema Shehe Abbas Al-qummiy katika “Muntahaa Al-aamaali” (2/59). Na Al-Arbiliy katika kitabu kiitwacho “Kashfu Alghumma fii maarifati Al-Aimma” (3/31) ametaja kuwa Imamu Musa Alkaazim ana mtoto jina lake ni (Omari). Tazama taasubi, namna zinavyopelekea kuangamia!    [25] “Al-Irshaadu” (uk 256), “Kashfu Al-ghumma” (2/293).[26] Lazima tuashirie wepesi wa mtu kuzua visa na miujiza kwa anayempenda. Al-Ismaailiya wametoa visa kumuhusu Imamu Ismaili bin Jafari Asswaadiq ili wamthibitishie Uimamu wake. Na Alrifaaiya wametoa visa vingi kumuhusu Alrifaaiyu na miujiza yake. Vile vile Attijaaniya… wepesi ulioje wa kutaja visa, lakini bila kuzingatia na uhalisia wa zama hizo.[27]  “Al-Kaafii” (1/471).[28]  “Al-Kaafii” (1/342).[29]  “Ikmaalu Al-diini” (uk 348, 350 – 351).[30] “Tafsiri Al-Aayaashiy” (2/117 – 118), na “Al-Imaama wa Al-Tabswira mina Al-Hiira). (uk 226). Na “Ikmaalu Al-Diinu” (uk 75). [31]  (uk 435).[32] “Ikmaalu Al-diin” (uk 75/76).[33] “Al-Kaafii” (1/351 – 352), na “Al-Irshaadu” (uk 291), na “Baswaairu Al-darajaati” (uk 250 – 251), na watu wa Al-Kabshiyi katika tarjama ya Hishamu bi Saalim.[34] “Al-kaafi” (1/351), na “Al-Irshaadu” (uk 291), na “Baswaairu Al-darajaati” (uk 250 – 258), na “Rijaalu Al-Kaashii” (Tarjamatu Hishaam bin Saalim).[35]“Alghaibatu”  cha Al-Twuusiyu (uk 47), na “Al-Kafii” (1/34), na “Uyuunu Akhbaari Al-Ridhwaa” (uk 39).[36]  “Alghaibatu” (uk 29 – 40).[37] “Al-Kaafii” (1/381).[38]  “Al-Kaafii” (1/385).[39]  “Al-Kaafii” (1/381 - 382).[40][40] “Hayaatu Al-imaami Musa bin Jafari Al-Baaqir Shariifu Al-Qurashiyyu” (uk 410 – 411). Imenukuliwa kutoka kwa “Tuhfatu Al-Aalami” cha Sayyid Jafari Aali Bahri Al-Uluumi (2/87)[41] “Al-Maaqaalaatu Wal-Firaqu” cha Al-Qummiyi (uk 96 – 98), na “Firaqu Al-Shiat” cha Nuubikhatii (88).[42] “Firaqu Al-Shiati” (uk 88), na “Al-Maqaalaatu” (uk 97).[43] “Al-Fusuulu Al-Mukhtaru” (uk 256).[44] “Muqaatilu Al-Twaalibiina” (uk 579) na “Taarikhu Al-Twabariy” (7/ 223).[45] “Al-Kaafii” (uk 1/325).[46]  “Al-Kaafii” (uk 1/324), na “Al-Irshaadu” (uk 328).[47]  "Firaqu Al-Shiiat" (uk 91).[48] "Al-Kaafii" (1/328), na "Al-ghaibatu" (uk 55, 130), na "Al-Irshaadu" (uk 337), na "Bihaaru Al-Anwaari" cha Al-Majlisiyu (50/241).[49]  “Al-Najmu Al-Thaaqibu” (1/185).[50] “Bihaaru Al-Anwaari” (51/163 – 164).[51]  Atamwaga damu, na katika chapa nyingine ya Bihaari: ataleta fitna, mkorogeko na mauaji.[52] Tazama: “Bihaaru Al-Anwaari” (52/333), Hamishi (1).[53]  Soko la kuuza watumwa wa kiume na wajakazi yaani watumwa wa kike.[54]  "Muntahaa Al-Aamaali" cha Abbasi Al-Qummitu (2/561).[55]  "Al-Iitikaadaatu" (uk 83).[56]  "Iilaamu Al-Waraa" cha Al-Twabrisiyu (uk 431), "Bihaaru Al-Anwaari" (52/152). [57]  "Usuli Al-kaafii" (1/397).[58] “Al-Irshaadu” cha Al-Mufiidu (uk 413), na “Iilaamu Al-Waraa” cha Al-Twabriisiyu (uk 433).[59] “Al-Ghaibatu” cha Al-Nuumaaniyu (uk 154), “Bihaaru Al-Anwaari” (52/354).[60] “Al-Ghaibatu” cha Al-Nuumaaniyu (uk 176), “Bihaaru Al-Anwaari” (52/135).[61] “Al-Ghaibatu” cha Al-Tuusiyu (uk 282), “Bihaaru Al-Anwaari” (52/338).[62]  “Al-Huuzatu Al-ilmiyatu Tudiinu Al-Inhirafi” (uk 27 – 28).[63]  Rejeo lililopita.[64] “Linalobadilika na linalogeuka, nayo ni kinyume na lililothabiti, na makusudio ya maneno hayo ni: mambo ya kudhaniwa ambayo ni vyanzo vya kujitahidi.[65]  “Tafsiiru min Wahyi Al-Quraan” (Al-Anaam 50).[66] “Ali Khamenei ameweka wazi hilo na kusema: “Kwa hakika kujiepusha kwetu na Quran ambayo inapatikana katika vikao vya elimu na kuacha kunukuu Quran, kumepelekea kupatikana kwa matatizo mengi kwa sasa na baadaye. Vile vile, kujiepusha na Quran kunaplekea tutumbukie katika muono mfupi”.Pia amesema: “Kinachonisikitisha ni kwamba, tunaweza kuanza somo na kuliendeleza hadi kupokea ijaza ya ijitihadi bila ya kuirejea Quran japo mara moja! Kwani nini iwe hivi? Kwa sababu masomo yetu hayategemei Quran…”. Pia amesema: “Mtu kama anataka kupata maqamu ya kielimu katika vikao vya kielimu inampasa asiifasiri Quran ili asituhumiwe ujinga… kwani mwanazuoni mfasiri anayewafaidisha watu kwa tafsiri yake alikuwa anaonekana mjinga wala hana uzito wowote kielimu. Kwa hiyo, analazimika kuacha kuisoma… Je, hilo hamlizingatii kuwa ni janga?! “Al-Huuzati Al-Ilimiya fii Fikri Al-Imaamu Al-Khaamenei”. (uk 100 – 101).  [67] “Muhammad Baakiru Al-Majlisiyu anasema katika kitabu chake “Mir-aatu  Al-uquuli” (12/525) baada ya kuleta hadithi ifuatayo: “Kwa hakika Quran aliyokuja nayo Jibrilu, Amani iwe juu yake, kwa Muhammad, Rehema na amani ziwe juu yake, ni aya elfu kumi na saba”. Baadaye akasema: “hadithi thika, na katika baadhi ya nakala zake kutoka kwa Hishaamu bin Saalim  Maudhui Haruna bin Saalim. Hadithi hii ni sahihi wala haifichikani kuwa hadithi hii na nyinginezo nyingi zilizo sahihii zinaeleza wazi kuwa Quran imepungua na kubadilishwa…”. Kuna maelezo mengi ya ziada yenye hatari sana. Rejea kitabu “Al-Shiat Watahriifu Al-Quraan” cha Muhammad Al-Saifu, au “Araau Haula Al-Quraan” cha Ayaatullah Al-Faaniy Al-Aswfaahaaniyu. Katika vitabu hivyo kuna mengi ya kutosheleza katika masuala haya.                              [68] Naaswabiya ni dhehebu linalompinga Ali bin Abuu Twaalib bila ya kumkufurisha.Ibnu Rajabu Al-Barsiyu amesema katika kitabu chake “Mashaariqu Anuwaari Al-Yaqiini” (uk 86): “Kwa hakika Aisha amekusanya dinari arobaini kwa njia ya khiana – yaani kwa uzinzi” Allah Mtukufu atuepushilie mbali.

التفاصيل