البحث

عبارات مقترحة:

الحق

كلمة (الحَقِّ) في اللغة تعني: الشيءَ الموجود حقيقةً.و(الحَقُّ)...

الواحد

كلمة (الواحد) في اللغة لها معنيان، أحدهما: أول العدد، والثاني:...

المعطي

كلمة (المعطي) في اللغة اسم فاعل من الإعطاء، الذي ينوّل غيره...

Masomo katika umuhimu wa Tawhiidi Muhtasari wa kitabu cha Al-Usulu AL-Thalathah

السواحلية - Kiswahili

المؤلف صالح بن فوزان الفوزان ، Yasini Twaha Hassani
القسم كتب وأبحاث
النوع نصي
اللغة السواحلية - Kiswahili
المفردات متون العقيدة
Kitabu hiki kinazungumzia masomo katika umuhimu wa Tawhiid kimezungumzia: Walaa na Balaa, na uislam ndio dini ya nabii Ibrahim, Niwajibu kwa Mwanadamu amuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, jambo kubwa alilo amrisha Mwenyezi Mungu waja wake ni Tawhiidi, na Nini maana ya Tawhiidi.?

التفاصيل

Masomo katika umuhimu wa Tawheed.  Muhtasari wa kitabu cha Al-Usulu AL-Thalathah Utangulizi: ILIMU MWENYEZI MUNGU AKUREHEMU: NILAZIMA JUU YETU KUJIFUNDISHA MAMBO MANNE. MAS'ALA MANNE: JAMBO LA KWANZA: ILIMU. KUMJUA MWENYEZI MUNGU: NA KUMJUA MTUME WAKE: NA KUIJUA DINI YA KIISLAM. KWA DALILI. KUIFANYIA KAZI ELIMU JAMBO LA PILI: KUIFANYIA KAZI. KULINGANIA KATIKA ILIMU. JAMBO LA TATU: KUILINGANIA KWAKE. KUFANYA SUBRA JUU YA MAUDHI YANAYO PATIKANA NDANI YAKE. JAMBO LA NNE: KUFANYA SUBRA JUU YA MAUDHI YANAYO PATIKANA NDANI YAKE. NI LIPI JIBU LA KIAPO? NA AKASEMA IMAMU BUKHARI (ﷺ‬.a): MLANGO UNAO ELEZEA ILIMU KABLA YA KAULI NA MATENDO. RISALA YA TATU MAMBO MATATU NI LAZIMA MUISLAM AJIFUNDISHE NA AYAFANYIE KAZI.   NI LAZIMA JUU YA KILA MUISLAM WAKIUME NA WAKIKE, YEYOTE ATAKAE MTII ATAINGIA PEPONI, NA YEYOTE ATAKAE MUASI ATAINGIA MOTONI. MAS’ALA YA PILI: WALAA NA BARAA. UJUMBE WA TATU UISLAM NDIO DINI YA NABII IBRAHIM. NA MAANA YA QAULI YA MWENYEZIMUNGU {ILI WANIABUDU}. JAMBO KUBWA ALILO AMRISHA MWENYEZI MUNGU WAJA WAKE NI TAUHIIDI. NINI MAANA YA TAUHIDI? Utangulizi: Jambo kubwa alilo liataza Mwenyezi Mungu ni Shirki.  Maana ya Shirki.  Dalili inayo onyesha kuwa Tawhiidi ni jambo kubwa alilo amrisha Mwenyezi Mungu. Ujumbe wa Nne  Misingi mitatu ambayo ni lazima kuifahamu. Kwanini ameihusisha misingi hii mitatu?.  Masomo katika umuhimu wa Tawheed.  Muhtasari wa kitabu cha Al-Usulu AL-Thalathah Utangulizi:   Kaanza kwa kusema Bismi llahi Rrahmani Rrahim; Kwajina la Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehma mwenye kurehemu.Ameanza Mwenyezi Mungu Amrehemu risala hii kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma mwenye kurehemu, kwa kufuata kitabu cha Mwenyezi Mungu mshindi na mtukufu, kwa sababu macho yako yakiangalia ndani ya msahafu na kabla ya kila sura kuna (Bismi llahi Rrahmani Rrahim).Kuanzia neno hili katika risala na katika vitabu nikufuata kitabu cha Mwenyezi Mungu mshindi na mtukufu, vilevile nabii Muhammad (s.a.w) Alikua -ana mwambia muandishi- a'ndike mwanzo wa kila barua wakati anapo watumia viongozi na maraisi na waliyoko mbali ana walingania katika Uislamu, anaanza kuandika:   Kwajina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma mwenye kurehemu.Na alikua Mtume (s.a.w) anaanza mazungumzo yake na maneno yake kwa: Bismi llahi Rrahmani Rrahim, yaonyesha kuanza kwa Bismi llahi Rrahmani Rrahim ni sunna ya Mtume (s.a.w), vilevile Nabii Sulaiman (s.a.w) alipo muandikia Malkia -Mfalme wa saba' Yemen- ameanza kuandika kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma mwenye kuruhemu: (Malkia akasema: Enyi wahishimiwa! Hakika nimeletewa barua tukufu* Imetoka kwa Sulaiman nayo ni:Kwajina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu* Msinifanyie jeuri, na fikeni kwangu nanyi mmekwisha kuwa wenye kusalimu amri). (An-Naml: 29-31). Inatakiwakuanza na jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu, katika kila jambo lenye umuhimu, na katika kila kitabu chenye umuhimu na thamani, na katika kila risala.Kwa sababu hii wale ambao hawaanzi kwenye vitabu vyao na risala zao kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu, hao wameacha sunna ya Mtume na kuto kufuata kitabu cha Mwenyezi Mungu Mshindi na mtukufu, huenda kwa sababu hiyo vitabu vyao na risala zao hazina baraka na ndani yake hakuna faida; kwa sababu ikiwa hakuna jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu huondolewa faida.Risala ya kwanza    Maswala manne ambayo yameambatana na Surati Al-Asr, ILIMUTambua Mwenyezi Mungu akurehemu.Hili ni neno linalo ashiria umuhimu wa mada, anapo sema: Tambua: lina maana ya kwamba atakacho kwambia nimuhimu sana. MWENYEZI MUNGU AKUREHEMU:Hii ni dua kwa mtafutaji wa Ilimu, anawaombea watafutaji wa elimu Mwenyezi Mungu awarehemu, na awape rehma zake, maneno haya ndani yake kuna upole kutoka kwa mwalimu kwenda kwa mwanafunzi, na kwamba yeye anaanza kwa maneno mazuri na dua njema, mpaka awaathiri kwa maneno hayo na wamuelekee mwalimu wao.  Lakini mwalimu akianza maneno kwa ukali na maneno yasio faa jambo hili lina wakimbiza -wanafunzi-, wajibu wa mwalimu na wale wanao lingania katika njia ya Mwenyezi Mungu, na nijuu ya yule anae amrisha mema na kukataza mabaya kuwa mpole kwa yule anae ongea nae, kwa kumuombea dua na kumsifu kwa maneno laini, kwani hili lapelekea kukubali.Lakini mtu mwenye kiburi mjeuri, yeye ana maneno maalumu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Wala msijadiliane na watu wa kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa, isipo kuwa wale walio dhulumu miongoni mwao. Na semeni: Tumeyaamini yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwenu. Na Mungu wetu na Mungu wenu ni Mmoja. Na sisi ni wenye kusilimu kwake).(Al-Ankabut: 46).Wake walio dhulumu nafsi zao miongoni mwa walio pewa kitabu, wakafanya ujeuri na kiburi, hao hawalinganiwi kwa upole, wao hulinganiwa kwa ukali. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:(Ewe Nabii! Pambana na makafiri na wanaafiki, na wakazanie. Na makaazi yao ni Jahannamu, na huo ndio mwisho mbaya). (At-Tawba: 73).Wanaafiki hawajadiliwi kwa silaha, lakini hujadiliwa kwa hoja na maneno makali, nakuwatahadharisha watu wasiwe karibu nao, na Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Na uwaambie maneno ya kuathiri na kuingia katika nafsi zao). (An-Nisaa: 63). Hao wana maneno yao maalumu; kwa sababu wao ni wapingaji wenye viburi, walahawataki haki bali wanataka kuwapoteza watu, hao huambiwa kwa wanayo stahiki. NILAZIMA JUU YETU KUJIFUNDISHA MAMBO MANNE.     Jambo hili sio hiyari, wala sio lenye kupendeza -ukitaka unafanya hukutaka unaacha- isipo kua ni lazima hasa.Tutapo acha kujifundisha mambo haya kwa hakika tuna pata madhambi, kwa sababu jambo hili ni lazima, hakusema: ni hiyari kwetu au yapendeza kwetu, lakini kasema: ni lazima kwetu, na jambo lazima maana yake: mwenye kuliacha hupata dhambi, na kwa sababu elimu haipatikani isipo kuwa kwa kujifundisha, na kujifundisha kuna hitaji umuhimu na juhudi na muda, na kuna hitaji ufahamu na kuhudhurisha moyo, huku ndiko kujifundisha.Mwenyezi Mungu Anasema katika Suratul Asr: kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma mwenye kurehemu (Naapa kwa Zama!* Hakika binaadamu bila ya shaka yumo katika khasara* Isipokuwa wale walio amini, na wakatenda mema, na wakausiana kwa haki, na wakausiana kusubiri). (Al-Asr: 1-3). MAS'ALA MANNE:yaani upekuzi, yameitwa mas'ala; kwa kuwa mambo hayo nilazima kuulizwa na kutiliwa umuhimu. JAMBO LA KWANZA: ILIMU.    Ilimu: makusudio ya ilimu hapa ni elimu ya kisheria; kwa sababu ndio ambayo ni lazima kujifundisha, na mas'ala haya ni lazima kujifundisha kwa kila Muislam, mwanamume au mwanamke, alie huru au mtumwa, tajiri au maskini, mfalme au raiya. Kila Muislam ni lazima kwake kujifundisha mas'ala haya manne.      Na hili ndio linaloitwa na wanachuoni Ulazima waki pekee, ndio ambao ni lazima kwa kila mmoja katika Waislam, swala tano kwa wanamume na wanawake, na swala ya jamaa misikitini kwa wanamume. Jambo hili ni lazima kwa kila Muislam kujifundisha, kwa sababu hiyo alisema: ni lazima juu yetu, na hakusema: ni lazima kwa baadhi yetu, ila kasema: ni lazima juu yetu, yaani sisi Waislam, hii nikatika elimu ambayo ni lazima kwa kila mtu; kwa sababu elimu zipo namna mbili: Jambo la kwanza ambayo ni lazima kwa kila mtu kujifundisha, hakuna udhuru kwa asiye jifundisha, nayo niile ambayo haisimami dini bila yenyewe, mfano nguzo za Uislamtano  ambazo ni:A.Shahada mbili,B.kusimamisha Swala,C.kutoa Zaka, D.kufunga Mwezi mtukufu wa Ramadhani,E. Kuhiji nyumba ya Mwenyezi Mungu,Haifai kwa Muislam kuto jua mambo haya ni lazima kujifundisha.Kwa sababu kujifundisha maana ya Shahada mbili ndiko kujifundisha Tauhidi, anajifundisha Muislam tauhidi ili aifanyie kazi, na ajifundishe yanayo kwenda kinyume na tauhidi ili ajiepushe nayo, haya ndio mafungamano ya Shahada mbili, vilevile ajifundishe nguzo za swala na sharti zake, na yalio yalazima ndani ya swala, na sunna za swala.Vilevile ajifundishe hukumu za zaka, na ajifundishe hukumu za funga, na ajifundishe hukumu za hija, anapotaka kuhiji ni lazima ajifundishe hukumu za hija na hukumu za umra, ili atekeleze ibada hizi katika njia ilio amrishwa.Na kipengele hiki hakuna udhuru kwa yeyote kuto kijua, nacho kinaitwa ulazima wa kila Muislam.Sehemu ya pili katika vigawanyo vya elimu: nayo ni tofauti na elimu ya kisheria ambayo umma unaihitaji kwa ujumla wake, nasio kila mtu huihitaji, mfano hukumu za kuuza na kununua na hukumu za muamala, na hukumu za kutoa wakfu,na mirathi na usia, na hukumu za kuoa, na hukumu za makosa ya jinai, mambo haya nilazima kwa umma; lakini sio lazima kwa kila mtu kujifundisha, isipokuwa watapo jifundisha wenye kutosheleza na malengo yakatimia miongoni mwa wanachuoni yatosha; jambo hili linaitwa: faradhi kifaya, wakifanya baadhi ya watu madhambi huondoka kwa wengine, na watapo liacha wote basi hupata dhambi wote.Ilimu ya lazima ndio ambayo ataulizwa mja siku ya kiyama, kwa nini hukujifundisha? Kwa nini hukuuliza? Ilimu ambayo ataisema pindi atapo wekwa ndani ya kaburi: Mola wangu ni Mwenyezi Mungu, na Uislam ndio dini yangu, na nabii wangu ni Muhammad (s.a.w) jambo hili laokoa, ataambiwa: umejifundisha wapi? Atasema: nimesoma kitabu cha Mwenyezi Mungu na nikajifundisha.Ama Yule alie jitenga mbali na elimu hiyo kwa hakika atapo ulizwa katika kaburi lake atasema: hahahaha sijuwi niliwasikia watu wakisema jambo Fulani nami nikalisema. Mtu kama huyu atawashiwa moto ndani ya kaburi lake -Allah atunusuru- na kaburi litambana hadi mbavu zake hupishana, na kaburi lake huwa ni shimo miongoni mwa mashimo ya moto wa Jahannam; kwa sababu yeye hakutaka kujifundisha wala kusoma, ataambiwa: (Hukutaka kujifundisha wala kusoma).Kapokea hadithi hii Imam Bukhari kwa ufupi kwa hadithi ya Anas (1338) na kaipokea pia Imam Muslim kwa ufupi hadithi ya Anas (ﷺ‬.a) (2870). Na kaipokea Abuudaud kwa hadithi ya Bara' bin A'zib (ﷺ‬.a) kwa urefu (4752). Yeye hakujifundisha, wala hakuwafuata wanachuoni, bali yeye kapoteza uhai wake, huyu ndio ambae atakua sehemu mbaya -Allah atunusuru.ILIMU: Hii ndio ilimu ya kisheria, kinacho takiwa kwa ujumla wetu na mmoja mmoja nako nikumjua Mwenyezi Mungu kwa Majina yake na Sifa zake, na kujua haki zake juu yetu, nayo ni Kumuabudu yeye peke yake hana mshirika katika u'ngu wake, jambo la kwanza kulitambua mwanadamu ni kumjua Mola wake Mtukufu, na namna ya kumuabudu.NA KUMJUA MWENYEZI MUNGU, NA KUMJUA MTUME WAKE. KUMJUA MWENYEZI MUNGU:  Vipi mja atamjua Mola wake? Atamjua kwa alama zake na viumbe wake, miongoni mwa alama za kumjua kwake: usiku na mchana, na katika viumbe vyake: jua na mwezi, kama tunavyo bainisha hapa kwa matakwa ya Allah.Hujulikana Mwenyezi Mungu kwa alama zake za kidunia na Aya zake za qur-ani. Anapo soma qur-ani, humtambua Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba yeye ndio ambae kaumba mbingu na ardhi, naye Mwenyezi Mungu ndie ambae kavifanya kuwa vyepesi vilivyoko mbinguni na ardhini, naye Mwenyezi Mungu ndie ambae Ana huisha na kufisha, naye nimuweza juu ya kila kitu, naye ni Mwingi wa rehma mwenye kurehemu, Qur-ani ina mtambulisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, naye Mwenyezi Mungu ndie ambae Ametune'mesha ne'ma zote, naye Mwenyezi Mungu ndie Alie tuumba na kuturuzuku, utapo soma qur-ani utamjua Mola wako Mshindi na Mtukufu kwa Majina yake na Sifa zake na vitendo vyake.Na utakapo angalia katika hii dunia utamtambua Mola wako Mtukufu kama yeye ndie alie umba, na akafanya  wepesi katika huu ulimwengu na akaupitisha kwa hikma yake na kwa Ujuzi wake, Hii ndio Elimu ya kumjua Mwenyezi Mungu Mtukufu. NA KUMJUA MTUME WAKE:Yeye ni Muhammad (s.a.w) kwa sababu yeye ni Mwenye kufikisha niaba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na yeye niwakati baina yetu na Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kufikisha ujumbe, hapana budi kumjua, unafahamu yeye ni nani? Unafahamu ukoo wake?na ujuwe mji wake, na ujuwe aliyo kuja nayo (s.a.w) unafahamu namana Wahyi ulivyo anza kushuka? Na namna alivyo simama katika kulingania katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika mji wa Makkah na Madina, unajua hestoria ya mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) japo kwa ufupi?.Mtume (s.a.w) yeye ni Muhammad bin Abdullah bin Abdul muttwalib bin Hashim bin Abdi manafi mpaka mwisha wa nasabu ya mtume mtukufu ambayo inaishia kwa NaBii Ibrahim (s.a.w), na unajua namna alivyo ishi kabla ya utume, na namna alivyo jiwa na wah'yi kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na nini alicho fanya (s.a.w) baada ya kupewa utume, utayajua yote hayo kwa kusoma hestoria yake (s.a.w). na haifai kwa Muislam kutomjua mtume (s.a.w) vipi unamfuata mtu hali yakua humjuwi?! Haiingii akilini. NA KUIJUA DINI YA KIISLAM.Kuijua dini ya kiislam: ambayo ndio dini ya huyu Mtume (s.a.w) bali ndio dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ambae kawaamrisha kwa dini hiyo waja wake, naye ndio ambae amekuamrisha kuifuata, na wewe watakiwa kuifuata, hapana budi kuijua hii dini, na Uislam ndio dini ya Mitume wete. Mitume wete dini yao Uislam kwa maana ya ujumla, yeyote alie mfuta Mtume miongoni mwa Mitume huyo ni Muislam mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu mwenye kumfuata yeye, mwenye kumpwekesha yeye. Huu ndio Uislam kwa maana ya ujumla, hakika ni dini ya Mitume wote, Uislam nao ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu kwa tauhidi, na kumfuata yeye kwa kutii, na kujiepusha na ushirikina na watu wake.Ama Uislam kwa maana yake halisi niule ambao amemtuma nao Mwenyezi Mungu Mtume wake Muhammad (s.a.w) kwa sababu baada ya kutumwa Mtume (s.a.w) hakuna dini isipokuwa dini yake (s.a.w), na Uislam umehusishwa katika kumfuata yeye (s.a.w) haiwezekani Yahudi akasema: Mimi ni Muislam, au Naswara aseme: Mimi Muislam baada ya kutumwa Mtume (s.a.w) haliyakua hamfuati, Uislam baada ya kutumwa Mtume (s.a.w) ni kumfuata, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni.)Al-Imran: 31).Huu ndio Uislam kwa maana ya ujumla na kwa maana yake halisi. KWA DALILI.Kwa dalili: sio kwa kuiga lakini kwa dalili katika Qur-ani na Sunna, hii ndio elimu.Amesema Ibnul-QaYyim katika kitabu chake Al-kafiyatu shafiya:                                                                                   Ilimu kasema Mwenyezi Mungu kasema Mtume wake kasema Swahaba hao ndiyo wajuzi Siyo elimu inayo sababisha tofauti za kijinga kati ya Mtume na maoni ya Fulani, hii ndio elimu. Elimu ni ile elimu ya kitabu(Quraan) na sunna, na kuhusu maneno ya wanachuoni yenyewe husherehesha na kuweka wazi zaidi maneno ya Mwenyezi Mungu na maneno ya Mtume wake (s.a.w)Na kwa hakika ndani ya maneno hayo au baadhi yake huwa kuna makosa. KUIFANYIA KAZI ELIMU JAMBO LA PILI: KUIFANYIA KAZI.      Kuifanyia kazi, maana yake: kwa elimu kwa sababu mwanadamu anafundisha na ana jifundisha hapana budi kuifanyia kazi elimu yake, elimu bila matendo itakua ni hatari kwa mwenye nayo, haiwi elimu yenye manufaa ila kwa matendo, ama Yule alie jifundisha na hakuifanyia kazi elimu yake huyo kakasirikiwa; kwa sababu yeye kaijuwa haki na akaiacha kwa elimu.Mtunzi  anasema: (Na Mwanachuoni hakuifanyia kazi elimu yake Ataadhibiwa kabla ya wenye kuabudia Masanamu).Na jambo hili limetajwa kwenye hadithi tukufu: (Mtu wa mwanzo kuingizwa katika moto siku ya kiyama, Mwanachuoni ambae hakuifanyia kazi elimu yake(.Kapokea hadithi hii Imam Tirmidhi (2382).nayo ni hadithi ndefu ndani yake: (Hao wenye sifa tatu ndio wa mwanzo kabisa kuingizwa katika moto siku ya kiyama), hadithi ya Abaa huraira (ﷺ‬.a).Elimu imeambatanishwa na vitendo, na vitendo ndio matunda ya elimu, elimu bila vitendo ni kama mtu bila matunda, hauna faida ndani yake, na elimu imeletwa ili ifanyiwe kazi.Kama yalivyo matendo yasio kua na elimu inakua ni msiba na upotevu kwa mtendaji. Ikiwa mwanadamu anafanya matendo bila elimu kwa hakika matendo yake yana kuwa ni msiba na tabu kwa mtendaji, Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w):(Yeyote atakae fanya Amali hakuna Amri yetu yatakuwa ni yenye kurejeshwa). Kapokea hadithi hii Imam Bukhari kabla ya hadithi (7350), na Muslim (18/1718), hadithi ya Bibi Aisha (ﷺ‬.a), na kapokea Bukhari (2697) na Muslim (17/1718) kutoka kwa Bibi Aisha (ﷺ‬.a) Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w): (Yeyote atakae zua katika dini yetu hii jambo lisilo kuwemo atarejeshewa).Na kwa sababu hii tuna soma katika suratul Fatiha katika kila raka: (Tuongoze njia iliyo nyooka* Njia ya wale ambao uliyo waneemesha, siyo ya wale waliyo kasirikiwa na wala waliyo potea). (Al-Fatiha: 6-7).Akataja Mwenyezi Mungu wale ambao wanafanya bila elimu walio potea, na wale ambao wanafahamu na hawayafanyii kazi wamekasirikiwa, tuzindukane na jambo hili kwa sababu ni muhimu sana. KULINGANIA KATIKA ILIMU. JAMBO LA TATU: KUILINGANIA KWAKE.Kuilingania katika njia ya Mwenyezi Mungu: maana yake: haitoshi kujifundisha mwanadamu na akafanya pekeyake, wala asilinganii katika njia ya Mwenyezi Mungu Mshindi na Mtukufu, hapana budi awalinganie wengine, ili ainufaishe nafsi yake na nafsi za wengine, na kwa sababu elimu hii ni amana, sio milki yako ukawa unailimbikiza tu na una wanyima watu, na watu wana shida nayo, ilio wajibu kwako kufikisha na kubainisha na kuwalingania watu katika kheri, hapana budi kuifikisha na kuibainisha kwa watu.                                               Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Na pindi Mwenyezi Mungu alipo funga ahadi na walio pewa Kitabu kuwa: Lazima mtawabainishia watu, wala hamtokificha). (Al-'Imran: 187). Ahadi hii kaichukua Mwenyezi Mungu kwa Wanachuoni wawabainishie watu yale walio fundishwa na Mwenyezi Mungu ili waeneze kheri, na wawatowe watu katika gize kuwaweka katika nuru, Hii ndio kazi ya Mitume (s.a.w) na wafuasi wao, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Sema: Hii ndiyo njia yangu ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa ilimu mimi na wanao nifuata.Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina). (Yusuf: 108). Hii ndiyo njia ya Mtume (s.a.w) na nhia ya wafuasi wake, ilimu na matendo na kulingania kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, yeyote asie lingania haliyakuwa anao uwezo wa kulingania na ilimu anayo akaificha, kwa hakika atafungwa kamba za moto mdomoni mwake siku ya kiyama kama ilivyo katika hadithi. Kaipokea Abuu daudi (3658), na Tirmidhi (2649), na Ibnu Maja (261) na (266) hadithi ya Abaa huraira (ﷺ‬.a) Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w): (Yeyote atakae ulizwa katika mambo ya ilimu akaficha, atafungwa kamba na Mwenyezi Mungu za moto mdomoni mwake siku ya kiyama). Na Ibnu Maja (265) kwa hadithi ya Abii Saidi l-khudri (ﷺ‬.a) Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w): (Yeyote atakae ficha Elimu katiaka Elimu anazo wanufaisha Mwenyezi Mungu watu, mambo ya dini, Allah atamfunga siku ya kiyama kamba za moto mdomoni mwake). KUFANYA SUBRA JUU YA MAUDHI YANAYO PATIKANA NDANI YAKE. JAMBO LA NNE:  KUFANYA SUBRA JUU YA MAUDHI YANAYO PATIKANA NDANI YAKE.Subra juu ya maudhi yanayo patikana ndani yake:kama inavyo julikana yeyote ane walingalia watu aka waamrisha mema na aka kataza mabaya, kwa hakika atafikwa na maudhi kwa watu waovu; kwa sababu watu wengu hawapendi kheri, bali hupenda matamaniyo na haramu na matakwa ya nafsi yaliyo mabaya, anapokuja mwenye kuwalingania kwa Mwenyezi Mungu, na kukemea matamanio yao, hapana budi.Miongoni mwao kufanya vibaya ima kwa maneno au kauli,     Ni lazima juu ya mwenye kulingania katika njia ya Mwenyezi Mungu na kutaka radhi za Mwenyezi Mungu asubiri maudhi, na aendelee katika kulingania, na kiigizo chake ni Mitume (s.a.w) na mbora wao na wa mwisho wao Muhammad (s.a.w).Yamemfika mangapi kutoka kwa watu? Na maudhi mangapia kayapata kwa maneno na vitendo? Walisema: mchawi, muongo, wakasema: mwandawazimu. Wakasema dhidi yake maneno ambayo ameyataja Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya   Qur-ani, wakamfanyia maudhi, kapigwa mawe mpaka miguu yake ikatoa damu (s.a.w) wakati alipo walingania katika njia ya Mwenyezi Mungu, kawekewa utumbo wa ngamia juu ya mgongo wake akiwa ana sujudu mbele ya Alkaaba, kaahidiwa kuuliwa katishwa, katika vita vya Uhudi ali dhuriwa yeye na maswahaba zake (s.a.w),kavunjwa memo yake manne ya mbele, kapasuliwa kichwani mwake (s.a.w) kasukumwa ndani ya shimo, haliyakuwa ni nabii wa Mwenyezi Mungu, madhara yote haya kayapata katika kulingania kwaajili ya Mwenyezi Mungu, lakini yeye kasubiri kavumilia haliyakua ndio mbora wa viumbe wote (s.a.w), hapana budi kwa Yule anae fanya kazi ya kulingania kufikwa na maudhi kiasi cha imani yake na dawa wake; pamoja na yote hayo yatakiwa asubiri, akiwa yupo katika haki, asubiri avumilie, yupo katika njia ya Mwenyezi Mungu na maudhi yanayo mfika yatakuwa katika mizani yake mema mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.Mambo haya ma nne nilazima tujifundishe kwa urefu,Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Naapa kwa Zama!). (Al-Asr1). Ameapa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa zama na wakati nao ni kiumbe, na Mwenyezi Mungu Mtukufu anaapa kwa anacho kitaka miongoni mwa viumbe, na kiumbe haapi isipokuwa kwa jina la Mwenyezi Mungu, Na Mwenyezi Mungu haapi isipokuwa kwa kitu chenye umuhimu, na ndani yake kuna alama miongoni mwa alama zake, Utakasifu niwake na ametukuka, ndani ya zama kuna mazingatio na umuhimu, na kwa sababu hiyo Ameapa Mwenyezi Mungu kwa muda wa Laasiri, na kwa usiku unapo funika na akaapa kwa mchana. Ama kiumbe haifai kuapa isipokua kwa jina la Mwenyezi Mungu, na haifai kwetu kuapa kwa asie kua Mwenyezi Mungu, Amesema Mtume (s.a.w): (Yeyote atakae apa kwa asiye kua Mwenyezi Mungu kwa hakika amekufuru au ameshirikisha). Kapokea hadithi hii Imam Abuu daudi (3251), na Tirmidhi (1535) kwa hadithi ya Ibni Omar (ﷺ‬.a).Na Akasema: (Yeyote anae taka kuapa Aape kwa jina la Mwenyezi Mungu au akae kimya).Kapokea hadithi hii Imam Bukhari (6108), na Muslim (1646) kwa hadithi ya Ibni Omar (ﷺ‬.a). NI LIPI JIBU LA KIAPO?    Ni kauli yake: (Hakika binaadamu bila ya shaka yumo katika hasara).(Al-Asr: 2).Mwanaadamu Binaadamu woote hakuvuliwa hata mmoja siyo wafalme wala maraisi, wala matajiri, walaMafakiri, wala walio huru, wala watumwa, wala wanamume wala wanawake, kila binaadamu yupo katika Hasara, maana yake: katika hasara na maangamio ikiwa wataupoteza huu muda ulio wa thamani, wakautumia katika kumuasi Mwenyezi Mungu, na katika yanayo wadhuru.Wanaadamu weete wamo ndani ya hasara na maangamio isipokuwa atakae sifika na sifa nne nazo: Ilimu, na Matendo, na kulingania katika njia ya Mwenyezi Mungu, na kufanya subra juu ya maudhi.Yeyote atakae sifika na sifa hizi nne ameokoka katika hii hasara. Wala haiwezekani kumuamini Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa Ilimu, Ambayo ndio kumjuwa Mwenyezi Mungu.(Na wakatenda mema). (Al-Asr: 3).Maana yake: wamefanya matendo yalio mazuri katika mambo ya lazima na yasio yalazima, wakatumia muda wao kwa matendo mema kwa yale yanayo wanufaisha katika dini yao na dunia yao.   Hata matendo ya kidunia ndani yake kuna ujira ikiwa utakusudia katika hayo matendo kuwa ni sababu ya kufanya twaa, itakuwaje matendo kwaajili ya akhera, lamsingi jitahidi usipoteze muda utumie katika mambo yanayo kunufaisha na yanayo kufiidisha.)Na wakausiana kwa haki). (Al-Asr: 3).Wameamrisha mema, na Wamekataza mabaya, na Wakalingania katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, Na Wakafundisha Ilimu yenye manufaa, na Wakazagaza Ilimu na kheri kwa watu.Wakawa walinganiaji katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.)Na wakausiana kusubiri). (Al-Asr: 3).Walifanya subra kwa yale walio yapata,Na Subra katiak lugha ya kiarabu: kuziwia, lakini makusudio hapa: kuiziwia nafsi katika kumcha Mwenyezi Mungu.Nazo zipo aina tatu:1. Kufanya subra katika kumtii Mwenyezi Mungu.2.Kufanya subra kwa yale aliyo kataza Mwenyezi Mungu.3.Kufanya subra juu ya makadara ya Mwenyezi Mungu.1.Subra katika kumtii Mwenyezi Mungu, kwa sababu nafsi inapenda uvivu na inapenda raha, hapana budi kuizoweza binaadam nafsi juu ya kutii na kusali na kufunga na kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu japokuwa mambo haya nafsi haiyapendi, anaiziwiya katika utiifi wa Mwenyezi Mungu.2.Kufanya subra kwa yale aliyo kataza Mwenyezi Mungu.   Nafsi inataka mambo ya haramu, na mambo ya matamanio, inaelekea huko na kuvutiwa sana, hapana budi aifunge na kuiziweya katika mambo ya haramu, jambo hili lahitaji subra, na siyo jambo rahisi kuizuiya nafsi katika mambo ya matamanio ya haramu, ambae hana subra kwa hakika nafsi yake itamshinda na itamvuta kwenye haramu.3.Kufanya subra juu ya makadara ya Mwenyezi Mungu yenye kuu miza. Matatizo yanayo mpata mwanaadamu kwa kufiliwa na mtu wake wa karibu, au kupoteza mali, au maradhi yanayo mpata mwanaadamu, hapana budi afanye subra juu ya hukumu na makadara ya Mwenyezi Mungu, asikate tamaa wala kuchukia, bali auziwiye ulimi na kuto omboleza na kutokata tamaa, na aiziwiye nafsi kutokata tamaa, na aziwiye viungo na kuto jipiga makofi na kuchana nguo kwa hasira, Hii ndiyo subira wakati wa matatizo.Kuhusu maasi asifanyi subra juu yake bali atubiye kwa Mwenyezi Mungu na ayakimbiye; lakini wakati wa mitihani ambayo hukuingia ndani yake, bali nikutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amekukadiria juu yako na kukupa mtihani au adhabu kwako kutokana na madhambi uliyo yafanya, kama alivyo sema Mwenyezi Mungu Mtukufu:(Na misiba inayo kupateni ni kwa sababu ya vitendo vya mikono yenu. Naye anasamehe mengi). (Ash-Shura: 30). Utapofika msiba kwa Muislam katika nafsi yake au mali zake au watoto zake au ndugu wa karibu au yeyote kati ya ndugu zake Waislam ni juu lako kufanya subra na kutegemea malipo kwa Mwenyezi Mungu.Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:(Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea *  Hao juu yao zitakuwa Baraka zitokazo kwa Mola wao Mlezi na rehema. Nao ndio wenye kuongoka). (Al-Baqara: 156-157).Hii ndio subra, na mfano wake kufanya subra juu ya maudhi unayo yapata katika kulingania neno la Mwenyezi Mungu Mtukufu hayo nikatika matatizo, nilazima ufanye subra kwa hayo unayo yapata katika njia ya kheri, Nawala usiachi kufanya kheri; kwa sababu baadhi ya watu wanataka kufanya kheri lakini akikutana na jambo linalo chukiza anasema: sio lazima juu yangu kuiweka nafsi yangu kwenye mambo kama haya, kisha anaacha kufundisha ikiwa ni mwalimu, anaacha kulingania katika njia ya Mwenyezi Mungu, anaacha kuongea ikiwa ni khatwibu wa muskiti, anaacha kusalisha muskitini, anaacha kuamrisha mema na kukataza mabaya,  Huyu hakusubiri kwa aliyo yapata miongoni mwa maudhi.Amesema Imam Shaafy (ﷺ‬.a):"Laiti Mwenyezi Mungu asinge teremsha dalili kwa waja wake ila surahii  ingeliwatosha".Kwa hakika kanukuu Imam Shafy: yeye ni Muhammad ibni Idrisa Ashaafy nasabu kwa babu yake wa nne jinalake shafy, nae ni mkuraishi, katika familia ya mutw-labi, kafariki mwaka (204) h.j.ﷺ‬. naye ni mmoja kati ya Maimamu wa nne, na akasema maneno haya kwa sababu Mwenyezi Mungu kabainisha kwanye sura hii sababu za kupotea na sababu za kuongoka.Kuhusu sababu za kuongoka: Asifike mwanaadamu na hizi sifa nne: Ilimu, na Matendo, na Kulingania, nakufanya subra juu ya maudhi yanayo tokea katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ikasimama hoja kutoka mwa Mwenyezi Mungu juu ya waja wake kwa sura hii, Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ana waambia: Hakika mimi Allah nime kubainishieni sababu za kuokoka katika sura hii fupi sana.Na Qur-ani yate pamoja na Sunna vime fafanuwa zaidi mambo haya ma nne, lakini sura hii imebainisha sababu za kuongoka kwa ujumla, ikasimama hoja kwa viumbe, na zikabaki dalili ndani ya qur-ani na sunna ziki fafanuwa zaidi na kuweka wazi mambo haya ma nne, na wala sio makusudio ya Imam Shafy kwamba sura hii yawatosha watu, kama asingeliteremsha Mwenyezi Mungu sura tofauti na hii, lakini hoja imesimama juu yao; kwa sababu Mwenyezi Mungu kisha bainisha ndani yake sababu za kuokoka na sababu za uongofu, asitokei yeyote siku ya kiyama akasema:Mimi sijuwi sababu za uongofu wala sijuwi sababu za kupotea naye akisoma sura hii fupi sana. NA AKASEMA IMAMU BUKHARI (ﷺ‬.a): MLANGO UNAO ELEZEA ILIMU KABLA YA KAULI NA MATENDO.Na dalili: (Basi jua ya kwamba hakuna Mungu anayefaa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na omba maghufira kwa dhambi zako na za Waumini wanaume na Waumini wanawake). (Muhammad: 19).Akaanza Ilimu kabla ya kauli na matendo.Bukhari: yeye ni Muhammad bin Ismail bin Imrahim   Al-Bukhary, kanasibishwa na Bukhara mji uliyoko Mashariki, ni Imam wa Hadithi bingwa wa kuhifadhi (ﷺ‬.a), mtunzi wa (Swahihi) kitabu ambacho kina usahihi baada ya kitabu cha Mwenyezi Mungu.Ilimu kabla ya kauli na matendo; kwa sababu matendo hayanufaishi isipokuwa yakijengewa juu ya ilimu, lakini matendo yaliyo jengeka juu kutenda.Na dalili: kuhusu kichwa cha habari kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Basi jua ya kwamba hakuna Mungu anayefaa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na omba maghufira kwa dhambi zako). (Muhammad: 19).Hakika kaanza na Ilimu, Na kauli ya ujinga kwa hakika hayamnufaishi mwenye nayo bali ni hasara kwake na upotovu juu yake siku ya kiyama, hapana budi atangulize kujifundisha kabla ya yake Tukufu: (Na omba maghufira) hii ndio Amali, Akaanza Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Elimu kabla ya amali; kwa sababu matendo yakiwa niya kijinga hakika hayamnufaishi mwenye nayo, Aanze mwanaadamu na Elimu kwanza kisha afanye yale aliyo jifundisha, huu ndio msingi wa dini ya uislam.Utangulizi:Kila sifa kamilifu niza Mwenyezi Mungu muumba wa vitu vyote sala na amani ziwe juu ya kipenzi cha Allah mtume wetu Muhammad (s.a.w) ambae ametuwa akiwa nirehma kwa walimwengu wote akiwa nimwenye kubashiri pepo na kukhpfisha moto, na ziwe juu ya maswahaba zake wote waongofu na wote watakao fuata muongozo wake mpaka siku ya qiyama. Kitabu hiki ni muendelezo wa sehemu ya kwanza ya kitabu kilicho tangulia tukiwa tunaendelea kunufaika na maneno alio andika imamu Imamu Sheikh Saleh bin Fauzan Al-Fawzan. Mwenyezi Mungu amhifadhi. RISALA YA TATU MAMBO MATATU NI LAZIMA MUISLAM AJIFUNDISHE NA AYAFANYIE KAZI.     Tambua Mwenyezi Mungu akurehemu ya kwamba nilazima juu ya kila Muislam wa Kiume na Wakike kujifundisha mambo haya matatu na kuyafanyia kazi.TAMBUA: ni neno ambalo huletwa kwaajili ya umuhimu wa kinacho elezwa baadae, na maana yake: jifundishe na ufahamu na uwe na yakini.MWENYEZI MUNGU AKUREHEMU: Hii ni dua kwako ya rehma, na hili pia limekwisha tangulia kwamba mwalimu yatakiwa awe mpole kwa mwanafunzi, na amuombee dua na kumuhimiza, kwa sababu haya nikatika njia bora za kufundisha, na wala haifai kwake kumkabili kwa ukali na uzito na chuki, kwa sababu haya nanapelekea achulie Elimu, pia yaonyesha nasaha ya mwanachuoni, na kwamba yeye anachotaka ni nasaha na kuelekeza na usawa.NI LAZIMA: Yaonyesha kwamba jambo hili siyo hiyari, anaetaka anafanya na asietaka anaacha, bali ulazima hapa ni katika namna ya mkazo kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na siyo ulazima kutoka kwa mwanachuoni, bali ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa yale aliyo yateremsha katika Kitabu na Sunna, katika kuwalazimisha waja kwa mambo haya. NI LAZIMA JUU YA KILA MUISLAM WAKIUME NA WAKIKE,    Maana yake: ni lazima juu yakila mwanamume na mwanamke miongoni mwa Waislam sawasawa wakiwa huru au watumwa au wanaume au wanawake, kwa sababu mwanamke hushirikiana na mwanaume kwenye mambo ya lazima mengi sana, isipokuwa yale yanayo wahusu wanaume pekeyao kwa dalili inayo wahusu wao tu, mfano: ulazima wa swala za jamaa misikitini, swala za ijumaa, na mfano wa kuzuru makaburi mambo haya ni haswa kwa wanaume, na mfano wa kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, sababu jambo hili ni maalumu kwa wanaume.MAMBO MATATU:  Kujifundisha maana yake hapa: kupata elimu kutoka kwa wanachuoni na kuhifadhi na kufahamu na kudiriki mambo sawasawa, hii ndiyo elimu, nawala siyo makusudio kujisomea tu ovyo au kutwalii tu.Na haifai kujifundisha kwenye vitabu kama hali ya zama tulizo nazo, kwa sababu kujifundisha kwa kutumia vitabu ni hatari sana, hupatikana madhara makubwa,  na kufundishana -kwanjia hiyo ya vitabu- kuna dhuru zaidi kuliko mjinga; kwa sababu mjinga anatambuwa kama yeye ni mjinga na husimama kwenye kiwango chake, lakini mwenye kujifundisha hujiona ya kwamba ni mjuzi, ana halalisha aliyo ya haramisha Mwenyezi Mungu, na ana haramisha aliyo ya halalisha Mwenyezi Mungu, na anaongea na husema juu ya Mwenyezi Mungu bila ya elimu, ni mambo hatari sana. Elimu haichukuliwi kutoka kwenye vitabu moja kwa moja, isipokuwa vitabu ni nyenzo tu, lakini uhakika wa elimu huchukuliwa kutoka kwa wanachuoni ambao wapo katika njia ya wema walio tangulia vizazi kwa vizazi, na vitabu ni nyenzo za kutafutia elimu.KUAMINI YA KWAMBA:A.MWENYEZI MUNGU AMETUUMBA.B. ANATURUZUKU.C. HAKUTUACHA BURE.                                                                                          Mwenyezi Mungu ametuumba na kuturuzuku na hajatuacha bure.1:kwamba Mwenyezi Mungu ametuumba, maana yake: Ametuweka baada ya kuto kuwepo, sisi kabla yakutuumba hatukuwa chochote, kama alivyo sema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Hakika ulimpitia binaadamu kipindi katika zama ambacho kwamba hakuwa kitu kinachoweza kutajwa). (Al-Insaan: 1).Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Akasema: Ndio hivyo hivyo amesema Mola wako: Haya ni rahisi kwangu. Na hakika Mimi nilikwisha kukuumba wewe zamani na hali hukuwa kitu). (Maryam: 9).    Alikuwa binaadamu kabla ya kuumbwa si chochote, ambae kamuweka na kumuumba ni Mwenyezi Mungu Mtukufu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji?). (Tuur: 35).2:Na kuturuzuku: Tulipokuwa niwenye kuhitajia rizki chakula kinywaji mavazi nyumba vipando na mazuri, alitambua Mwenyezi Mungu Mtukufu shida zetu akawepesisha vilivyoko mbinguni na aridhini vyote kwa masilahi yetu kwaajili tubakie kwenye uhai, na kwaajili ya kuvitumia ili tufanye lengo la kuumbwa kwetu, nalo ni Ibada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.3:Na hakutuacha bure: ni kitu kilicho achwa ambacho hakina faida yoyote, Mwenyezi Mungu ametuumba na kuturuzuku kwa hikma, hakutuumba kwa mchezo wala bure, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Je! Mlidhani ya kwamba tuli kuumbeni bure na yakwamba nyinyi kwetu hamtarejeshwa?). (Al-Muuminuun: 115).Na akasema Mwenyez Mungu Mtukufu: (Ati anadhani mwanadamu kuwa ataachwa bure?* Kwani hakuwa yeye ni tone ya manii lilio shushwa?* Kisha akawa pande la damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo). (Al-Qiyamah: 36-38).Na akasema: (Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yao bure. Hiyo ni dhana ya walio kufuru. Ole wao walio kufuru kwa Moto utakao wapata). (Swaad: 27.( Mwenyezi Mungu ametuumba na katuumbia hizi rizki na yanayo wezekana kwa hikma kubwa na lengo nzuri, nalo ni kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wala hakutuumba kama wanyama ambao wameumbwa kwa maslahi ya viumbe kisha vinakufa na kuondoka; kwa sababu havija kalifishwa wala kuamrishwa wala kukatazwa, kwa hakika Ametuumba kwaajili ya ibada yake, kama alivyo sema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi* Na sitaki kwao riziki, wala sitaki wanilishe* Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti). (Adh-Dhaariyaat: 56-58).    Wala hakutuumba kwaajili ya maisha ya dunia tu, ili tuishi ndani yake, tukeshe tucheze, na tule na tunywe, tujitanue ndani yake kisha pisiwe na chochote, na kwa hakika maisha ni shamba, na sokoni ni nyumba ya akhera, tunajiandaa kwa matendo mema, kisha tunakufa na tunaelekea huko, kisha tunafufuliwa, kisha tuna hesabiwa na tunalipwa kwa matendo yetu.Haya ndio makusudio ya kuumbwa majini na watu, na ushahidi wa hayo ni mwingi sana wakuonyesha kufufuliwa na malipo na hesabu, na akili inaonyesha hili, kwa sababu haiwezekani kwa hikma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuumba kiumbe waajabu, na akaufanya huu ulimwengu kwaajili ya binadamu kisha awaache wafe waondoke bila faida. Huu ni mchezo, hapana budi kujulikana majibu ya matendo katika nyumba ya akhera.    Kwa hili kuna baadhi ya watu wanao maliza umri wao katika Ibada ya Mwenyezi Mungu na katika kumtii yeye, hali ya kuwa yupo katika ufakiri na shida, na huenda akawa ni mwenye kudhulumiwa kubanwa kuonewa na wala asilipiwe katika hii dunia, na kinyume chake, unakuta mwengine kafiri hamuamini Mungu na ni muovu lakini amekunjuliwa ana furaha katika hii dunia, ana neemeka amepewa anayo yataka, anafanya aliyo haramisha Mwenyezi Mungu, anawadhulumu waja anawafanyia vibaya, anakula mali zao, anaua bila haki, anawasaliti watu anajinyanyuwa kisha anakufa katika hali hiyo, hakupata chochote katika adhabu.Je! Yafaa kwa uadilifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na hekima zake amuache huyu mtiifu bila malipo?, na amuwache huyu kafiri bila kumlipa?, jambo hili halifai kutokana na Uadilifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu,Kwa sababu hiyo kajaaliya nyumba ya akhera aliye fanya wema kulipwa kwa wema wake, na aliye fanya mabaya kwa mabaya yake, patadhihirika matunda ya matendo.Dunia ni nyumba ya matendo, lakini akhera yao ni nyumba ya malipo, ima pepo au moto, na hakutuacha bure kama wanavyo dhani wasio muamini Mwenyezi Mungu na wanao amini uhai wa dunia bila akhera, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:  (Na walisema: Hapana isipokuwa huu uhai wetu wa duniani tunakufa na tunaishi, na hapana kinacho tuhiliki isipokuwa zama. Lakini wao hawana ilimu ya hayo, isipokuwa wao wanadhani tu). (Al-Jaathiyah: 24). Haya ndio maneno ya wasio muamini Mwenyezi Mungu ambao hawaamini kufufuliwa.Na kwa hakika Mwenyezi Mungu kawakanusha Akasema: (Kwani tutawafanya Waislamu mfano wa wakosefu?* Mna nini? Mnahukumu vipi?). (Al-Qalam: 35-36).Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Je! Wanadhani wanao tenda maovu kuwa tutawafanya kama walio amini, na wakatenda mema, sawa sawa uhai wao na kufa kwao? Ni hukumu mbaya wanayo ihukumu!). (Al-Jaathiyah: 21).    Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Ama! Tuwajaalie walio amini na wakatenda mema kama wafanyao uharibifu katika ardhi? Au tuwajaalie wachamungu kama waovu?). (Swaad: 28).                                                                              Hili haliwezekani na wala haliwi.BALI KATUTUMIA MITUME.     Ilivyokuwa Ibada haifai tuichukue kutoka kwa Fulani na Fulani tutakao waona wazuri, au kumuiga Fulani na Fulani katika wanadamu, katutumia Mwenyezi Mungu Mitume watubainishie Namna tutakavyo muabudu; kwa sababu Ibada ni kitu rasmi, na haifai kumuabudu Mwenyezi Mungu kwa chochote isipokuwa kwa aliyo amrisha.Ibada ni kitu rasmi juu ya yale walio kujanayo Mitume (s.a.w), na hekima ya kutumwa Mitume ili wawabainishie watu namna watakavyo muabudu Mungu wao, na wawakataze shirki na kumkufuru Mwenyezi Mungu Mtukufu.Hii ndiyo kazi ya Mitume (s.a.w), kwa sababu hii anasema Mtume (s.a.w): (Yeyote atakae zuwa katika dini yetu mambo ambayo hayapo atarejeshwa mwenyewe). Kapokea hadithi hii Imam Bukhari kabla ya hadithi (7350), na Muslim (18/1718), hadithi ya Bibi Aisha (ﷺ‬.a( .Ibada ni kitu rasmi, na bida'a ni yenye kurejeshwa, na mambo yasio faa ni yenye kurejeshwa, na kufuata kama kipofu imekatazwa. Ibada hazichukuliwi isipokuwa katika sheria alio kujanayo Mtume (s.a.w).BALI KATUTUMIA MTUME:       Nae ni Muhammad (s.a.w) mwisho wa manabii, amemtuma ili atubainishie kwa nini Ametuumba? Na atubainishie namna ya kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu, na atukataze ushirikina na ukafiri na maasi, hii ndio kazi ya Mtume (s.a.w) na amefikisha kwa uwazi, na akatekeleza amana, na akaunasihi Umma (s.a.w), na akabainisha na akaweka wazi, na akatuacha katika njia nyeupe usiku wake ni kama mchana wake, yeyeto atakae kwenda kinyume ataangamia, kama ilivyo katika maneno yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe ndiyo Dini). (Al-Maaida: 3). YEYOTE ATAKAE MTII ATAINGIA PEPONI, NA YEYOTE ATAKAE MUASI ATAINGIA MOTONI.Atakae mtii, maana yake: kwa yale aliyo amrisha ataingia Peponi, na atakae muasi, maana yake: kwa yale aliyo kataza ataingia Motoni. Ukweli wa haya ni mwingi ndani ya Qur-ani, kama alivyo sema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Mwenye kumti'i Mtume basi kwa hakika ndio amemti'i Mwenyezi Mungu). (An-Nisaa: 80). Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Na mkimtii yeye mtaongoka). (An-Nuur: 54).Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Na mtiini Mtume, ili mpate kurehemewa). (An-Nuur: 56).Yeyote atakae mtii ataongoka na ataingia Peponi, na yeyote atakae muasi atapotea na ataingia Motoni, amesema Mtume (s.a.w): (Nyoote mtaingia Peponi isipokuwa Yule atakaekataa, wakasema: ni nani atakae kataa ewe Mtume? Akasema: Yeyote atakae nitii Mimi ataingia Peponi na yeyote atakae niasi Mimi huyo ndiyo alie kata(. Kapokea hadithi hii Imam Bukhari (7280). hadithi ya Abaa huraira (ﷺ‬.a).Kauli yake Mtume (s.a.w): ATAKAE KATAA, maana yake: Amekataa kuingia Peponi. Na akasema Mtume (s.a.w): (Hato nisikia mimi yahudi au mkristo kisha hakuamini yale niliyo kujanayo isipokuwa ataingia Motoni). Kapokea hadithi hii Imam Muslim (153), hadithi ya Abaa huraira (ﷺ‬.a).       Yeyote atakae mtii ataingia peponi na yeyote atakae muasi ataingia motoni, na hii ndio tofauti kati ya muislamu na kafiri.Na dalili kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Hakika Sisi tumemtuma kwenu Mtume aliye shahidi juu yenu kama tulivyo mtuma Mtume kwa Firauni* Lakini Firauni alimuasi huyo Mtume, basi tukamkamata mkamato wa mateso).  (Al-Muzammil: 15-16).  Na dalili, maana yake: juu ya kutumwa Mitume kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Hakika Sisi tumemtuma kwenu Mtume aliye shahidi juu yenu kama tulivyo mtuma Mtume kwa Firauni* Lakini Firauni alimuasi huyo Mtume, basi tukamkamata mkamato wa mateso). Na maana ya: Tumemtuma: tumemtumia na tumemfunulia.KWENU: Enyi makundi aina mbili majini na watu, ni maneno kwa watu wote; kwa sababu ujumbe wa Nabii Huyu unaenea watu wote hadi kusimama kiyama. MTUME: ndie Muhammad (s.a.w).SHAHIDI JUU YENU: maana yake: mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ya kiyama kama yeye kakufikishieni ujumbe wa Mwenyezi Mungu na hoja ikasimama juu yenu, kama alivyo sema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Mitume hao ni wabashiriaji na waonyaji, ili watu wasiwe na hoja juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kuletewa Mitume. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima).  (An-Nisaa: 165).Asitokee yeyote siku ya kiyama akasema: mimi sijui kama nimeumbwa kwaajili ya Ibada, mimi sijui yepi ni lazima kwangu, na sijui yepi ni haramu kwangu, haiwezekani akasema haya, kwa sababu Mitume (s.a.w) wamekwisha wafikishia, na huu Umma wa Muhammad (s.a.w) utashuhudiya juu yao, kama alivyo sema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wastani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe ni shahidi juu yenu).  (Al-Baqara: 143). Umma huu utakuwa ni shahidi juu ya nyumati zilizo tanguliya siku ya kiyama kwamaba Mitume wao wamewafikishia ujumbe wa Mwenyezi Mungu, kwa yale walio yakuta ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa sababu Mwenyezi Mungu katusimulia habari za nyumati zilizo tanguliya na Mitume na walio yasema kwa nyumati zao. Yote hayo tumeyajua kupitia kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu kitabu ambacho Hautakifikia upotovu mbele yake wala nyuma yake, kimeteremshwa na mwenye hikima, msifiwa.NA ATAKUWA MTUME: Nae ni Muhammad (s.a.w), atakuwa ni shahidi juu yenu Ummati Muhammad, atashuhudia juu yenu mbele ya Mwenyezi Mungu kwamba yeye amesimamisha juu yenu hoja, na akafikisha kwenu Ujumbe, na akakupeni nasaha kwaajili Mwenyezi Mungu, hapatakuwa na hoja kwa yeyote siku ya kiyama kwa kusema: sikufikiwa na chochote, sikufikiwa na muonyaji, hadi makafiri Watakiri wakati watakapo tupwa motoni, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Kila mara likitupiwa kundi humo walinzi wake huwauliza: Kwani hakukujieni mwonyaji? Watasema: Kwani! Ametuijia mwonyaji, lakini tulimkadhibisha, na tukasema: Mwenyezi Mungu hakuteremsha chochote. Nyinyi hamumo isipokuwa katika upotovu mkubwa!). (Al-Mulk: 8-9). Wanasema kwa Mitume: Nyinyi mpo katika upotovu, wao wanawakadhibisha Mitume na kuwafanya ni wapotovu. Hii ndio hikima ya kutumwa Mitume; kwaajili ya kusimamisha hoja kwa waja, na muongozo kwa yule anaetakiwa na Mwenyezi Mungu uongofu, Mwenyezi Mungu huwaongoza waja wake awatakao kupitia mitume, na husimamisha hoja juu ya wenye kupinga na kukanusha na kukufuru. KAMA TULIVYO MTUMA MTUME KWA FIRAUNI: Mtume: ni Nabii Mussa (s.a.w), na Firauni ndie mfalme jeuri wa Misri, ambae alidai Uungu, na Firauni: ni jina la kubandikwa kila anae tawala Misri huitwa Firauni. Makusudio hapa ni Firauni alie dai Uungu: (Akasema: Mimi ndiye Mola wenu mkuu kabisa). (An-Naziat: 24). LAKINI FIRAUNI ALIMUASI HUYO MTUME: Huyo ni Nabii Mussa (s.a.w), alipingwa na Firauni kama alivyo simulia Mwenyezi Mungu katika kitabu chake yaliyo tokea kati ya Nabii Mussa na Firauni, na alipo fikia Firauni na watu wake. BASI TUKAMKAMATA,  Maana yake: Tulimkamata  Firauni kwa adhabu, nayo: hakika Mwenyezi Mungu alimzamisha yeye na watu wake ndani ya bahari kisha akawaingiza motoni: (Basi kwa ajili ya makosa yao waligharikishwa wakaingizwa Motoni). (Nuuh: 25).Akawa katika moto katika barzakhi (Kaburini), Amesema Mwenyezi Mungu  mtukufu: )Wanaonyeshwa Moto asubuhi na jioni). (Suuratul Ghaafir 46(.Adhabu hii itakuwa kaburini kabla ya akhera,wataonyeshwa motoni asubuhi na jioni,yaani kuchomwa namoto mpaka kitakapo simama kiyama,na huu niushahidi tosha wakuthibitisha kuwepo kwa adhabu kaburini,Allah atukinge, Allah anasema:(Na itapo fika Saa ya Kiyama patasemwa: Waingizeni watu wa Firauni katika adhabu kali kabisa!) (Suuratul Ghaafir 46).ADHABU TATU ZA WATU WA FIRAUN:1-Hakika mwenyezi mungu aliwazamisha na kuwapoteza kwamuda mmoja.2-Hakika wao wana adhibiwa Katika makaburi yao mpaka kitakapo simama kiyama.3-Watakapo fufuliwa siku yakiyama wataingia katika adhabu kali,Allah atukinge.Vilevile yeyote atakae muasi mtume (s.a.w) hakika mafikio yake yatakua katika adhabu kali kuliko Firauni, kwasababu mtume Muhamad (s.a.w) ni mtume bora kuliko mitume walio pita, atakae muasi adhabu yake inakuwa kubwa zaidi.Mwenyezi mungu anasema kuhusu firauna: (basi tukamshika mshiko wa mateso).Yaani kwa ukali na nguvu bila ulaini ndani yake.Anasema Mwenyezi Mungu katika surati Hudi:{Na ndio kama hivyo ndivyo inavyo kuwa Mola wako Mlezi anapo ikamata miji inapo kuwa imedhulumu. Hakika mkamato wake ni mchungu na mkali.} ( Hudi 102).Aya hii ni ushahidi tosha juu ya neema ya Mwenyezi mungu juu yetu kwa kumtuma mtume Muhamad (s.a.w) kwetu na hakika lengo la kumtuma ni kutubainishia njia sahihi ya kufanya ibada, yoyote atakae mtii ataingia peponi, na yoyote atakae muasi ataingia motoni, kama alivyo ingia firauni na watu wake motoni, pindi walipo muasi Nabii Mussa (a.s), vilevile maadui wa mitume wote hii ndio njia yao.Mwenyezi Mungu mtukufu haridhii kushirikishwa nayoyote katika ibada. MAS’ALA YA PILI:Hakika Mwenyezi Mungu haridhii kushirikishwa na yoyote katika ibada.Haya mas’ala yanaambatana na mas’ala ya kwanza, kwa kuwa ya kwanza:Yanabainisha uwajibu wa kumuabudu Mwenyezimungu na kumfuata mtume (s.a.w), na ndio maana ya shahada mbili, shahada ya (Lailaha ila Allah Muhamadu rasulu Allah).Na mas’ala yapili: Nikwamba ibada inapo changanyika na ushirikina haikubaliwi, kwasababu ni lazima iwe ibada kwaajili ya Mwenyezi Mungu mshindi mtukufu.Yoyote atakae muabudu Mwenyezi Mungu akamshirikisha na kitu kingine ibada yake inakuwa batili, kuwepo ibada hiyo na kuto kuwepo ni sawa, kwasababu ibada haifai bila ikhlas na kumpwekesha Mwenyezi Mungu, pindi zitakapo changanyika na ushirikina zitaharibika, kama alivyosema Mwenyezi Mungu mtukufu:{ Na kwa yakini yamefunuliwa kwako na kwa walio kuwa kabla yako: Bila ya shaka ukimshirikisha Mwenyezi Mungu a'mali zako zitaanguka, na lazima utakuwa miongoni mwa wenye kukhasiri{.(Azzumar 65).Na amesema Mwenyezi Mungu mtukufu:}Na lau wangeli mshirikisha yangeli waharibikia waliyo kuwa wakiyatenda}(An'aam-88).Ibada haiwezi kuitwa ibada ila ikiwa ni kwalengo la kumpwekesha Mwenyezi Mungu (tauhiidi), kama ilivyo swala haiwezi kuitwa swala mpaka uiswali ukiwa msafi (twahara(.Ikichanganywa swala na kinacho tengua udhu basi kinaiharibu swala na kuibatilisha, ndio maana unakuta Mwenyezi Mungu anakusanya katika aya nyingi baina ya kuamrisha watu wafanye ibada na anawakataza shirki.Alisema Mwenyezi Mungu:{Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote.{ (An-Nisaai-36).Alisema Mwenyezi Mungu {Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Sala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti}. (Al-bayyinah 5).Na alisema Mwenyezi Mungu:{Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipo kuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu}. (Anbiyaa 25).Mwenyezi Mungu kusema:{hapana mungu isipo kuwa Mimi}.Kunamambo mawili:1- kukanusha ushirikina.2-kuthibitisha ibada kwa Mwenyezi Mungu mtukufu pekeyake.Na alisema Mwenyezi Mungu mtukufu:{Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu}. (Sura Al Israai23){Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani.} (An Nahl 36). Amekutanisha baina ya kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake na kujiepusha na ibada za matwaghuti (Mashetani).Kwasababu ibada ya Mwenyezi Mungu haiwi ibada ila ikiwa ni pamoja na kujiepusha na matwaghuti, nao ni kufanya ushirikina.Anasema Mwenyezi Mungu mtukufu:{Basi anaye mkataa Shet'ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.} (Al-Baqara256).Kumuamini Mwenyezi Mungu peke yake haitoshi mpaka uyakufuru mashetani, na kama siyo hivyo hakika washirikina wanamuamini Mwenyezi Mungu pamoja na kuwa wanamshirikisha.Anasema Mwenyezi Mungu mtukufu: {Na wengi katika wao hawamuamini Mwenyezi Mungu pasina kuwa ni washirikina}(yusuf 106).Amebainisha Mwenyezi Mungu kwamba washirikina wanamuamini  Mwenyezi Mmungu, lakini imani yao wanaiharibu kwa kumshirikisha Mwenyezi Mmungu katika ibada zao.Hii ndiyo maana ya kusema: yeyote mwenye kumuabudu Mwenyezi Mungu na akamtii Mtume (s.a.w) hakika mtu huyo hawezi kumshirikisha Mwenyezi Mmungu na chochote, kwasababu Mwenyezi Mungu haridhii ashirikishwe na chochote katika viumbe vyake.Kutoka kwa abuu huraira (ﷺ‬.a) alisema: alisema Mtume (s.a.w) katika yale anayo yapokea kutoka kwa Mola wake mshindi mwenye nguvu: (Alisema Mwenyezi Mungu mtukufu: Mimi ndio tajiri wa washirika kwa ushirikina wanao ufanya, mwenye kufanya ibada yoyote akamshirikisha katika ibada hiyo asiyekuwa mimi basi nitamuacha na ushirikina wake). Amepokea hadithi hii imamu Muslim (2985).Kuna watu wanaswali na wanashahidilia kuwa hapana Mola apasae kuabudiwa kwa kahi ila Mwenyezi Mungu, na Muhamad (s.a.w) ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na wanakithirisha kusema hivyo, na wanafunga na wanahiji, lakini wanayaomba makaburi, na wamuabudu Imamu Hassan na Husein, na Albadawiy, na Fulani na Fulani, Na wanaomba nusura kwa watu walio kufa, hao ndio ibada zao nibatili, kwasababu wao wanamshirikisha Mwenyezi Mungu mshindi mwenye nguvu, wanachanganya ibada na ushirikina, basi ibada zao ni batili, na nizenye kuporomoka, mpaka watakapo mpwekesha Mwenyezi Mungu mshindi mwenye nguvu, na wamtakasie utii Mwenyezi Mungu na waache kuabudu kisichokuwa Mwenyezi Mmungu.Na kama siyo hivyo hawatakuwa na chochote, basi ni wajibu kuzinduka kwa hilo, kwasababu Mwenyezi Mungu haridhii kushirikishwa na chochote katika ibada yake kwa vyovyote atakavyo kua. Mwenyezi Mungu haridhii kushirikishwa na yeyote atakavyo kua, ili asiseme yeyote: mimi nachukua kwa watu wema, na watu wazuri uombezi, mimi siabudu masanamu wala mizimu kama ilivyokua enzi za ujinga, mimi nawafanya hawa ni waombezi wangu na siwaabudu.Tunamuambia kuwa: hayo ni maneno ya watu wa zama za ujinga waliwafanya waombezi wao kwa Mwenyezi Mungu kwasababu ni watu wema, na ni mawalii katika mawalii wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu haridhii hayo.Sio kwa malaika alie karibu na Mwenyezi Mungu wala Mtume aliye tumwa na Mwenyezi Mungu.Malaika aliye karibu na Mwenyezi Mungu ni malaika bora, kama jibrilu amani ziwe juu yake, na malaika wanao ibeba arshi ya Mwenyezi Mungu, na malaika walio karibu nao, na malaika walio karibu na Mwenyezi Mungu mtukufu.Pamoja na ukaribu na Mwenyezi Mungu na ukaribu wa waja wa Mwenyezi Mungu, na daraja kwa Mwenyezi Mungu, laiti angemshirikisha pamoja na asiye kuwa Mwenyezi Mungu pamoja na Mwenyezi Mungu katika ibada hakika Mwenyezi Mungu haridhii kushirikishwa pamoja nae malaika alie karibu na Mwenyezi Mungu, wala Nabii aliye tumwa, kama Muhamad (s.a.w).Na Nabii Issa na Nuhu na Ibrahim ambao ni Mitume walio pewa sheria, au walio tumwa kwa watu wote, au walio thibiti katika utume wao.Mwenyezi Mungu haridhii ashirikishwe na yoyote, hata kama atakua ni mbora wa malaika, au ni mbora wa watu.Yeye Mwenyezi Mungu haridhii ashirikishwe na yoyote katika malaika, au katika mitume, itakuaje kwa viumbe wasio kuwa mitume na malaika miongoni mwa watu wema na mawalii walio wema!Basi wasio kuwa malaika na mitume ndio kabisa, hawezi Mwenyezi Mungu kumridhia kwa kumshirikisha pamoja nae kitu kingine, katika ibada.Na haya ni majibu ya wale ambao wanao dai kwamba wao wanawafanya wale wema walio pita na mawalii uombezi kwa Mwenyezi Mungu ili awakurubishe hao kwa Mwenyezi Mungu, kama walivyo sema:{Sisi hatuwaabudu ila wapate kutujongeza tu kumkaribia Mwenyezi Mungu} (Azzumar3).Na kama siyo hivyo hakika wao wanaitakidi kwamba hao hawaumbi wala hawatoi rizki na hawamiliki kifo wala uhai wala kufufuka, bali makusudio yao ni kupata mtu wa katikati ili awaombee kwa Mwenyezi Mungu mshindi mwenye nguvu, kwasababu hiyo waliwafanyia ibada kwa lengo la kujikurubisha kwao, walichinja kwaajili ya makaburi, na wakatoa nadhiri kwa ajili ya ibada, na wakaomba nusra na kuwaita walio kufa. Na ushahidi ni kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu:{Na hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu} (Al-Jinn18(.Mwenyezi Mungu haridhii kushirikiana na yeyote atakavyo kua, na haya yametajwa wazi katika Qur'an, na Sunna za Mtume Muhamad (s.a.w), lakini yeyote ambae hakuwa na akili wala mazingatio, na kuacha kufuaata mtu kipofu, na kuleta sababu ambazo ni batili, na azinduke na nafsi yake.Na ushahidi kua Mwnyezi Mungu haridhii kushirikishwa na yeyote, ni kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu: {Na hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu} (Al-Jinn18(Misikiti ni nyumba za Mwenyezi Mungu, na ni sehemu zilizo andaliwa kwa ajili ya swala, nazo ni sehemu zinazo pendwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu, nazo ni nyumba ameidhinisha Mwenyezi Mungu zinyanyuliwe na litaje jina la Mwenyezi Mungu, na inapaswa iwe misikiti hii ni sehemu ya ibada ya Mwenyezi Mungu pekeyake, na kisitokee chochote katika misikiti ambacho ni cha kumshirikisha Mwenyezi Mungu, yasiwekwe ndani yake makaburi, kwasababu mtume (s.a.w) amemlaani mwenye kufanya kitendo hicho, na akaeleza kuwa kufanya hivyo ni kitendo cha mayahudi, na manaswara, na akatukataza kufanya hivyo mwisho wa uhai wake akiwa katika wakati wa kutolewa roho yake akisema: kutoka kwa Jundabi bin Abdillah albajaliy (ﷺ‬.a) alisema: alisema Mtume (s.a.w): "Fahamuni hakika walio kuwa kabla yenu walikua wakiyafanya makaburi ndio misikiti basi fahamuni msilifanye kaburi langu kua msikiti hakika mimi nawakataza hilo" Imepokelewa na Muslim (532(alikuwa akiyasema haya akiwa katika wakati wa kutolewa roho yake.Na kutoka kwa Aisha (ﷺ‬.a) alisema: alikuwa akisema Mtume (s.a.w) "Laana za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya mayahudi na manaswara waliyafanya makaburi ya mitume wao kuwa ni misikiti" Ameipokea na Bukhari (435,436) na Muslim(531).Misikiti inatakiwa itwaharishwe kutokana na athari za ushirikina na mizimu, na yasisimamiwe makaburi kwa kuyatukuza, au kuyajengea, bali misikiti ifanywe ni sehemu za ibada ya Mwenyezi Mungu peke yake, isimamishwe ndani yake swala, na litajwe jina la Mwenyezi Mungu ndani yake, na kisomwe ndani yake kitabu cha Mwenyezi Mungu, na ziwekwe ndani yake darsa mbalimbali zenye manufaa, na watu wakae itikafu kwaajili ya kufanya ibada, huu ndio wadhfa wa misikiti.Ama kusimamishwa msikitini mizimu inayo abudiwa kinyume cha Mwenyezi Mungu, basi hiyo sio misikiti, na kufanya hivyo ni ushirikina hata kama wenye misikiti hiyo wataiita kua ni misikiti, kwa sababu Mwenyezi Mungu anasema: {Na hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu…{.Yaani misikiti siyo ya kisichokua Mwenyezi Mungu, na kwakuwa misikiti ni sehemu ya mkusanyiko wa watu, basi inatakiwa iwe ni sehemu twahara kutokana na ushirikina, na uzushi, na mambo yasiyo kubalika kisheria, kwasababu watu wanapata elimu na wanafanya ibada katika misikiti, pindi watakapo kuta katika misikiti ushirikina au mambo yasio faa kisheria huenda wakaathirika nayo au wakayachukua na kuyatangaza duniani kote, Kwahiyo ni wajibu iwe misikiti ni yenye kutwaharishwa kutokana na ushirikina.Na miongoni mwa misikiti mitukufu kulio yote ni msikiti mtukufu wa Makkah, kama alivyo amrisha Mwenyezi Mungu alie tukuka alie wa juu utwaharishwe, alisema Mwenyezi Mungu mtukufu:}Na pale tulipo muweka Ibrahim pahala penye ile Nyumba tukamwambia: Usinishirikishe na chochote; na isafishe Nyumba yangu kwa ajili ya wanao izunguka kwa kut'ufu, na wanao kaa hapo kwa ibada, na wanao rukuu, na wanao sujudu} (Hajj 26(.Mwenyezi Mungu aliutwaharisha kutokana na nini? aliutwaharisha kutokana na ushirikina na uzushi na mambo yasiyo kubalika katika dini kama alivyo utwaharisha kutokana na na najsi au uchafu wa takataka.Msiombe enyi watu pamoja na Mwenyezi Mungu yeyote, msiombe nusra kwa yoyote pamoja na Mwenyezi Mungu, kama vile kusema: ewe Mwenyezi Mungu, ewe Muhammad, ewe Mwenyezi Mungu, ewe Abdul Qaadir, au kusema: ewe Abdul Qaadir, ewe Muhamad, au mfano wa hayo, hakika Mwenyezi Mungu haridhii hayo na hayakubali.Hakuna yeyote anae toka katika hukumu hiyo hakuna malaika alie karibu na Mwenyezi Mungu, wala mtume alie tumwa na Mwenyezi Mungu, wala sanamu au mzimu, wala kaburi la shekh, au walii, wala aliye kufa, vyovyote atakavyo kuwa.Qauli ya Mwenyezi Mungu {…basi msimuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu} (Al-Jinn18).Inakusanya wote wenye kuombwa kinyume cha Mwenyezi Mungu, na Aya hii imeonyesha kuwa ibada  haikupi manufaa mpaka uifanye ukiwa na Tauhiidi, na kwa hakika ukiichanganya na ushirikina basi inabatilika, na inakua ni mzigo kwa mfanyaji, kisha akasema Mwenyezi Mungu: {Nahakika misikiti ninyumba za Mwenyezi Mungu...} ni wajibu ijengwe misikiti kwa nia ilio takasika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na siyo kwa ajili ya kujionyesha, au kutaka asikike, au kwasababu ubaki utajo wake baada ya kufa kama wanavyo sema, au uwe msikiti ni athari za kiislam, kujenga msikiti kwa sababu ya mambo hayo haifai.Misikiti inajengwa kwasababu ya kufanya ibada, na kwa nia ya kufanya ibada, na iwe nia imetakasika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mwenye nguvu alie tukuka, na misikiti inajengwa kwa lengo la kuchuma thawabu, na haijengwi kwasababu ya kuchuma haramu, kwasababu misikiti ni ya Mwenyezi Mungu, Kutoka kwa Abii Hurayra (ﷺ‬.a) alisema: alisema Mtume (s.a.w): "Na hakika Mwenyezi Mungu hapokei ila kitu kizuri" Imepokelewa na Muslim (1015).Na misikiti inajengwa kwa pesa ya halali, na iwe niya ya kujenga hiyo misikiti ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mwenye nguvu aliye tukuka, hataki ingwe kwa sifa za watu au kubakia utajo wa mtu, au kujionyesha au kutaka asikike, hakika kujenga msikiti ni ibada na ibada ni wajibu iwe kwaajili ya Mwenyezi Mungu mshindi na mtukufu.  Ndugu katika imani hii nisehemu ya pili katika kitabu hiki cha Masomo katika umuhimu wa Tawhiid .(2) Muhtasari wa kitabu cha Al-Usulu AL-Thalathah cha Imamu Fawzani Allah amuhifadhi tuwe pamoja katika sehemu ya tatu Allah akiipenda . WALAA NA BARAA.3.Mwenye kumtii Mtume (s.a.w) na akampwekesha Mwenyezi Mungu,haifai kwake kuwapenda wale wenye kumfanyia uadui Mwenyezi Mungu na mtume wake hata kama watakuwa niwatu wakaribu zaidi.Haifai kwa mwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu kumpenda mwenye kumfanyia uadui Mwenyezi Mungu na mtume wake hatakama atakuwa nimtu wakaribu zaidi.Haya maswala ya walaa na baraa(kupenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kuchukia kwajili ya Mwenyezi Mungu) Nikatika maswala ya tauhiidi,pia nikatika haki ya tauhidi kuwapenda mawalii wa Mwenyezi Mungu,na kuwachukia maadui wa Mwenyezi Mungu.Muislam anawapenda wapenzi wa Mwenyezi Mungu,yaani hatakiwi kupenda ila vipenzi vya Mwenyezi Mungu,na awanusuru muislam anatakiwa awe karibu na waislam wapendane,kama alivyo sema Mwenyezi Mungu:{….Na jamaa wa nasaba wanastahikiana wenyewe kwa wenyewe zaidi katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu…. }(Al Anfaal 75) hayawi mapenzi baina ya muislam na kafiri,bali yanakuwa baina ya waislam,kama alivyo sema Mwenyezi Mungu:{….wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini }.(An-Nisaa 141).Hivyo ndivyo inavyo paswa kwa waumini watambulike kwa makafiri,haifai kwa yoyote mwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu,na akamtii mtume (s.a.w)kuwapenda wenye kumfanyia uadui Mwenyezi Mungu.Na kufanya uaduia maana yake:nimtu kua katika upande na Mwenyezi Mungu mtukufu na mtume wake kua upande mwingine,(yaani wako tofauti).Maana ya kusema (Hatakama nindugu wakaribu):Yaani katika upande wa nasabu,pindi atakapo kua nindugu yako wakaribu nimwenye kumfanyia uadui Mwenyezi Mungu na mtume wake(s.a.w)niwajibu juu yako kumfanyia uadui na kukata undugu nae.Na yoyote atakae kua kipenzi wa Mwenyezi Mungu na mtume wake (s.a.w) niwajibu juu yako kumpenda na umfanye kuwa rafiki yako hatakama nimtu wako wambali katika nasabu,hatakama atakuwa nimuejemi(Mtu asie kuwa wa rangi yako au lugha yako) au mweusi,au mweupe,au mwekundu, niwajibu kwako kumfanya rafiki na kumpenda, akiwa niwakutoka katika mji wako au niwakutoka mashariki ya mbali,au magharibi yambali,alisema Mwenyezi Mungu mtukufu:{ Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi…}(Tawba71)Yaani baina ya waumini kuna mapenzi na kunusuriana na kusaidiana,na baina yao kuna kuzoweana baina ya waislam.Na ushahidi nikaulia ya Mwenyezi Mungu:{Huwakuti watu wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wanao mpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hata wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao ameandika katika nyoyo zao Imani, na amewapa nguvu kwa Roho itokayo kwake. Na atawaingiza katika Mabustani yapitayo mito kati yake. Humo watakaa daima. Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na wao wawe radhi naye. Hao ndio Hizbullahi, Kundi la Mwenyezi Mungu. Hakika Kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kufanikiwa}.(AlMujaadalah 22)Maneno hayo ameelezwa mtume (s.a.w) kwamba hayatokei hayo wala hayapo kamwe kwamba awe mtu nimwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na mtume wake akawa anawapenda makafiri,ikiwa atawapenda basi huyo hawi nimuumini hatakama anadai kua yeye ni muumini.Alisema ibn Qayyim Allah amrehemu:  Unawapenda maadui wa kipenzi na unadai Kumpenda!Haiwezekani kupatikana mapenzi.Kisha unawafanyia uadui nakuwapiga vita wapenzi wake!Yakowapi mapenzi ewe ndugu wa Shetani!Hilo haliwezekani kamwe kuwapenda makafiri,kasha anasema:mimi nampenda Mwenyezi Mungu na mtume wake (s.a.w) kwakauli yake Mwenyezi Mungu: {Enyi mlio amini! Msiwafanye adui zangu na adui zenu kuwa marafiki mkiwapa mapenzi,…}( Al Mumtah'inah1) mpaka alipo sema Mwenyezi Mungu:{Hakika nyinyi mna mfano mzuri kwenu kwa Ibrahim na wale walio kuwa pamoja naye, walipo waambia watu wao: Hakika sisi tumejitenga nanyi na hayo mnayo yaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Tunakukataeni; na umekwisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapo muamini Mwenyezi Mungu peke yake…}(Al Mumtah'inah 4).Na amesema Mwenyezi Mungu:{Wala haikuwa Ibrahim kumtakia msamaha baba yake ila kwa sababu wa ahadi aliyo fanya naye. Lakini ilipo mbainikia kwamba yeye ni adui ya Mwenyezi Mungu, alijiepusha naye. Hakika Ibrahim alikuwa mwingi wa kuomba, mnyenyekevu, mvumilivu}(Tawba114).Hii ndio dini ya nabii Ibrahim alimkana baba yake na ndie mtu wakaribu wakati alipo baini kua niaduwi wa Mwenyezi Mungu.Na aya zimeonyesha pia kua kuwapenda makafiri kunapingana na imani ya kumuamini Mwenyezi Mungu nasiku ya Qiyama,ima katika asili ya imani au ukamilifu wake,lakini ikiwa kuwapenda kwao nipamoja na kuwaunga mkono katika midhehebu yao au mwenendo wao na ukafiri wao basi huko nikutoka katika uislam.Na ama ikiwa nikuwapenda bila  ya kuwanusuru hii inazingatiwa kua niyenye kupunguza imani,na niuovu ambao una dhofisha imani.Na kauli ya Mwenyezi Mungu :{hao}inakusudia wale ambao wanao wanajitenga mbali na mapenzi ya kuwapenda wale wenye kumfanyia uadui Mwenyezi Mungu na mtume wake.Na maana ya kauli ya Mwenyezi Mungu:{ Hao ameandika katika nyoyo zao Imani }Yaani amethibitisha Mwenyezi Mungu katika nyoyo zao na akazamisha katika nyoyo zao imani.Na ndio Mwenyezi Mungu akasema{na amewapa nguvu kwa Roho itokayo kwake. Na atawaingiza katika Mabustani yapitayo mito kati yake}.Alisema Mwenyezi Mungu mtukufu{Sema: Ameiteremsha hii Roho takatifu kutokana na Mola wako Mlezi kwa haki, ili awathibitishe wale walio amini, na kuwa ni uwongofu, na ni bishara kwa Waislamu}(An Nahl102)Na alisema Mwenyezi Mungu:{Ameuteremsha Roho muaminifu, } (Shu'araa193).Na amewapa nguvu kwa Roho itokayo kwake,yaani aliwapa nguvu kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu,na nguvu ya imani katika dunia,na akhera atawaingiza peponi pepo ambayo ina miti ilio shikana na mito na majumba mazuri.Na amesema Mwenyezi Mungu katika kuisifu pepo:{Na atawaingiza katika Mabustani yapitayo mito kati yake…}na wataishi humo bila kutolewa,alisema Mwenyezi Mungu mtukufu{ Watadumu humo; hawatataka kuondoka}(kahf 108. )Hawata ogopa kifo wala yoyote atakae kuja kuwatowa peponi,au kuwafukuza mfano wa yaliomo duniani,anaweza kua mtu duniani katika majumba mazuri lakini hawezi kusalimika na umauti ukamtowa katika majumba hayo,na pia hasalimiki na maadui kumvamia na kumtoa,mwanadamu daima katika dunia nimwenye kuogopa.Kauli ya Mwenyezi Mungu:{Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na wao wawe radhi naye…}walipo wachukiza ndugu zao makafiri na wakawafanyia uadui aliwapa Mwenyezi Mungu ridhaa kutoka kwake Mwenyezi Mungu mtukufu malipo yao,hakika wao walipewa badala ya ya yale maudhi ya ndugu zao makafiri walipewa ridhaa ya Mwenyezi Mungu mtukufu aliwaridhia Mwenyezi Mungu na wao wakaridhika.Kauli ya Mwenyezi Mungu{hao ndio kundi la Mwenyezi Mungu }yaani ndio jamaa wa Mwenyezi Mungu ama makafiri nikundi la shetani amesema Mwenyezi Mungu {hao ndio kundi la shetani}(almujaadala 19) .yaani ndio jamaa wa shetani na ndio wanao mnusuru shetani,Na ama waumini ndio wanao mnusuru Mwenyezi Mungu mtukufu.Maswala haya yana ambatanana kuwafanyia uadui makafiri na kuto kuwapenda,na haipelekei kwamba tukate uhusiyano na makafiri katika mambo yenye manufaa ya kidunia bali kuna mambo ambayo yanayo toka katika hukumu hii:1.Pamoja na kuwachukia na kuwafanyia uadui niwajibu kwetu kuwalingania wamfuate Mwenyezi Mungu mtukufu,niwajibu tuwalinganie waingie ndani ya uislam na tusiwaache tukasema:Hao nimaaduwi wa Mwenyezi Mungu na nimaadui zetu na inapaswa kwetu tuwalinganie wamfuate Mwenyezi Mungu huwenda Mwenyezi Mungu akawaongoza.2.Hakuna pingamizi kufanya mkataba na makafiri ikiwa waislam watahitaji hilo,kwakuwa waislam hawawezi kuwapiga vita,na inahofiwa kwa waislam shari zao.3.Hakuna pingamizi kuwalipa kwa wema wao kwa waislam,hakuma kiziwizi kuwalipa kwa wema walio ufanya,amesema Mwenyezi Mungu mtukufu:{Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu}.(Al Mumtah'inah 8).4.Mzazi akiwa nikafiri inapasa kwa mtoto wake muislam amfanyie wema,lakini asimtii katika ukafiri kwa kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu:{Na tumemuusia mtu kwa wazazi wake wawili. Mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumwachisha ziwa baada ya miaka miwili. (Tumemuusia): Nishukuru Mimi na wazazi wako. Ni kwangu Mimi ndiyo marudio(14).Na pindi wakikushikilia kunishirikisha na ambayo huna ilimu nayo, basi usiwat'ii. Lakini kaa nao kwa wema duniani, nawe ishike njia ya anaye elekea kwangu. Kisha marejeo yenu ni kwangu Mimi, na Mimi nitakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda}( Luqman14-15)Mzazi ana haki akiwa kafiri, lakini usimpende mapenzi ya moyoni, bali unamfanyia wema kama ujira wa kukulea nakwasababu yeye nimzazi,na ana haki kwako umfanyie wema.5.Kubadilishana biashara pamoja na makafiri na kununua kwao, na kununua mahitaji kwao na kuchukua bidhaa na silaha utoka kwa makafiri kwa kulipia pesa hilo halina tatizo,na alikuwa Mtume (s.a.w) ana alifanya kazi na makafiri,na alifanya kazi mtume (s.a.w)na watu wa khaybar nao ni Mayahudi alifanya nao kazi ya walime shamba kwa makubaliyano ya kile kitakacho vunwa kutoka shambani,kufanya hivyo sio kuwapenda makafiri,bali nikubadilishana masilahi.Niwajibu tufahamu mambo haya,na hayaingii katika kuwapenda makafiri na hayakukatazwa.Hakuna makatazo ya haya kwasababu mambo hayo niyakidunia na maslahi hayana maana ya mapenzi moyoni,lazima tutofautishe baina ya maslahi na kupenda,kwasababu kuna baadhi ya watu wakisikia dalili za kuwafanyia uaduwi makafiri na kuto kuwapenda huwenda wakafahamu kua hawafanyi nao kazi za kidunia,na hawafanyi mawasiliano na makafiri,na wanaelewa kua nikukata mafungamano nao moja kwa moja,Hapana!kuwapenda makafiri na kuwafanyia uadui kumewekewa mipaka kwa hukumu na mipaka na masharti zinazo julikana kwa wana wachuoni ilio chukuliwa kutoka katika Quraan na sunna za mtume (s.a.w).6.Mwenyezi Mungu Alihalalisha kuoa wanawake wa kiyahudi na kinaswara kwa sharti wawe niwenye kujihifadhi na kujiweka mbali na zinaa katika heshima zao,na akahalalisha Mwenyezi Mungu kula wanyama walio chinjwa na mayahudi na manaswara.7.Hakuna ubaya kuitikia wito wao na kula chakula cha halali kama alivyo fanya mtume (s.a.w).8.Kuwafanyia wema majirani ambao nimakafiri kwasababu wana haki ya ujirani.9.Haifai kuwadhulumu makafiri alisema Mwenyezi Mungu mtukufu:{…Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu…}(Al-Maida8).Fahamu Mwenyezi Mungu akuongoze kwa kumtiiManeno haya nikama mwanzo wa ujumbe watatu kwasababu zimepita jumbe mbili:-Ujumbe wakwanza: Nimaswala manne ambayo yalikusanya suratu Al Asri,-Ujumbe wapili: Nimaswala ya matatu ambayo yamepita.-Ujumbe watatu: Ndio hii,na utakuja ujumbe wa Nne nao una maswala ma Nne.Kaanza mtunzi wa kitabu kwa kusema :(Mwenyezi Mungu akuongoze) hii ni dua ya shekh Allah amrehemu kwa kila atakae soma ujumbe huu kwa lengo la kuufahamu na kutafuta elimu kwa kusoma ujumbe huu,kwamba Mwenyezi Mungu amuongoze,Na muongozo ni Mwenyezi Mungu kukuongoza kupita njia ya sawa na kukupa taufiiqi ya kupata elimu yenye manfaa,na kufanya matendo mema,na uongofu nikinyume cha upotovu,Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu:{Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu}( Al-Baqara 256)Na amesema Mwenyezi Mungu mtukufu:{Na wao wakiona kila Ishara hawaiamini. Wakiiona njia ya uwongofu hawaishiki kuwa ndiyo njia; lakini wakiiona njia ya upotofu wanaishika kuwa ndiyo njia}.( Al-A'raaf)Na uongofu katika aya makusudio yake nidini ya uislam,na upotovu unakusudiwa dini ya Abuu Jahli,(Allah amlani).Hakika muislam pindi anapo ongozwa na Mwenyezi Mungu akawa nimenye kumtii basi atakuwa nimwenye kufanikiwa katika duniani na akhera,na kutii nikutekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu nakujiepusha makatazo yake,huko ndio kumtii Mwenyezi Mungu,Mwanadamu anatakiwa umtii Mwenyezi Mungu katika maamrsho yake uyafanye,na katika makatazo yake ujiepushe kuyafanya kwakutekeleza amri za Mwenyezi Mungu,na kutarajia malipo yake Mwenyezi Mungu mshindi mtukufu na utarajie thawabu zake,na uogope adhabu zake,yoyote atakae pewa taufiiqi ya kumtii Mwenyezi Munguna akaongozwa kuwa nimwenye umtii Mwenyezi Mungu hakika atakuwa nimwenye mafanikio duniani na akhera. UJUMBE WA TATU UISLAM NDIO DINI YA NABII IBRAHIM.Nini maana ya Uhanafiyyah:Uhanafiya ambao muislam anatakiwa ajifundishe na aujue nikwamab uhanafiyyah:Nidini ambayo alikuwa nayo Nabii Ibrahim (s.a.w).Nayo nidini ambayo inapingana na ushirikina na inaamrisha wanadamu woote washikamane na Tauhiid(kumpwekesha Mwenyezi Mungu mmoja bila kumshirikisha na chochote).Na nabii Ibrahim (s.a.w) alikuwa mwenye Uhanafiyyah na ni Muislam, Uhanafiya wa nabii Ibrahimu maana yake alikuwa nimwenye kupinga ushirikina, na nimwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu(Tauhidi),na nimwenye kufanya ibada zake zoote kwajili ya Mwenyezi Mungu,alisema Mwenyezi Mungu mtukufu:{. Hakika Ibrahim alikuwa mfano mwema, mnyenyekevu kwa MwenyeziMungu, mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina}( An Nahl 120).Uhanafiyyah nikatika sifa za nabii Ibrahim (s.a.w) ambayo maana yake nikupuuziya na kupiga vita ushirikina na nimwenye kuelekea moja kwamoja kwenye Tauhidi.Alielekea kwenye Tauhidi katika mambo yake yote nakuwa na ikhlasi katika mambo yake yote,amesema MwenyeziMungu mtukufu:{ Kisha tukakufunulia ya kwamba ufuate mila ya Ibrahim, mwongofu,wala hakuwa miongoni mwa washirikina}(An Nahl 123).Na amesema Mwenyezi Mungu mrukufu:{ Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu Muislamu, wala hakuwa katika washirikina}(Al 'Imran67)Hizi nisifa kubwa za nabii Ibrahim(s.a.w) ambazo miongoni mwazo ni Alhanafiyyah nakwamba dini yake ni Alhanafiya nayo nidini ilio takasika kwaajili ya Mwenyezi Mungu mshindi mwenye nguvu,dini ambayo haina ushirikina ndani yake,na ameamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu mtume wake Muhammad (s.a.w)aifate dini ya nabii Ibrahim kwa kusema:{Kisha tukakufunulia ya kwamba ufuate mila ya Ibrahim, mwongofu,wala hakuwa miongoni mwa washirikina}.(An Nahl 123.)Na tukaamrishwa pia tufuate dini ya nabii Ibrahim (s.a.w) kwakusema:{Yeye amekuteueni. Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim. Yeye (Mwenyezi Mungu) alikuiteni Waislamu }(Hajj78). Nayo ndio dini ya mitume wote.Lakini kwakuwa nabii Ibrahim (s.a.w) nimbora wa mitume baada ya Muhammad(s.a.w)alikutana katika njia ya kulingania kwenye Tauhiidi(kumpwekesha Mwenyezi Mungu peke yake bila kumshirikisha na chochote) na adhabu na mitihani ambayo hakuna mtume alie kutana nayo akasubiri,Nakwakua nabii Ibrahim(s.a.w) ndio baba wa mitume,hakika mitume walio kuja baada yake woote nikatika kizazi chake(s.a.w) basi uislam ndio dini ya mitume wote,na uislam(Alhanafiyyah) nikulingania watu wampwekeshe Mwenyezi Mungu mmoja na wasimshirikishe na chochote,hii ndio dini ya manabii wote,lakini zama ilipo kua kwa nabii Ibrahim msimamo kwa dini hii basi alinasibishwa kwake na mitume walio kuja baada yake,na mitume wote baada yakeWalikuwa kwenye dini ya nabii Ibrahim,nayo nidini ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu mmoja bila kumshirikisha na chochote na kumtakasia utii Mwenyezi Mungu mtukufu(yaani ibada zako zote ziwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu).Niipi dini hii ambayo ameamrishwa mtume Muhamad (s.a.w)kuifuata na tume amrishwa na sisi uifuata?Niwajibu juu yetu kuijiwa,kwasababu muislam niwajibu kwake kuyajuwa yale aliyo muamrisha Mwenyezi Mungu ili kuyatekeleza,na haitoshi kujinasibisha na uislam bila kuufahamu uislam wake,na hajuwi mambo ambayo yanatengua uislam,na nizipi sheria za uislam, na hukumu za uislam, na haitoshi kujinasibisha na dini ya nabii Ibrahim(s.a.w) ilihali hauijuwi,na utakapo ulizwa kuhusu dini ya nabii Ibrahim(s.a.w) unasema: sijuwi, kuwa hivyo kwa muislam haifai, niwajibu uijuwe dini yako vizuri ili uifuate ukiwa unaijuwa na ili usiache chochote ila umekitekeleza.NIWAJIBU KWA MWANADAMU AMUABUDU MWENYEZI MUNGU PEKE YAKE NA AFANYE IBADA ZOTE KWAAJILI YA MWENYEZI MUNGU.Dini ya nabii Ibrahim(s.a.w),inafundisha kumuabudu Mwenyezi Mungu mmoja na kufanya ibada zote kwa ajili ya Mwenyezi Mungu,nakumtakasia dini.Kufanya hivyo kunatakiwa mambo mawili:1.Kufanya Ibada.2.Kuwa na Ikhlasi (kufanya ibada zote kwa ajili ya Mwenyezi Mungu).Atakae muabudu Mwenyezi Mungu na hakuwa na ikhlasi haitakuwa amefanya ibada yoyote, mwenye kumuabudu Mwenyezi Mungu ,akafunga na akahiji,na akaswali au kufanya umra,na akatoa sadaka,na akatoa zaka,na akafanya ibada nyingi lakini hakuzifanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mtukufu katika ibada zake,ima kwasababu ya kujionyesha(Riyaa) au kwa kutaka sifa,au amechanganya ibada yake na chochote katika mambo ya ushirikina,kama kuomba kisichokua Mwenyezi Mungu,au kuomba nusra kwa asie kua Mwenyezi Mungu,au kuchinja kwa asie kua Mwenyezi Mungu,hakika mtu wa namna hiyo hatakuwa amefanya ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu,bali atakuwa ni Mshirikina,na hatakuwa katika dini ya nabii Ibrahim(s.a.w).Wengi miongoni mwa wanao jinasibisha kwenye uislam katika zama zetu wana angukia katika shirki kubwa kwa sababu ya kuomba asie kuwa Mwenyezi Mungu,nakuabudu makaburi nakuchinja kwenye makaburi,na kuyatolea nadhiri makaburi,na kutufu kwenye makaburi na kutabaruku (kutaka baraka) kwenye makaburi,nakuomba nusra kwa watu waio kufa namengineyo,nawao wanasema niwaislam.Hao hawakujuwa dini yao au waliijuwa wakapinga wakiwa wanajuwa na hali hii ndio mbaya zaidi Mwenyezi Mungu atukinge.Dini ya nabii Ibrahim (s.a.w) haikubali ushirikina kwa namna yoyote itakavyo kuwa na atakae changanya ibada yake na ushirikina basi hatakuwa katika dini ya nabii Ibrahim (s.a.w),hatakama atajinasibisha na dini hiyo,na akadai kuwa ni muislam,jambo la wajibu nikuijua dini ya nabii Ibrahim (s.a.w) na kuifanyia kazi na ujilazimishe nayo kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake na kumtakasia ibada bila ya kumshirikisha.Isiwe katika ibada zako chochote katika ushirikina sawa ikiwa nishirki ndogo au shirki kubwa.Hii ndio dini ya nabii I brahim (s.a.w) ilio takasika na shirki na kuupiga vita ushirikina kwa aina zake zote na ikahimiza watu washikamane na Tauhiidi kwa ujumla wake nakuwataka watu wote wamuabudu Mwenyezi Mungu mmoja na kumtakasia ibada.Na kwasababu hiyo ameamrisha Mwenyezi Mungu watu wote  na aliwaumba kwasababu ya ibada.Katia maneno kuna ishara ya kua mwanadamu anatakiwa amuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia dini,yani afanye ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu,ameamrisha Mwenyezi Mungu watu wote,kawaamrisha watu wajinsia zote ,watu wote tangu kwa Adamu mpaka kwa binadamu wamwisho katika dunia hii,wote Mwenyezi Mungu kawa amrisha Mwenyezi Mungu wamuabudu yeye na wamtakasie ibada, anasema Mwenyezi Mungu mtukufu:{ Enyi watu! muabuduni Mola wenu mlezi aliye kuumbeni nyinyi na wale wa kabla yenu, ili mpate kuokoka{.Mwenyezi Mungu) ambaye amekufanyieni hii ardhi kuwa kama tandiko, na mbingu kama paa, na akateremsha maji kutoka mbinguni, na kwayo akatoa matunda yawe riziki zenu. Basi msimfanyizie Mwenyezi Mungu washirika, na hali nyinyi mnajua}.(Al Baqaraa21-22) Hakika Mwenyezi Mungu hana mfano,na hana anae fanana nae, wala wala anae lingana nae, nahaya nimakatazo ya shirki kubwa na shirki ndogo.Ameamrisha Mwenyezi Mungu watu wote wakwanza wao na wamwisho wao.Na Mwenyezi Mungu kawaumba kwasababu ya ibada wamuabudu yeye peke yake bila kumshirikisha, na wanadamu wameumbwa kwasababu ya ibada,kama alivyo sema Mwenyezi Mungu :{Nasikuumba majini wala watu ila kwasababu waniabudu}(Al dhariyati 56). na wameamrishwa hivyo katika k kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu:{Enyi watu mlio amini muabuduni mola wenu ambae ale kuumbeni}(Al Baqara 21).Hii ndio maana ya kusema (Kakuumbeni Mwenyezi Mungu kwasababu ya ibada na akawaamrisha waitekeleze ibada),Imekusanya kauli hii mambo mawili:1.Mwenyezi Mungu amewamrisha waja wake wafanye ibada.2. Mwenyezi Mungu amewaumba waja wake kwasababu ya ibada,Kama alivyo sema Mwenyezi mungu:{Sikuwaumba majini na wanadamu ila waniabudu}kauli ya Mwenyezi mungu{sikuwaumba majini na watu} Mwenyezi mungu ndie muumbaji yeye ndie alie umba vitu vyote na kayika hivyo aliumba majini na watu na akawapa akili na akawalazimisha wamuabudu yeye peke yake wasimshirikishe na lolote na akatowa amri maalumu kwa majini na watu wamuabudu yeye Mwenyezi mungu peke yake,kwasababu Mwenyezi mungu amewapa akili na akawapa maarifa yakupambanua kitu chenya madhara na chenye manufaa,na ja jambo lahaki na labatili,na akaumba mambo mengi kwa maslahi ya majini na watu na manufaa yao.anasema Mwenyezi mungu:{ Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, vyote vimetoka kwake. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanao fikiri }(Al jathiya13)Vyote vimewekwa kwa ajili ya mwanadamu ili avitumie kuweza kufikia lengo la kuletwa hapa duniani ambalo ni Ibada.Anasema Mwenyezi mungu {Sikuwaumba majini wala watu ila waniabudu}.Majini niulimwengu usio onekana hatuwaoni majini,na majini wamelazimishwa kufanya ibada,na wamekatazwa kufanya shirki na maasi kama mwanadamu,ispokua majini wametofautiyana na wanadamu katika maumbile.Ama upande wa maamrisho na makatazo majini nikama bianadamu hakuna tofauti wao wameamrishwa na wamekatazwa,majini hawaonekani na hatuwezi kuwaona ila wapo na watu ndio watoto wa Adamu(s.a.w)wanadamu wanasifa ya kufurahishana na wanaishi pamoja hii ndio sababu ya kuitwa binadamu kua (Watu).Ama majini wameitwa majini kwasababu wamejificha na hatuwezi kuwaona,Majini wamefichwa kwa wanadamu na hatuwezi kuwaona.Ulimwengu wa majini upon a mwenye kukanusha kuto kuwepo majini basi atakuwa amekufuru,kwasababu atakuwa amemkadhibisha Mwenyezi mungu na mtume wake (s.a.w) na makubaliano ya wanachuoni,hakika amebainisha Mwenyezi mungu mwenye nguvu kwamba yeye hakuumba majini na watu ispokuwa kawaumba kwa ajili ya Ibada na sio kwasababu nyingine.Mwenyezi mungu hakuwaumba majini na watu ili wamnufaishe au wamdhuru,au ajitukuze kwasababu ya kuwaumba kutokana na udhaifu,au ajione yuko na watu au majini wengi hayko mpweke,kwasababu Mwenyezi anajitoshelezea na walimwengu,na hakuwaumba kwasababu anawahitajia,hakuwaumba ili wamruzuku au wamtafutie mali,bali Mwenyezi mungu anasema kuyakanusha yote hayo :{Na sitaki kwao riziki, wala sitaki wanilishe (57) Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti }(Dhaariyaat 57-58).Mwenyezi mungu hana haja na viumbe,ispokuwa aliwaumba majini na wanadaamu kwa kitu kimoja nacho ni ibada, Mwenyezi mungu hana haja ya ibada zao bali wao ndio wanao hzihitajia ibada zao,kwasababu watakapo muabudu Mwenyezi munguAtawakirimu na atawaingiza peponi,basi maslahi ya Ibada yanawarudia wanadamu wenyewe,na madhara ya maasi yanawarudia wenyewe,ama Mwenyezi mungu alie tukuka na wajuu hakumdhuru kutii kwa mwenye kumtii wala maasi ya mwenye kumuasi,alisema Mwenyezi mungu :{Na Musa alisema: Mkikufuru nyinyi na wote waliomo duniani, hakika Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Anajitosha, Msifiwa}(Ibrahim 8)Mwenyezi mungu hayamdhuru maasi ya mwenye kumuasi wala hakumnufaishi kutii kwa mwenye kumtii ispokua ibada na maasi yanarudi kwa nafsi zao wenyewe,pindi watakapo mtii Mwenyezi mungu watanufaika na wakimuasi Mwenyezi Mungu watadhurika kwa kumuasi Mwenyezi Mungu. NA MAANA YA QAULI YA MWENYEZIMUNGU {ILI WANIABUDU}.Maana yake ili wampwekeshe Mwenyezi mungu na wamfanye Mwenyezi mungu kuwa nimmoja pekeyake katika ibada,Na katika maneno hayo kuna majibu kwawale wanao sema kua Tuhiidi: Nikukiri kuwa Mwenyezi mungu nindie muumbaji na nimwenye kutowa rizki na ndie mwenye kuhuyisha na nimwenye kufisha,na ndie mwenye kupangilia mipango yote ya duniani,hii nitauhidi lakini sio tauhidi ambayo kwasababu yake aliumba Mwenyezi mungu viumbe ,ispokua aliumbwa viumbe kwasababu ya kumpwekesha Mwenyezi mungu katika kumfanyia ibada.Ama mwenye kukiri kuwa Mwenyezi mungu ndio mwenye kuumba na kutoa rizki imani hiyo haitoshi kua nimwenye tauhidi na hawezi kuingia peponi kwa imani hiyo,bali atakuwa katika watu wa motoni kwasababu hakuleta tauhidi ambayo ndio sababu ya kuumbwa kwake ambayo ni Kumpwekesha Mwenyezi mungu katika utekelezaji wa ibada nakuzifanya ibada zote ziwe kwa ajili ya Mwenyezi mungu. JAMBO KUBWA ALILO AMRISHA MWENYEZI MUNGU WAJA WAKE NI TAUHIIDI.Hakika tauhiid ndio jambo kubwa alilo amrisha Mwenyezi mungu sheria zote za Mwenyezi mungu zilikuja baada ya tauhiid.Na ushahidi wa hilo nikauli ya Mwenyezi mungu mtukufu idemayo:{Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita njia, na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wanao jifakhiri, }(Al-Nnisaa 36)Aya hii ndani yake kuna haki kumi(10),kwasababu hiyo inaitwa aya hiyo : (Ayya yenye haki kumi).Haki hizo kumi yakwanza nihaki ya Mwenyezi mungu mtukufu ambayo nikumuabudu Mwenyezi mungu pekeyake bila kumshirikisha na chochote, nakuwafanyia wema wazazi wawili, nakuwafanyia wema jamaa wakaribu,na mayatima nk.Jambo lamuhimu nikwamba Mwenyezi mungu katika hizo haki kaanza kwakutaja haki yake pale alipo sema : {na msimshirikishe na lolote} hakutosheka nakusema :{Muabuduni Mwenyezi mungu},kwasababu ibada haiswihi ikiwa na shirki ndani yake na haina manufaa yoyote,na haiitwi ibada mpaka itakapo kuwa nikwaajili ya Mwenyezi mungu peke yake na ikiwa pamoja na shirki basi haiwi ni ibada kwavyovyote atakavyo pata shida na taabu katika kuifanya hiyo ibada, amekutanisha amrri ya kumuabudu Mwenyezi mungu pamoja na amri ya kujiepusha na shirki kuonyesha kuwa haiswihi ibada yoyote ikiwa na shirki ndani yake.Hii nidalili kuwa jambo kubwa alilo amrisha Mwenyezi mungu ni tauhiid(Kumpwekesha Mwenyezi mungu katika ibada) kwasababu Mwenyezi mungu kaanza kuizungumzia katika aya nyingi ikiwemo ayay ilio pita,na katika ayah ii :{Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu} (Israa23).Akaanza Mwenyezi mungu kuizungumzia tauhiid,nah ii inaonyesha kuwa tauhiid ndio jambo kubwa alilo amrisha Mwenyezi mungu.Amesema Mwenyezi mungu mtukufu:{ Sema: Njooni nikusomeeni aliyo kuharimishieni Mola wenu Mlezi. Nayo ni kuwa, msimshirikishe Yeye na chochote. Na wazazi wenu wafanyieni wema. Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunakuruzukuni nyinyi na wao. Wala msikaribie mambo machafu, yanayo onekana, na yanayo fichikana. Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharimisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki. Hayo amekuusieni ili myatie akilini }(Al Anaam  151).Hii ni dalili ya mambo yanayokuja ya kwamba jambo kubwa aliloliikataza Allah ni shirki, basi itakapokua jambo kubwa aliloliamrisha ni tauheed, niwajibu kwa mwanadam aanze kuisoma aqidah kabla ya kitu chochote, aqidah ndio msingi,  basi ni wajibu kwa mwanadam aanze kuisoma na kuifundisha, na adum katika kuifundisha na kuibainisha kwa watu, kwa sababu ndio jambo kubwa aliloliamrisha Allah, siyo munasaba kulifanya liwe jambo la mwisho au lipewe umuhimu, kwasababu kuna walinganiaji wanaacha kuifundisha tauheed na aqidah, watu wamepewa mtihani katika jambo hili.Na kwasababu kulipuuzia jambo hili nikuipuuzia dini basi niwajibu kulipa kipao mbele. NINI MAANA YA TAUHIDI?Je Tauhiid nikukiri kuwa Mwenyezi mungu nimuumba na nimtoa rizki na ndie anaefisha na kuhuyisha?La , Tauhiid nikumpwekesha Mwenyezi mungu kwakufanya ibada,kwasababu Mwenyezi mungu alisema:{Sikuumba majini wala watu ila waniabudu}(Dhariyat 56).Walisema wanawachuoni wa tafsiri : maana ya neon (Ili waniabudu):maana yake wanipwekeshe,walitafsiri neno Tauhiid kwamaana ya Ibada.Ikiwa nihivyo Maana ya Tauhiid ;Nikumpwekesha Mwenyezi mungu kwakufanya ibada,na sio kukiri kuwa  Mwenyezi mungu ndie muumbaji na mtowa rizki na mwenye kuhuyisha na kufisha na kupangilia mipango yoote ya ulimwengu,kwasababu hayo yanajulikana kimaumbile,na yapo akilini ,hakuna yoyote mwenye akili asie juwa kuwa Mwenyezi mungu alie umba mbingu na ardhi kuwa ni Mwenyezi mungu, nahakuna yoyote duniani akiwemo kafiri na mwenye kupinga kuwepo kwa Mwenyezi mungu anae amini kuwa kuna binaadamu alie umba mwanadamu mwanadamu mwenzake, alisema Mwenyezi mungu mtukufu:{Na pindi utakapo wauliza nani alie waumba wanasema ni Mwenyezi mungu}(Al Zukhruf 87) hakuna yoyote mwenye akili  duniani anae amini kuwa mwanadamu anaweza kumuumba mwanadamu mwenzake kasha akatembea na akala chakula  na kuzuzungumza je yupo yoyote ambae anae weza kufanya hivyo?Mwenyezi mungu  mtukufu anasema :{Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji? ( 36). Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana na yakini.}(Al Tuur 35-36).Tauhiid ya kumpwekesha  Mwenyezi mungu  kwa matendo ya Mwenyezi mungu  kama kuumba nk ipo katika maumbile ya mwanadamu na katika akili za wanadamu, lakini haitoshi bila mwanadamu kumpwekesha Mwenyezi mungu katika kufanya ibada nako nikufanya ibada kwa ajili ya Mwenyezi mungu.Tauhiid  nikumpwekesha Mwenyezi Mungu ,na sio kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa kuumba kwake na kutowa rizki na kuhuyisha  na kufisha ,kwasababu mambo hayo yanajulikana ,na haitoshi tauhiid ya vitendo vya Mwenyezi Mungu katika kuitambulisha tauhidi.TNB: Ndugu katika imani hii nisehemu ya tatu katika kitabu hiki cha Masomo katika umuhimu wa Tawhiid . Muhtasari wa kitabu cha Al-Usulu AL-Thalathah cha Imamu Fawzani Allah amuhifadhi tuwe pamoja katika sehemu ya nne ijayo Allah akiipenda . Utangulizi:Kaanza kwa kusema Bismi llahi Rrahmani Rrahim; Kwajina la Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehma mwenye kurehemu.Ameanza Mwenyezi Mungu Amrehemu risala hii kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma mwenye kurehemu, kwa kufuata kitabu cha Mwenyezi Mungu mshindi na mtukufu, kwa sababu macho yako yakiangalia ndani ya msahafu na kabla ya kila sura kuna (Bismi llahi Rrahmani Rrahim).Kuanzia neno hili katika risala na katika vitabu nikufuata kitabu cha Mwenyezi Mungu mshindi na mtukufu, vilevile nabii Muhammad (s.a.w) Alikua -ana mwambia muandishi- a'ndike mwanzo wa kila barua wakati anapo watumia viongozi na maraisi na waliyoko mbali ana walingania katika Uislamu, anaanza kuandika:  Kwajina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma mwenye kurehemu.Na alikua Mtume (s.a.w) anaanza mazungumzo yake na maneno yake kwa: Bismi llahi Rrahmani Rrahim, yaonyesha kuanza kwa Bismi llahi Rrahmani Rrahim ni sunna ya Mtume (s.a.w), vilevile Nabii Sulaiman (s.a.w) alipo muandikia Malkia -Mfalme wa saba' Yemen- ameanza kuandika kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma mwenye kuruhemu: (Malkia akasema: Enyi wahishimiwa! Hakika nimeletewa barua tukufu* Imetoka kwa Sulaiman nayo ni:Kwajina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu* Msinifanyie jeuri, na fikeni kwangu nanyi mmekwisha kuwa wenye kusalimu amri). (An-Naml: 29-31). Inatakiwa kuanza na jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu, katika kila jambo lenye umuhimu, na katika kila kitabu chenye umuhimu na thamani, na katika kila risala.Kwa sababu hii wale ambao hawaanzi kwenye vitabu vyao na risala zao kwa jina la MwenyeziMungu Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu, hao wameacha sunna ya Mtume na kuto kufuata kitabu cha Mwenyezi Mungu Mshindi na mtukufu, huenda kwa sababu hiyo vitabu vyao na risala zao hazina baraka na ndani yake hakuna faida; kwa sababu ikiwa hakuna jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu huondolewa faida.Risala ya kwanza    Maswala manne ambayo yameambatana na Surati Al-Asr. Jambo kubwa alilo liataza Mwenyezi Mungu ni Shirki.na nijambo kubwa alilokataza Mwenyezi Mungu, anasema: Ni Riba, ndio jambo kubwa alilokataza Mwenyezi Mungu, Uzinifu ndio jambo kubwa alilo kataza Mwenyezi Mungu,kwasababu hiyo wanatilia mkazo kukataza Riba na Uzinifu na tabia mbovu, lakini hawatilii umuhimu  jambo la ushirikina na hawatahadharishi watu na ushirikina,haliyakuwa wanaona watu wameangukia katika ushirikina,huu niujinga mkubwa wakuto kujua sheria ya Mwenyezi Mungu mtukufu.Jambo kubwa alilo kataza Mwenyezi Mungu niushirikina,nijambo kubwa kuliko ribaa  na kunywa pombe, kuibana kula mali zawatu kwa batili,na nikubwa kuliko kamari, shirki nidhambi kubwa kuliko dhambi yeyote, anasema Mwenyezi Mungu mtukufu:{Sema: Njooni nikusomeeni aliyo kuharimishieni Mola wenu Mlezi, Nayo ni kuwa, msimshirikishe Yeye na chochote. Na wazazi wenu wafanyieni wema. Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunakuruzukuni ninyi na wao, Wala msikaribie mambo machafu, yanayo onekana, na yanayo fichikana. Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharamisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki. Hayo amekuusieni ili muyatie akilini (151) Wala msiyakaribie mali ya yatima ila kwa njia ya wema kabisa, mpaka afikie utu uzima. Na timizeni vipimo na mizani kwa uadilifu. Sisi hatumkalifishi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake. Na msemapo semeni kwa uadilifu ingawa ni jamaa. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu itekelezeni. Hayo amekuusieni ili mpate kukumbuka}(Anaam 151-152) .Na Aya hizi zinaitwa: (Nasaha kumi).Haya mambo yaharamu kaanza kuyazungumzia kwa kuanza na Shirki ikaonyesha kua ushirikina nidhambi kubwa aliyo ikataza Mwenyezi Mungu.Na amesema Mwenyezi Mungu katika Aya nyingine:{Usimfanye mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, usije ukawa wa kulaumiwa uliye tupika} (Al Israa 22). Ameanza kukataza ushirikina na akamalizia kwa kukataza ushirikina kwa kusema :{Haya ni katika hikima alizo kufunulia Mola wako Mlezi. Wala usimweke pamoja na Mwenyezi Mungu mungu mwengine, usije ukatupwa katika Jahannamu ukilaumiwa na kufurushwa}( Al Israa 39), ikaonyesha kua jambo kubwa alilo likataza Mwenyezi Mungu ni ushirikina.Na katika hadithi sahihi  kutoka kwa Abdillah Bin Masuudi (ﷺ‬.a) hakika Mtume (s.a.w) aliulizwa: nidhambi gani kubwa? Akasema Mtume (s.a.w): ((Nikumfanya Mwenyezi Mungu kuwa na msaidizi nayeye ndiye aliye kuumba)) kisha akaulizwa: kisha nini ?: akasema Mtume (s.a.w): ((Ni kumuua mtoto wako kwakuogopa asile na wewe)) kisha akaulizwa: kisha nini?: akasema Mtume (s.a.w) :((Nikuzini na binti wa jirani yako)) Imepokelewa na Bukhari (6861) na Muslim (86).Akateremsha Mwenyezi Mungu kusadikisha hayo katika Kauli yake:{Na wale wasio mwomba mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi aliyo iharamisha Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwa haki, wala hawazini - na atakaye fanya hayo atapata madhara} (Al furuqan-68) akaanza Mwenyezi Mungu kukataza Shirki.Katika kauli ya Mtume (s.a.w): "Nikumfanya Mwenyezi Mungu kuwa na msaidizi ilihali amekuumba" hii  ni ishara ya kua Shirki nidhambi kubwa, kwasababu aliulizwa Mtume (s.a.w): Ni ipi dhambi kubwa? Akajibu kwa kuanza na shirki.Kutoka kwa Abuu Hurayra (ﷺ‬.a) hakika Mtume (s.a.w) Alisema: ((Jiepusheni na Madhambi saba yenye kuangamiza)) Akaulizwa: Niyapi hayo madhambi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?! Akasema:((Nikumshirikisha Mwenyezi Mungu, na uchawi,na kuuwa nafsi ambayo aliyo iharamisha Mwenyezi Mungu isiuliwe ila kwa haki)) Imetolewa na Bukhary (2766) na Muslim)89) .Alianza Mmtume (s.a.w) kuelezea hayo madhambi yenye kuangamiza kwa kuitaja shirki ikiwa ni dalili tosha kua shirki nidhambi kubwa,kwasababu hiyo hakika mwenye kufanya shirki haingii peponi milele,Alisema Mwenyezi Mungu mtukufu:{Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharamishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru}(Al Maida 72) Mwenye kufanya Shirki hatosamehewa na Mwenyezi Mungu, alisema Mwenyezi Mungu mtukufu:{Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika amezua dhambi kubwa.}(Al Nnisaai 48).Aya hizi zimeonyesha uharamu wa kuingia peponi kwa Mwenye kufanya shirki, na hakika Mwenyezi Mungu hatomsamehe mwenye kufanya Ushirikina, na ikaonyesha kuwa ushirikina nidhambi kubwa,kwasababu madhambi yasio kuwa Shiriki yanasameheka.Anasema Mwenyezi Mungu mtukufu:{Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye}, hakika zinaa na wizi na kunywa pombe na kula ribaa, atakaekufa bila kutubia atakuwa chini ya utashi wa Mwenyezi Mungu,akipenda atamsamehe na akipenda atamuadhibu.Ama ushirikina hakika hausameheki, alihukumu Mwenyezi Mungu kwamba yeye hamsamehemshirikina akifa kabla hajatubia, vile vile mwenye kufanya maasi hatakama anamadhambi makubwa yaliyo duni na shirki hakika madhambi hayo hayamfanyi pepo iwe haramu kwake,ima Mwenyezi Mungu amsamehe awe wakwanza kuingia peponi, ima amuingize motoni kisha atamtoa motoni baada ya kumuadhibu na amuingize peponi, Muumini vyovyote atakavyo kuwa na uovu na maasi ambayo yako chini ya shirki hakika hapaswi kukata tamaa na rehma ya Mwenyezi Mungu,na pepo haiwi ni haramu kwake, nayeye atakuwa chini ya msamaha wa Mwenyezi Mungu kwa utashi wake Mwenyezi Mungu mtukufu.Ama mshirikina hakika yeye amenyimwa hayo yote - Mwenyezi Mungu  atukinge na shirki-yote hayo yanaonyesha kuwa Shirki nidhambi kubwa, alisema Mwenyezi Mungu mtukufu :{Hakika Shirki nidhulma kubwa} (Luqmaan 13).Na alisema Mwenyezi Mungu mtukufu:{Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika amezua dhambi kubwa } (An Nisaai 48).{Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi huyo amepotea upotovu wa mbali }(An Nisaa 116)Yote haya yanaonyesha kuwa ushirikina nidhambi kubwa, na itakapo kuwa ushirikina nidhambi kubwa kwahakika niwajibu kwa wana wachuoni na waliosoma kukataza nakutahadharisha watu wasiingie katika dhambi kubwa, na wasinyamanze, na niwajibu kuwapiga vita washirikina kama kuna uwezo wakufanya hivyo,kama alivyo wapiga vita Mtume (S.a.w).Alisema Mwenyezi Mungu mtukufu: {basi wauweni washirikina popote muwakutapo, na washikeni na wazungukeni, na wavizieni katika kila njia. Lakini wakitubu, wakashika Sala, na wakatoa Zaka, basi waachilieni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu} Al Tawbah-5 niwajibu kutahadharisha watu kutokana na ushirikina nakuwabainishia watu mpaka watakapo jiepusha na ushirikina, haya ndio yanayo paswa.Ama kunyamanzia ushirikina na kuwaacha watu wana tanga tanga na kuingia katika ibada ya asie kuwa Mwenyezi Mungu, ilihali wanajidai kuwa niwaislam,na hakuna anae kataza wala hakuna anae hadharisha,basi hilo nijambo la khatari sana, kuna watu wanaelekea kwenye kukataza watu wasile Riba, na zinaa,na kuharibika tabia, mambo haya yote niharamu na ndani yake kuna uovu,lakini Ushirikina   ni zaidi, kwanini hawatilii umuhimu kuwakataza watu na shirki, na kubainisha yale yanayo tokea kwa  watu wengi kutokana na kuingia katika shirki kubwa haliyakuwa wanajidai kuwa  niwaislam.Kwanini kuna kupuuzia katika jambo hili la ushirikina na kujighafilisha nakuwaacha watu wakiangukia katika shirki, ilihali kuna wanachuoni bali wanaishi pamoja nahao walio angukia katika shirki, na wana nyamanza?Jambo la wajibu nikuelekea mmoja kwenda kukataza, hatari hii kubwa ambayo imeteketeza ummah vibaya,Hakika kila dhambi isio kuwa shirki ninyepesi, lamsingi ni kuanza na jambo lenye umuhimu zaidi, kisha la chini yake.nk  Maana ya Shirki.Nikumuomba asie kuwa Mwenyezi Mungu pamoja na Mwenyezi Mungu Maana ya maneno hayo: Nikukipeleka kitu chochote katika ibada kwa asie kuwa  Mwenyezi Mungu, kama Malaika, au Nabii au mtu mwema, au majini, au vitu vingine katika viumbe, yeyote mwenye kupeleka ibada kwa asiye kua Mwenyezi Mungu basi hili ndilo jambo kubwa alilo kataza Mwenyezi Mungu, na ndio ushirikina.Basi tambueni tafsiri ya Tawhiid na Shirki, kwasababu kuna baadhi yawatu wanatafsiri tawhidi kwatafsiri isiyokuwa yake na kuna anae tafsiri Shirki kwamaana isiyokuwa yake.Kuna baadhi ya watu wanasema: hakika shirki ni shirki katika kuhukumiana, na maana hii imedhihiri katika zama hizi,Kuhukumu kwa sheria isiokua ya Mwenyezi Mungu ninamna miongoni mwa namna za shirki na inaitwa shirki ya kutii(Twaa), hakuna shaka kwamba kumtii kiumbe  katika kuhalalisha  yale aliyo haramisha Mwenyezi Mungu au kuharamisha yale aliyo halalisha Mwenyezi Mungu hii niaina ya shirki lakini kuna shirki kubwa kuliko hii, nayo ni kukiabudu kisicho kua  Mwenyezi Mungu kwa kuchinja nakutoa nadhiri na kutufu nakuomba nusra,jambo la wajibu nikujitahadharisha na shirki  zote asichukue aina moja ya shirki akaikataza kisha akaacha iliyo kubwa  na yenye khatari zaidi, na asitafsiri maana ya shirki kuwa nikwenda  kuhukumiana kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu basi, au maana ya shirki ni shirki katika siasa.Na wengine wanasema: shirki katika makaburi nishirki nyepesi,maneno hayo nikufanya ujeuri kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, kwakua shirki ndilo jambo kubwa alilo likataza Mwenyezi Mungu,nalo nikukiomba kisichokuwa Mwenyezi Mungu pamoja na Mwenyezi Mungu.hii ndio Shirki.Na miongoni mwao kuna anae sema:Shirki nikuipenda dunia na kuchukia mali.Mali aliifanya Mwenyezi Mungu niyenye kupendwa mapenzi ya kikawaida na kitabia, anasema Mwenyezi Mungu mtukufu {Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi} al fajri 20.{Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali! }(Al Adiyat8)Na amesema Mwenyezi Mungu {Sema: Ikiwa baba zenu, na wanenu, na ndugu zenu, na wake zenu, na jamaa zenu, na mali mliyo yachuma na biashara mnazo ogopa kuharibika, na majumba mnayo yapenda, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Jihadi katika Njia yake, basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu alete amri yake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wapotovu} (Attawba 24).Alisema: kile mnacho kipenda zaidi, hakuwakataza wasikipende,lakini alicho wakataza nikutanguliza mapenzi ya kitu hicho juu ya mapenzi ya kumpenda Mwenyezi Mungu, kupenda mali sio ushirikina, kwasababu hayo nimapenzi ya kimaumbile, watu wanahitaji mali na wanapenda mali basi mtu kupenda mali sio ushirikina, kwasababu nikatika kupenda manufaa ambayo wanajinufaisha watu, lakini hao ambao wanao sema maneno hayo ima ni kwasababu hawajui hawakujifunza tauhiid na hawaijui shirki, au niwapingaji wanataka wawapeleke watu katika upotovu wakuto itambuwa Tawhiid na wafate matamanio ya nafsi zao, na Mwenyezi Mungu ndiye mjuzizaidi ya wanavyo kusudia.Jambo lamsingi nikwamba hiyo sio shirki,kwasababu ushirikina nikumuomba asie kuwa Mwenyezi Mungu pamoja na Mwenyezi Mungu, au kukipeleka kitu katika ibada kwa asie kua Mwenyezi Mungu, kama kuchinja na kutoa nadhri na kuomba dua nakuomba nusra na kuomba msaada nakukikimbilia kitu na kuogopa na kutarajia namengine mengi,Kufanya hivyo ndio kuingia katika shirki ambayo ndiyo dhambi kubwa kwa Mwenyezi Mungu,kumuomba asie kuwa Mwenyezi Mungu kwasababu dua ndio aina kubwa ya ibada.Anasema Mwenyezi Mungu mtukufu: {Wa kuombwa kweli ni Yeye tu. Na hao wanao waomba badala yake hawawajibu chochote}.(Araad)na Anasema Mwenyezi Mungu mtukufu:{Basi mwombeni Mwenyezi Mungu mkimsafia Dini Yeye tu, na wangachukia makafiri} Ghaafir14. Basi kukiomba kisicho kua Mwenyezi Mungu ni shirki ambayo ameiharamisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w) ama haya baadhi ya vifungu wanavyo viweka baadhi ya watukatika kuelezea maana ya tawhid hivyo sio Shirki.Tunaweza kusema kuwa hakika baadhi ya hivyo vifungu nisehemu katika shirki na katika hivyo kunavingine nihatari zaidi ya shirki, kwasababu shirki inatofautiana, baadhi yake ni mbaya zaidi kuliko nyingine, tunaomba hifadhi kwa Mwenyezi Mungu.  Dalili inayo onyesha kuwa Tawhiidi ni jambo kubwa alilo amrisha Mwenyezi Mungu.Amesema Mwenyezi Mungumtukufu:{Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote}(An Nisaa 36).Aya hii ni dalili kubwa inayoonyesha kuwa jambo kubwa ambalo Mwenyezi Munguamewaamrisha waja wake ni Tawhid kisha ndio mambo mengine kama alivyo eleza katika Ayahii, Mwenyezi Mungu ameanza katika Aya hii kwa kuamrisha waja wake Tawhid na akawakataza ushirikina, hii nidalili yakwamba Tawhid nijambo kubwa alilo amrisha Mwenyezi Mungu na ushirikina nijambo kubwa alilo likataza Mwenyezi Mungu.Na Mwenyezi Mungu haanzi kuamrisha jambo ila linakuwa nikubwa na hakatazi jambo ila linakuwa nibaya, Mwenyezi Mungu huanza lamuhimu zaidi kisha linalo fuatia katika umuhimu. Ujumbe wa Nne  Misingi mitatu ambayo ni lazima kuifahamu.Msingi wa kwanza: Kumtambua Mwenyezimungu Mtukufu:Pindi pakisemwa kwako, ipi misingi mitatu ambayo ni lazima kuitambua? Basi sema: Mja kumtambua Mola wake na dini yake na Mtume wake Muhammad (s.a.w).Misingi: Mkusanyiko (wingi) wa msingi,na msingi ambao wenye kujengewa juu yake kitu kingine na tawi ambalo lenye kujengewa juu yake kitu kingine, basi kwa hivyo imeitwa misingi kwani inajengewa juu yake jambo la dini,.Na dini yote inazunguka juu ya misingi hii mitatu. Kwanini ameihusisha misingi hii mitatu?.Kwanini kwamba ndio misingi katika dini ya ki-islamu,na ni kwamba ni maswali ambayo anaulizwa kwake mja pindi anapowekwa ndani ya kaburi lake, kwani hakika ya mja pindi anapowekwa ndani ya kaburi lake na pakasawazishwa juu yake udongo, na watu wakaondoka kutoka kaburini, hali wakirejea kwa jamaa zao,wanamjilia Malaika wawili ndani ya kaburi, basi kisha inarejeshwa roho yake katika kiwiliwili chake na anakua hai uhai wa maisha ya kaburini,sio kama maisha mfano wa maisha ya duniani, maisha ya Mwenyezi Mungu yeye mjuzi zaidi, basi wanamuweka kitako ndani ya kaburi lake na kisha wanasema kumwambia yeye: Nani Mola wako,na dini yako, na Mtume wako? basi Muumini anasema: Mwenyezi Mungu Mola wangu,na dini yangu uislamu, na Muhammad (s.a.w)Mtume wangu, basi panasemwa kwake yeye: Vipi umefahamu? Anasema: Nimesoma kitabu cha Mwenyezi Mungu nikatambua na kufahamu, basi anaita muitaji kwamba amesadikisha (amesema kweli) mja wangu basi mtandikieni katika pepo na mfungulieni yeye mlango katika pepo, na hutanuliwa kwake yeye kaburi lake urefu wa upeo wa jicho, na huletewa yeye harufu ya pepo na roho yake, basi anaangalia makazi yake katika pepo, kisha anasema: Ee Mola wangu simamisha kiama mpaka nirejee kwa watu wangu na mali zangu.Na ama mwenye shaka ambae ameishi juu ya shaka na wasi wasi na kukosa uyakinifu, na japokua anadai kua muislamu, pindi ikiwa kwake yeye kuna wasiwasi na Shaka katika dini ya mMwenyezi Mungu kama mnafiki,basi kwamba yeye anagagasia maneno, (kujitafuna) pindi pakisemwa kwake yeye: Nani Mola wako? Anasema sitambui, na pindi pakisemwa: Ipi dini yako?Anasema:sitambui,na pindi pakisemwa:Nani Nabii wako: Anasema sitambui haah haah hapana sitambui nimesikia watu wanasema kitu basi na mimi nikasema.Yani katika dunia anasema yale yanayosemwa na watu pasi na imani ya kuamini tunamuomba Mwenyezi Mungu atulinde na hayo,huyu ni mnafiki ambae amedhihirisha uislamu na hali yakua wala haitakidi (kufungamanisha) katika moyo wake, isipokua amedhihirisha kwake kwa ajili ya maslahi yake ya kidunia,basi anasema: katika dunia: Mola ni Mwenyezi Mungu, nae si mwenye kuamini hayo,moyo wake unapinga tunamuomba Mwenyezi Mungu atulinde na hayo!!Anasema:Dini yangu uislamu hali yakua haamini, moyo wake unapinga!! Anasema: Mtume wangu Muhammad (s.a.w) nae si mwenye kuamini ujumbe wa Muhammad katika moyo wake!! Hakika kwamba anasema katika kinywa chake tu(ulimi), huyu ni mnafiki, basi panasemwa kwake: usingelijua,na ukasoma, basi anapigwa nyundo itokanayo na chuma, anapiga kelele kutokana na maumivu laiti wangemsikia yeye vizito viwii(majini na wanadamu)wangezimia, wanamsikia kila kitu isipokua mwanadamu lau angelisikia angelizimia,kwamba:angekufa kutokana na uzito wake,na hubanwa ndani ya kaburi lake mpaka zinatofautina mbavu zake,na unafunguliwa kwake mlango wa motoni basi kisha inamjilia sumu yake na joto lake basi kisha anasema: Ee Mola wangu usisimamishe kiama, haya ni maisha yake na hali yake katika kaburi, tunamuomba Mwenyezi Mungu atulinde na haya, kwani hakujibu majibu yaliyo sahihi.Pindi pakisemwa kwako: Nani Mola wako? basi sema: Mola wangu ni Mwenyezi Mungu ambaye alienilea na akalea walimwengu wote (viumbe) kwa neema zake.Na kwa hivyo anaita muitaji kua kwamba umekanusha mja wangu basi mtandikie katika moto, na fungua kwake mlango katika moto, tunamuomba Mwenyezi Mungu atulinde, basi pindi ikiwa haya maswali kwa umuhimu huu inawajibika juu yetu tuwe ni wenye kujifundisha na kuitakidi nayo (kua na imani nayo ndani ya moyo) na wala haitoshi kujifunza pekee, bali kujifunza na kuitakidi na kuamini na kuyafanyia kazi, pale ambapo tunadumu juu ya mfumo wa maisha, huenda Mwenyezi Mungu akawa mwenye kututhibitisha wakati wa maswali ndani ya kaburi.Anasema Mwenyezi Mungu mtukufu: (Mwenyezi Mungu huwathibitisha walioamini kwa kauli iliyo thabiti katika maisha ya dunia na katika akhera. Na Mwenyezi Mungu huwaacha kupotea hao wenye kudhulumu. Na Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo)Ibrahimu:27.Basi hii misingi mitatu ina umuhimu mkubwa na kwa hivyo ni lazima kujengwaItikadi juu ya dalili za kitabu (Qur-ani) na Sunnah (Hadithi)na juu ya kuangalia katika Aya za Mwenyezi Mungu za kuumba,kwa ajili ya kua mwenye kusafisha akili na kuthibitisha katika moyo na kuondosha wasiwasi (shaka)Na ama itikadi zenye kujengwa juu ya mifanano na na juu ya shaka na juu ya maneno ya watu, na ufuataji wa upofu,basi kwamba hakika ni itikadi zenye kuondoka hazithibiti,nazo zinaelekewa na hatari ya kuvunjwa na kuelekewa na hatari ya kubatilishwa,Basi hapathibiti itikadi na wala hukumu za kisheria zilizosalia isipokua kwa dalili Qur-ani na Sunnah na kwa dalili za akili zilizosalimika.Pindi pakisemwa kwako  kwamba: Umeulizwa nani Mola wako?na hili swali limepokewa utaulizwa kwake katika maisha ya dunia na akhera, basi lazima uwe unafahamu Mola wako mwenye ushindi na utukufu, na uwe mwenye kujibu kwa majibu yaliyo sahihi yenye kujengewa na uyakinifu na hoja,basi sema: Mola wangu ni Mwenyezi Mungu,hili ndilo jibu, ambae amenilea mimi na akalea wote walimwengu kwa neema yake hii dalili ya kiakili.Basi Mola alietakasika na utukufu wake yeye ndiye ambae analea viumbe vyake wote kwa neema zake,Katika matumbo ya mama zao umbile baada umbile katika viza(giza) vitatu,na kuwapatia kwao riziki mpaka katika matumbo ya mama zao,na kwa hivyo kinakua kiwiliwili cha mimba katika tumbo la mama yake na kua mkubwa,kwani inapata kwake yeye riziki kutoka kwa Mwenyezi Mungu alietakasika na utukufu wake, na inamfikia kwake yeye chakula.Kisha panapulizwa ndani yake roho basi kisha anacheza na kua hai kwa idhini ya Mwenyezi Mungu haya ni malezi katika tumbo, kisha pindi akitoka basi hakika ya Mwenyezi Mungu subhaanah anamlea kwa uzima na afya na kumtambulisha juu yake maziwa ya mama yake,basi anakunywa mpaka pale atakapokua mwenye kula chakula na akawa mwenye kutosheka na maziwa,kisha anakua kidogo kidogo mpaka anakua baleghe, kisha anakua na anakua mpaka anakua mtu mzima kisha anafikisha miaka arobaini,anakua mpaka mwisho wa kukua.Basi ni nani ambae anamlisha toka siku ambayo amemuumba katika tumbo la mama yake mpaka kufikia kufa? nani ambae anamlisha kisha nani ambae anateremsha hiki chakula na hiki kinywaji katika kiwiliwili basi kisha kinafika katika kila viungo na kwenda katika kila sehemu katika kiwili wili,nani ambae anamtamanisha kwake yeye chakula na kinywaji, nani ambae humgeuza na kumtoa kwake madhara  kwake,nani ambae anafanya haya na kumlea huyu mwanadamu, hivi haikuwa Mwenyezi Mungu alietakasika na utukufu wake? Huyu yeye Mwenyezi Mungu alietakasika na utukufu wake ambae anamlea, yeye ambae amenilea mimi na akalea walimwengu wote kwa neema zake.Na yeye ni mwenye kumuabudu mimi hapana kwangu mimi mwenye kumuabudu isiokua yeye.Kila ambae yupo juu ya sura ya ardhi katika ulimwengu wa wanaadamu na wanyama, na ulimwengu wa nchi kavu na baharini, kutoka viumbe wakubwa mpaka kufikia viumbe wadogo, katika nchi kavu na baharini wote wanakula kwa neema zake na riziki yake,amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Au ni nani huyo ambaye atakupeni riziki kama Yeye akizuia riziki  yake?)Almulk: 2. Na akasema: (Na hakuna mnyama yeyote katika ardhi ila riziki yake iko kwa Mwenyezi Mungu.Naye  anajua makao yake na mapito yake) Hud:6. Na akasema: (Na wanyama wangapi hawawezi kujimiliki riziki zao! Mwenyezi Mungu anawaruzuku  hao na nyinyi pia. Na yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua) Huyu, yeye Mwenyezi Mungu alitakasika:(Huyo ndiye Mwenyezi Mungu,Mola wenu Basi muabuduni yeye) Yunus:3. Ama asiekua Mwenyezi Mungu mwenye ushindi alietakasika akawa juu basi hamiliki kwake chochote si masanamu na wala kinginecho hapana mmoja yeyote anamiliki katika riziki kitu isipokua yeye anaruzukiwa, kiumbe mfano wako.Na yeye Mwenye kuabudiwa: Mola ambae hili jambo lake yeye ambaeanastahiki ibada kwangu mimi na mwengineo haitoshi kukubali tu kua yeye kwa Uungu (kwamba Muumbaji)haitoshi kua mwenye kusema Mola wangu ni Mwenyezi Mungu ambae alienilea kwa neema zake.Hii haitoshi hapana budi kua mwenye kukubali kwake yeye kwa uabuduji,na kutakasa kwake kwa ibada, nahii ndio tofauti kati ya mpwekeshaji na mshirikina, mpwekeshaji anakiri kwa Ungu wake Mwenyezi Mungu mwenye ushindi na utukufu na uabudiwaji wake  pekee usio kua na ushirikina kwake, Na mshirikina anakiri kwa Uungu wa Mwenyezi Mungu, lakini yeye mshirikina katika ibada zake Mola,anashirikisha pamoja nae mwengine katika ibada zake, anashirikisha pamoja nae ambaeasieumba wala kuruzuku na wala hamiliki chochote, hii ndio tofauti kati ya amabae ni mpwekeshaji na mshirikina, Mpwekeshaji anasema: Mola wangu ni Mwenzyezi Mungu, nae namuabudu,na hapana kwangu mimi kinyume chake,ama mshirikina basi anasema:Mola ni Mwenyezi Mungu, lakini ibada kwake yeye si maalumu kwa Mweneyezi Mungu, basi anaabudu pamoja na Mwenyezi Mungu miti na mawe na mawalii na wema na makaburi, basi kwa hivyo anakua mwenye kushirikisha na wala haimnufaishi kwake yeye kukubali kwake na kukiri kwa Mwenyezi Mungu na wala hajaingia katika uislamu.Nae Mwenye kuabudiwa, kwamba Mwenyezi Mungu ambae namuabudu.Hapana kwangu muabudiwaji isipokua yeye: si katika Malaika na wala katika Mitume  na wala katika wema (waja) na wala katika miti na wala katika mawe na wala katika kitu chochote, hapana muabudiwa kwangu kinyume chake alietakasika na utukufu wake, hii ni kukubali tawhidi kwa dalili, na hii dalili ya akili, kisha kataja dalili ya kisomi kutoka ndani ya Qur-ani, na dalili tamko lake Mtukufu: (Kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe wote) Alfaatiha:2.Hii aya ambayo ipo mwanzo wa Qur-ani katika msahafu, hapana kabla yake isipokua kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu, nalo tamko la mwisho la watu wa peponi, amesema: (Na mwisho wa wito wao ni: Alhamdu lillah Rabbil alamiin “Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote”)na Mwenyezi Mungu mtukufu ameanza kwake(kueleza)uumbaji, amesema mtukufu:(Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu alie umba mbingu na ardhi, na akafanya giza na mwangaza) An-aam:1, Na kisha akamalizia kwake (maelezo) kwa kuumba amesema Mtukufu Mwenyezi Mungu: (Na patahukumiwa kati yao kwa haki na patasemwa:Sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe vyote) Azzumar:75. Basi alianza kwake kwa kuumba na kumalizia kwake kwa kuumba basi hilo tamko kubwa.Na mpaka mja(kiumbe)akikutimizia (akikutekelezea) kitu kwako katika ihsani basi kwamba hayo yanatokana  kwa Mwenyezi Mungu,yeye ndiye ambae amedhalilisha kwako huyu kiumbe,nae ambae aliemuwezesha kua mwenye kufanya uzuri kwako,basi shukrani zinarejea kwa Mwenyezi Mungu alietakasika na utukufu wake.Na Mwenyezi Mungu: maana yake:ni mwenye Uungu na kuabudiwa juu viumbe vyake vyote, na hili jina halitamkwi isipokua kwake yeye tuu subhaanah, hapana yeyote mwenye kujiita Mwenyezi Mungu,hata firauni hakupata kusema: mimi Mungu, isipokua kasema mimi mola wenu,basi jina ni maalumu tu kwa Mwenyezi Mungu, hapana mmoja yeyote mwenye kujiita kwake yeye na wala mmoja yeyote mwenye ushupavu wa kusema mimi ni Mwenyezi Mungu.Basi ni wazi kwamba shukrani zote na sifa zote ni kwa Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe wote.Na ulimwengu wa Malaika na ulimwengu wa vitu na vyote vikavu na ndege na ulimwengu wa wanyama wakali na ulimwengu wa wanyama wasio wakali na ulimwengu wa wadudu na vidudu, ulimwengu katika nchi kavu na baharini hakuna ajuae isipokua Mwenyezi Mungu na hapana mdhibiti isipokua Mwenyezi Mungu vyote Mwenyezi Mungu ndiye bwana wao na Mola wao.Mola wa walimwengu: na hili haliitwi isipokua juu ya Mwenyezi Mungu mwenye ushindi mtukufu,haiwezekani kwa yeyote awe mwenye kujisema kwake yeye: Mola wa walimwengu.Pindi pakisemwa:Mola:Basi hii hapaitwi isipokua juu ya Mwenyezi Mungu,juu ya Mwenyezi Mungu mtukufu aliye juu,wala hapageukwi isipokua kuelekea kwake, ama viumbe panafungamanishwa, basi kusemwa: mlezi wa nyumba,mlezi wa wanyama, kwamba:mfalme wao na rafiki yao.Na yote hapana isipokua Mwenyezi Mungu katika ulimwengu, na mimi ni mmoja katika huo ulimwengu.Na yote hapana isipokua Mwenyezi Mungu katika ulimwengu,na mimi ni mmoja katika huo ulimwengu, basi inakua Mwenyezi Mungu Mola wangu, kwani Mwenyezi Mungu ni Mola wa walimwengu,na mimi ni mmoja katika huo ulimwengu, basi hapana yeyote anaweza kua mwenye kusema:Na mimi ni Mola asiyekua Mola wa walimwengu, si kwa kafiri wala muislamu, hili haliwezekani milele na wala hasemi mwenye akili, hii ni dalili juu ya Uungu wake Mwenyezi Mungu mwenye ushindi mwenye kutukuka, na kwakua kwamba hakika yeye ni Mola wa walimwengu basi yeye anastahiki kuabudiwa, na hii inabatilisha ibada isiokua yeye aliyetakasika na utukufu na kwahivyo kasema baada yake: (Wewe peke yako ndiye tunaekuabudu na wewe peke yako ndiye tunaekuomba msaada) Alfaatiha:5Na ibada haikubaliki isipokua pamoja na kukanusha na kuthibitisha, nayo ni maana ya Laa Ilaaha illa llah (Hapana Mola ambae anaestahikiwa kuabudiwa kwa haki isipokua Mwenyezi Mungu) ndani yake kuna kukanusha na kuthibitisha, kupinga Uungu usiokua wa Mwenyezi Mungu, na kuthibitisha kwake kwa Mwenyezi Mungu mwenye ushindi na utukufu.Pindi pakisemwa kwako: Kwa vipi unamtambua Mola wako? Basi sema: Kwa dalili zake na viumbe wake.Wewe umesema: Mwenyezi Mungu Mola wangu au Mola wangu Mwenyezi Mungu ambae ni mlezi wangu kwa neema zake, ni ipi dalili juu ya kwamba Mwenyezi Mungu ni Mola wako ambae amekulea kwa neema zake? pindi pakisemwa kwako: kwa lipi unamtambua Mola wako?kwani kwamba mwenye kudai kitu basi hapana budi awe mwenye kusimamisha hoja juu ya madai yake.Wadaiji pindi si wenye kusimamisha ** juu yake hoja watu wake watamdai Hapana budi kwa kila mdaiji awe mwenye kusimamisha dalili juu ya madai yake, kinyume chake itakua madai yake sio sahihi, wewe umesema: Mola wangu ni Mwenyezi Mungu ambae ni mlezi wangu na mlezi wa walimwengu wote kwa neema zake, ipi dalili? basi sema: Dalili ni Aya zake na viumbe wake.Aya zake, kwamba: Alama zake na dalili zake zijulishazo juu yake subhaanah (aliyetakasika na utukufu wake) basi viumbe vyote ambavyo unavyoviona vyote vilikua havipo kisha Mwenyezi Mungu akavifanya viwepo na akaviumba kwa uwezo wake aliyetakasika na utukufu.Na kwake yeye ameumba vinapatikana mfano wa mimea na vizaliwavyo na vitu havikui vyenye kupatikana kisha vikapatikana na hali yakua mkawa mnaangalia hivyo kwake, nani ambae anaumba kwake? ni yeye Mwenyezi Mungu alietakasika na utukufu.jee vinajiumba vyenyewe,jee mmoja yeyote katika watu ameumba? hapana yeyote mwenye kudai haya, na wala hawezi kudai. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu :(Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote,au ni wao ndio waumbaji? ** Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana yakini) At-tuur 35-36  Hivi vitu si vyenye kujipatisha vyenyewe au amevipatisha mwenginewe katika viumbe kamwe, haikua na wala haiwi anaumba yeyote mti au mbu au nzi: (Hakika wale mnao waomba kinyume na Mwenyezi Mungu,hawatoumba hata nzi japo kua watajumuika kwa hilo)Alhajj:73.Basi huu uumbaji unajulisha juu ya Muumbaji Subhaanah mtukufu, na kwa hivyo pindi paliposemwa kuambiwa mwarabu mbedui juu ya mshangao: Vipi unamtambua Mola wako? Ngamia anajulisha juu ya ngamia, na athari inajulisha juu ya mtembeaji, hivi haijulishi huu ulimwengu juu ya alie Mpole  Mjuaji?.Pindi ukiangalia alama za nyayo juu ya ardhi, hivi haikujulishi haya juu ya kwamba kuna mmoja ametembea juu ya hii ardhi? Na pindi ukiangalia kanyago za ngamia hivi haikujulishi?.Na katika dalili zake usiku na mchana jua na mwezi, na katika viumbe wake: mbingu saba na ardhi saba na vilivyomo ndani yake na kati yake.Hii hakika kwamba inajulisha ardhi ndani yake kuna ngamia au kapita juu yake ngamia, nakanyago inajulisha juu ngamia na alama inajulisha juu ya mtembeaji.Na katika dalili zake usiku na mchana jua na mwezi:na Aya zimegawanyika sehem mbili: kigawanyo cha kwanza: Dalili za ulimwengu zinaonyesha, mfano wa mbingu na ardhi na nyota jua na mwezi na majabali miti na bahari, zimeitwa ni alama,kwani kwamba zinajulisha juu ya muumbaji alietakasika na utukufu wake,na kwa hivyo anasema Abuu l- ataahy katika shairi zake:Basi hushangai vipi anaasiwa Mungu**ama vipi anapinga mpingajiNa katika kila kitu kwake ni dalili ** inajulisha kwamba  ni mmojaNa kwa Mungu kila kitu kitingishikacho ** na kituliacho katika nyuma angalia.Vipi anapinga mmoja Mwenyezi Mungu alietakasika na utukufu anasema:Hakuna huko Mola kwa huu ulimwengu wote, na hivi viumbe vimepatakina pasi na muumbaji,na vikipatikana na muumbaji basi nani huyu muumbaji isiyokua Mwenyezi Mungu aliemtukufu nibainishie mimi? hautokuta muumbaji asiokua Mwenyezi Mungu alietakasika na utukufu wake: (Au wamemfanyia Mwenyezi  Mungu washirikia walioumba kama alivyoumba yeye, na viumbe hivyo vikawadanganyikia? Sema: Mwenyezi Mungu ndie Muumba wa kila kituna yeye ni mmoja mwenye kushinda) Ar-raadi:16.Kigawanyiko cha pili: Dalili za qur-ani ambazo zinasomwa kutoka katika wahyi wa mshushaji juu ya Mtume (s.a.w.)hizi zote dalili juu ya kupatikana Mwenyezi Mungu alitakasika na utukufu wake, na juu ya ukamilifu wake na sifa zake na majina yake na juu ya kwamba anastahiki kwa ibada pekee pasi na mshirika kwake, yote yanajulisha juu ya aya za ulimwengu na aya za qur-ani.Na dalili za ulimwengu zilizopo zinajulisha juu yake kwamba yeye muumbaji na mpatishaji na mwendeshaji ulimwengu,na dalili za qur-ani ndani yake kuna amri za kuabudu Mwenyezi Mungu,na ndani mna kukiri kupwekeka kwa umola wake, kila qur-ani inazunguka katika maana hii,na kuteremshwa katika hii maaana.Na katika aya zake usiku na mchana jua na mwezi, hii ni katika dalili kubwa alietakasika na utukufu wake, usiku wa kiza ambao unafunika huu ulimwengu, na mchana wenye kung’ara ambao unang’arisha huu ulimwengu, basi kisha watu wanashughulishwa  amesema mtukufu: (Sema:Mnaonaje,Mwenyezi Mungu ange ufanya usiku ubakie moja kwa moja mpaka siku ya Kiyama,mungu gani asiye kua Mwenyezi Mungu atakye kuleteeni mwangaza?Basi je hamsikii?  Sema:Mnaonaje, Mwenyezi Mungu ange ufanya mchana ubakie moja kwa moja mpaka siku mpaka siku ya Kiyama, mungu gani asiye kua Mwenyezi Mungu atakaye kuleteeni usiku mkapumzika humo? Basi je hamuoni? Na kutokana na rehema zake amekujaalieni usiku na mchana mpate kupumzika humo na mtafute fadhila zake, na ili mpate kushukuru) Alqaswas:71-73Hii ni katika dalili kubwa za Mwenyezi Mungu huu mchana na usiku, na si mda wote usiku, na si mda wote mchana, kwani kwamba lau ingelikua hivyo hivyo tuu yangeharibika maslahi ya waja na wangechoka.Amefanya Mwenyezi Mungu kwao usiku na mchana vinafuatana, kisha usiku na mchana vimepangiliana haendi kinyume mmoja yeyote na wala hapabadiliki, juu ya mpango mmoja katika unaojulisha juu ya hekima wa Muhukumu alietakasika na utukufu wake, vitendo vya waja havibadiliki na vitendo vyao vinaharibika na kutofautiana vyovyote iwavyo na kuharibika, ama viumbe wa Mwenyezi Mungu basi kwamba hapaharibiki isipokua kwa mda anaoruhusu Mweneyzi Mungu kwamba paharibike kwake.Mchana na usiku vyenye kuendelea hapaharibiki kimoja wapo, ama pale katika utengezaji wa kiumbe panaharibika na kubomoka na kwisha ijapokua ngumu na kubwa.Kama manvyoona katika magari yatembeayo na ndege na meli pamoja kwamba vina nguvu na kutiliwa nguvu kwake lakini vianaharibika na kubomoka, jee umeharibika usiku au mchana? Hapana, kwani kwamba mtengezaji wake mwenye uwezo mwenye hekima alietakasika na utukufu wake: (Huo ndio ufundi wa Mwenyezi Mungu alietengeneza vilivyo kila kitu) An-namli:88.Na dalili juu Umola wake na Ungu wake (wakuabudiwa) alietakasika na utukufu wakeNa dalili tamko la Mtukufu: (Na katika aya zake ni usiku na mchana,na jua na mwezi, basi msilisujudie jua wala mwezi, bali msujudieni Mwenyezi Mungu alie viumba, ikiwa nyinyi mnamuabudu Yeye tu) Fuswilat:37.Hii dalili juu Umola wake na Ungu wake wa kuabudiwa subhaanah wata-aalah: (Na katika aya zake ni usiku na mchana, na jua na mwezi).Jua na mwezi: Jua ni sayari kubwa ambayo inaangaza ulimwengu na kupatisha joto kama alivyotamka Mwenyezi Mungu mtukufu:(Na tukaifanya taa yenye mwanga na joto) Annabai:13.Na mwezi ni nuru unaangaza usiku na unaangaza njia kwa watu,na katika maslahi yake viwili hivyo pia kutengeza ulimwengu kwa miti yake na matunda yake na bahari yake, basi lau Jua likajificha katika ulimwengu ungeharibika ulimwengu na pangeharibika mengi katiak maisha ya watu na maslahi yao, na ungelijificha mwezi hivyo hivyo, na mwezi pia ndani mna manufaa kwa matunda na miti, pamoja yale yaliopo ndani yake vile vile katika kutambua hesabu ya kalenda,amesema mtukufu: (Na mwezi ukawa na nuru,na akaupimia vituo ili mjue idadi ya miaka na hesabu) Yunusu:5.Na amesema: (wanakuuliza khabari ya mwezi(mwandamo).Sema hiyo ni vipimo vya nyakati kwa ajili ya watu na hija) Albaqara:189.Basi katika mwezi kuna masilahi ya kutambua nyakati na muda,muda wa madeni, na muda wa hesabu za desturi za wanawake (hedhi) na nyakati za ibada na funga na hija, vyote vinatambulika kwa hesabu inayojengewa juu ya hizi nuru mbili: Juana mwezi,basi hesabu ya jua na hesabu ya mwezi basi ndani yake kuna maslahi ya viumbe wote.Na katika viumbe wake mbingu saba amesema mtukufu: (Mwenyezi Mungu ni yule ambaye ameziumba mbingu saba,na ardhi kwa mfano wa hizo)Attalaaq12. (Alieumba mbingu saba kwa matabaka).Almulk:3.Baadhi yake juu baadhi ya nyengine, mbingu ya dunia kisha ambayo inayofuata mpaka kufikia ya sabana juu ya vyote kuna kiti chake cha enzi (arshi) Mwenyezi Mungu alietakasika na utuku wake.Na ardhi saba kama alivyosema mtukufu :( Na ardhi kwa mfano wa hizo) Basi ni matabaka saba vilevile na kila tabaka katika matabaka ya mbingu saba na ardhi saba ina wakazi na majengo, ila katika mbingu kuna nyota na sayari mwezi na jua, na ila katika ardhi kuna viumbe katika wanyama kwa kutofautiana namna zake na katika majabali na miti na mawe na madini na bahari hizi ni alama za Mwenyezi Mungu mtukufu alietakasika, dalili za kiulimwengu ambazo huonwa na kushuhudiliwa.Amesema rehema za Mwenyezi Mungu zimwendee:na dalili kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu: (Na katika aya zake ni usiku na mchana, na jua na mwezi, basi msilisujudie jua wala mwezi, bali msujudieni Mwenyezi Mungu alie viumba, ikiwa nyinyi mnamuabudu Yeye tu) Fuswilat:37.Katika aya zake usiku: yani katika alama zake zijulishazo juu ya Ungu wake na uwezo wake na kwamba anastahikiwa kwa ibada kinyume na mwengine usiku ambao unatia kiza na mchana ambao unaangaza ulimwengu mzima, hii ni katika maajabu ya alama za Mwenyezi Mungu alietakasika na utukufu wake.Basi ni nani ambaye anafanya ulimwengu wote kiza katika mda mmoja? kisha anafanya ulimwengu mwangaza katika wakati mmoja?ni Mwenyezi Mungu alietakasika na utukufu wake.lau pangelikusanyika viumbe juu ya kwamba waangaze nuru sehemu katika ardhi wasingeliweza kua wenye kuangaza nuru isispokua ni sehemu zenye mipaka maalumu,lau wangelikuja na umeme ambao upo katika dunia yote hauangazi isipokua sehemu maalum katika ardhi.Ama jua na mwezi viwili hivi vinaangaza ardhi yote, usiku na mchana unafuatana na jua na mwezi vile vile.Amesema mwenyezi Mungu: (Msilisujudie jua wala mwezi, bali msujudieni Mwenyezi Mungu alie viumba,ikiwa nyinyi mnamuabudu Yeye tu) Fuswilat:37.Hii ni ubatilifu kwa washirikina,msisujudie kwa viumbe,kwani katika ukubwa wa viumbe jua na mwezi, na kwamba washirikina ilikua wanaabudu jua na kusujudia, na miongoni mwao wapo wanaabudu makaburi na nyota mfano watu wa Ibrahimu (Nabii) wanajenga kwake hekalu juu ya sura nyota na kuabudia kwake, basi tamko lake mtukufu: (Msilisujudie jua) sijida maana yake kuweka bapa ra uso juu ya ardhi kwa unyenyekevu,nalo kubwa katika namna za ibada,anasema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w): ((Ukaribifu zaidi unakua kati ya mja na Mola wake nae katika hali ya sijida)).Basi ukubwa wa namna za ibada kusujudu juu ya ardhi,kwani uso wako ambao ni kitu kitukufu kwako umeweka kwa Mwenyezi Mungu hali ukiabudu na kunyenyekea kati ya mbele ya Mwenyezi Mungu alietakasika na utukufu,huku ndio kusujudu kwa hakika,na haifai isipokua kuabudu kwake yeye Mwenyezi Mungu pekee.Ama kusujudia jua na mwezi basi kusujudu kwa viumbe haistahiki kua ni vyenye kusujudiwa kwake,basi haifai kusujudia viumbe,isipokua kwamba kusujudu kwa muumbaji viumbe,ama viumbe basi mfano wako viumbe vinaendeshwa na kuamrishwa,jee unasujudia kiumbe kinachoshindwa mfano wako? hii haifai, wapi akili zako zimeenda?!!.Na tamko lake Mwenyezi Mungu: (Hakika Mola wenu ni Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita,kisha akatawala juu ya kiti Cha enzi, huufunika usiku mchana, ufuatao upesi upesi, na jua na mwezi,na nyota zinazo tumika kwa amri yake, fahamuni kuumba na amri ni yake,ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe vyote) Aaraaf:54.Kusujudu ni kwamba kunastahiki kwa muumba alietakasika na utukufu wake ambaye hashindwi na chochote,basi kusujudu ni haki kwa Mwenyezi Mungu alietakasika na utukufu wake na hapana haki kwa viumbe vyovyote imekua huyu kiumbe ana ukubwa na utukufu basi kwamba kiumbe ni dhaifu mwenye kuendeshwa na mwenye kuamuliwa kwake (Basi msilisujudie jua wala mwezi bali msujudieni Mwenyezi Mungu aliye viumba ikiwa nyinyi  mnaabudu yeye tu) fuswilat:37.Basi lililo wajibu kwamba tusiwe wenye kuabudu isipokua Mwenyezi Mungu,pindi mkisujudu kwake na mkasujudu kwa mwenginewe basi inakua nyinyi mnaabdu kwa Mwenyezi Mungu ibada iliyo sahihi,bali mnaabudu pamoja na kufanya ushirika,na ushirika(shirki)unaharibu ibada.Hakia ya Mola wenu, kwamba: yule aliekuumbeni na akakutunzeni kwa neema zake, hapana Mungu apasae kuabudiwa kwa haki ila yeye alietakasika na utukufu wake.Kisha akataja dalili juu ya hayo basi akasema: (Ambae ameumba mbingu na ardhi) Aaraaf:54.Hii ni hoja juu Ungu wa Mwenyezi Mungu mwenye ushindi alietukuka,kwamba ameumba mbingu na ardhi, na hapana yeyote ameumba kitu katika viwili hivyo, na wala mmoja  yeyote amemsaidia alietakasika na utukufu wake juu ya hilo,bali yeye amepwekeka kwa viumbe wake (Ameumba mbingu na radhi) jee kuna mmoja katika washirikina au wapingaji (wakengeukaji) anapinga hili na kusema:Hajaumba Mwenyezi Mungu mbingu wala ardhi,ambae alieumba viwili hivi Fulani, au mimi ndie nilieumba,au ameumba sanamu fulani? jee amesema haya mmoja katika ulimwengu wa mwanzo na wa mwisho, pamoja kwamba hii aya inasomwa usiku na mchana? wala hakuna mmoja yeyote anapinga na hawezi kupinga milele.Katika siku sita:Hivi viumbe vikubwa ameviumba Mwenyezi Mungu katika siku sita,nae ni muweza juu ya kuumba katika mda mmoja tu,lakini ameumba katika siku sita kwa hekima anajua yeye alietakasika na utukufu, na masiku sita mwanzo wake siku ya jumapili na mwisho wake siku ya ijumaa,katika siku ya ijumaa pamekamilika uumbaji, na kwa hivyo imekua hii siku kubwa katika masiku ya wiki, nayo ni bwana wa masiku na idi ya wiki siku hii,nayo ni siku bora.Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w): ((Bora ya siku iliyochomoza kwake jua siku ya ijumaa))  kwani kwamba pamekamilika kwake kuumba viumbe,na kuumbwa kwake Adamu na kuingizwa peponi na kutolewa (kuteremshwa) kwake,na siku ambayo kwake itatokea kiyama,yote hayo siku ya ijumaa, basi siku ilo bora kwa masiku,nayo siku ya mwisho kuumbwa kaumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake. (Hakika Mwenyezi Mungu ndiye anaye zuilia mbingu na radhi zisianguke.Na zikidondoka hapana yeyote wa kuzizuia isipo kua Yeye.)) Faatir:41.Basi kiti cha enzi ni muhitaji kwa Mwenyezi Mungu mwenye ushindi alietukuka kwani kwamba yeye muumbwa (arshi),na Mwenyezi Mungu ni mkwasi (tajiri) kutokana na arshi(kiti cha enzi)na venginevyo,lakini yeye Mwenyezi Mungu ametengemaa juu yake kwa hekima anajua yeye alietakasika na utukufu,na kutengemaa ni namna katika ujuu (kutukuka) lakini kua juu sifa ya nafsi (pekee), ama kutengemaa basi sifa amefanya na anafanya anapotaka alietakasika na utukufu wake.(Unaufunika usiku mchana) kwamba unaufunika usiku mchana,na unaufunika mchana usiku basi pale ambapo unaona ulimwengu unaangaza mwanga basi pindi tu usiku  unaufunika na unakua giza.Na usiku unaufunika mchana unakua unaangaza (uanutafuta haraka) inakuja hii baada hii papo kwa papo pasi na kuchelewa,basi pindi ukigeuka usiku umekuja mchana,na pindi ukigeuka mchna umekuja usiku papo kwa papo, hapachelewi huu kwa huu,na hii ni katika ukamilifu wa alietakasika na utukufu wake,haidhoofishi hii kutokana na hii,na jua ni sayari kubwa iliyo maarufu na mwezi vile vile sayar katika sayari saba zitembeazo na kila katika viwili hivyo vinatembea na kuzunguka juu ya ardhi.Na nyota:nayo ni sayari,yenye kudhalilishwa kwa amri yake,kudhalilishwa katika kutembea na kuzunguka daima na wala hazichelewi,na hii marejesho ya majibu juu ya wale ambao wanaabudu jua na mwezi na nyota kwamba vimedhalilishwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu vimeamrishwa,Mwenyezi Mungu ambaye anavipitisha,na Mwenyezi Mungu ambaye anavisimamisha pindi akitaka alietakasika na utukufu wake, basi yeye mdhoofishaji muendeshaji hapana kwake yeye katika kitu amri yoyote. Kuumba:Nako ni kupatisha basi yeye Muweza juu ya viumbe pindi akitaka alietakasika na utukufu wake anaumba kile atakacho.Na amri: Ameamrisha alietakasika na utukufu wake,Ameamrisha ulimwengu:Ambaye anaamrisha kwake yeye viumbe basi vinatii na kuitikia kwake mfano wa tamko lake: (Akaziambia hizo na ardhi: Njooni kwa khiyari au kwa nguvu )Fusilat:11. ameamrisha hizo alietakasika na utukufu,na hii amri ya ulimwengu ameamrisha kwake mbingu na ardhi basi zikatengenezeka, (Hakika amri yake anapotaka kitu kitu ni kukiambia tu,Kuwa! Na kikawa) Yasini:82, hii amri ya kiulimwengu. Ama amri ya kisheria:Basi nayo ni ufunuo (wahyi) unaoshushwa ambae anaamrisha kwake waja wake, anawaamrisha kwa kumuabudu kwake,anawaamrisha kwa swala, anawaamrisha kwa zaka,anawaamrisha kwao kuwafanyia wema wazazi wawili,hii amri ya kisheria,panaingia ndani yake amri nyingi na makatazo mengi ambayo katika qur-ani na hadithi za Mtume (s.a.w) zilizo sahihi,hii katika amri ya Mwenyezi Mungu alietakasika na utukufu wake.Ikiwa kwake kuna uumbaji na amri basi kitu gani kimesalia kinginecho isiyokua alietakasika na utukufu wake? na kwa hivyo anasema Ibnu Omari pale aliposoma hii aya,kasema:Mwenye kitu basi aamrishe.Na Mola ni mwenye kuabudiwa,na dalili tamko lake mtukufu: (Enyi watu!Muabuduni Mola wenu ambaye amewaumbeni ninyi na wale waliyokuwa kabla yenu;ili kuokoka.Mwenyezi Mungu ambaye aliyewafanyia ardhi hii kama tandiko,na mbingu kama paa na akateremsha maji kutoka mawinguni,na kwa hayo akatoa matunda yawe riziki kwenu,Basi msimfanyie Mwenyezi Mungu washirika,ili hali mnaelewa.) Albaqarah:22.Mola wa walimwengu: Mfano wa yaliyotangulia basi katika hii aya ni kukiri upwekesho,upwekesho wa uumba na upwekesho wa Ungu kama namna ilivyotangulia,Na Mola mwenye kuabudiwa,kwamba yeye ambaye anastahiki ibada,ama mwengineyo hastahiki ibada,kwani kwamba si Mola,kisha vile vile haitoshi kwamba mwanadamu anakiri kwa Uumba wake Mwenyezi Mungu bali lazima awe anakubali kuabudu kwa Mwenyezi Mungu  alietakasika na utukufu wake,na anafanya hali ya kumtakasia kwake Mwenyezi Mungu ibada alietakasika na utukufu,basi midhali amekubali kwamba yeye Mola,basi kwamba inamlazimu awe mwenye kukubali kua yeye ni mwenye kuabudiwa,na hakika mwenginewe hastahiki chochote katika ibada,na dalili juu ya kwamba ibada pekee kwa Mwenyezi Mungu tamko lake: (Enyi watu!Muabuduni Mola wenu ambaye amewaumbeni ninyi na wale waliyokuwa kabla yenu;ili kuokoka.Mwenyezi Mungu ambaye aliyewafanyia ardhi hii kama tandiko,na mbingu kama paa na akateremsha maji kutoka mawinguni,na kwa hayo akatoa matunda yawe riziki kwenu,Basi msimfanyie Mwenyezi Mungu washirika,ili hali mnaelewa.) Albaqarah:22.Enyi watu:Huuwito kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa watu wote waumini na makafiri,kwani Mwenyezi Mungu ametaja katika hii sura surat albaqarah vigawanyiko vya watu watatu:Kigawanyiko cha kwanza: Waumini ambao wanaamini yasioonekana na wanaamini siku ya mwisho na akawasifu kwamba wao ndio wenye kufaulu katika tamko lake: (Hao wapo katika uwongofu utokao kwa Mola wao na hao ndio waliofaulu). Albaqarah:5.Kigawanyiko cha pili: Makafiri ambao wamedhihirisha ukafiri na kupinga,amesema mtukufu: (Hakika wale waliokufuru ni sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawaamini). Albaqarah:6.Kigawanyiko cha tatu:Wanafiki ambao si pamoja na makafiri na si pamoja na waumini (Wanatangatanga baina ya huku na huko,huku hawako na huko hawako) Annisaai:143.Basi wao ni waumini nje lakini wao ni makafiri ndani yake,na wao ni shari kuliko makafiri wenye kudhihirisha ukafiri wao,na kwa hivyo ameteremsha basi kwao sehemu ya aya kumi,wakati ambapo ameteremsha kwa aya za waumini ni chache,na kwa makafiri aya mbili (kwa ubaya wao) ama wanafiki basi akaanza kuwataja wao katika tamko lake: (Na miongoni mwa watu wapo wasemao tumeamini) Albaqarah:8. mpaka katika tamko lake: (Unakaribia umetaka kunyakua macho yao)Albaqarah:20.Haya yote kwa wanafiki kwa ukubwa wa hatari yao na ubaya wa vitendo vyao,na pindi alipoeleza hizi aina tatu kasema: ((Enyi watu) huu ni wito kwa wote aina waumini,na makafiri,na wanafiki,wamesema wanazuoni:Mwanzo wa wito katika qur-ani ni huu (Enyi watu muabuduni Mola wenu) Albaqarah:21.    Muabuduni:kwamba takaseni kwake ibada,kwanini? kwamba yeye Mola wenu,na ibada haitendeki isipokua kwa Mola alietakasika na utukufu,kisha akataja dalili juu ya hayo nayo tamko lake: (Ambae amekuumbeni nyinyi).Na wale ambao kabla yenu nyinyi:katika uma zote (zilizopita) ameumba Mwenyezi Mungu alietakasika na utukufu wake kaumba Malaika na majini na wanadamu na viumbe wote.Ili mupate kuwa wachamungu:Mukizingatia nyinyi haya,basi huenda hii ikawasababishia uchamungu pindi mukizingatia kwamba yeye ndie ambae amekuumbeni na akaumba ambao waliokua kabla yenu,ili mupate kumcha yeye alietakasika na utukufu wake,ili mupate nyinyi kuogopa adhabu yangu na kujikinga na moto,kwani kwamba haikukingini isipokua ibada kwake yeye Mola wenu ambaye amekuumbeni nyinyi na wale waliokuwa kabla yenu.      Kisha akaendelea kuwatambulisha juu ya Ungu wake na kuabudu kwake  alietakasika na utukufu wake kwa tamko lake: (Amefanya kwenu nyinyi ardhi tandiko) kwamba busati(Na Mwenyezi Mungu amefanya kwenu ardhi tandiko) Nuh:19.TNB: Hii ni sehemu ya nne ya kitabu hiki cha Masomo katika Umuhimu wa Tawheed.Muhtasari wa kitabu cha (Al-Usulu AL-Thalathah)Kilicho tungwa na Imamu Sheikh Saleh bin Fauzan Al-Fawzan. Bado kinaendelea tufatilie toleo la 5 inshallah.